12/04/2020
NIMEPITIA PICHA NYINGI KUHUSU PASAKA ILA HII NDIO SAHIHI ZAIDI UKILINGANISHA NA JUMBE NYINGINE
NB. EASTER FOR PAGANS BUT PASSOVER IS FOR CHRISTIAN
We are SON OF GOD and not SUN OF GOD
• • • • • •
"Pasaka" linatokana na neno la kiebrania "PESACH" kwa kiingereza ni lenye maana "PASS OVER" yaani "KUPITA JUU YA". »Mwanzo wa Pasaka ulikuwa ni wakati wa nabii Musa (KUTOKA 12:14,17-18,21, KUTOKA 13:3-4; HESABU 9:21-30). »Pasaka ni tendo la Bwana kupita juu ya nyumba za wana wa Israeli huko Misri, pale alipoiona damu ya mwanakondoo wa Pasaka katika vizingiti vya juu na miimo miwili ya milango yao alipita juu na kuacha kuwaharibu. Walioharibiwa walikuwa ni Wamisri ambao alama ya damu haikuonekana katika nyumba zao (KUTOKA 12:21-30). »Mungu aliwaagiza wana wa Israeli kuikumbuka siku hii. »Siku kuu hii ya Pasaka ilifanyika kuwa kumbukumbu kila mwaka katika mwezi wa Kiyahudi unaoitwa " NISAN" (NEHEMIA 2:1) au "ABIB" (KUTOKA 13:3-4). Siku kuu hii ilifanyikwa kwa juma moja yaani siku ya 14 hadi siku ya 21.(KUTOKA 12:14,17-18; HESABU 9:1-5). »Mwezi wa "NISAN" au "ABIB" katika kalenda yetu ni kati ya mwezi "MARCHI" na "APRILI". Kuanza kwa mwezi ABIB kunategemeanana mwandamo wa mwezi . Ndiyo maana tarehe za siku kuu ya Pasaka hubadilika kila mwaka, Lakini huwa ni kati ya mwezi Marchi na Aprili. »Siku kuu hii iliendelea hadi katika kipindi cha Yesu Kristo. Yesu kristo mwenyewe alikuwa akienda kusherekea Pasaka(LUKA 2:41-52; YOHANA 2:13,23). »Hiki kilikuwa ni kivuli cha Yesu Kristo k**a mwanakondoo wa Pasaka aliyechinjwa msalabani.
Yesu kristo alitolewa kusulubishwa wakati wa pasaka k**a Pasaka wetu(YOHANA 18:39, 19:14-18; 1 WAKORINTHO 5:7). Kwa sababu hiyo, sasa hatuna haja ya kuchinja wanyamatena k**a sadaka bali ni kumwamini Yesu ambaye ndiye sadaka yetu.
YESU KRISTO NYIYE PASAKA WETU
HAPPY PASS OVER👋👋