Dodoma Magazine

Dodoma Magazine KWA HABARI NA MATUKIO MBALI MBALI YALIYOJIRI NCHINI NA DUNIANI KOTE PIA KWAMATANGAZO YA BIASHARA NA MENGINEYO...HABARI ZA MICHEZO BURUDANI

Inadaiwa kuwa uongozi wa Simba SC inajiandaa kuachana na na mlinzi wao wa kulia Shomari Kapombe baada ya kudumu kwenye k...
15/06/2024

Inadaiwa kuwa uongozi wa Simba SC inajiandaa kuachana na na mlinzi wao wa kulia Shomari Kapombe baada ya kudumu kwenye kikosi Kwa muda mrefu.

Baadhi ya klabu za Ligi Kuu Bara zimeonyesha Nia ya kumtaka nyota huyo.

Usiache kufollowFRIENDS WHO LIKE SIMULIZI NA MICHEZO 2022

🚨 TETESI: Taarifa ilizozipata  ni kwamba, Klabu ya Yanga kwa muda mrefu wanamfukuzia winga fundi, Philippe Kinzumbi, na ...
15/06/2024

🚨 TETESI: Taarifa ilizozipata ni kwamba, Klabu ya Yanga kwa muda mrefu wanamfukuzia winga fundi, Philippe Kinzumbi, na TP Mazembe wamekubali kumuachia kwa sharti la wao kupewa Kennedy Musonda.
“Inavyoonekana makubaliano hayo yatafikia pazuri na msimu ujao mkamuona Kinzumbi akiwa na jezi ya Yanga,” kilidokeza chanzo chetu ndani ya Yanga. TP Mazembe wameona ndani ya Yanga kuna mali, hivyo wamekubaliana kubadilishana vifaa. l
Yanga inatafuta winga mwingine mwenye kasi kuelekea msimu ujao ili kuimarisha eneo lao la ushambuliaji hivyo wanaamini Kinzumbi ndiye mtu sahihi na wanaweza kumpata kirahisi kutokana na urafiki wa klabu hizo mbili.

Klabu ya Simba imetuma ofa ya kutaka saini ya kiungo wa klabu ya Azam Faisal Abdala Toto, Baada ya kutuma ofa hiyo klabu...
15/06/2024

Klabu ya Simba imetuma ofa ya kutaka saini ya kiungo wa klabu ya Azam Faisal Abdala Toto, Baada ya kutuma ofa hiyo klabu ya Azam walimfuata mchezaji wao na kumwambia kuwa kuna ofa hapa kutoka klabu ya Simba je tuipokee, Mchezaji alikubali ofa hiyo.

Baada ya kuona mchezaji yupo tayari tena kwa haraka wakamua kuwapa klabu ya Simba mashariti ya a kuvunja mkataba wake ikiwemo kutoa 1B.

Huku kwa upande wa mchezaji pia klabu ilimwambia k**a uko tayari kuondoka basi tutafuta mikataba yote tuliyokubaliana binafsi na ile ya kifamilia ambayo pia tulikubaliana.

Klabu ya Simba wanao nia ya dhati tatizo kubwa kwenye 1b japo wamewambia Azam watarudi kutimiza mashariti yao.

Hizi zinaweza kuwa  dalili za kansa ya mat**iMat**i ni kiungo muhimu katika mwili wa mwanamke. K**a vilivyo viungo vingi...
21/10/2022

Hizi zinaweza kuwa dalili za kansa ya mat**i

Mat**i ni kiungo muhimu katika mwili wa mwanamke. K**a vilivyo viungo vingine mat**i huathiriwa na magonjwa mbalimbali. Mojawapo ya magonjwa hayo ni saratani(kansa).

Zifuatazo zinaweza kuwa dalili zinazo ashiria saratani ya mat**i
✔Uvimbe ambao hauna maumivu kwenye t**i moja au mat**i yote
✔Ngozi kuwa na rangi nyekundu au kidonda
✔Chuchu kukunjamana
✔Chuchu kuingia ndani
✔Kutoka damu au majimaji yenye damu
au rangi isiyokuwa ya kawaida kwenye t**i

Ukiwa dalili mojawapo au zote nenda mara moja kwenye kituo cha afya ili uweze kupata ushauri,uchunguzi na matibabu

Pia kwa ushauri Na msaada zaidi, unaweza kuzungumza nasi kwa whatsapp namba #0789699225 ,

04/06/2021

➡️ G S M
Mfadhili wa Yanga SC Ghalib Said Mohammed - GSM Juu ya ujio wa Yusuph Manji
"Kwa sasa mimi siwezi kusema chochote nini nitawafanyia Yanga SC ila ngoja tupate mfumo sahihi wa mabadiliko wa timu yetu ya Yanga ndipo nitawaonesha kwa mara nyingine mapenzi yangu kwa timu hii ya Yanga nini nitawafanyia".
"Najua Yusuph manji aliifanyia makubwa sana Timu hii wakati yeye alivyokuwa hapa kitu ambacho mimi bado sijafikia ila hainikatishi tamaa kuacha kuendelea kuisaida Yanga nitapambana hadi mwisho wa msimu huu kuwa karibu na timu yangu ya Yanga kwa kuwapa ufadhili wote unaohitajika",
"Ujio wa Manji Tanzania umenipa furaha sana na nilishawahi kuongeaga nae awali kabla ya kurudi nchini alinambia nia yake ya dhati kabisa kuja kutaka kuifanya Yanga iwe moja ya timu kubwa barani afrika baada ya kunipongeza kwa hatua ya mabadiliko tunayoendelea kuyafanyia ya kimuundo wa klabu yetu kwa sasa".
"Imani yangu atakuja tena Yanga na tutaunganisha nguvu kwa pamoja kuipeleka Yanga kule mashabiki na wanachama wote wa Yanga wanaopataka kuiona timu yetu inapostahili",

13/03/2019

MWENYEKITI WA CHADEMA MH FREEMAN MBOWE ATOA SHUKRANI
Waheshimiwa Wanachama, Viongozi na Wabunge!.
Naomba niwashukuru sana wale wote walioshiriki nasi kupigana, kulia na hata kuimarishana kwa njia mbalimbali katika kipindi chote cha miezi mitatu na nusu tuliyoishi gerezani.

Natambua na kuheshimu mno ushiriki wenu kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sala, ushauri, huduma ya chakula, michango ya fedha, solidarity support mahak**ani na zaidi walioweza kutenga muda wao na kuja kututembelea na kutufariji gerezani Segerea kulikoambatana na zawadi mbalimbali vikiwemo vitabu & magazeti, matunda, maji, juice na hata machozi!!!.
Nitambue kipekee kazi kubwa na ya kutukuka iliyofanywa na Mawakili Wasomi waliounda defence team yetu!! You were great all the way through!! Nitoe shukrani vilevile kwa wale wote waliotoa support kwa familia zetu na hata kututunzia na kujenga kwa njia mbalimbali Majimbo yetu ya uchaguzi ikiwemo zoezi la Chadema ni Msingi.

Kwa wale walioshindwa vyote hivyo, watambue kwa dhati nawapenda na kuwaombea yote yaliyo mema..... au k**a wapo wengine waliokwazika kwa njia moja au nyingine..... Pia nichukue fursa hii kuwaomba msamaha na kuitaka amani miongoni mwetu!! Aidha, niwape pole nyingi wenzetu wote waliokumbwa na maswahibu mbalimbali katika kipindi chote hiki!!
Tuimarishwe zaidi katika mapito haya ili itimie kauli ya “kesho yetu kuwa bora kuliko jana “.
Mbarikiwe sana!!
Freeman Aikaeli Mbowe
Mkt (T), KUB & Mp Hai

Hujafa hujaumbika
10/10/2018

Hujafa hujaumbika

TANZIAUONGONZI WA DODOMA MAGAZINE UNASIKITIKA KUTOA POLE KWA WATANZANIA WALIOPOTENZA NDUGU NA JAMAA NA WATOTO WAO KATIKA...
22/09/2018

TANZIA

UONGONZI WA DODOMA MAGAZINE UNASIKITIKA KUTOA POLE KWA WATANZANIA WALIOPOTENZA NDUGU NA JAMAA NA WATOTO WAO KATIKA AJALI YA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV NYERERE ILIYOTOKEA JUZI 20 09 2018 ZIWA VICTORIA ...

MBELE YETU NYUMA YAO

R.I.P

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mbunge wa huyo ameikosoa kauli ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Joel Mo...
21/09/2018

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mbunge wa huyo ameikosoa kauli ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Joel Mongela kuwa zoezi la Uokoaji lilisimamishwa kwa sababu ya giza.
“Hii ni ajali ya kujitakia, kwa sababu Mbunge wa Ukerewe alitahadharisha mapema, elimu ya Mv Bukoba, Mv-Spice ilikua elimu tosha isingepelekea kutokea ajali ya jana, haingii akilini kwa historia ya majanga nchini, ni aibu kuona shughuli za uokoaji zinasimamishwa kwa sababu ya giza, inatia uchungu inaumiza, Tanzania ni yetu sote.”
Aidha James Mbatia amependekeza kwa serikali kuundwa kwa wakala maalum ya kushughulikia maafa Tanzania Disaster Management Agency K**a sheria ya maafa ya mwaka 2015 inavyotaka.
“Ni ajabu tumerudia makosa yaleyale ya miaka 22 iliyopita, k**ati za ulinzi na usalama hawana utaalamu wa kushughulika na maafa, tukaamua kuanzisha sheria namba 7 2015 kwa ajili ya kuunda wakala wa kushughulika na maafa ili tuondokane na mambo ya kubahatisha…”
Watu mbalimbali wameendelea kutoa salamu za rambirambi kwa watanzania waliopoteza ndugu na jamaa zao kataka ajali hii

‪  Huyu ndie Mariam Nabatanzi (39) wa Uganda ambae anatajwa kuwa ndio Mwanamke mwenye Watoto wengi zaidi kwa sasa dunian...
19/09/2018

‪ Huyu ndie Mariam Nabatanzi (39) wa Uganda ambae anatajwa kuwa ndio Mwanamke mwenye Watoto wengi zaidi kwa sasa duniani, Mariam mpaka sasa ameshazaa Watoto 44 na Mwanaume mmoja huku akiwa na seti 4 ya mapacha 3, seti 3 ya mapacha 4, seti 6 ya mapacha 2 na wengine 8.‬

MAISHA NI HATARISHIHaijakaa vizuri,maisha yanatishia,Ukipita duniani,maisha yao yatatisha,Wapitia dhiki nyingi,tuwaonee ...
13/09/2018

MAISHA NI HATARISHI
Haijakaa vizuri,maisha yanatishia,
Ukipita duniani,maisha yao yatatisha,
Wapitia dhiki nyingi,tuwaonee huru
ma,
Watoto wanateseka,maisha nihatari
shi.
Wengi watupwa vyooni,wengine kute
lekezwa,
Wengine majaralani,wanatupwa k**a taka,
Na wengine ni motoni,wachomwa bila
huruma,
Watoto wanateseka,maisha ni hatari
shi.
Wauwa mashuleni,kwa vipigo k**a
nyoka,
Na wengine ni vitani,kikatili wauwa
wa,
Watoto wanahatari,nyingi zinawafu
atia,
Watoto wateketea,kwa mazingira hatarishi.
Tupinge unyanyasaji,watoto kuwao
koa,
Tuzizuwie hatari,watoto wategeme
wa,
Tuchukuwe tahadhari,vifo kwao vita
koma,
Tuweze kuwaokoa,wasipatwe na hata
ri.

Neno moja kwake huyu jamaaa kioo cha jamii
04/09/2018

Neno moja kwake huyu jamaaa kioo cha jamii

Makonda ajimilikisha “kijiji kizima” ukubwa wa viwanja 15 vyasoka.PAUL Makonda, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, amemvua n...
02/09/2018

Makonda ajimilikisha “kijiji kizima” ukubwa wa viwanja 15 vyasoka.
PAUL Makonda, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, amemvua nguo Rais John Magufuli katika vita ya ufisadi.
Siri zake zimeanza kuvuja na imeanza kudhihirika kuwa hasira zote na bidii ya kunyamazisha bunge, wapinzani, wakosoaji, na vyombo vya habari ni mbinu ya kuwezesha wajanja kuvuna wasikopanda na kujilimbikizia mali kwa kutumia ofisi ya umma.
Shaka ya wananchi juu ya sababu za rais kudekeza na kumpendelea Makonda, ambaye kwa kutambua kuwa ni kipenzi cha Rais Magufuli amekuwa anatumia cheo chake na ukaribu wake na rais kupora mali na kujimbilikizia mali zisizo na maelezo ya kutosha, imeanza kupata majibu.
Mali nyingi alizonazo hazijulikani kwa tume ya maadili ya viongozi, na haziendani na kipato chake.
SAUTI KUBWA inaanza na viwanja vya ardhi sita vikubwa vinavyomilikiwa na Makonda katika mkoa wa Dodoma pekee.
Viwanja hivi sita anavyomiliki Dodoma vipo katika eneo linalojulikana k**a Iyumbu New Town Centre, katika block R na S, vikiwa na ukubwa kuanzia mita za mraba kati ya 5,000 na 40,000 kwa kila kiwanja.
SAUTI KUBWA inasema pasipo shaka kuwa katika ujumla wake, viwanja vyote sita vya Makonda vinachukua eneo la mita za mraba 92,341.
Eneo hilo ni sawa na hekta 9.23 au ekari 22.3 za ardhi, ambazo ni sawa na ukubwa wa viwanja 15 vya mpira wa miguu (soka). Ni sawa na kijiji kidogo.
Viwanja hivyo, ambavyo vielelezo vyake vimeambatanishwa hapa, havijulikani kwa tume ya maadili ya viongozi.
Katika block R kuna viwanja vinne namba 1, 28, 32 na 33. Kiwanja namba 1 kina mita za mraba 40,973, na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 2,581,300.
Kiwanja namba 28 kina ukubwa wa mita za mraba 18,210 na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 1,147,250.
Kiwanja namba 32 kina ukubwa wa mita za mraba 13,080 na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 824,050.
Kiwanja namba 33 kina ukubwa wa mita za mraba 9,932 na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 625,750.
Katika block S, Makonda anamiliki viwanja viwili, namba 17 na 18.
Kiwanja namba 17 kina ukubwa wa mita za mraba 5051, na kinalipiwa kodi na riba ya Sh. 318,250. Kiwanja namba 18 kina ukubwa wa mita za mraba 5,095, na kinalipiwa Sh. 321,000.
Kwa mujibu wa vielelezo ambavyo SAUTI KUBWA inavyo, hadi tarehe 21 Mei 2018, viwanja hivyo vilikuwa vimehakikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma. Ingawa mmiliki ni Makonda, vyote vinaonekana vimesajiliwa kwa ajili ya taasisi.
Suala la viwanja vya Makonda linaibuka wakati kuna sintofahamu juu ya makontena 20 bandarini ambayo Makonda anagoma kuyalipia kodi, huku Mamlaka ya Mapato Tanzania ikiamuru yapigwe mnada kuokoa kodi ya serikali.
Makontena hayo, ambayo awali Makonda aliyakana, yameandikwa jina lake, naye anadai kwamba vifaa vilivyomo ni kwa ajili ya shule ambazo hata hivyo hazijulikani.
Hata huko Marekani anakodai vilichangwa, kuna utata juu ya watu wanaodaiwa walivichanga. Hapo hapo kumezuka hoja kwamba ndani ya makontena ya makonda kuna vifaa vingi zaidi ya samani za shule, na kwamba samani hizo zimetumika kufunika “mzigo” halisi.
Tayari kuna maelezo kuwa Makonda aliingiza makontena hayo kwa ajili ya miradi yake binafsi kwa kutumia ofisi ya serikali. Ubabe aliotumia kushambulia wanaohoji kuhusu makontena hayo, huku akitumia jina la rais ni baadhi ya mambo yanayoleta hisia kwamba kati ya Makonda na rais kuna biashara ambayo wananchi hawajaijua.
Baadhi ya wachabuzi wa siasa wameiambia SAUTI KUBWA kuwa uswahiba uliopitiliza kati ya Makonda na Rais Magufuli una harufu ya ufisadi.
Wanasema hata mabavu ya rais na Makonda kutumia vyombo vya dola dhidi ya raia wanaokosoa utawala wake ni mazalia ya ufisadi mkubwa utakaoibuka taratibu, hasa baada ya muda wa Rais Magufuli kuondoka madarakani.
Chanzo kimoja kimeiambia SAUTI KUBWA: “Usidhani Magufuli hajui uchafu wa Makonda. Anamlinda kwa sababu wana mradi wao. Makonda ni mtoto wa baba, ni mmoja wa viongozi wapendwa wanaojua dili chafu za baba; ndiyo sababu ya ushirika wao kunyamazisha wakosoaji.”
“K**a Watanzania walidhani Magufuli ni mwadilifu k**a anavyojitapa mbele yao, walikosea sana; huyu anajulikana kwani katika wizara zote alikopitia, kulikuwa na kelele na mbwembwe nyingi za takwimu, lakini ufisadi ulitamalaki. Ataacha leo kwa vile yupo Ikulu?,” kimehoji chanzo kingine, na kuongeza:
“Hawa jamaa wana majengo na viwanja nchi nzima. Wanajimilikisha nchi utadhani dunia inaisha kesho au wanamkomoa mtu. Si uliona hata majuzi rais akiwa Mwanza, baada ya kumtembelea dada yake hospitalini, alisimama pale Nyerere Road kuzindua kwa siri jengo lake linaloitwa Nyerere Plaza, akajidai anazungumza na wananchi. Ni Mali yake ile.
“Tutajua mengi sana kadiri muda unavyokwenda, na watu watashangaa. Hili la Makonda limeshamchafua rais, nasikia anajipanga kujifanya anamtumbua kwa lawama za juu juu k**a njia ya kuficha uchafu wao. Hata akitumbuliwa leo ni geresha tu. Utasikia Makonda ametokea mlango mwingine.
“Hata huyu mhuni (Cyprian) Musiba ameagizwa kurusha mashabulizi dhidi ya Makonda kwa malengo maalumu maana wote ni kambi moja. Ni sanaa inachezwa kuzuga wananchi, kumsafisha rais.

Mchoma mishikaki pichani amekili kuchinja Paka zaidi ya 1000 kwaajili ya Mishikaki na kuwauzia watu.Nini Maoni yako?
02/09/2018

Mchoma mishikaki pichani amekili kuchinja Paka zaidi ya 1000 kwaajili ya Mishikaki na kuwauzia watu.

Nini Maoni yako?

NAOMBA TUMSAIDIE KUSHARE DADA YETU HII HABARI YAKE, AS MUCH AS WE CAN..!!Naitwa MISHALY SUMARY naishi Kibaha Maili moja,...
01/09/2018

NAOMBA TUMSAIDIE KUSHARE DADA YETU HII HABARI YAKE, AS MUCH AS WE CAN..!!
Naitwa MISHALY SUMARY naishi Kibaha Maili moja, nilikuwa nikifanya kazi katika Hospitali ya Burere k**a Muuguzi kuanzia mwaka 2008 mpaka tarehe 26/12/2011 siku ambayo sitaweza kuisahau katika historia ya maisha yangu, nilikuwa natoka kazini naenda nyumbani majira ya SAA 12 jioni nikiwa Njia ghafla nilivamiwa Na watu nisiyo wafahamu walikuwa wanaume wawili waliotokea nyuma yangu, mmoja alinishika shingoni na mwingine alinishika miguuni yule aliyenishika shingoni aliniambia sali dua yako ya mwisho Leo ni mwisho Wa maisha yako.
Walinipiga sana na wakanivunja uti Wa mgongo, nyonga, taya, meno Na shingo, nilipata maumivu makali Sana nililia kwa uchungu huku nikipiga kelele za kuomba msaada, kwa mbali zilisikika sauti za watu wakisogelea eneo lile mmoja kati ya wale wanaume wale wasiyo Na uruma alisema tumalize kazi tunauza gazeti, walichukua chuma na kunipiga usoni maeneo ya mdomo na kunivunja taya Na meno, wasamaria wema walipofika watu wale wasiyo Na huruma walikimbia Na kuingia vichakani, nipelekwa kituo cha polisi kupata PF3 nakupelekwa hospital ya Tumbi hali yangu iliendelea kuwa mbaya ambapo nilipata Rufaa ya kwenda Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kwa bahati mbaya nilikutana Na mgomo mkali Wa madaktari Na hali iliendelea kuwa mbaya Sana kwani viungo vyangu viliendelea kuingia ganzi mwishowe nikapoteza fahamu. Nilirudishwa katika Hospitali ya Burere ambako nilikuwa nafanyia kazi na kupatiwa vipimo ambavyo vilionesha kuwa pingili 3 za uti mgongo Na shingo ilikuwa zimepanguka, nililazwa pale kwa muda wa miezi 8 nikarudishwa MOI kwa madaktari bingwa Wa mishipa ya fahamu, waliniambia kwamba wangenifanyia operation ya Uti Wa mgongo ila kulikuwa Na uhaba Wa vitanda.
Niliendelea kuhudhuria kila tarehe nilizopangiwa, mwisho waliniambia hawawezi kunifanyia operation kwani maisha yangu yatakuwa hatarini, kiukweli niliumia Sana kupokea majibu hayo... Walinipa rufaa tena kwenda Daktari bingwa wa Mishipa ya fahamu kwani yeye ndiye angetoa maamuzi nifanyiwe operation au nisifanyiwe, nilipipelekwa kwa Daktari bingea huyo alisema operation hii ni ngumu inachukuwa zaidi ya SAA 8 hivyo K**a kuna uwezekano nipelekwe India, lakini wakati nikisubiri kwenda India nilitakiwa kuchongeshewa Viatu kwani miguu ilikuwa ikitoa Maji, kunywea Na kupinda, pia nilitakiwa kufanya mazoezi kila siku Na kumeza Dawa ya kulisha never zisiendelee kunywea.
Nilirudisha Muhimbili kwa mazoezi Na kuchongeshewa Viatu, nikiwa kliniki dada mmoja alinisogelea na kunijulia hali baada ya kuzungumza na kumuelezea hali halisi aliniahidi atakuja kuniona nyumbani , kweli siku chache baadaye alinitembelea nyumbani nakujitambulisha kuwa yeye ni Mwandishi Wa habari, nilimwelezea hatua ambayo tayari nilikuwa nimeshafikia kuwa nimeshatuma vipimo nje ya nchi (India) ila sina pesa Na family pia haina uwezo.. Aliniambia atairusha habari kwenye gazeti nitapata msaada Wa kwenda kutibiwa kweli namshukuru Mungu kupitia habari hile ilinikutanisha Na Baba mmoja Wa kule nyumbani Arusha yeye aliniambia anastaafu K**a nitakuwa sijapata pesa ya matibabu atanisaidia napia atawaomba marafiki zake wamsapoti.
Yule baba Alituma vipimo India walimjibu kuwa wanaweza kunitibu mgongo pekee kwa $ 18,000 na nitatakiwa kukaa kule kwa siku 18. Nilifanikiwa kwenda India kwa udhamini wa huyo baba lakini nilipofika hospitalini India walifanya vipimo upya wakagundua shida ni kubwa siyo sawa na vipimo vya Tanzania vilivyo kuwa vimetumwa mwanzo, hivyo Nikaambiwa kuwa natakiwa kukaa miezi 6 badala ya siku 18 k**a ilivyokuwa mwanzo kabla ya kuondoka nchini, gharama ziliongezeka.
Nikiwa India waligundua nerves zote zilikuwa zimesinyaa na haziwezi kufanya kazi kabisa yaani nilikuwa nimepooza mwili mzima, kwahiyo wakaanza ku bust zile nerves kwanza maana Zilikuwa 0 zikapanda mpaka 46 . Na baadhi ya viungo k**a mikono vikaanza kufanya kazi na nikawa na uwezo wa hata kujiburuza mwenyewe na kuketi.... Kwahiyo matumaini ya kupona yakaanza kurejea. Lakini baada ya miezi 3 ile pesa niliyokwenda nayo ikaisha kabisa na hakuwa na namna tena na mdhamini akawa hana njia nyingine ya kunisaidia.
Nilirejea Tanzania kutafuta namna ya kupata pesa ili nik**alizie matibabu lakini sikuweza kufanikiwa mpaka sasa ninavyoandika ujumbe huu...
Kwa sasa viungo vyote vimeanza kurudi katika hali ya mwanzoni kabla ya kwenda India. ile ganzi tena imerudi mwilini na mkono mmoja tu sasa ndo unaweza ku move. Ninaomba msaada kwa watanzania wenzangu ili niweze kupata pesa kwa ajili ya matibabu ambapo kwa makadirio si chini ya $ 20,000/- sawa na 40m.
Naomba kwa yeyote anayeweza kuniunganisha na Taasisi au mtu mwenye uwezo wa kunisaidia anisaidie. *Namba zangu ni 0622015530*
*MWENYEZI MUNGU AWABARIKI*

HUYU NDIYE MWALIMU HERIETH ALIYESAHAU POCHIMwanafunzi wa darasa la 5 katika Shule ya Msingi Kibeta, Sperius Eradius(13) ...
31/08/2018

HUYU NDIYE MWALIMU HERIETH ALIYESAHAU POCHI

Mwanafunzi wa darasa la 5 katika Shule ya Msingi Kibeta, Sperius Eradius(13) amefariki dunia akidaiwa kupigwa na mwalimu wake wa nidhamu kwa kutuhumiwa kuiba pochi ya mwalimu Herieth Gerard.

Baadhi ya Wanafunzi walioshuhudia tukio hilo lililotokea wamesema mwanafunzi huyo alikwenda kumpokea mizigo mwalimu wake Herieth aliyefika shuleni hapo kwa usafiri wa bodaboda.

Alipoingia ofisini Mwalimu Herieth alianza kulalamika kutoiona pochi yake ndipo Sperius alipoitwa na kuhojiwa lakini akakana kuichukua pochi hiyo hali iliyosababisha kuanza kupigwa na mwalimu wa nidhamu akitakiwa kuirejesha.

Aidha, waliongeza kuwa baadaye walitakiwa kuitafuta pochi hiyo hadi chooni, lakini hawakuiona huku mwanafunzi huyo akiendelea kuadhibiwa.

Hata hivyo, dereva bodaboda alifika shuleni hapo akimtafuta mwalimu Herieth aliyepoteza pochi na kumkabidhi pochi yake aliyokuwa ameisahau kwenye pikipiki yake.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufani ya Mkoani humo, Dkt. John Mwombeki, alikiri kupokea mwili wa mtoto huyo majira ya saa mbili asubuhi ukionekana kuwa na majeraha ya kipigo.

Mwalimu huyu anayetuhumiwa kumpiga kikatili Mwanafunzi hadi kufariki kwa tuhuma za kuiba mkoba wa Mwalimu mwingine aitwaye Herieth, amek**atwa na Jeshi la Polisi.

Mwalimu Respicius Patrick (50) alichukua jukumu la kumuadhibu Mwanafunzi Sperius Eradius(13) pichani baada ya kuambiwa ameiba mkoba wa Mwalimu Herieth Gerald.

K**anda wa Polisi mkoani humo amepata wakati mgumu alipofika shuleni hapo baada ya kupokewa kwa nyimbo za kudai haki kutoka kwa Wanafunzi.

K**anda wa Polisi amesema kuwa Jeshi la polisi mkoani Kagera linamshikilia mwalimu wa nidhamu wa shule ya msingi Kibeta iliyoko katika manispaa ya Bukoba, Respicius Patrick (50) kwa tuhuma za kumpiga na kumsababishia kifo mwanafunzi wa darasa la 5 katika shule hiyo, aitwaye Sperius Eradius(13).

Aidha, mkoba huo uliokuwa na Tshs 75,000 baadaye uliletwa na dereva Bodaboda na kueleza kuwa Mwalimu Herieth aliusahau

31/08/2018
31/08/2018

*TUWAACHE WASOME KWANZA.*
Kuna wasichana warembo sana mashuleni ambao ndio matoleo mapya kwenye gemu ya mahaba, wanavutia sana ndio maana vijana wengi wanawatolea macho na wengine kujitosa kula mzigo bila kuhofia jela. walimu nao k**a nawaona vile mnavyovuna mlichokipanda! Juzi kuna rafiki alinitumia sms akasema "Jay naomba unitungie meseji ya kutongoza iwe nzuri maana kuna mwanafunzi namtemea cheche ila hataki kunipa penzi anadai hadi amalize shule!"
Nikamuuliza kwani anasoma darasa la ngapi? akajibu "Yupo form four (kidato cha nne)" Nikamwambia basi hiyo meseji sikupi hadi akimaliza shule ndio unitafute . Bahati yake kapata mshichana mwenye msimamo kidogo ingawa akilainishwa anaweza kulainika. Lakini kuna vitoto vingine vya shule vinashobo sana na wanaume, havina woga vinatembea hadi na waume za watu.
Sio mara zote mwanaume ndio humtongoza mwanamke ila hawa watoto washule ni watongozaji wazuri sana, wakati mwingine unaweza kushangaa nakujiuliza "Hivi hawa watoto wanaenda shuleni kusoma au kukua??" K**a miaka 30 jela ni kitu cha kawaida kwako basi endelea kuwaendekeza hawa watoto.
Vyuoni siwagusi najua nyie ni watu wazima na siku hizi mnafanya kazi nzuri mnaenda chuo na kurudi na vidigrii na vi PHD vya watoto tu. Kila mtu akijali hatma ya mapenzi na huyo unaemuona wa maana kwako utagundua tu huyu ananipenda/anataka mzigo tu! Anaekupenda atakusubiri umalize shule kwanza ndio aje kuleta barua nyumbani kwenu upendo wa kweli una subira ndani yake.. ....LOVE MSG ZIPO TELE... 👉IKIWA UNAZIHITAJI TUMA UJUMBE MFUPI WENYE JINA LAKO NA MKOA UNAOISHI KUJA 0755 826 931 NAMI NITAKUTUMIA SMS YENYE MAELEKEZO YA JINSI YA KUJIUNGA NA HUDUMA YA LOVE MSG.
👉UKIHITAJI KUMSAHAU HARAKA MPENZI ALIYEKUUMIZA NITAFUTE. KWA KUANDIKA NENO. "MSAADA"
✍ FACEBOOK like page Inaitwa JUMA NGOMA PF.
👉MSANII UNAEHITAJI NIKUTUNGIE WIMBO NITAFUTE 0755 826 931

31/08/2018

M
TUNZI-lydia
stor- KISASI
NO- 0746686435
sehemu ya kwnza
**
ilisikika sauti ya mwanamke akilia kwa uchungu sana katika poli kubwa lilikuwa mbali na mkazi ya watu, ivyo hakuna aliyeweza kumsaidia wla kumsikia kilio chake, hivyo hakuna alilia bila kupata msaada wowote, lilikuwa ni kundi la vijana walilikuwa wakimbaka kwa ngu na kumsababishia maumiv makali kana katika sehemu zake za siri alimwaga damu nying sana mpaka kupoteza fahamu,
****
alshtuka akiwa katika chumba alipojalibu kukiangalia aligundua kuwa kulikuwa hosptalini, alipoendelea kushanga ghafla mlango ulifunguka aliingia mwanamke aliyevalia gauni leupe bila shaka alikuwa ness, alitabasamu alipumuona emi kafumbua macho, ness alitoa dripu lilikuwa limeisha nakumbadlishia lengne"unaendeleaje' aliuza ness lakini emi hakujibu alianza kudondosha machozi akikumbuka yale anayoyapita,"usilie mtoto mzuri utapona mwanangu'lakni emi alimshangaa tu alichowaza nijinsi yakumaliza mapito ayo, walipokuwa wanaongea ghafla aliingia baba aliyevaa kawaaid sana.

SIMULIZI;MARAFIKI WAWILIMTUNZI;RAJA SAIDY.WHATSAPP;0756920739.SMS;0621047841.(MAISHA)SEHEMU YA PILI.SONGA NAYO.........M...
31/08/2018

SIMULIZI;MARAFIKI WAWILI
MTUNZI;RAJA SAIDY.
WHATSAPP;0756920739.
SMS;0621047841.
(MAISHA)
SEHEMU YA PILI.
SONGA NAYO.........
Mazungumzo yaliendelea ndani ya gari huku yakiwa ni baina ya john na thomas.
"John punguza uoga ndugu!!!!"
"Thomas mimi ni mtu mwenye huruma yani wale watu hawajanikuta kwenye mudi la sivyo nilikuwa nakula nyama ya mtu"
"John kwa taarifa nilizo zipata ni yakuwa police mkuu anafata nyayo zetu kila tuendapo cha msingi tufanye mchakato wa kumteka raisi na kumuamrisha atoe amri hili tuweze kupewa madaraka yatakayo tufanya tumuondoe police yule madarakani na sisi kujitawala"
"thomas umeongea cha maana.sema ugumu upo sehemu moja!!!!!ni vipi tutafanikiwa kuhusu hilo,alafu ukizingatia hiyo mishoni ni ngumu k**a nini,cha msingi ongea kuhusu jambo jingine na siyo la kumteka raisi."
"Sikia john ebu fikiria kwa sasa hivi tutafanya jambo gani litakalo tufanya tuwe katika mikono iliyo salama"
"Thomas mi naona tumuuwe police mkuu"
"hata tukimuuwa bado serikali itakuwa inatufuatilia,cha msingi ambacho tunatakiwa kufanya ni kumteka raisi"
"k**a umeamua hivyo itabidi nifuate utakavyo"
Thomas aliendesha gari kwa speed kali huku ukimya ukiwa umetawala jambo lililo mfanya john apitie na usingizi wa ghafla na kumuacha thomas aendelea kuendesha gari,thomas aliwasha redio kwa ajiri ya kusikiliza taarifa mbalimbali za siku hiyo kwani tayari mda wa taarifa ulikuwa umekwisha timia.
"HABARI KAMILI KUNA VIJANA WAWILI WANAO JULIKANA KWA JINA LA JOHN NA THOMAS WAMEMUUWA MTOTO WA POLICE MKUU KWA MADAI YA KUWA WALIHITAJI FEDHA KUTOKA KWA POLICE HUYO HILA HAWA KUZIPATA.BAADA YA KUWA WAMEMUUWA BINT HUYO,WALIFANIKIWA KUUPELEKA MWILI NYUMBANI KWAO KISHA WAKAUTIA MOTO,KABLA YA YOTE HAYO WALIMUUWA MLIZI WA GETI ALIYE JARIBU KUWAZUIA WASIINGIE NDANI BILA YA KUKAGULIWA GETINI.KUTOKANA NA TUKIO HILO LA KIARIFU RAISI WETU BWANA BREMO MAKALE AMETOA TAMKO KWA YEYOTE ATAYE FANIKIWA KUWAONA WATU HAWA ATAZAWADIWA MILIONI 60 KWA AJIRI YA KUENDESHA MAISHA YAKE,WATU HAWA UNAWEZA KUWATAMBUA KUTOKANA NA MUONEKANO WAO ULIVYO;JOHN NI MFUPI MWEUSI KIDOGO PIA THOMAS NI MWEUPE PIA NI MWEMBABA.WAHENGA WANASEMA WATU HUFANANA UKIONA JAMBO HILI LINAKUPA UTATA NJOO UCHUKUE PICHA ZAO KATIKA KITUO CHA POLICE CHA ZWAGENDA JIJINI DAR ES SALAAM AU TUTAFTE KUPITIA WHATSAPP NAMBA 07*********** TUWEZE KUKUTUMIA PICHA HIZO AHSANTE,ZIFUATAZO NI HABARI ZA MICHEZO......"
Thomas alizima redio kisha akaachia pumzi nzito iliyomfanya john kuamka kwa pupa na kwa hofu kubwa.
"thomas kuna nini???" john alizungumza huku akichomoa leso yake mfukoni na kufuta baadhi ya jasho zilizo kuwa zimemtawala hasa maeneo ya usoni.
"John tuko hatarini!!!!!!mfuuuuuuuuu"thomas alizungumza kisha akashusha pumzi kwa mara nyingine.
"Thomas kwani kuna nini kinacho endelea????" johna alihoji kwa mara nyingine na kumfanya thomas kugeuza gari na kurudi msituni ambapo tayari alikuwa amesha toka,jambo hilo lilimshangaza john kwa kumfanya ake mdomo wazi kwa mda mchache huku akibaki kutazama upande wa nyuma kwa kushuudia giza totoro lililo tawala maeneo waliyo kuwa wanataka kurudi.
Thomas alionekana kuwa mwenye mawazo kwa kushindwa afanye nini maana kati ya vitu alivyokuwa anaogopa ni amri ya raisi kwani raisi akitoa amri lazima itekelezwe hata k**a ni kwa mda wa miaka mitano.
"john nimetoka kusililiza taarifa ya habari,tuko mashakani nimeamua turudi msituni kwani asilimia kubwa ya watu wanao tufuatilia wanajua ya kuwa sisi tupo humu mjini lakini kati ya sehemu zote ambazo watu hawawezi kufikiria kwaba tuna uwezo wa kukaa ni huku msituni ,lakini sivyo hawagundui ya kuwa tunauwezo wa kukaa katika mazingira hatarishi kwa binadamu k**a yale,nadhani hii itakuwa moja kati ya vitu vitakavyo tufanya sisi tufanye mipango yetu kwa hali na mali."
"Thomas nimekuelewa............"
Safari iliendelea kwa mda kadhaa kisha wakafanikiwa kufika msituni,walitumia mwanga wa taa za gari kwa ajiri ya kuangaza makazi sahii,kitu walicho kigundua kwa wakati huo,ni kuwa ifikapo mchana watu wataanza sakata la kuwatafta kwani miliono 60 siyo ndogo.
thomas alijaribu kulazimisha gari lake kupita kwenye njia mbalimbali zisizo kuwa maalumu,wakiwa kwenye harakati zile za kutafta makazi salama ndani ya msitu hule,ghafla gari lao lilikwama katika ya msitu na kumfanya john ajikunyate mithili ya mtu aliye pigwa na baridi kali.thomas kwa ujasiri aliyokuwa nao alitoaka ndani ya gari kisha akasimama kwa kuangaza mahali walipokuwa wamekwama na nini!!!! kilichofanya jambo lile litokeee,thomas alirudi ndani ya gari kisha akaanza kuzungumza na john ambaye tayari alionekana kuwa muoga kuliko maelezo.
"John naomba simu yako!!!!"
"yani nini????"
"Naomba bwana"
john bila ya kufikiria alimkabizi simu thomas kisha thomas akatoka ndani ya gari na kuwasha tourch ya simu ya john kwa ajiri ya kuangaza mbele ya gari nini kilicho fanya gari ikwame,aliinama chini ya uvungu wa gari na kukutana na kitu kilichomfanya ashangae kutokana na maajabu ya gari hilo,kwani hakuamini macho yake baada ya kukuta gari hilo limenasa chuma kilichopo eneo hilo.
Thomas alirudi ndani ya gari kisha akachomeka ufunguo wa gari,baada ya kuwa amehakikisha gari limesha waka,alibonyeza batani ya njano iliyopo pembeni ya eneo la kuchomokea ufunguo wa gari,baada ya kuwa amesha bonyeza.
Gari ilianza kutoa sauti mithili ya mashine ya kusagia unga.sauti hiyo ilisikika kwa mda mchache kisha ikatoweka na kulifanya gari hilo kusogea mbele na kuacha shimo kubwa mahali pale.
john alitoka ndani ya gari na kumkibilia thomas kisha akahoji.
"thomas kuna nini!??"
"tazama pale..." thomas aliungumza kwa kutumia ishara kwa kunyoosha viganja vyake vya mkono hili john apate kufahamu nini kinacho endelea.
John aliaanza kujificha nyuma ya mgogo wa thomas kwani hakuamini alicho kiona mbele yake.....
je nini kitaendelea......
MPENZI MSOMAJI WANGU WA NGUVU,JARIBU KUTOA MAONI KWA UREFU ZAIDI USITOE MAONI K**A NZURI,NC,IKO POW,SIO MAONI MAZURI HATA KIDOGO,UNAPO TOA MAONI KWA UREFU WATU WENGI WANAKUUNGA MKONO KWA KILE UNACHO KIANDIKA HATA MIMI PIA NAKUUNGA MKONO.
KUPENDA PAGE HII,JUU KABISA YA PAGE HII KISHA SHARE NA LIKE KWA WINGI PAGE HII.
KUPITIA WHATSAPP NAMBA 0756920739 ILI NIWEZE KUKUUNGA KWENYE GROUP WHATSAPP LA SIMULIZI KALI KALI ZA KICHAWI ZA KUSIKILIZA NA KUSOMA KWA ADA YA 4000 TU.
**A UNATAKA MWENDELEZO NITAFTE WHATSAPP NAMBA 0756920739.
YAKO NI MUHIMU,SHARE KWA WINGI SIMULIZI HII..............

SIMULIZI;MARAFIKI WAWILI.MTUNZI;RAJA SAIDY.WHATSAPP;0784581043SMS;0784581043(MAISHA)ANZA NAYO.............Simu iliita ku...
31/08/2018

SIMULIZI;MARAFIKI WAWILI.
MTUNZI;RAJA SAIDY.
WHATSAPP;0784581043
SMS;0784581043
(MAISHA)
ANZA NAYO.............
Simu iliita kutoka upande wa pili kisha ikapokelewa.
"Hallow"
"Habari ndugu???"sauti ilisikika kutoka simuni mwa john na kufanya akae kwa makini kwa kusikiliza kinacho endelea na dhumuni la simu hile lilikuwa ni nini maana mda sio mrefu alikuwa amefanya tukio la kiharifu na kumuuwa bint wa mkuu wa police na hii ni kwa sababu walimtumia bint yule katika kumuomba mkuu wa police hili aweze kutuma hela itakayofanya mwanae aachiwe,lakini mkuu wa police alitoa amri ya kuwa wafanye wanacho kijua na yeye hayuko tayari kutoa kiasi chochote cha fedha na wakijaribu kumuuwa mwanae sheria itafuata mkondo wake.
kutokana na kauli ya police yule iliwakasirisha marafiki hao na kuchukua maamuzi ya kumuuwa bint huyo jambo lililo pelekea john kuingia na hofu kubwa ya kimaisha.
"Nzuri sijui naongea na nani mwenzangu??"john alizungumza kwa sauti ya chini chini iliyo tawaliwa na hofu na ya uoga zaidi kwani alijua tayari mkuu wa police amesha pata taarifa mwanae amesha uwawa na vijana hao ni kutokana na thomas kumpigia simu mkuu wa police na kumwambia atakula jeuri yake.
"Haa john hata sauti yangu umesha isahau???"
"kwani we nani lakini???"john alihoji.
"Du,inaonekana kitendo cha kumuuwa jeska kimekuchanganya sana me thomas"
"aha thomas unanipigiaje mda k**a huu na unajua ni sehemu hatari na pia una hatarisha maisha yangu."
thomas aliachia kicheko kilicho zidi kumpa hofu john.
"hahahahahahahha"
"Thomas zungumza haraka kwani sipo sehemu salama alafu nahisi police wako humu msituni"
"John usiohofu nakuja kwani nilikuwa nimeupeleka mwili wa bint yule kwao"
"unamaanisha uko salama????"
"siko salama ni kwa sababu baada ya kuwa nimefika getini kwenye nyumba ya police mkuu mlinzi wake alinipiga risasi ya bega hila nilifanikiwa kumuuwa na kisha nikauingiza mwili mpaka huwani mwa nyumba hile.
"Thomas umekuwa katili kweli,ama kweli tumejiajiri wenyewe"
"Nakuja kukuchukua rafiki usihofu'"
"Sawa ndugu nakuja"
"saw........"
john akiwa bado ajakata simu,alisikia kishindo cha watu wengi huku wakinyata kwa kuja upande ulipo,john alitamani kuchimba shimo ajifikie kwani akujua ni kina nani wanao karibia eneo alilopo.
John alianza kukimbia bila kujua anaelekea upande gani!!!!,baada ya kuwa john ameanza bio zake na kuelekea mahali alipo hisi kuwa kuna usalama zaidi,kundi kubwa la watu lilianza kumkibiza huku wakiendelea kumsihi asimame.
John aliongeza hatua k**a mwanaliaza aliyekuwa mafunzoni na kufanikiwa kufikia barabara ya rami iliyokuwa kando kando ya msitu na kuanza kuunga nao kwa ajiri ya kuwakimbia watu wale aliyoshindwa kuwafahamu kutokana na mavazi yao,kwani mawazi waliyo kuwa wameyavaa yanapendwa sana kuvaliwa na watu wanaotengeza barabara za rami na kumchanganya john.
johna akiwa anaongeza speed mbele yake alikutana na gari kubwa lililo mmulika na kumfanya asimame huku akiendelea kusari sala zake za mwisho kwani alijua mwisho wake umakaribia.
Kutokana mwanga ule mkali uliokuwa ukipenya machoni mwa kila mtu,uliwafanya hata kundi lile lililokuwa lilkimkimbiza john kusimama na kuanza kuzima macho,kijana mmoja mtanshati alitoa ndani ya gari lile huku akiwa amelipaki katikati ya barabara na kupiga hatua chache za kuelekea mahali john alipo kisha akamvuta mkono.
"Dogo simama"
john alisimama huku akiwa tayari kaisha jikojolea na kumtazama mtu aliyekuwa akimsihi asimame na kugundua ni rafiki yake thomas,john alipiga hatua za uoga za kuelekea ndani ya gari lile kwani alijua wale waliokuwa wakimfuata wanaweza kuwafanya kitu chochote kutokana na siraha kali walizokuwa nazo.
"wewe john kimbia kwenye gari wale si watu wakawaida"
Thomas alianza kupatwa na hofu baada ya kuona kundi lile lililokuwa likimfuata john kusimama na kuanza kunyoosha bastora eneo walilopo.
Thomas alikimbia na kuingia ndani ya gari,kabla ajawasha gari aligeuka upande wa nyuma na kumkuta john amelala siti ya nyuma,kisha akabonyeza batani nyekundu iliyopo katikati ya uskani,ghafla gari lilianza kutoa sauti kali kwa budalisha milio ya ajabu na kuwafanya watu wale kuziba sikio kwani walikereka na sauti zile,hii ilimfanya thomas kuwasha gari aina ya vani alilokuwa amemuibia raisi wa kenya na kuja nalo tanzania kwa kutumia njia za mkato, kisha akabonyeza batani iliyopo kwenye kuta ya kioo cha gari(tinted) kwa kurihusu gari lile kurusha mabomu ya machozi kitendo kilicho wafanya watokomee eneo lile kwani baada ya kutupa bomu zile zilifanya kundi lile lililo gundulika k**a watu waliyo tumwa na police. kuanza kupekecha macho kwa kutafta msaada wa maji hili wapate kuona vizuri.
maana mabomu yale yaliwapata vyema.
je nini kitaendelea.......
NDUGU MPENZI MSOMAJI WANGU WA NGUVU,JARIBU KUTOA MAONI KWA UREFU ZAIDI USITOE MAONI K**A NZURI,NC,IKO POW,SIO MAONI MAZURI HATA KIDOGO,UNAPO TOA MAONI KWA UREFU WATU WENGI WANAKUUNGA MKONO KWA KILE UNACHO KIANDIKA HATA MIMI PIA NAKUUNGA MKONO.
KUPENDA PAGE HII,JUU KABISA YA PAGE HII KISHA SHARE NA LIKE KWA WINGI PAGE HII.
KUPITIA WHATSAPP NAMBA 0756920739 ILI NIWEZE KUKUUNGA KWENYE GROUP WHATSAPP LA SIMULIZI KALI KALI ZA KICHAWI ZA KUSIKILIZA NA KUSOMA KWA ADA YA 4000 TU.
**A UNATAKA MWENDELEZO NITAFTE WHATSAPP NAMBA 0756920739.
YAKO NI MUHIMU,SHARE KWA WINGI SIMULIZI HII..............

Address

Nzuguni
Dodoma

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00

Telephone

+255689994369

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dodoma Magazine posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Dodoma Magazine:

Videos

Share

Category


Other Magazines in Dodoma

Show All