15/01/2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan, ametoa pole kutokana na changamoto ya kuzimwa kwa mtandao siku na baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.
βKwa Washirika wetu katika Jamii ya Kidiplomasia na wageni wanaoishi hapa nchini Tanzania, ninatoa pole ya dhati kutokana na hali ya kutokuwa na uhakika, usumbufu wa huduma, na kufungwa kwa mtandao wa intaneti. Nawaahidi kuwa tutakuwa makini kuhakikisha usalama wenu na kuzuia hali k**a hiyo kujirudia katika siku zijazo.β
Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema hayo katika hafla ya kufungua mwaka mpya 2026 pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania, Wawakilishi wa Heshima, na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa leo Januari 15, 2026, Ikulu Chamwino.
βπΏ
π¦