Ikiwa ni miaka 24 imepita Tangu afariki Rais na Muasisi wa nchi ya Tanganyika (Baadae Tanzania) hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo leo Oktoba 14 watanzania wanaadhimisha kifo chake.
Abdallah Mkokoi ambaye ni mfuasi mkubwa wa Falsafa za Mwalimu Nyerere, anaeleza Namna Mwalimu alivyoijenga Tanzania kwa nia njema na misingi bora ambayo anawasihi Watanzania na Viongozi kuziishi Falsafa hizo.
#LDNews
#NyerereDay
#october14
#LDNews
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu Edith Swebe amezungumza na waganga wa tiba za asili na tiba mbadala kuhusu masuala ya ukiukwaji wa taratibu za kisheria kutokana na kuwepo kwa shutuma nyingi kama za mauwaji ambazo zinazowahusisha moja kwa moja kutokana na huduma wanazotoa kwa wateja wao.
#LDNews
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mohammed Moyo amesema, kupitia fedha za makato ya Wakulima Shilingi 30 fedha hizo zitarudi kwa wananchi kwaajili ya kujenga zahanati kwa kuendeleza hatua iliyoanza kupigwa na wananchi hao.
#LDNews
Wananchi wa kijiji cha Namkula Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi, wamekiri kusikitishwa na adha ya kukosa Zahanati kijijini kwao, jambo linalowasukuma kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya Afya, changamoto inayowaathiri zaidi watoto na akina mama wajawazito kijijini hapo.
#LDNews
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mohammed Moyo amewataka viongozi KUACHA TABIA YA KUFICHA MAMBO na kwamba sio wakati wote viongozi wawe ni wa kusifiwa tu.
Shule ya Namkula ni wanufaika wa ujenzi wa madarasa matatu ya mradi wa Boost lakini pia wananchi wamepewa ahadi ya kupatiwa fedha zingine kwaajili ya kurekebisha miundombinu ya shule za msingi.
Mkurugenzi na Afisa elimu wa Wilaya ya Nachingwea wameagizwa kutafuta haraka shilingi milioni 72 za kujenga vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya hiyo kutokana na vilivyopo sasa kuchakaa kiasi cha kuhatarisha usalama wa wanafunzi.
#LDNews
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea MOHAMMED MOYO akizungumza kwenye mkutano na wananchi wa kata ya Mnero Baada ya kusikiliza hoja ya msisitizo iliyotolewa na Diwani na wananchi wa kata hiyo ameamrisha ujenzi wa madarasa katika shule ya Namkula kuanza mara moja ili kudhibiti hatari ya wanafunzi kusoma katika mazingira yasiyo rafiki kwa usalama wao.
#LDNews
Wakazi wa Kata ya Mnero Miembeni Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi wamelalamika kuhusu ubovu wa madarasa katika Shule ya msingi Namkula madarasa ambayo yanatishia usalama wa watoto kwani ni mabovu mno.
Wananchi hao wamesema, serikali ilijenga madarasa matatu katika shule hiyo Kongwe lakini hali ni mbaya katika madarasa mengine kwani hayajafanyiwa ukarabati kwa kitambo kirefu na Bado wanafunzi wanayatumia katika masomo.
#LDNews
Mratibu wa Shirika la TUNA NDOTO, shirika lililo chini ya Kanisa la FPCT Mkoani Lindi, Suleiman Moses katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ambapo Shirika hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wametoa elimu kwa wanafunzi Wa Sekondari na Msingi - ametaka elimu ya ukatili iendelee kutolewa kwa watoto wa kike kwani wamekuwa ni wahanga wakubwa wa matukio hayo.
Aidha, watoto nao wameeleza ni kwa namna gani wameelewa mafunzo waliyopatiwa na namna watakavyotumia ujuzi huo kujilinda ili wasifanyiwe vitendo vya ukatili.
#LDNews
Katika kuadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Lindi Pili Mande amezindua kampeni ya "ONGEA NAO" iliyodhamiria kuweka bayana matendo ya ukatili na namna ya kujikinga kwa watoto mashuleni.
Aidha, ameeleza ya kuwa elimu hiyo itawafikia watoto wa jinsia yote kwani suala la ukatili hufanyiwa yeyote na ili kuwaweka watoto wote katika mazingira salama ni lazima wafahamu ukweli.
#LDNews
Ikiwa ni Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, Jeshi la Polisi Mkoani Lindi kupitia mtandao wa Askari wanawake wa Mkoa wa Lindi wameiadhimisha siku hiyo kwa kutoa elimu na kuzungumza na wanafunzi wa kike na wakiume kuhusu Masuala ya Ukatili, elimu iliyotolewa katika shule ya sekondari Lindi wakijumuishwa na wanafunzi wengine kutoka katika shule za msingi mbalimbali mkoani humo.
Akizungumza na wanafunzi hao SSP Anna Tembo ambaye ni Kaimu Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya jinai Mkoani Lindi, amewataka watoto wa kike kuwa makini na viashiria vyote vinavyoweza kuwasababishia kufanyiwa ukatili ikiwa ni pamoja na kuacha tabia ya kusikiliza hadaa za wanaume wanapowashawishi kuonana nao. SSP Tembo anasema, kwa umri wa watoto wa darasa la nne na kuendelea ni rahisi kung'amua dalili za hatari hivyo amewataka kujilinda dhidi ya tabia zote hatarishi zinazoweza kuwasababishia kufanyiwa ukatili.
#ldnews
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amepiga marufuku maandamano yanayoashiria uvunjifu wa amani na kuwataka wananchi kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa ili kuepuka kuvunja sheria hasa nyakati hizi za mwisho wa Mwaka.
Magomi ametoa agizo hilo mara baada ya kumaliza mazoezi ya utayari kwa Jeshi la polisi ikiwa ni kuelekea mwisho wa mwaka huku akitoa rai kwa watu wanaojihusisha na uhalifu kuacha mara moja.
#ldnews
Katika Wiki ya Shirika la Posta duniani na maadhimisho ya siku ya Shirika hilo, Posta Mkoani Lindi wamempatia mlemavu wa miguu bi TERESIA MWANGA kiti maalumu na vyakula kwa Walemavu wote wa LASIBULA hii ikiwa kama Desturi yao katika kuadhimisha siku yao. Aidha, wamewaomba wadau wengine kujitokeza kuwasaidia wazee hao kwani msaada wao pekee hautoshi na uhitaji katika kituo hiko ni Mkubwa.
#ldnews
Bibi mlemavu wa viungo anayeishi katika nyumba ya kulea wazee akifurahia zawadi ya Kiti Mwendo alichopewa na shirika la Posta Mkoani Lindi katika maadhimisho ya siku/wiki ya Posta Duniani.
Furaha
#ldnews
Aidha Mary Laizer amesema mila ya kuchomeka mkuki mlangoni kwa jamii hiyo ilitokea zamani kutokana na kutokuwa na maradhi tofauti na sasa, pia kwa sasa elimu imeingia kwa jamii ya kimaasai.
#LDNews
Akitoa ufafanuzi mwakilishi wa TAKUKURU amesema siyo sahihi kiongozi kuchukua fedha za mnufaika wa TASAF huku mkuu wa wilaya Hassan Bomboko akitoa onyo kwa viongozi wa serikali za vijiji wanaofanya kazi mazoea na kutanguliza maslahi binafsi.
#LDNews
Baadhi ya wananchi katika wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza wamelalamikia kukatwa fedha zao za mfuko wa kaya maskini TASAF bila ihali yao huku baadhi yao wakiwatuhumu viongozi wa serikali za mtaa kuwa na upendeleo wakati wa kusajili kaya hizo.
Wameeleza hayo wakati wa mkutano wa kusikiliza kero za wananchi ulioandaliwa na mkuu wa wilaya hiyo Hassan Bomboko, ambapo wamemuomba kuwasaidia kutatua changamoto hiyo.
#ldnews