Vox News Tz

Vox News Tz The Host Elias sasa inapatikana YouTube

ingia YouTube search the host elias kisha subscribe baada bonyeza alama ya kengele ili uw wa kwanza kupata habari kupitia the host elias

30/06/2023
Mt Hanang in Hanang District on Manyara
15/10/2022

Mt Hanang in Hanang District on Manyara

At work
20/09/2021

At work

MKUTANO WA WADAU WA SEKTA YA AFYA ULIOFANTIKA MKOANI MANYARA AMBAO UMEWAASHIRIKISHA VIONGOZI MBALIMBALI WA SERIKALI NA S...
18/06/2021

MKUTANO WA WADAU WA SEKTA YA AFYA ULIOFANTIKA MKOANI MANYARA AMBAO UMEWAASHIRIKISHA VIONGOZI MBALIMBALI WA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI.. MGENI RASMI KATIKA MKUTANO HUO NI MKUU WA MKOA WA MANYARA CHARLES MAKONGORO NYERERE

07/05/2021

Jeuri Yanga kwa Simba iko hapa
Thursday May 06 2021
JEURI ya Yanga kwa Simba imelalia hapa. Uwepo wa mechi sita ngumu na zenye ushindani kwa Simba unaweka hai matumaini ya Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu licha ya Simba kuongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na mechi mbili za kiporo dhidi yao.

Pamoja na hesabu kuonekana zinaiweka Simba katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa msimu huu, ikiwa itachanga vyema karata zake katika mechi hizo sita inaweza kutimiza lengo lake hilo lakini k**a ikishindwa kutimiza hilo, ni wazi kwamba inaweza kujikuta inawapa fursa watani wao Yanga ama kuwafikia au kutwaa ubingwa msimu huu.

Ushindani ambao Simba imekuwa ikipata dhidi ya timu hizo sita na pia kumbukumbu ya mechi za mzunguko wa kwanza ambazo baadhi Simba iliangusha pointi, vinaweka hai matumaini ya ubingwa kwa Yanga licha ya kutanguliwa kwa pointi nne na Simba ambazo zinaweza kufika 10 ikiwa watani zao hao watapata ushindi katika mechi zao mbili za viporo.

Katika idadi hiyo ya mechi sita, matumaini makubwa kwa Yanga, kupunguza pengo la pointi baina yake na Simba ni mechi ya watani wa jadi nchini itakayopigwa Jumamosi hii Mei 8 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ushindi katika mechi hiyo utaifanya Yanga kuipunguza kasi Simba kwani itafikisha jumla ya pointi 60 na hivyo kuwa nyuma ya Simba kwa pointi mmoja. Ikumbukwe katika mzunguko wa kwanza, Yanga iliinyima Simba pointi mbili baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.

Ukiondoa mechi hiyo ya wikiendi, upo mchezo ambao unaweza kutibua hesabu za ubingwa za Simba ikiwa itaangusha pointi dhidi ya Azam FC. Ugumu wa mechi hiyo kwa Simba ni aina ya uwanja utakaochezewa wa Azam Complex ambao huwa hawachezi hapo mara kwa mara kulinganisha na wenyeji wao pia mzunguko wa kwanza, Azam FC iliwavuta shati baada ya kutoka sare ya mabao 2-2.

Rekodi ya kutopata ushindi ugenini dhidi ya Namungo FC ni kiashirio tosha kwamba vita ya ubingwa bado ni mbichi kwa Simba. Mara mbili ambazo Simba wamecheza na Namungo kwenye Uwanja wa Majaliwa huko Ruangwa, mechi zilimalizika kwa sare na timu hizo bado hazijakutana katika mechi mbili za msimu huu ambapo ya kwanza, Simba itakuwa mwenyeji na ya marudiano, Namungo watakuwa nyumbani.

Ukiondoa mechi dhidi ya Yanga, Azam na Namungo FC, Simba pia imebakiza michezo miwili migumu dhidi ya Ruvu Shooting na Polisi Tanzania ambazo k**a ikizikabili bila kujiandaa vyema zinaweza kutibua mipango yao ya ubingwa.

Ruvu inayonolewa na Boniface Mkwasa, iliwashangaza Simba baada ya kuwachapa bao 1-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza msimu huu, na kiwango chao katika siku za hivi karibuni kimeonekana kuimarika.

Ingawa Polisi Tanzania wamekuwa hawana takwimu bora pindi wakutanapo na Simba, ushindani mkubwa ambao wamekuwa wakionyesha pindi wanapokuwa katika uwanja wao wa nyumbani, unawalazimisha Simba kujiandaa vyema kuwakabili, vinginevyo wanaweza kutia mchanga kitumbua chao.

Kocha msaidizi wa Yanga, Razack Siwa alisema kuwa timu yake haiwezi kukata tamaa kwenye mbio za ubingwa na watahakikisha wanapambana hadi mwisho

“Bado nafasi ya kutwaa ubingwa tunayo hivyo jambo la msingi ni kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi zetu zilizosalia badala ya kukata tamaa kwani hata wao wapinzani wanaweza pia kupoteza mchezo na pointi,” alisema Siwa.

Kwa upande wa Simba, Kocha Mkuu Didier Gomes Da Rosa alisema pamoja na ugumu wa ratiba iliyo mbele yao, anaamini lengo lao la kutwaa ubingwa litatimia.

Address

Kinondoni

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Vox News Tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Vox News Tz:

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share