25/03/2020
*CORONA NI K**A INATAKA KUIJARIBU DUNIA KIIMANI!!?*
Corona ni gonjwa linalotaka kuitawala dunia na kuiweka chini ya mamlaka yake kwa lazima??
Kila kona ya dunia sasa wanalia na kulazimishwa kujifungia, kufunga kila kitu, kana kwamba hakuna mwanadamu mwenye mamlaka juu yake!
Makusanyiko ya dini nayo yamepigwa marufuku!
Hii ni kumaanisha, Mungu pia amepigwa stop asiabudiwe na wanadamu ila corona tu!?
*AJABU NA KWELI!!*
Rais wa kwanza duniani kuruhusu ibada za kumwabudu Mungu ziendelee k**a kawaida, mbele ya tishio hili, ni Mh John Pombe Magufuli, Rais wa Tanzania!
Watu wamemchukua k**a mtu asiyejali!
Lakini mbele za Mungu wa Mbinguni ndiye Rais pekee aliyemkabidhi Mungu watu wake, na nchi yake pia!
Hapa ndipo watanzaia tunapomngojea Bwana ajitukuze mwenyewe.
Pia naitafakari sana kauli ya Mh Waziri wa Afya wa Tanzania.
Alichosema Mh Waziri kwamba, Tanzania hatuna uwezo wa kuithibiti corona,
Kibinadamu huo ni ukweli wenye asilimia mia na moja! (101%).
*HII INATUFUNDISHA NINI!!?*
Inatufundisha kwamba,
*Tanzania imemchagua Mungu awe ndiye mwokozi wetu, katika jaribu hili la uvuli wa bonde la mauti ya corona!*
Na maandiko yanakiri hivi,
*Heri Taifa ambalo Bwana ni Mungu wao..!*
Kwanini!?
*Kwasababu, Hapana mfalme aokokaye kwa wingi wa uwezo, Wala shujaa haokoki kwa wingi wa nguvu!*
Zaburi 33:12-22.
Mh Rais wetu, umetuonyesha njia.
Kiimani, hakika huu ni ujasiri unaotakiwa na Mungu kuonekana juu ya watu wake aliowaumba kwa sura yake.
Hapa namsifu sana Mheshimiwa Rais wetu kwa kumpa Mungu nchi hii.
*Sisi tunakuelewa.*
Kwa hii corona, hata tukijibaraguza sana, Sisi hatuwezi neno lolote.
Lakini kwa kumwamini Mungu tu, kwake yote yanawezakana!
Mbele zake Mungu wetu Corona lazima inyamazishwe tu.
*Amenikumbusha pia juu ya vijana wa imani akina Shedrack, Meshack, na Abedinego,
Waliogoma kuiabudu sanamu ya mfalme wa Babeli hata wakawa tayari kufa!
*Walitupwa katika moto, lakini moto haukuwateketeza kabisa!*
Ndiyo maana Neno linasema,
Ujapopita katika moto.. hautakuteketeza!
Corona kuingia Tanzania yawezekana,
Lakini hautateketeza.
Umeingia kwa njia moja, lazima utatokomezwa kwa njia saba,
Kwa Jina la Yesu,
Amen.
Haijalishi,
Hata k**a wewe huamini haya,
Sisi tunaamini,
Na ndivyo itakavyotokea.
Pia Imenikumbusha juu ya yale maneno aliyosema Mungu hivi;
*Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake;*
*Bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema Bwana.*
Yeremia 9:23-24.
Waauh!?
Maneno haya yamenipa nguvu tele ya kusonga mbele na Bwana wangu!
Usijisifiwe uwezo ulionao, hauwezi kukuokoa..!
Hekima na ujuzi umeshindwa kuwasaidia wanadamu!
Fedha, na nguvu zao nazo zimeshindwa kulizuilia janga hili!
Lakini neno la ushindi ni hili,
*Mwenye kujisifu na ajisifu kwa sababu hii tu,*
*1. Ananifahamu mimi,*
*2. Na kunijua ya kuwa mimi ni Bwana..!*
*SALA, DUA NA MAOMBEZI YETU*
Ee Mungu Baba yetu,
Watanzania tumekufahamu kuwa wewe ndiye Mungu wa miungu, na kwamba zaidi yako hakuna Mungu k**a wewe.
Tena tunakujua kuwa wewe ndiye Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana..
Uwezo wako ni mkuu kuliko nguvu zozote..
Itoshe kwetu kukwambia kuwa,
Wewe Bwana watosha.
Kwasababu hii, tunakuomba utusamehe watanzania, kwa kuwa tumejaa maovu, dhihaka, na maneno maovu!
TUSAMEHE NA WATOTO WETU.
*Wewe si mwepesi wa hasira, wewe ni mwingi wa rehema,*
Katika ghadhabu yako twakusihi ukumbuke rehema,
Ukatuhurumie na kutuokoa,
Kupitia Damu ya mwanao mpendwa Yesu.
*Ee Mungu mwenye rehema, twakusihi sasa ukaitazame Tanzania ndani ya Damu ya Yesu,*
*Kwa kuwa hii ndiyo Sadaka pekee ya kuteketezwa uliyoitoa kwa ajili ya wokovu wa ulimwengu huu,*
Kwa damu hiyo Mungu wetu ukatusamehe maovu yetu na kuyafuta mbele za macho yako,
Kisha ukatuokoe sasa, na kutuvusha salama.
Na ijulikane upo, ee Mungu wa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo.
Sisi tumesema, wewe ndiye Mungu wetu,
Zuia mauti ya corona isiue mtanzania, hapa nchini, na popote aliko duniani.
Nasi tutayashuhudia haya matendo yako makuu popote,
Tumeamini haya, kuwa ni yetu sasa,
*Kwa Jina la Yesu,*
*Amen.*
_Watumie na wenzako ujumbe huu._
Waombaji msikae kimya,
*Enyi wenye kumkumbusha Bwana, msinyamaze kimya, mpaka hapo Mungu atakapoifanya Tanzania yetu imara.*
_Mtabarikiwa sana by Godii Urassa🤓._