20/05/2023
KUNA MWANGA MWISHO MWA HANDAKI, WASHA TOCHI.
Wanazitazama bahasha zilizobeba CV zetu k**a vyeti vya kuonesha ufahari wa elimu yetu lakini laiti wangejua ni thamani ya jasho ambalo Wazazi na Ndugu wamevuja ili twende shule, mashamba yaliuzwa na mikopo ilichukuliwa ili mtazamo maarufu kusoma ndio ajira utimie.
Mshtuko mkubwa utaendelea kati yetu, tangu juzi Mwanetu alienda kununua vitumbua aanze siku na akakuta CV yake ndio kifungashio, tumeanza kuelewa mchezo kuwa Interview nyingi ni fashion na tayari Kocha ameshapanga kikosi chake, anajua sana yule ila hakuna anayejuana nae.
Machozi yetu yanamwagika na maumivu ni mazito, tukikumbuka iman ya mitaa dhidi yetu! Mama anaumwa kichwa na hatuna pesa ya panadol! Baba umri umeenda na bado anatupiga tafu, maisha maseke hatuna hata afu tatu.
Usiku haujawa wakati wa kupumzika tena bali nafasi ya kulia na matatizo yetu, kulia na Muumba wetu kuwa lini tutaipata keki yetu! Dunia ya mwenye nacho anaongezewa na sayari ya Mtoto wa Mbuzi kamba mali yake, sad truth.
Bado fumbo la rizki limekuwa changamoto hata Mgote hawezi kutatua! Tenzi za kesho zimekuwa ngumu hata Ali Kiba hawezi kutunga, amini nakwambia Mtoto wa Fukara kakosa mkopo ila mwenye nazo ana 100% how do you feel? Life is not fair tunakosea?
Tuendelee kupiga magoti kwenye Madhabahu yote? Tutafuta namba za Waganga mashuhuri watupe njia za kupita? Tuzingatie meseji kuhusu Freemason? Hapana yote yatapita hata k**a Wastaafu wanarudi kazini na wahitimu wanaishi hatarini.
Wengine walishangilia Kaka yao na yule Dada yetu kupata ajira lakini Mshahara ukitoka unapigwa k**a mpira! Bodi ya mikopo, PAYE na gharama zote! Kinachosalia hakitoshi hata Kuku kumeza punje ya mtama! Sherehe pekee ya Mfanyakazi ni kuwa Boss.
Waliotoboa kati yetu wanatupa stori ngumu hata k**a ni laini, hata yule aliyesema tujiajiri naye yupo kwenye Wi-Fi ya Boss wake akisubiri email ya posho za safari, aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa.
NA KESHO TENA๐