14/06/2023
TAARIFA: ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM KATIKA JIJI LA DODOMA KUANZIA TAREHE 15 JUNI 2023.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo atafanya Ziara ya Kuimarisha Chama, Ukaguzi wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 - 2025 na Usikilizaji na Utatuzi wa Kero za Wananchi katika jiji la Dodoma kuanzia mnamo tarehe 15 Juni 2023 hadi tarehe 25 Juni 2023.
Ndg. Chongolo ataongozana na wajumbe wawili wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, Katibu wa NEC - Organaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi (Gavu) na Katibu wa NEC - Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema.
Nyote Mnakaribishwa.
TunaImaniNaSamia