Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Karibu Kusini
TUKUTANE #Iringa2022
Cc @halimadendego
CHANGARAWE WAMUENZI WALIMU KWA VITENDO, "ALIKUWA MZALENDO, MCHAPAKAZI"
AFISA Elimu Sekondari Halmashauri ya Mji wa Mafinga Ndg. Steven Semdoe ameungana na Mwalimu Mkuu Peter Mbata pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Changarawe kufanya usafi katika maeneo ya Hospital ya Mji Mafinga ikiwa ni kumbukizi ya Miaka 23 ya kifo Cha Baba wa taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere mapema Leo tar 14/10/2022.
Cc @tenyabrown_
ULEMAVU SIO KUSHINDWA KUMUDU SHUGHULI ZA MAISHA
WANAFUNZI Ladiladius Massawe na Theofista Obeid wa shule ya sekondari Mtera wilayani Iringa ni walemavu wa kuona lakini licha ya changamoto hiyo wamefanikiwa katika masomo yao na wana ndoto kubwa hapo baadaye.
Wanafunzi hao wamewaomba watu wengine wenye ulemavu wa aina yoyote kutokubali kupoteza mwelekeo katika maisha kwa kukata tamaa huku wakiwakumbusha wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu kuwapenda watoto wao.
Cc Clement Sanga
UMUHIMU WA KUZIHAMISHA KAYA 374 KUTUNZA VYANZO VYA MAJI
TUME ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais imeishauri Serikali katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa kuona umuhimu wa kuzihamisha kaya 374 zilizopo kwenye kingo za bwawa la Mtera ili kumaliza shughuli za kibinadamu zinazofanyika kwenye maeneo hayo ambazo ni tishio kwa ustawi wa bwawa hilo ambalo ni nyeti kwenye uzalishaji wa nishati ya umeme nchini.
Cc Clement Sanga
AFISA USALAMA FEKI ANASWA NA POLISI
JESHI la Polisi mkoani Iringa linamshikilia mtu mmoja Gabriel Kaserikali (34) mkazi wa Mbezi Mwisho Jijini Dar Es Salaam kwa tuhuma za kujifanya mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa ambaye siku ya tarehe 1/10/2022 alikuwa akipita kwa baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wilaya ya Iringa na kuwaelekeza wajumbe wamchague mmoja wa wagombea aliyejulikana kama Leonard Mgina ambaye alikuwa anagombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo.
@polisi_iringa
'UCHAGUZI UMEKUWA MZITO'
WAJUMBE JUMUIYA YA VIJANA CCM WILAYA YA MUFINDI wakitoa maoni yao baada ya kufanyika uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti
UVCCM MUFINDI WALIA NA SEMINA ZA UONGOZI WATAKA KUIJUA ZAIDI CCM
MWENYEKITI wa UVCCM Wilaya ya Mufindi Ndg. Christian Mahenge aliyemaliza muda wake akizungumza Leo 23Sep ,22 kwenye ukumbi wa CCM Mufindi unapofanyika uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya wa UVCCM Wilaya ya Mufindi, ameomba kuwepo kwa semina za Mara kwa mara za UONGOZI ili kuwafunza vijana juu ya kukijua zaidi Chama Cha Mapinduzi.
Amesema Muda mwingi Vijana wa CCM wanabaki tu kuwa Mashabiki.
Wachezaji wa Timu ya Taifa “Taifa Stars” wakiwa kwenye mazoezi yaliyofanyika Azam Complex, Chamazi kujiandaa na michezo miwili ya kirafiki kwenye Kalenda ya FIFA dhidi ya Uganda na Libya itakayochezwa Libya.
"PANYA ROAD HAWANA NAFASI YA KUFANYA
UHALIFU IRINGA"-RPC ALLAN BUKUMBI
JESHI la Polisi mkoani Iringa limesema magenge ya vijana wanaofanya uharifu na unyanganyi kwa kutumia silaha maarufu kama panya road hayana nafasi mkoani humo kwani jeshi hilo limejipanga kuhakikisha linachukua hatua madhubuti kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
ZAIDI YA VIJANA 1247 WAHITIMU MAFUNZO YA JKT MAFINGA
Na RAYMOND MINJA MAFINGA
Zaidi ya Vijana 1247 wamehitimu Mafunzo ya awali JKT kwa mujibu wa sheria ya operesheni Venance Mabeyo Katika Kikosi cha Jeshi Mafinga JKT Kilichopo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa.
Mafunzo hayo yamehitimishwa na Mgeni Rasmi Mhe. halima Dendegu Mkuu wa mkoa wa Iringa na Kushuhudiwa na mkurugenzi wa mafunzo na utendaji kivita kanali Amosi Mollaa aliyemuwakilisha mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa meja jenerali Rajabu Ndiku Mabele .
Akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo hayo mkuu huyo wa mkoa Dendegu aliwataka vijana hao kutumia mafunzo na weledi walioupata kwenye mafunzo hayo kwenda kulitumikia taifa lao .
𝗣𝗥𝗘𝗦𝗦💬
Kocha Mkuu Nasreddine Nabi akizungumzia maandalizi ya kuwakabili Zalan FC kwenye mchezo wa kimataifa #totalenergiescafcl ambao utapigwa kesho kwenye Dimba la Mkapa
@yangasc
SAA 48 ZATOSHA KUKAMATA WAHALIFU 100 TEMEKE.
@amosmakalla
@jokatemwegelo
@bupe_hezron
@abdallah_mtinika
@elihurumamabelya
@temeke_mc