Speakuplive

Speakuplive Karibu Kutangaza nasi kwa Bei Nafuu Sawa na Bure, Maana Tunajua Thamani Yako Kwetu. https://www.facebook.com/Talklivenow/

Karibuni - 2021.

Page Hii Inahusiana na Mambo Mbali Mbali ikiwemo HABARI | HADITHI | SIMULIZI | AFYA | SIASA | MICHEZO na BURUDANI.


- Tunapokea Matangazo ya Biashara | Ndogo + Kubwa Kwa Bei Nafuu Kabisa.

| Talklivenow.

03/04/2024

SABABU 5 ZENYE KUFANYA WANAUME WAPOLE SANA, WENYE KUJALI SANA,WENYE KUSAIDIA SANA HUISHIA KUPATA MWENZA DIKTETA, MGOMVI MGOMVI, MBABE
Huwa tunasikia hadithi za kila aina kwamba wanawake hawajui wanataka nini lakini uhalisia ni kwamba kumuelewa mwanamke ni rahisi sana.Ikiwa wewe ni mwanaume na umekuwa unateseka sana kwenye mahusiano yako na mwenza wako mwisho wa soma ujumbe huu mpaka mwisho nakupa guarantee kwamba hautakuja kupitia "Stress" za mapenzi katika maisha yako yote.

Kuna sifa k**a upole, huruma,kujali, kusamehe makosa, unyenyekevu, uvumilivu n.k hizi ni sifa nzuri sana kuzisikia tu lakini ukija kwenye ulimwengu halisi mwanaume mwenye sifa hizo huonekana DHAIFU SANA mbele ya jamii na hudharauliwa sana.

Unaweza kupatwa na mshangao lakini soma ujumbe mpaka mwisho.
Wanaume wenye sifa za kujali sana, kusamehe makosa haraka, uvumilivu kupita kiasi, unyenyekevu,kuogopa ugomvi na hasira ya mwanamke huitwa NICE GUYS kuna msemo unasema "Nice Guys finish last" kwa maana mwanaume mwenye kuonekana mstaarabu sana huishia kuwa wa mwisho katika kila sekta ya maisha yake.
Utajuaje k**a wewe ni "Nice Guys" jibu maswali yafuatayo kwa kuandika NDIYO au HAPANA kulingana na hali yako kisha utagundua kwanini "NICE GUYS finish last"
1.Umekuwa unalalamika kwamba hakuna mwanamke anavutiwa na wanaume wastaarabu?
2.Je huwa unaumia sana pale ambapo mwanamke amekukataa?
3. Je huwa unaishia kupata marafiki wengi wa k**e lakini haupati mwenza?
4. Umewahi kumsikiliza rafiki yako wa k**e akilalamika kuhusu mahusiano yake kisha ulijenga matarajio kwamba anakwenda kumuacha mwenza wake kwa ajili yako wewe ?

5.Umekuwa mara kwa mara unasema kwamba wewe ni mtu mstaarabu,mwenye kujali sana watu na kuheshimu sana wanawake?
6.Umewahi kumwambia mwanamke ambaye ameumizwa na mapenzi kwamba wewe ni wa tofauti na utamjali sana kuliko mwenza wake anavyofanya ?
7.Huwa unashangaa kwanini wanaume ambao hawana huruma,hawajali kabisa Mapenzi wanapata wanawake wastaarabu haraka lakini wewe haupati?
8. Je unaamini kwamba k**a ukimpenda mwanamke hautakiwi kukata tamaa hata k**a amekukataa mara nyingi?

9.unaamini wewe ni mtu mstaarabu, mwenye kujali sana,mwenye huruma,mwenye tabia njema sana katika jamii kuliko wanaume wengine?
10. Je unajiona mnyanyasaji au mkosaji k**a ukiona mwanamke yupo na huzuni,hasira,au anajisikia vibaya kisha unadhani ni wajibu wako kufanya chochote ili kumfurahisha?
11. Je huwa unaomba msamaha mara kwa mara k**a ukiona mwanamke yupo na hasira kupita kiasi mbele yako na unaongea kwa sauti ya upole kupita kiasi k**a mwanamke anaongea kwa sauti ya ukali kupita kiasi?
12. Je huwa unaanza kwa kujenga urafiki na mwanamke kwa kumsaidia sana kazi zake,kubeba mizigo yake,kumpa zawadi,kuongea vichekesho vichekesho bila kuzungumza moja kwa moja unataka nini kwake ?

K**a umejibu NDIYO nusu ya maswali hayo maana yake wewe ni NICE GUY kwa maana hiyo unaonekana mpole sana, mnyenyekevu, mwenye huruma kupita kiasi, uvumilivu,kusaidia sana,kuogopa ugomvi na migogoro ukiamini ndiyo tiketi ya kupendwa na wanawake lakini uhalisia ni tofauti kabisa.

Chanzo cha kujenga tabia hizo ni
I.KULELEWA BILA BABA AU KUPATA BABA DHAIFU SANA
vyanzo vya kumkosa baba utotoni au kupata baba dhaifu sana ni kifo cha baba, talaka, kutengana kwa wazazi, baba kufungwa gerezani, baba kuishi mbali sana na familia, baba kuitelekeza familia, baba kukataa ujauzito, baba kuhama makazi,baba kuathirika na dawa za kulevya, pombe kupindukia, kuvuta bangi,

kuwa mzee sana au mgonjwa sana au mlemavu ambaye alikuwa hana uwezo wa kukuwajibisha ukifanya makosa utotoni.

II.KUWEPO BABA AMBAYE HANA ATHARI ZOZOTE KWAKO.
Unaweza kuwa "Nice guy" kwa sababu katika familia yenu mwenye kauli ya mwisho ni mama huku baba yupo k**a bendera tu.
Hivyo unaishi kwa kugombezwa na mama huku baba anakuacha huru uishi vile ambavyo unataka bila kujali athari zake ukubwani.

III.KUMLEA MZAZI BADALA YA MZAZI KUKULEA WEWE
Unaweza kuwa "Nice guy" kwa sababu umeanza kulea familia yenu ukiwa mdogo sana labda kwa sababu ya umasikini kupita kiasi,ugomvi wa mara kwa mara wa wazazi,baba kufungwa gerezani, baba kuitelekeza familia, baba kuwa mzee sana au mgonjwa sana au mlemavu au mlevi kupindukia hivyo ulibeba majukumu makubwa kabla ya umri.

SABABU 5 ZENYE KUFANYA WANAUME WAPOLE SANA, WENYE KUJALI SANA, WENYE KUSAIDIA SANA HUISHIA KUPATA MWENZA DIKTETA, MGOMVI MGOMVI,NA MBABE
Zifuatazo ni sababu 5 zenye kufanya wanaume wenye tabia za upole kupita kiasi, uvumilivu kupita kiasi, unyenyekevu, huruma kupita kiasi,kujali sana, kusamehe makosa kupata mwenza dikteta, mgomvi mgomvi, mwenye lugha ya udhalilishaji.
1.KUSHINDWA KUSIMAMA K**A KIONGOZI NDANI YA FAMILIA
Mwanaume Rijali huwa kichwa cha familia kisha mwanamke anakuwa chini ya uangalizi.Lakini hawa Nice guy huwa kinyume chake anaweza kuwa "Mario" ambaye anaishi kwa kumtegemea mwanamke kwa kila kitu au anaishi huku anatoa huduma zote ndani ya familia lakini maamuzi yote hufanywa na mwanamke yeye anafuata maagizo ya mwanamke.

Kwa kawaida wanawake wenye upendo, huruma,kujali, kunyenyekea huvutiwa kimapenzi na mwanaume mwenye kujiamini,mwenye kusimama k**a kiongozi.

Hivyo wakiona mwanaume mpole sana wanamuona k**a mwanamke mwenzao hivyo wanajenga nae urafiki tu.

Ukiwa mwanaume mstaarabu sana kisha unaona upo "single" na umezungukwa na marafiki wengi sana wa k**e ni kwa sababu wanakuona k**a mwanamke mwenzao.

Wanawake wenye tabia za ubabe, ukali kupita kiasi,jeuri,dharau na majigambo na majivuno huwa wanasema kwa mwanaume "Chagua mimi au mama yako mzazi" kwa mwanaume Rijali akisikia kauli hiyo papohapo hapo anamfukuza mwanamke bila maelezo yoyote lakini kwa wanaume ambao ni nice Guys huanza kutafuta ushauri wa kubadilisha tabia ya MWANAMKE jambo ambalo sio sifa ya mwanaume.

2.KUOGOPA UGOMVI NA MIGOGORO
Sifa ya mwanaume Rijali huwa haogopi ugomvi wala migogoro na mtu yeyote lakini wanaume ambao ni nice Guys huwa wapo k**a "Wife material" kwa maana sifa ya upole, huruma,kujali, kusamehe makosa, unyenyekevu, uvumilivu huwa utambulisho wao uhalisia ni kwamba hizo ni sifa za mwanamke siyo mwanaume.

Sifa za mwanaume ni kuwa kiongozi,kuwa shujaa, mpambanaji, asieogopa kusemwa vibaya,hataki kupendwa na kila mtu,hataki kuungwa mkono na kila mtu.

K**a ni mwanaume unaogopa migogoro na ugomvi utafanya mwanamke aishi kwa dhiki,taabu, simanzi, huzuni na upweke kila siku kwa sababu dada zako na mama yako watakuona hauna sifa za mwanaume hivyo wataamua wao kuingilia maisha yako na mwenza wako wataanza kukupangia namna ya kuishi na mwenza wako,wakiamua kumfukuza mwenzao wako na kuleta mwanamke wanamtaka watafanya hivyo kwa sababu hawaoni k**a unaweza kujiongoza.

Mwanaume Rijali anamlinda , kumtetea mwenza wake,anamlindia heshima, anahudumia kulingana na uwezo wake,na vilevile haonekani kunyenyekea sana mapenzi kwa hofu ya kusalitiwa au kuachwa na vilevile endapo mwanamke atafanya utovu wa nidhamu anapewa onyo kali na akileta jeuri anarudishwa kwao bila maelezo yoyote.

3.HAWANA UWEZO WA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU
Nice Guys huwa wanaume wenye sifa za k**e japokuwa wao hujiona ni wastaarabu saba kwenye jamii lakini uhalisia ni tofauti.
Kwa mfano mwanamke akitaka kuachana na mwanaume huonyesha tabia zifuatazo kumfokea, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia, kutoroka kwenda kwao mara kwa mara,kuzusha uongo,kutishia muachane kila siku,kuomba fedha nyingi sana kuliko uwezo wa mwanaume ,kutafuta ugomvi mara kwa mara ili apate sababu ya kurudi nyumbani kwao.

Anaweza kuchati na wanaume wengine mpaka saa 8 usiku, anaweza kutongozwa mbele ya mwanaume wake na kusingizia hakuna kitu chochote kibaya kinaendelea baina yao.

Hapa anafanya makusudi ili mahusiano yavunjike,hataki risala, hataki vitisho,hataki ushauri,hataki kukumbushwa wema ambao mwanaume amefanya .Kitu pekee anataka ni mahusiano kuvunjika tu..

Hawa wanaume ambao ni nice Guys huanza kulia, kuomba msamaha, kupiga magoti,kupiga simu mfululizo kwa ndugu wa mwanamke ,kutishia kujiua hizo ni sifa za wanawake sio wanaume .

Kwa upande wa mwanaume Rijali akiona utovu wa nidhamu tu ampa onyo kali sana mwanamke na kusisitiza anataka heshima na ikiwa hakuna heshima basi wataachana papohapo.

Hawa wanaume ambao ni nice Guys wanaweza kukaa kimya, kuvumilia usaliti, kuvumilia matusi, vipigo, lawama,vitisho, tuhuma za uongo kwa miaka mingi sana kwa sababu ya kukosa sifa za uanaume ndani ya familia.

4.KUSHINDWA KUVUTIA WANAWAKE WENGINE
Kwa kawaida wanawake huvutiwa kimapenzi na mwanaume ambaye anapendwa na wanawake wengine , wanaamini huyu atakuwa na mbegu nzuri ya kuzaa watoto na kuwapa matunzo na ulinzi.

Nice Guys huwa kinyume chake.Anakuwa mwanaume anataka wanawake wakimuona tu wampende na kujenga nae familia bila yeye kufanya juhudi za kumfuata mwanamke..

Kwa asili wanawake hawana ujasiri wa kumwambia mwanaume k**a wanampenda bali hufanya mitego, kujipitisha pitisha,kumtega kwa uvaaji na sauti lakini sio kuongea moja kwa moja.

Hawa wanaume ambao ni nice Guys huonyesha tabia hizohizo za k**e k**a vile kujenga urafiki kwanza,kumsaidia sana mwanamke kisha baadaye wanataka mwanamke aone kwamba wanafaa kuwa "Husband material" kwa wema ambao wamefanya.

Wanawake hupenda kupitia wivu ,akiona wivu kwa mwanaume anaamini mwanaume huyo akimpata atakuwa na furaha sana.
Haiwezekani kwa mwanamke kuona wivu kwa nice Guys kwa sababu haonekani k**a mwanaume mwenye kuvutia katika jamii.

5.KUSHINDWA KUJIWEKEA MIPAKA
Nice Guys hawana mipaka baina yao na wanawake..
Kwa kawaida mwanaume huonekana mwenye kuvutia k**a hapatikani kwa urahisi, vilevile hatabiriki..
Anaweza kupokea simu na wakati mwingine hapokei kwa sababu anakuwa busy sana.

Nice Guys huwa anapatikana muda wote saa 24 anaamini akikaa kimya bila mawasiliano hata kwa dakika kadhaa ataziumiza hisia za mwanamke na kufanya mwanamke amchukie lakini uhalisia ni kwamba wanaume ambao hawapatikani kwa urahisi huwa ndiyo wenye kuvutia sana machoni kuliko hawa wanaopatikana muda wote.
Nice Guys akiombwa fedha nyingi sana yupo tayari kwenda kukopa ,jambo ambalo hufanya anapoteza mvuto moja kwa moja.

Mwanamke akiomba kitu chochote anapewa papohapo jambo ambalo husababisha mwanamke kumchoka mwanaume haraka kuna wakati mwanamke anaomba kitu chochote ili ukatae ajisikie furaha kuona unasema "HAPANA"

Uhalisia ni kwamba mwanamke anampenda sana mwanaume pale ambapo hana uhakika wa kupata mahitaji yake yote kwa sababu inakuwa k**a surprise na siku zote surprise huzidisha mapenzi kuliko kitu chenye kutabirika.



03/04/2024

JE HUWA UNAPANIKI HARAKA UKIPATA TAARIFA MBAYA AU KIKWAZO?
Fahamu tatizo la kupaniki, viashiria vyake,vyanzo vyake ,madhara yake na ufumbuzi wake

Tatizo la kupaniki (panic disorder) ni hali ya hofu kupita kiasi ambayo hutokea ghafla na kufanya mwili kupata mabadiliko k**a moyo kwenda mbio sana,kupumua haraka haraka sana, kutetemeka sana, miguu kuishiwa nguvu, kutokwa jasho bila joto, kubanwa kifua,kushindwa kuvuta pumzi,kuhisi kupaliwa kooni na kichefuchefu.

Hali hiyo inaweza kujitokeza muda wowote ukiwa mahali popote bila kutarajia.

Mtu mwenye kupatwa na tatizo la kupaniki ghafla ataona mabadiliko yafuatayo kwa ujumla mwilini

A.KICHWANI
Atajisikia kizunguzungu, kuchanganyikiwa,kuumwa kichwa,kuhisi unataka kufa ghafla, kuhisi unataka kurukwa akili, kuhisi unataka kudondoka ghafla,kushindwa kutuliza akili sehemu moja,macho kuona ukungu ,kujiona k**a upo ndotoni,kuwa na hasira kupita kiasi,macho kushindwa kuona vizuri k**a unasoma karatasi unaona maandishi yapo juu chini au kurasa huzioni kabisa unapekuwa na kurudia mara mbili mbili.

B.MWILI KWA UJUMLA
Mtu atajisikia uchovu, mwili kuishiwa nguvu,kutokwa jasho bila joto, kubanwa kifua, kupoteza hisia kwenye vidole,mwili kufa ganzi,

C.MIDOMO NA KOONI
Midomo inakauka mate,unashindwa kumeza mate, kuhisi kupaliwa kooni,kuhisi umekabwa koo,kushindwa kuongea ,sauti kukwaruza

D.KIFUANI
Moyo kwenda mbio sana, kifua kubana sana,kuumia kifuani, kushindwa kuvuta pumzi,kupumua haraka haraka sana, màumivu makali sana wakati wa kuvuta pumzi.

E.TUMBONI
Tumbo kuvurugika sana,kuhisi kichefuchefu,

F.MISULI
Misuli kukaza sana kwenye shingo na mabega,mikono kushika vitu kwa nguvu sana huku jasho linatoka.

K**a hali hiyo imetokea ukiwa unazungumza mbele ya watu utaanza kukwepa kusimama mbele za watu

K**a hali hiyo imetokea ukiwa safarini utaanza kuahirisha safari na matembezi

K**a imetokea ukiwa sokoni au kwenye mikusanyiko ya watu wengi utaacha kuhudhuria mikusanyiko ya watu

K**a hali hiyo imetokea ukiwa pekeako utaanza kuwa king'ang'anizi wa kukaa karibu na mwenza wako au mtoto,au rafiki muda wote utakuwa huwezi kulala au kula au kutembea ukiwa pekeako.

VYANZO VYA TATIZO LA KUPANIKI
Unaweza kupata tatizo la kupaniki kwa sababu zifuatazo
a.Magonjwa ya moyo,Stroke, asthma,

b.Mwanamke akiwa mjamzito au anakaribia hedhi anaweza kupata tatizo la kupaniki

c.Mwanamke baada ya kujifungua anaweza kupata tatizo la kupaniki

d.Matumizi ya vidonge au dawa mbalimbali husababisha hali ya kupaniki ghafla au kuacha matumizi ya dawa au vidonge husababisha hali ya kupaniki

e.Unywaji wa pombe au kuacha kunywa pombe husababisha hali ya kupaniki

f.Unywaji kupita kiasi wa kahawa ,chai ya rangi au dawa za kulevya

g.Kupata jeraha kichwani.

SABABU ZA KIHISTORIA
Angalia maswali yafuatayo kujua chanzo cha tatizo la kupaniki
1. Je mama yako mzazi alikuwa na huzuni kupita kiasi au hofu kupita kiasi ukiwa tumboni mwake?
2. Je wazazi wako walikuwa na ugomvi wakati ukiwa tumboni mwa mama yako?

3. Je umezaliwa kwa njia ya oparesheni?
4. je mama yako alikuwa mgonjwa sana au mwenye huzuni sana baada ya wewe kuzaliwa (ulipozaliwa)

5. Je ulitenganishwa na mama yako mzazi mapema baada ya kuzaliwa ? Je umepata malezi ya mama tofauti baada ya kuzaliwa ?

6. Je umeishi mbali na mama yako mzazi miaka 3 baada ya kuzaliwa kwako?

7. Je kuna mtoto yoyote wa mama yako mzazi alifariki kabla ya kuzaliwa kwako au kuna ujauzito wowote wa mama yako mzazi uliharibika kabla hujazaliwa ?

8. Je mama yako mzazi alishindwa kuonyesha upendo kwako na kukujali ghafla kwa sababu ya ujauzito,ndugu yako kuugua au kifo cha mdogo au mkubwa wako au yeye mwenyewe kuugua

Kupitia maswali hayo unaweza kupata mwanga kuhusu chanzo cha tatizo la kupaniki

TATIZO LA KUPANIKI NA HOFU YA KUJUMUIKA NA WATU
Watu wenye tatizo la kupaniki wakiwa na hofu ya kujumuika na watu (Agoraphobia) hupata wakati mgumu sana kukabiliana na tatizo hilo.

Watu wenye hofu ya kujumuika na watu wengine huogopa mazingira yafuatayo kwenda sehemu zenye mikusanyiko k**a vile mikutano,stoo,migawaha/ restaurant,huogopa usafiri wa umma,huogopa kuwepo mbali na mazingira ya nyumbani kwao,huogopa madaraja marefu

Pia watu wenye hofu ya kujumuika na watu wengine (Agoraphobia) huogopa sana watu wenye hasira,huogopa ugomvi au majibizano,huogopa mijadala .

WATU WENYE HOFU YA KUJUMUIKA HUOGOPA KUPANIKI KWA SABABU
Wanajenga hofu kubwa sana kuwa wanaweza kupoteza fahamu mbele ya watu,huogopa kufa akiwa mbali na nyumbani,huogopa kupata tatizo akiwa mbali na nyumbani,

Hofu ya kupaniki ghafla huzidi kuongezeka kwa mtu ambaye anaamini hana thamani mbele ya wengine, anaamini kwamba k**a mahusiano yake yamevunjika basi anahisi chanzo ni yeye mwenyewe kwa kushindwa kumridhisha mwenzake kisha wanaamini watabaki katika upweke milele

Wanaamini kwamba ili kupendwa wanatakiwa kuacha kujali mahitaji yao na kujali mahitaji ya wengine muda wote

Wanaamini bila kupendwa sana wao hawataweza kukabiliana na matatizo yao ya kila siku

Wanaamini hawana uwezo wa kustahimili kukosolewa baada ya kufanya makosa

MADHARA YA TATIZO LA KUPANIKI
Husababisha mtu kuwa hatarini kupata magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, kupooza, kuugua mara kwa mara,kuumwa kichwa na mgongo,tatizo la kupaniki linaweza kufanya mtu kuishi maisha ya upweke kupita kiasi kwa kuogopa kupata matatizo akiwa mbele ya wengine.

UFUMBUZI WAKE
K**a umekuwa na tatizo la kupaniki mara kwa mara ni vizuri kwenda kwa daktari kujua afya yako kabla ya kufuata ushauri huu

Zifuatazo ni njia za kukabiliana na tatizo la kupaniki
A.KUHUSU KUKOSOLEWA
Unaweza kupaniki ghafla watu wakikusema vibaya au kukukosoa kupita kiasi fanya yafuatayo
Angalia wapi unaweza kujirekebisha tabia zako tu kisha jifunze kwa nyakati za baadaye ila sio kujuta kwa kile ambacho umefanya.

Acha kujipa majina mabaya baaada ya kusemwa vibaya jiulize k**a ni rafiki yako amefanya makosa utakuwa na kauli nzuri au mbaya kwake .

B.NJIA ZA KUPATA UTULIVU
Vuta pumzi ndefu kisha hesabu 1 mpaka 5 kisha iache pumzi polepole itoke huku unahesabu 1 mpaka 5 kwa muda wa dakika 5 utaona mabadiliko mwilini ikiwemo mapigo ya moyo kushuka

Zoezi la kupiga miayo (YAWNING) piga miayo mfululizo kwa muda wa dakika 2

Zoezi la kuvuta pumzi polepole kaa kwa utulivu vuta pumzi polepole sana kisha unaiachia pumzi itoke polepole sana

Fanya mazoezi ya viungo,tembea mara kwa mara,kunywa maji mengi,epuka pombe, punguza matumizi ya chai ya rangi au kahawa,pata usingizi wa kutosha,fanya kazi kisha pumzika.

Ukihisi upo hatarini jiulize k**a ni kweli upo hatarini au unaamini upo hatarini kisha ukiwa na hofu sema upo sehemu salama na hata k**a kuna hatari inaweza kutokea haiwezi kuwa mwisho wa ulimwengu.

Rudia kauli hiyo mara kwa mara ukiwa na hofu utaona mabadiliko mwilini ikiwemo mapigo ya moyo kushuka na pumzi kuipata kwa urahisi.



03/04/2024

NJIA 4 ZA KUISHINDA HOFU, WASIWASI, NA WOGA WA NINI KINAWEZA KUTOKEA LEO AU SIKU ZA BAADAYE
Kila mtu huwa mwenye kuishi kwa hofu, wasiwasi, woga na kushindwa kujiamini kwa kuhisi kitu kibaya kinaweza kutokea ghafla, lakini wapo watu hofu ya kitu kibaya kutokea ghafla ipo muda wote kwa maana hawawezi kupata utulivu hata k**a wakiambiwa wapo sehemu salama.

Kwa sababu ya uwepo wa watu wengi wenye kuishi huku wanasumbuliwa na hofu, wasiwasi, woga juu ya maisha au kitu kibaya kutokea ghafla bila maandalizi basi suluhisho limepatikana ndani ya kitabu cha JINSI YA KUPONA MAUMIVU MAKALI SANA MOYONI Utakutana na majibu ya maswali yote kuhusu hofu,woga,na wasiwasi.Hii si ya kukosa
👇🏿
Hofu ya kitu kibaya kutokea inaweza kujitokeza kwa vyanzo 4 na dalili za hofu ya kitu kibaya kutokea ghafla ni k**a ifuatavyo

VIASHIRIA VYA HOFU , WASIWASI WA KITU KIBAYA KUTOKEA NI
a.Hisia za kuona vitu ambavyo siyo halisi, kupoteza mawasiliano ya mwili mzima au baadhi ya viungo mwilini,kupata hisia za kupaniki ghafla

b.Kuchanganyikiwa,kushindwa kutuliza akili sehemu moja,fikra kuvurugika,kuhisi unataka kudondoka ghafla,kuhisi unataka kurukwa akili,kuhisi unataka kujirusha sehemu

C.Hofu ya kuonekana kituko,hofu ya kufa ghafla,hofu ya kuugua ghafla,hofu ya kupata mshtuko wa moyo,hofu ya kuachwa mpweke,hofu ya kusemwa vibaya,hofu ya kukosolewa

d.Moyo kwenda mbio, miguu kuishiwa nguvu, kizunguzungu, kichefuchefu, hasira, tumbo kuvurugika, kujichukia, kujikosoa, kujilaumu,kutamani kulia, kutokwa machozi

e.Kuumia mabegani na shingoni, kutetemeka sana, kujiona upo hatarini muda wote,kuumia kooni,kuona ukungu, kupumua haraka haraka sana,kuumwa kichwa na mgongo,misuli kukaza.

Baada ya kuona viashiria hivyo vifuatavyo ni vyanzo vya tatizo la hofu, wasiwasi, woga wa kitu kibaya kutokea ghafla.

1.MAHUSIANO/FAMILIA
Unaweza kupata hofu, wasiwasi, woga, kutetemeka sana pale ambapo unaona mahusiano yako na mwenza wako hawaeleweki vizuri kwa vyanzo vifuatavyo

-Kukata mawasiliano ghafla, kumfumania mwenza wako,mwenza wako kukuomba fedha nyingi sana kuliko uwezo wako

-Mwenza wako kutishia muachane ghafla,mwenza wako kukataa msikutane kimwili, mwenza wako kukataa ujauzito,mwenza wako kuhama makazi na kuanza kuishi na mwanaume au mwanamke mwingine bila sababu zozote za msingi

-Mwenza kuonekana ameathirika na ugonjwa usiokuwa na tiba k**a ukimwi,mwenza wako kuanza tabia za ajabu ajabu ghafla

-mwenza wako kuibua ugomvi kila wakati bila sababu zozote za msingi,mwenza wako kukumbusha makosa ya zamani kila siku, Mwenza wako kusikiliza sana maneno ya watu wengine bila kuhoji chochote

-Malengo ya mwenza wako kubadilika ghafla, mwanamke au mwanaume unaempenda sana kukataa kukuoa au kuolewa na wewe bila sababu zozote za msingi.

2.FEDHA/BIASHARA
Unaweza kupatwa na hofu, wasiwasi, woga, kutetemeka sana, kuchanganyikiwa kwa kuona majukumu ya kuhudumia familia yanazidi kuongezeka bila kipato kuongezeka.

Wasiwasi kuhusu fedha unaweza kujitokeza kwa vyanzo vifuatavyo
-Kudaiwa fedha nyingi sana,mauzo ya bidhaa kupungua ghafla,malipo ya mshahara kupunguzwa ghafla

-Kufilisika,kufilisiwa,watu kukopa fedha zako nyingi lakini hawarudishi,

-Kuibiwa fedha, kuvamiwa na majambazi,majanga ya asili k**a ukame, mafuriko, tetemeko, kimbunga n.k

-migomo ya wafanyakazi, migogoro ya wakulima na wafugaji,kuuguza ugonjwa sugu wenye kuhitaji fedha nyingi sana za matibabu.

3.MASUALA BINAFSI
Unaweza kupatwa na wasiwasi, woga, kutetemeka sana, kujiona upo hatarini muda wote kwa sababu binafsi k**a ifuatavyo
-Tishio la kufungwa gerezani,tishio la usalama wako, mabadiliko ya teknolojia,kifo cha ghafla cha Mwenza/mzazi/rafiki yako wa karibu

-kufanya kazi ambayo hauna uzoefu nayo , kupelekeshwa sana kazini, kukosolewa sana na msimamizi wako

-kusalitiwa na wafanyakazi wenzako,kupewa ahadi hewa, majukumu ya kazini kuingilia maisha ya kifamilia,unaogopa kuzungumza mbele za watu

4.AFYA
Unaweza kupatwa na wasiwasi, woga, mshtuko kwa sababu za kiafya kwa vyanzo vifuatavyo
-kugundulika umeathirika na ugonjwa usiokuwa na tiba k**a ukimwi, kusumbuliwa na ugonjwa sugu k**a kisukari, uvimbe, saratani, shinikizo la damu, ugonjwa wa moyo,kuumwa kichwa na mgongo,ugonjwa wa ngozi

-Upungufu wa nguvu za kiume, ujauzito kuharibika mara kwa mara,kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya sehemu za siri n.k

NJIA ZA KUISHINDA HOFU, WASIWASI NA WOGA WA NINI KINAWEZA KUTOKEA LEO AU SIKU ZA BAADAYE NI
Njia hizo za kukabiliana na tatizo hilo ni k**a ifuatavyo
1.MAISHA NI HISTORIA YENYE KUJIRUDIA
Maisha ni historia yenye kujirudia.
Tangu utotoni mwako mpaka uzeeni mwako utakuwa unapokea taarifa zenye kujirudia rudia
Taarifa zenye kujirudia rudia ni k**a vile mtu kuua au kujiua,vita ya nchi na nchi,njaa na ukame,talaka, kutengana kwa wazazi,watu kufukuzwa kazi,uhaba wa ajira,magonjwa , kashfa kwa wanasiasa,majanga ya asili,watu kutoa ujauzito,wanafunzi kuacha shule, usaliti kwa wenza ,watu kuiba na kuibiwa,

-watu kufilisika, wafanyakazi kufanya migomo kazini, mabadiliko ya hali ya hewa,magonjwa kuibuka na kutoweka,ajali zenye kusababisha vifo na ulemavu wa kudumu

-yatima kudhulumiwa mali za urithi , mfumuko wa bei,baadhi ya bidhaa kuadimika sokoni, malalamiko ya watu kuhusu utoaji wa huduma mbovu,

-huku msiba kule sherehe,huyu amehukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela,yule amepata msamaha,

Kwa kuzingatia kwamba hakuna jipya katika matukio ya kijamii isipokuwa majina ya wahusika ndiyo yatakuwa tofauti utaishi kwa kuondoa hofu na wasiwasi.

2.HATUWEZI KUMALIZA MAUMIVU NA MATESO KATIKA HUU ULIMWENGU
Haijalishi utaweka malengo gani, haijalishi utakuja na kampeni gani, haijalishi utaanzisha taasisi au kampini gani,haijalishi utakuwa bilionea leo au baadaye, haijalishi utakuwa profesa leo au siku za baadaye, haijalishi utakuwa mshindi wa tuzo ya Nobel leo au miaka ya baadaye bado haiwezi kumaliza maumivu na mateso kwa watu wote ulimwenguni.

Chochote ambacho utafanikiwa kukipata au utakipoteza hakiwezi kumaliza maumivu na mateso hapa ulimwenguni.

Haijalishi watu watafanya kazi kwa bidii kiasi gani,wafanye ibada kwa kiwango gani,wajiwekee malengo makubwa kiasi gani,wasome vitabu gani,bado haiwezi kuwa guarantee ya kumaliza maumivu na mateso hapa ulimwenguni.

Zingatia yafuatayo
Baadhi ya watu watapata ajali yenye kusababisha ulemavu wa kudumu na wengine kupoteza maisha,baadhi ya watu watafukuzwa kazi,baadhi ya watu watakuwa masikini lofa wakutupwa,baadhi ya watu watasaliti wenza wao,baadhi ya watu wataugua ugonjwa sugu

-Baadhi ya watu watahukumiwa kifungo cha maisha gerezani,baadhi ya watu watazusha uongo,baadhi ya watu watafilisika,baadhi ya watu watapata maambukizo ya ugonjwa wa virusi vya ukimwi,

-baadhi ya watu watajiua,baadhi ya watu watakuwa na ugumba,baadhi ya watu watakufa katika umri mdogo,baadhi ya watu watapata ujauzito masomoni,baadhi ya watu watabakwa,baadhi ya watu watafanyiwa ulawiti,baadhi ya watu wataacha shule.

Kwa sababu haya ni matukio ya miaka yote tangu utotoni mwako mpaka unaingia kaburini na hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kuyaondoa hapa ulimwenguni.

Uwepo wa matukio hayo ndiyo yanafanya huu uitwe ulimwengu na yataendelea kuwepo matukio hayo ilimradi binadamu wataendelea kuishi hapa ulimwenguni.

3.K**A KUNA KITU KIBAYA KINAWEZA KUTOKEA KITATOKEA TU NA HAIWEZI KUWA MWISHO WA ULIMWENGU
K**a kuna tatizo lolote linaweza kutokea litatokea tu,hofu haiwezi kuzuia mabadiliko ya huu ulimwengu.
Machozi yako hayawezi kuzuia mvua kunyesha au kujua kuwaka,

Upweke wako hauwezi kuzuia watu wengine kuoa au kuolewa,kufeli masomo kwa mtu yeyote haiwezi kuzuia watu wengine kuendelea na masomo,mtu mmoja kusalitiwa na Mwenza wake haiwezi kuzuia watu wengine kupenda ,mtu mmoja kuacha kazi haiwezi kuzuia watu wengine kuomba kazi ,

Mtu mmoja kuamua kuacha kuzaa haiwezi kuzuia watu wengine kuzaa,mtu mmoja kufunga biashara haiwezi kuzuia watu wengine kufungua biashara

Mtu mmoja kukata tamaa ya maisha haiwezi kuzuia watu wengine kupata hamasa ya kupambana maishani mwao.

Dunia haiwezi kufika mwisho kwa sababu kuna mtu amefilisika au kutajirika,dunia haiwezi kufika mwisho kwa sababu mtu mmoja ameacha kazi au kupanda cheo

Dunia haiwezi kufika mwisho kwa sababu mtu mmoja kusalitiwa na Mwenza wake

Dunia haiwezi kufika mwisho kwa sababu kuna mtu yupo na hasira kupita kiasi juu ya ugumu wa maisha

Mtu mmoja kujuta kwa sababu amesoma lakini haoni manufaa ya kusoma bado haiwezi kuzuia watu wengine kusoma kwa bidii

Mtu mmoja kuacha kilimo kwa sababu amepata hasara haiwezi kuzuia watu wengine kuingia kwenye kilimo

Mtu mmoja kupata faida kubwa sana kwenye kilimo haiwezi kumhamasisha kila mtu kuingia kwenye kilimo.

Chochote ambacho kinaweza kutokea leo kiwe kizuri au kibaya haiwezi kuwa mwisho wa ulimwengu.

Ukiwa na furaha au huzuni haiwezi kuwa mwisho wa ulimwengu

Uwe na njaa au umeshiba haiwezi kuwa mwisho wa ulimwengu
Uwe mgonjwa au mzima wa afya bado haiwezi kuwa mwisho wa ulimwengu.

Upate ushindi au upoteze ushindi bado haiwezi kuwa mwisho wa ulimwengu.

4.MAISHA HAYATABIRIKI
Huenda mabadiliko ambayo unajenga hofu kubwa kwamba maisha yako yatakuwa HATARINI sana kumbe maisha yako ndiyo yatakuwa bora kuliko hivi sasa

Kile ambacho leo unajenga hofu kubwa kwamba endapo kikitokea maisha yako yatakuwa HATARINI sana kesho kinaweza kugeuka fursa ya kuandika historia mpya katika jamii.

Huenda kile ambacho unaona kitakuwa BARAKA kwako kesho kinaweza kugeuka BALAA
Tukio ambalo unaamini endapo likitokea itakuwa FURSA ya kuboresha maisha yako linaweza kutokea k**a ambavyo unavyofikiria kisha linageuka kuwa BALAA yenye kukutoa machozi na kile ambacho unaona kitakuwa HATARI kwako kesho kinaweza kugeuka BARAKA kwako na kukuacha mdomo wazi.

kazi ambayo leo unaona aibu kuifanya kesho inaweza kukupa heshima katika jamii na kazi ambayo leo unaona fahari kuifanya kesho inaweza kukufanya ufungwe gerezani maisha
Mtu ambaye leo ni muaminifu sana kesho anaweza kugeuka msaliti,na yule ambaye leo unamuona msaliti kesho anaweza kugeuka muaminifu

Mtu ambaye leo unamuona faraja yako ,kesho anaweza kugeuka mzigo kwako na yule ambaye leo unamuona mzigo kesho anaweza kugeuka kimbilio lako.

Kila siku inakuja na riziki yake na balaa zake .Kwenye uzuri wa kitu kuna ubaya ndani yake na kwenye ubaya wa kitu chochote kuna uzuri ndani yake.
Hakuna kitu kibaya kwa 100% au kizuri kwa 100%.



03/04/2024

ATHARI ZA KUKOSA BABA ANAEJITAMBUA /KUISHI BILA BABA KATIKA UMRI WA UTOTO NA MAJANGA YA UKUBWANI:
Fahamu majanga ya kumpenda mwanaume au mwanamke ambaye amezaliwa na kulelewa bila baba au ameishi na baba ambaye hajitambui

Umewahi kuona familia ambayo mwanamke anataka kuwa kichwa cha familia na mwanaume kuwa bendera?
Umewahi kuona familia ambayo mwanaume ni Mario/ambaye anategemea maamuzi ya mama au dada zake kuongoza familia?

Umewahi kuona familia ambayo mama mkwe ndiyo anai-control vile atakavyo na majanga ya familia hizo ?

Katika kitabu cha JINSI YA KUPONA MAUMIVU MAKALI SANA MOYONI utakutana na habari kamili leo natoa OFA kwa Tsh 7,000 unapata Softcopy yake .Ofa inaisha baada ya saa 24

Soma ujumbe mpaka mwisho 👇🏿
Namna maisha huwa magumu sana ukubwani kwa kumkosa baba utotoni:
Kuna nyimbo, misemo mingi sana yenye kumsifia sana mama k**a vile "Nani k**a mama" n.k lakini tafiti zinaonyesha kwamba kukosa upendo wa baba katika umri wa utotoni husababisha maisha kuwa magumu sana ukubwani kwa jinsia zote mbili za k**e na kiume.

K**a hauna furaha kabisa katika maisha yako,k**a hauna maelewano mazuri na mwenza wako au kazini kwako jaribu kuangalia uhusiano uliopo kati yako na baba yako mzazi k**a kuna dosari lazima kila kitu utaona kinayumba.

Utajuaje k**a umeathirika kwa kukosa upendo wa baba nyakati za utotoni?
Utaangalia yafuatayo
I.Kupuuzwa
II.Adhabu kupita kiasi

Kisha utaangalia sababu za kukosa upendo wa baba mzazi nyakati za utotoni kisha utaangalia madhara ya kukosa upendo wa baba mzazi kwa matatizo ambayo unapitia kwa sasa

I.KUPUUZWA UTOTONI
Kupuuzwa utotoni kunatokea kwa njia zifuatazo
wewe na mahitaji yako,kulishwa chakula kisichofaa kuliwa, kulazimishwa kujilisha ukiwa na umri mdogo sana,kuachwa mpweke katika baridi kali sana bila sweta

uvae nguo chafu sana kwa muda mrefu sana, kutembelea bila viatu,kuishi bila kuoga siku kadhaa,kuachwa mpweke siku,wiki,miezi kadhaa chini ya uangalizi wa mtu ambaye hana upendo wowote kwako.

ukae sehemu hatari sana kwa usalama wako,kukuzuia kujenga urafiki na watoto wengine ,kufungiwa ndani muda mrefu sana k**a wiki,, miezi kadhaa bila kujenga ukaribu na watoto wengine.

II.ADHABU KUPITA KIASI
Adhabu kupita kiasi utotoni zinaweza kujitokeza kwa njia zifuatazo
A.MANYANYASO YA KIHISIA
Manyanyaso ya kihisia ni mfululizo wa kauli na vitendo vyenye lengo la kukuumiza kihisia badala ya kukujenga k**a ifuatavyo
, kukutukana, kukudhalilisha hadharani, kukuita majina ya udhalilishaji, kuzomewa,kufanywa kichekesho, kubaguliwa, kutengwa,

mara kwa mara,kuzuiwa kujitetea,kupewa kesi za uongo,kulishwa chakula cha mifugo,kukulea k**a mtoto wa jinsia tofauti na maumbile yako,

upendeleo kwa ndugu zako kwa makusudi kwa kuzingatia jinsia, ufaulu,rangi, muonekano,jina la ukoo n.k

kwenda shule, kukulazimisha ufanye uhalifu,

B.MANYANYASO YA KIMWILI
Manyanyaso ya kimwili hapa yanahusisha matukio ya kupigwa mara kwa mara.
Adhabu kupita kiasi hujumuisha yafuatayo
kitu kizito mwilini, kubamizwa ukutani, kurushiwa mawe, kupigwa ngumi, kupigwa shoti ya umeme, kukabwa shingoni, kuzibwa midomo na mito usivute pumzi.

ngozi,kupigwa mikanda, kuvunjwa mifupa,kuchomwa moto,kuchomwa na pasi,kuchomwa na kitu chenye ncha kali.

ndani ,kuzuiwa kwenda chooni,kugeuzwa kichwa chini miguu juu,kuvutwa nywele kwa nguvu,kumwagiwa maji ya baridi kali sana asubuhi,

unywe dawa kwa nguvu wakati afya yako ni nzuri,kukupa kazi ngumu sana kuliko umri.

SABABU ZA KUKOSA UPENDO WA BABA KATIKA UMRI WA UTOTO
K**a utakuwa haujapata upendo wa baba mzazi utotoni vyanzo huwa k**a ifuatavyo
1.Kukosekana baba imara ndani ya familia (Absent of strong male role model) chanzo chake ni kifo, talaka, wazazi kutengana, kufungwa gerezani, baba kuishi mbali sana na familia,baba kuhudumia familia nyingi sana, kuitelekeza familia,kukataa ujauzito,kuhama makazi , kuathirika na dawa za kulevya pamoja na bangi,kuwa busy sana na kazi muda wote hana muda wa kuzungumza na wewe lakini anatoa huduma zote.

na kucheza k**ari, uhalifu wa silaha,wizi, ujambazi,kuugua muda mrefu sana,kuugua mara kwa mara,kuwa mzee sana,kuwa mlemavu,kurukwa akili mpaka anafungwa kamba,kuzongwa na msongo wa mawazo,mlevi kupindukia ambaye hahudumii chochote ndani ya familia.

2.Kuwepo baba ambaye hana athari zozote kwa mtoto (PASSIVE FATHER)
Hapa baba anakuwepo lakini malezi yote yanakuwa chini ya mama kwa maana baba hana kauli yoyote wala hatoi huduma zozote,au anaweza kuhudumia familia lakini hana ukaribu wowote na wewe kwa kifupi anakuwa k**a hakujui japokuwa mnaishi nyumba moja.

Hapa unakuwa hauna ukaribu na baba wala mama,kwa kifupi mama hapa anakuwa mkali kupita kiasi na vilevile baba anakuwa hana huruma wala ushirikiano wowote kwako,ukiwa hai au umekufa kwake sawa tu.

Hapa ukiamua kusoma sawa na ukiamua kuacha shule hakuna kuhojiwa chochote.

Hapa unakuwa huru kula chochote, kuvaa nguo yoyote, kwenda popote muda wowote,unakuwa na rafiki yoyote.

Huyu anakuwa baba ambaye hata ufanye vizuri kiasi gani hatoi pongezi wala zawadi,hata ufanye vibaya kiasi gani haongei chochote

3.KUMLEA MZAZI BADALA YA MZAZI KUKULEA WEWE
Hapa unakuwa mzazi kabla ya umri wako.
Kwa maana mzazi ataonyesha tabia zifuatazo kisha wewe unageuka mzazi wake kwa kumlea
muathirika wa dawa za kulevya,kufanya uhalifu, kucheza k**ari,kuwa mwizi sugu,kuwa mzee sana,kuwa mgonjwa sana,kuwa mlemavu, kurukwa akili mpaka anafungwa kamba, kuzongwa na msongo wa mawazo,kukosa kazi,

wa wazazi wenye kujirudia rudia kisha wewe unaingilia kati kuamua ugomvi.
Hii inaweza kusababishwa na kushuhudia mzazi mmoja (baba /mama) anapigwa, kufokewa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kudhalilishwa hadharani, kuburuzwa chini,kunyimwa chakula, kufukuzwa nyumbani, kunyang'anywa mali zake,kukabwa shingoni,kutishiwa kuuawa kisha ufanye kazi ya kumfariji yule ambaye anapitia maumivu makali sana ikiwemo huzuni,msongo wa mawazo,kulia,kutokwa machozi n.k hali hiyo kujitokeza katika umri mdogo sana.

ATHARI ZA KUKOSA UPENDO WA BABA UTOTONI NA MAJANGA YA UKUBWANI
athari za kukosa upendo wa baba mzazi utotoni kwa watoto wa kiume huathiriwa sana kwa kuonyesha matokeo yafuatayo

1.UMASIKINI KUPITA KIASI
Umasikini kupita kiasi - chanzo huwa kushindwa kujenga nidhamu ya fedha,kucheza k**ari,kufanya starehe sana,kukosa dira ya maisha,kuishi bila malengo,kuishi kwa kutegemea fedha za watu wengine,kukimbia majukumu,kuacha kazi bila sababu za msingi, utoro kazini,uvivu na uzembe kazini yote kwa sababu ya kukosa "Mentor" ambaye angeweza kumjenga mtoto tangu akiwa mdogo .

2.URAIBU
Kukosa baba imara utotoni husababisha athari za uraibu kwa watoto wa kiume ukubwani - uraibu wa kunywa pombe kupindukia, kuvuta bangi na dawa za kulevya, kufanya starehe sana, kubadilisha wanawake mara kwa mara, kuangalia video za ngono (pornography),kujichua (masterbation),kutazama Tv muda wote,kucheza video games muda wote,kula sana vyakula vyenye mafuta na sukari

3.UHALIFU
Kukosa baba imara utotoni husababisha watoto wa kiume kuingia kwenye matukio ya uhalifu ukubwani k**a wizi, ujambazi, biashara haramu, uhalifu wa silaha, ubakaji na ulawiti,kuacha shule mapema, kufungwa gerezani kwa uhalifu,

4.Kuzaa kila mtoto na mama yake bila kuhudumia chochote,kushindwa kudumu katika mahusiano yoyote iwe urafiki au mwenza,

5.Kuwa chokoraa, watoto wa mtaani,kupiga roba vichochoroni,kugombana na uongozi kila siku,kuanzisha migomo kazini mara kwa mara,

6.Kufanya vurugu,kupigana kwa silaha mara kwa mara,wengine kuingia kwenye ushoga (LGBTQ),kuwa na wivu wa mapenzi kupita kiasi,ukatili kwa wanawake,

7.Kuishi kwa kutegemea wanawake/Mishangazi na sugar mommy,kuishi kwa kunyenyekea sana wanawake wenye tabia za ubabe na udikteta

8.Kung'ang'ania mahusiano yenye ugomvi na migogoro na kuyakataa mahusiano yenye upendo, amani, huruma na utulivu kwa kushindwa kujiamini

ATHARI ZA KUKOSA UPENDO WA BABA UTOTONI KWA WATOTO WA K**E NA MAJANGA YA UKUBWANI
Mwanamke ambaye tangu utotoni ameishi bila kumuona baba mzazi au hana maelewano mazuri na baba yake mzazi huonyesha tabia zifuatazo ukubwani
1.Kung'ang'ania mahusiano yenye manyanyaso, vipigo, kufokewa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kudhalilishwa hadharani, kuingiliwa kinguvu, kuingiliwa kinyume na maumbile, kunyang'anywa mali lakini hawezi kuondoka katika mahusiano hayo kwa kuhofia upweke ,anafanya hivyo kwa sababu baba yake mzazi alikuwa na tabia hizohizo k**a huyo mwenza wake.Anaamini akiwa mvumilivu ataweza kumbadilisha tabia mwanaume bila mafanikio yoyote.

2.Anaweza kujitoa mhanga kwa mwanaume kwa kumhonga fedha nyingi sana,kujitolea mahari yeye mwenyewe,kujiweka karibu na ndugu wa mwanaume, kumlea na kumhudumia mwanaume ,kuogopa kupishana kauli na mwanaume miaka yote lakini bado anashindwa kujiamini - anatumia nguvu nyingi sana na fedha nyingi sana kuepuka mahusiano kuvunjika kwa sababu hakuwa na ukaribu wowote na baba yake mzazi.
Akipata mwanaume mpole, mwenye huruma, upendo na uvumilivu atafanya vituko mpaka utokee ugomvi waachane.

3.Anaweza kujenga mahusiano ya juu juu na wanaume wengi sana lakini hana hisia kwa mwanaume yoyote (kundi hili huwa wenye kujiuza /Pr******te)

4.Anajichukia sana,hajui sifa za mwanaume bora yupoje hivyo akipata mwanaume mwenye sifa nzuri katika jamii anakimbia kisha anakwenda kung'ang'ania sehemu anapigwa, kufokewa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kudhalilishwa hadharani kwa sababu baba yake mzazi alikuwa na tabia hizo nyakati za utotoni mwake.

5.Hujikuta wanapata msongo wa mawazo,hofu, wasiwasi,woga, kutetemeka sana mbele ya wanaume, kujichukia kwa muonekano,

6.Huwa wapo hatarini kuzaa kila mtoto na baba yake kwa sababu hawajui sifa za mwanaume bora zipoje kwa sababu wamepata malezi ya single mothers au kukosa maelewano na baba yake mzazi.Single mother huwa hawana uwezo wa kumjenga kiakili mtoto wa k**e kujua sifa za mwanaume bora zipoje hivyo huwaandaa kuwachukia wanaume na wengine huingia kwenye Feminist movement k**a njia ya kulipa kisasi kwa wanaume

7.Huwa wanavutiwa kimapenzi na wanaume ambao hawana uwezo wala mpango wa kujenga familia kisha wao huwa wanataka kumbadilisha tabia mwanaume bila mafanikio yoyote - hufanya hivyo bila kujijua kwa sababu utotoni walifanya kazi ya kutafuta upendo wa baba mzazi bila mafanikio yoyote hivyo wamezoea kutafuta upendo sio kupokea upendo.

Kwa sababu hawajui sifa za mwanaume bora zipoje mara kwa mara hupigwa matukio ya fumanizi,kuachwa ghafla baada ya kujitoa mhanga kwa mwanaume.



Address

Kilimanjaro
Kigoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Speakuplive posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Speakuplive:

Share


Other Media/News Companies in Kigoma

Show All