Katika kuhakikisha ushirika unaendelea kusalia katika Mkoa wa Kilimanjaro Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) imeendelea kufanya vizuri katika kipindi Cha miaka miwili mfululizo kwa kufikisha mtaji wa Billioni 4.4 kutoka Billion 2.7 ulivyokuwa Mwaka 2021.
Meneja wa Benki hiyo Godfrey Ng'urah ameyasema hayo April 13,2023 Mkoani Kilimanjaro alipokuwa akizungumza katika Mkutano na wanahabari.
Ng'urah amesema kwa sasa Benki hiyo imeimarika katika soko kwani mpaka sasa vyama vya ushirika kote nchini wamewekeza Billion 3.7 katika katika Benki hiyo ya KCBL.
Naye Mrajisi wa vyama vya ushirika Tanzania, Dr Benson Ndiege, amewata Wanaushirika, wadau na wafanyaBiashara kuwekeza kwa kununua hisa katika Benki hiyo.
Cc Banana Fm Tz Esther Machangu
#BURUDANI: "Msanii uje na mradi wa Sanaa tukukopeshe hela" hii ni kauli ya naibu waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mwinjuma (Mwana FA) aliyoitoa wakati akizungumza na Jukwaa la Wasanii Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro mara baada ya kuwatembelea Alhamisi Aprili 13,2023.
Naibu waziri amefika katika wilaya hiyo kuzungumza na wasanii hao ikiwa nikuitikia ombi la Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafuwe aliyeomba naibu waziri huyo kufika na kusikiliza changamoto mbalimbali pamoja na mahitaji waliyonayo wasanii wa wilaya hiyo.
Anaripoti @praygodmunisi_tz
mwanafa @saashishamafuwe
#HABARI: Mamia ya watumiaji wa Barabara kuu ya Moshi Arusha wamekwama katika eneo la Kwa wasomali nje kidogo ya Mji wa Bomang'ombe wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro baada ya Daraja la Mto Biriri Kujaa maji ya mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika ukanda wa juu wa wilaya ya Siha.
Hata hivyo daraja hilo limekuwa likikumbwa na mkasa huo mara kwa mara pindi mvua zinaponyesha licha yakufanyiwa maboresho lakini bado changamoto hiyo imebaki palepale.
Mpaka wakati huu tunapochapisha taarifa hizi bado maji hayo ni mengi ambayo yamepelekea pia kuaribu kingo za daraja hilo ambalo ni kiungo muhimu kwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na wale wanaoelekea Mikoa ya Dodoma, Mwanza kupitia barabara hiyo.
Katika eneo hilo hakuna njia Mbadala hivyo watumiaji wanalazimika kukaa na kusubiri maji hayo yapungue na taratibu nyingine zakiusalama.
Anaripoti @praygodmunisi_tz
#bananafmdigitalupdates
Dereva wa Bodaboda ambae jina lake halikufahamika mara moja amejeruhiwa vibaya baada ya pikipiki aliyokuwa akiendesha kugonga ubavuni mwa gari la abiria aina ya Costa na kisha kuingia uvunguni mwa lori la mizigo.
Ajali hiyo imetokea jioni ya leo Jumapili April 2,2023 barabara kuu ya Moshi Arusha katika eneo la Stendi ya Sanya Bomang'ombe wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro.
Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema kuwa dereva huyo wa bodaboda amekumbwa na maswahibu hayo baada ya kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake kwa upande wakushoto ndipo akaenda kujigonga kwenye gari hilo la abiria kwa ubavu na kisha baadae kuingia kwenye lori hilo lililokuwa likipita katika eneo hilo kuelekea upande wa Moshi.
Baada yakutokea kwa ajali hiyo dereva huyo alichukuliwa mara moja na kuwahishwa hospitali kwaajili ya matibabu zaidi kutokana na majeraha aliyoyapata ikiwemo eneo la kichwani.
Hata hivyo Costa hiyo iliondoka eneo la tukio kabla ya askari wa usalama barabarani kufika kwaajli ya taratibu za kiusalama barabarani huku dereva wa lori hilo akisalia eneo la tukio kwa muda wa dakika 37 kutokana na pikipiki hiyo kukwama chini ya Lori hilo.
Mdhamini Mkuu wa Michuano ya Ramadhani CUP Wilayani Hai Hashim Mwanga, Ameeleza kilichosababisha kuyadhamini mashindano hayo.
#bananafmupdates
Kutokakatika viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan anawatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi kundi la 03/19 (Shahada ya Sayansi ya Kijeshi) na kundi la 69/21, pamoja na Mahafali ya 3 ya Shahada ya Sayansi ya kijeshi kundi la 03/19.
Cc.@denisdigitaltza
#bananadigital
#bananafmupdates
#chapakazikularaha
Kocha wa Makipa wa Klabu ya Simba, Muharami Said Sultan amekamatwa na madawa ya kulevya aina ya Heroine.
Taarifa hizo zimetolewa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Cc, @denisdigitaltza
#bananadigital
#bananafmupdates
Shujaa Majaliwa Jackson amemshukuru Rais Samia @samia_suluhu_hassan baada ya kupewa kiasi cha shilingi 5,023,000, na wabunge , wakimpongeza kwa ujasiri aliouonesha wakati wa ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Bukoba - Kagera.
Mchango huo wameutoa leo Ijumaa Novemba 11,2022 Bungeni Jijini Dodoma ambapo majaliwa alifika leo kama mgeni.
Cc Denis Digitaltz
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania @samia_suluhu_hassan, amezinduzi Mradi wa Maji Kigamboni na kugawa Mitambo ya Kuchimba visima katika Ujenzi wa Mabwawa na Makabidhiano ya Eneo la Ujenzi wa Bwawa la Kidunda.
Cc, @denisdigitaltza
#bananadigital
#bananafmupdates
Kijana mwenye umri wa miaka 23 amekamatwa na Polisi baada ya kumrushia mayai Mfalme wa Uingereza, Charles aliyekuwa akifanya ziara huko Yorkshire Kaskazini.
Kabla ya kijana huyo kutekeleza tukio hilo, Polisi walimzuia mwanaume huyo kwenye umati wa watu uliokusanyika katika eneo la Micklegate.
Kijana huyo alisikika akipiga kelele na kueleza kuwa nchi hiyo ilijengwa kwa damu ya watumwa huku akiendelea kuzomea.
Watu wengine walisikika wakisema kuwa Mungu mwokoe Mfalme na aibu juu yake kutoka kwa mwanandamanaji huyo.
Kupitia video zilizosambaa mitandaoni zilimuonesha Mfalme Charles akipeana mikono na watu mashuhuri akiwemo Meya wa eneo la Micklegate huku mayai yakiruka kuelekea kwake.
Polisi wa Yorkshire Kaskazini walisema mwanaume huyo alikamatwa kwa tuhuma za kosa hilo na tayari amewekwa chini ya ulinzi.
Tukio hilo lilitokea siku ya pili ya ziara rasmi ya kifalme huko Yorkshire, wakati ambapo Mfalme na Malkia Consort wakisafiri kwenda Doncaster.
Cc, @denisdigitaltza
#bananadigital
#bananafmupdates
@bbcswahili
Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha mrakibu wa Polisi SP Solomoni Mwangamilo, amewataka madereva wa vyombo vya moto kuwa makini katika matumizi ya vyombo hivyo Pamoja nakufuata sheria za usalama barabarani.
Cc, @denisdigitaltza
#bananadigital
#bananafmupdates
#chapakazikularaha
DC MTANDA AKABIDHI MILIONI 400 KWA VIKUNDI VYA MKOPO JIJI LA ARUSHA.
Cc, @denisdigitaltza
@said_mtanda
#bananadigital
#bananafmupdates
#chapakazikularaha
Baada ya Rais Samia @samia_suluhu_hassan kuagiza Majaliwa Jackson, kijana aliyejitosa kuwaokoa abiria waliokuwa ndani ya ndege ya Precision Air @precisionairtz , ilipoanguka Ziwa Victoria mkoani Kagera, akabidhiwe kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ili apatiwe nafasi katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa ajili ya mafunzo.
Cc, @denisdigitaltza
#bananadigital
Jitihada za vikosi vya uokoaji na wananchi, hatimaye zimewezesha kuvutwa kwa ndege ya Precision Air mpaka ufukweni.
Taarifa mpya zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, imeeleza kuwa jumla ya watu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo, ni 19.
Cc, @denisdigitaltza
#bananadigital
NDEGE YA PRECISION YAANGUKA ZIWA VICTORIA.
Ndege ya abiria shirika la ndege la Precision Air imeanguka ziwa Victoria Bukoba Kagera Asubuhi ya leo jumapili Novemba 6,2022, shughuli za uokoaji zinaendelea.
Taarifa zaidi zitakujia.
Cc, @denisdigitaltza
#bananadigital