31/07/2024
MIAKA 5 YA NDOA NA MAREHEMU (Bila Wazazi Kujua)
SEHEMU YA 1
Mtunzi: Mnyonge Wakchuu
Baada Ya Kumaliza kidato cha sita Nelson alifanikiwa kujiunga na moja ya Chuo Kikubwa hapa Tanzania. Muda mfupi aliingia kwenye dimbwi la mapenzi na Bint mrembo aliyefahamika kwa Jina La Suzan.
Suzan alikuwa ni bint mrembo sana Mrefu Kiasi Mwembamba mwenye rangi nzuri ya kuvutia katika ngozi yake na nywele zake ndefu Natural yaani alizikuza bila ya kutia Dawa ambazo ziliwafanya wasichana wengi chuoni hapo wamuone Suzan ni Bint Anaeringa kutokana na uzuri wake ila kiukweli Suzan alikuwa anaringa Haswa.
Tofauti na Uzuri aliokuwa nao Suzan ambao ulikuwa ukiwachanganya Wanaume wengi chuoni Suzan alikuwa ni Binti aliyezaliwa kwenye Familia ya Kitajiri
Familia ambayo ilimfanya binti huyo asiweze Kufanya kitu chochote kutokana na Baba ake kumuwekea wasichana wa kazi ndani ambao walimfanyia kila kitu Suzan.
Suzan alikuwa sio mwanamke wa kupika Wala Kuosha Viombo Yaani Sio Wa Kufua au Kusafisha Baadhi Ya maeneo ya nyumba yao. Suzan yeye alikuwa ni Bint wa Kula Kulala Kuchezea simu yake na kwenda viwanja vya starehe kwa ajili ya Kujirusha na Marafiki zake tu. Hata Pesa alizokuwa akipewa na baba ake zilimpa Sana Jeuri Suzan
ikiwa Nelson yeye ni Kijana Handsome sana Mrefu kiasi na Body fulani hivi ya Mazoezi ambayo iliwachanganya wasichana wengi Chuoni Hapo. Alikuwa ni Mweupe kiasi na mweusi kias yaan yupo Katikat Ukirud kwa hawa Waswahil wenzetu utaskia Nelson alikuwa na Rangi Ya Maji Ya Kunde. Sijui Mmenielewa. Ila Nelson Bwana Ni Kijana Aliyezaliwa kwenye familia maskini sana Baada ya baba ake kufariki akiwa amemuacha Mama Nelson na Ujauzito wa Miezi 8 Wa kijana wao Nelson. Hivyo Majukumu yote ya malezi aliachiwa mama ambaye alihakikisha Kumlea Nelson mpaka kufikia sasa ingawa walihama hama nyumba nyingi kutokana na kukosa kodi lakini mama Nelson alisimama kidete na kuhakikisha Kijana wake anapata malezi na Elimu iliyokuwa Bora.
Ingawa Matukio mengi ya kutisha, visa vya maisha na migogoro katika familia ni miongoni mwa mambo yanayopatikana katika Dunia. Ila Acha Tuitafsiri Dunia katika Maumbo Mengi na maana tofauti tofauti ambazo mpaka leo hakuna ajuae asili ya Dunia.
Hii Leo Nelson anaishi na Msichana Ambaye ni marehemu katika ndoa yake Bila ya wazazi Kujua Yaani Bila Kufahamu Chochote kwa kipindi Chote cha Maisha Yao.
Endelea Sasa……
Zilikuwa ni shamra shamra za pekee kwa kila mwanafunzi, waliopiga picha na wazazi wao kwa pamoja huku wakifurahi na marafiki kwa nyakati hizo. Ni Mwaka wa tatu sasa wanafunzi wakifurahi kuhitimu mafunzo yao katika Moja ya chuo kikubwa Tanzania. Kwa Maana Sherehe ni Miongoni mwa maisha ya Furaha hasa wanafunzi wanapokuwa wakihitimi mafunzo yao.
Mwanadada mtanashati aliyegemeza kichwa katika mapaja ya Nelson huku yakimtoka Maneno yaliyojawa na sauti ya Hub kwa wakati huo.
“Nelson kuna kitu naomba nikueleze, Inawezekana kikajenga kitu katika maisha yetu hapo baadae” Maneno ambayo yalimfanya Nelson Ajiweke vizuri kumsikiliza Suz.
“Niambie Mpenzi wangu, Wewe ndio kila kitu kwangu, Unaweza kusema Chochote” Alizungumza Nelson huku akimfuta suzan Jasho kwa Kiganja chake cha mkono katika Paji la Uso.
“Kweli Nelson ” Suz alisisitiza na kumfanya ainuke na kuanza kutazamana huku wakitabasamu.
Ghafla Sura ya Nelson ilipoteza nuru ya tabasamu huku akiwa katika mshangao uliomstajabisha Suz na Kutoelewa kwanini ilikuwa hivyo kwa wakati huo.
Nelson aliinuka na kumuacha Suz chini, Alielekea upande wa getini ambalo wageni waalikwa walilitumia kuingia katika uwanja wa chuo. Suzan aligeuka kwa haraka kumtazama Nelson kule alipoelekea.
“Nelson Nelson...” Suz aliita, alijitahidi nae kuinuka ili kumfuata James alipoelekea.
Mama aliyeingia ukumbini huku akiwa ameshikilia daftari lililochoka kwa kutunza kwa muda mrefu kwa sehemu tofauti tofauti. Nelson alifika na Kumsukuma Mama huyo aliyefanya Daftari hilo kuruka na kupeperuka kwa baadh ya karatasi.
“Nooooo Nelson... Usifanye Hivyo” Suz aliwahi na Kumshika Nelson.
Yule Mama alifika chini na kujiwahi na mikono yake ili asiweze kuanguka vibaya na kusababisha majeraha katika mwili wake.
“Niache Suzy... Niache” Nelson alikiwa mkali ghafla. Alionekana mtu mwenye kukasirishwa na yule mama kuingia katika sherehe yao.
Wanafunzi, Walimu kwa Wazazi na waalikwa wengine tofauti walisogea kwa Nelson na Kumzonga huku wakimzuia kufanya jambo lengine tofauti na hayo aliyoyafanya kwa kumsukuma yule Mama.
“Nelson Mwanangu, Ulitegemea kuyafanya haya kweli.... Nimekukosea nini Mwanangu” Kauli hii ilimfanya kila mmoja kushangazwa na yale aliyoyafanya Nelson.
Minong’ono ya watu waliokuwa wakijiuliza maswali juu ya yule mama alikuwa nani kwa Nelson wote walikaa kimya.
“Mama..!” Suz aliita kwa Mshangao mkubwa.
Nelson alimtazama Suz pasipo kuzungumza chochote. Suz alisogea karibu na mama yake Nelson. Alimshika mkono na kumuinua kwa kumuweka kitako pale alipokuwa ameanguka.
“Asante Mwanangu” Mama Nelson kwa Sauti ya Chini yenye Kutia huruma na kumfanya kila mmoja kuhisi uchungu kwa kile alichofanyiwa.
Nelson alijawa na Hasira huku akizungumza kwa Jazba ya Juu Kabisa “Suz Muache huyo Mama... Muache, Aumfahamu na hauna sababu za kumfahamu. Ni Mama angu lakini siwezi kuwa na mama masikini kiasi hicho Mama gani kipato chake cha kuunga unga si bora nisiwe na mama tu katika dunia ya Leo” Nelson alitoka kwa hasira huku akilia na kuelekea upande wa madarasa yao.
Suz alitoka kumfuata Nelson. Alifika na kumtazama Nelson kwa Hasira. Alihisi amemkosea sana Mpenzi wake jambo ambalo hakuweza kuliwaza kwa Kipindi chote katika mahusiano yao.
Mama Nelson aliinuka taratibu alijipangusa na kutoweka eneo hilo. Ingawa aliwaacha watu wakizungumza kwa kile kilichotokea lakini hakulifikiria hilo kuwa ni jambo kubwa kwake. Akili yake iliwaza kwa mtoto wake Nelson Juu ya Kumkataa na Kumsukuma Mbele za Watu.
Alisimama na kutazama nyuma, alimuona Nelson kwa mbali akiwa amekumbatiwa na Suzy. Aliinua Upande wa kanga na kufuta chozi lilitoka jicho la kushoto kufuatana na kulia kwa wakati huo. Mama Nelson aliinua Mikono Juu kumshukuru Mwenyezi Mungu kisha aliendelea na Safari yake ya kurejea Nyumbani.
Mnamo saa 12 Jioni Majira ya anga yaliyobadili muonekano wake na kuleta mwangaza hafifu uliyoashiria giza kuingia katika Uso wa Dunia.
Watu walitawanyika kuelekea majumbani Mwao. Wanafunzi waliojumuika na wazazi wao katika usafiri mmoja mbali na wale waliorudi kivyao na wapenzi wao. Hata kwa Nelson na Suz ilikuwa tofauti Pia.
Saa 9 Usiku, Mama Nelson alilala hali ya kuwa na dukuduku moyoni mwake. Nelson alirudi akiwa amelewa alitembea kwa kupepesuka akitokea kwenye gari na rafiki zake. Nelson aliinua mkono kuwapungui kwa ishara ya kwa heri. Aliingia ndani na kujilaza kwenye sofa, Pasipo kufikiria mama yake atakuwa kwenye hali gani kwa wakati huu.
Asubuhi kulipokucha Mama Nelson alikuwa wa kwanza Kuamka, Alitoka na kuelekea katika harakati zake za kila siku. Mara kadhaa mama Nelson alikuwa akihudumu katika maofisi mbalimbali kwa kuwapatia vitafunwa kwa ajili ya kifungua kinywa wafanyakazi wa maofisi. Hivyo kulimlazimu kuamka mapema sana. Hata alipomuona Nelson hakuhitaji kufahamu alirudi saa ngapi.
Nelson alijihisi kuwa sawa hata kitendo alichokifanya jana kwa Mzazi wake haikuwa tatizo kwake.
Mnamo saa 2 Asubuhi Suz alistuka kutoka Usingizini. Alijinyoosha viungo vyake, Alivuta shuka pembeni alichukua simu yake na kutoa Nywila (password). Alijihisi kuwa ni mtu mwenye uchovu sana alitupia simu pembeni na kujilaza Tena.
“Suz... Suzan... Embu njoo mara moja” sauti nzito ya kiume kwa jazba iliyomuamsha Suz. Huku Suzy akijisonya kwa uchovu na kuhisi kusumbuliwa.
“John Naomba nipumzike kidogo, Nikiamka tutazungumza vizuri” Suzan alizungumza kwa uchovu, alipinduka upande mwengine na kujilaza.
“Sawa Ukiamka, Uje tu namaelezo tosherezi kuhusu Nelson ni nani yako” John alishika kitasa cha mlango alifungua na kuufunga kwa Hasira. Kisha alitoweka.
“Aah Ushaanza tena” Suzan aliinuka na kujiweka sawa kitandani akimfikiria John ambaye Suz amekuwa akimfanyia kila kitu John Kuanzia kumvisha, Kumlisha na Kumlipia pango la sehemu wanapoishi. ila ndo amekuwa Mwanaume anaemuumiza sana Kichwa Suz kuliko Nelson.
Nelson alistuka kutoka usingizini akiwa na hali ya uchovu sana na vile hali yake ya jana aliyorudi nayo ilichangia kwa kiasi kikubwa kuwa hivyo.
Aliininuka kutoka katika viti ambavyo maisha yake yote amekuwa akilala hapo tofauti na kipindi ambacho yupo chuo mara nyingi alijichanganya na marafiki zake au kuishi maisha ya starehe na Suzan kupitia Mikopo ya Wanafunzi Chuoni. Nelson aliweka sawa Mito Sebreni huku akijisonya sonya.
Haikuchukua Muda Mama Nelson Kurud kutoka katika mizunguko yake. Na siku hii ya Leo hakuweza kuwapikia vitumbua mtaani k**a kawaida yake ambayo hufanya kila siku baada ya kurud Kutoka ofisini. Siku zote huwa anapika Vitumbua vingine mtaani.
Mama Nelson aliingia ndani huku Nelson akiwa Sebreni anamsubir mama ake ambaye hakutaka hata kutoka nje kufahamu k**a amerud na anapika au Lah.
“Shikamoo Mama” Nelson alimsalimu mama ake huku akitazama chini kwa Aibu.
Mama Nelson aliingia chumbani kwake pasipo kuitikia Salam ya Mwanae. Aliingia huku akiwa amejawa na Jazba alifika ndani na kujitupa kitandani…kwa Sauti kubwa Mama Nelson aliangusha kilio kilichoambatana na maneno makali yenye Kumuumiza juu Ya mwanae Nelson.
Nelson aliingia taratibu chumbani kwa mama ake huku akiwa Mnyonge Mwenye sura iliyojawa na huzini baada ya kumsikia mama ake akilia kwa uchungu.
“Mama… Mama…Mama Mi Mwanao Nelson Mama.. Mwanao mimi Mama nimekuwa mkosefu Mimi Mama kila siku aaah Mama naomba Nisikilize mwanao walau kidogo tu Mama angu… Mama Mama Nisamehe Mwanao Mama najua nimekukosea na sikutarajia kufanya kitu k**a kile Nilijikuta tu nimekuwa na Jazba Mama mpaka kufikia kufanya hilo Jambo Mama…. Mama angu Mama Nisamehe Mwanao.. Angalia watu wamejaa Nje wanakuita na kufikiria kuwa tunatatizo Kubwa Mama” Nelson Alizungumza kwa Uchungu huku chozi likimtoka hata ule ujasiri aliojipa asubuh na kuhisi Mama ake ajachukiwa na kile kitendo cha Jana Ulimtoka ghafla.
Mama Nelson aliinuka pasipo kumjibu Mwanae chochote. Alitoka nje na Kuelekea Uwani ambapo baadhi ya wapangaji walitoka kuja kumsikiliza Mama Nelson alikuwa amepatwa na nin mpaka kufikia kulia kwa sauti kubwa hivyo.
Kila mmoja alitamani kufahamu Kwanini Mama Nelson alikuwa akilia. Mama Nelson alifuta Machozi Nelson naye alitoka Ndani na kumfuata mama ake alipo.
“Mama Mama… Naomba unifichie hii aibu yangu mimi mwanao najua nimekukosea mama angu… Nakuomba mama” Nelson alipiga magoti mbele ya mama ake.
Mama Nelson alimuangalia mwanae kwa huruma na maneno aliyoambiwa na mwanae alimuinua na kumkumbatia huku machozi yakimtoka pasipo kuzungumza chochote. Kisha alimuacha na Kuelekea chumbani kwake.
Nelson alibakiwa na mshangao wakutofahamu nini mama ake alimaanisha kwa wakati huo. Naye alimfuata tena ndani Mama yake lakini hakuweza kuingia baada ya Mlango wachumbani kwa Mama ake Kufungwa.
Sura ya Nelson iliyovimba kwa kulia macho Yaliyokuwa mekundu yaliyojawa na majimaji Kuashiria wakati wote Nelson atakuwa mliaji kwa makosa juu ya Mama ake. Mwili Wa Nelson Uliochoka kwa kuhisi joto lililoteketeza nguvu katika mwili wake. Nelson alisota Kwa Mgongo mlangoni mwa Chumba cha Mama ake alipoteza fahamu na kuanguka chini misil ya mzigo aliotupwa kutoka Juu kwa Umbali mrefu.
Huku Mlio wa Simu ya Nelson ikisikika kuita Jina likiwa Limetokea Suzy Pasipo Majibu yeyote Mpaka Simu kukatika.
Ulikuwa Unaskiliza Sehemu Ya Kwanza Ya Simulizi Hii Ya Miaka 5 Ya Ndoa na Marehemu Bila Ya wazazi Kujua.
Je Nelson Atakapozinduka ataweza kusamehewa na Mama ake au Lah na Vipi kuhusu Suzan ambaye anamtafuta Nelson pasipo Kuwa Na Majibu yeyote Kwenye Simu Yake… Au Kibenten John ambaye anahitaji kufaham Nelson ni Nani Kwa Suzan…!?
kuendelea kufuatilia mkasa huu Usisahau Kutufuata kupitia page zetu za Instagrams | Facebook | Pamoja na Tiktok Kwa Jina La Wakchuu au Subscribe Channel Yangu Ya Youtube Ya Wakchuu Uwe wa Kwanza Kufuatilia Mkasa Huu Mwanzo Mwisho
Ila Kwa Maoni Na Ushauri Nifuate Kupitia Whatsapp Au Ujumbe Mfupi wa Maneno Kwa No 0719193809
USIKOSE SEHEMU YA PILI….