
08/02/2025
K**ati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imebaini changamoto ya mtandao na ukosefu wa vitendea kazi kwa watumishi wa umma waliopo vijijini, hali inayowakwamisha kutumia mfumo wa kupima utendaji kazi wa watumishi (PEPMIS) ambao sasa unajulikana k**a e-Utendaji.
Februari 5, 2025, Mwenyekiti wa K**ati hiyo, Dkt. Joseph Mhagama, amesema changamoto hiyo inasababisha baadhi ya watumishi kushindwa kujaza taarifa zao kwa wakati, hivyo kushindwa kufikia viwango vinavyohitajika.
Kutokana na hilo, Bunge limeazimia kuwa matumizi ya PEPMIS yaendane na utoaji wa vitendea kazi na kuboreshwa kwa mtandao katika maeneo ya vijijini. Pia, Serikali ifanye tathmini ya mfumo huo na kutatua changamoto zilizojitokeza tangu kuanza kwake. Wabunge wameikubali na kupitisha maazimio ya k**ati hiyo likiwemo hilo la PEPMIS.