13/11/2022
Ndege mbili za kijeshi zimegongana angani (mid-air collision) na kulipuka huko Dallas, Texas Marekani zikishiriki kwenye maonesho ya kumbukumbu ya vita vya pili vya dunia. Ndege aina ya Bell P-63 Kingcobra iliyokua na rubani peke yake, imeigonga Boeing B-17 Flying Fortress iliyokua na rubani na maafisa wanne wa jeshi la Marekani. Inasadikika watu wote wamefariki katika ajali hiyo.
Ajali hiyo imetokea karibu na uwanja wa ndege wa Dallas Executive Airport (RBD) ambapo ndege hizo mbili za zamani za kivita zilikuwa katika maonesho ya kumbukumbu ya vita vya pili vya dunia. Maonesho hayo yameandaliwa na kampuni ya Commemorative Air Force (CAF) ili kuonesha uwezo wa ndege za Marekani zilizotumika wakati wa vita vya pili vya dunia. Mamlaka nchini humo zimeanza uchunguzi kubaini sababu za rubani wa Bell P-63 Kingcobra kuigonga Boeing B-17 Flying Fortress, k**a ni uzembe, makosa ya kiufundi, au alikusudia.!
Credit By