05/03/2021
ELIMU YA MATUMIZI YA FEDHA
Fedha inatakiwa uwe na nidhamu nayo katika kuitumia. Kanuni ifuatayo imetumika kwenye vyanzo vyako vyote vya fedha ili uwe na mafanikio yenye amani.
*Kanuni*
•Fungu la kumi 10%
•Akiba 30%
•Matumizi 40%
•Dharura 10%
•Msaada 5%
•Sadaka 5%
*Jumla 100%*
Hii kanuni inafanya kazi katika kila fedha unayopata k**a pato lako la mwezi.
*Mfano* K**a unapata Sh. Laki 5 kwa mwezi (500,000/=) fungu la 10 ni Sh. 50,000/=, hii ni mali ya Mungu si yako. Unatakiwa utoe kanisani kila mwezi, pia hata k**a umepewa fedha k**a zawadi unapaswa uitolee fungu la 10.
*Faida za Fungu la kumi*
•Hulinda kazi au biashara unayoifanya dhidi ya adui.
•Magonjwa, ajali(vitu vitakavyokufanya utumie fedha bila mpangilio) n.k yanakuwa mbali nawe.
*Akiba 30*
•Fedha hii unaiweka kwa matumizi yako ya baadae k**a kujenga, kusomesha, kulima, vitega uchumi n.k.
*mfano* k**a pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/= asilimia 30 ni sh. 150,000/=
*Matumizi 40*
•Fedha hii itatumika kwa matumizi ya kila siku, chakula, maji, umeme n.k
•Hutumika pia kwa matumizi mengine ya starehe, mavazi n.k
•K**a pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/=, asilimia 40 ni sh. 200,000/=
• *angalizo* matumizi yasizidi fedha hiyo.
*Dharura 10*
•Hii ni fedha unayotunza kwa ajili ya mambo usiyoyatalajia k**a msiba, magonjwa au kukwama jambo lolote n.k.
•K**a pato lako ni sh. 500,000/= unatunza sh. 50,000/= kwa ajili ya dharura kwa mwezi.
*Msaada 5%*
•Hii ni fedha ya msaada kwa watu wenye shida; watoto yatima, wajane, walemavu n.k
• k**a pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/= unatunza sh. 25,000/= kwa ajili ya msaada.
*Sadaka 5%*
•K**a pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/= tenga sh. 25,000/= kwa ajili ya sadaka kwa mwezi.
•Igawe fedha hii Mara 4 kwa sababu mwezi una jumapili 4 ambapo utapata ni sh. 6,250/=. Hivyo kila jumapili utae days kutoa sh. 6,250/=.
*Kumbuka*;
Kitu chochote kinachoitwa sadaka kiombee kabla hujakitoa siku mbili 2 au 3 ndipo uitoe sadaka.
Credit to Michael Lukindo