10/07/2023
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassani,amesema Dhamira ya Serikali ni kuiboresha JKT ili liwe Jeshi la kisasa zaidi linaloendana na wakati na kutimiza majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu, mafunzo yanayotolewa na JKT yawasaidie vijana kuwa wazalendo wa kweli wanaothamini utaifa, umoja na mshik**ano wa Watanzania na wanaopenda kufanya kazi kwa moyo wa kujituma na kujitolea.
Ameyasema hayo,leo Julai 10,2023 jijini Dodoma wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). JKT lililoanzishwa rasmi Julai 10, 1963, hatua hii ilikuwa ni utekelezaji wa azimio la kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Aprili 19, 1963 chini ya uongozi wa Rais wa Awamu ya Kwanza, Hayati Mwl. Julius Nyerere.
Aidha ameelekeza Wizara ya Ulinzi na JKT kuandaa mpango mkakati wa kurekebisha makambi kwenye Jeshi la JKT katika upande wa malezi ya vijana. pia kuliwezesha Shirika la SUMA JKT kupata mikopo ili wazalishe na waweze kurejesha mikopo na shirika liweze kuendelea.
"Dhamira ya Serikali ni kuiboresha JKT ili liwe Jeshi la kisasa zaidi linaloendana na wakati na kutimiza majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu, mafunzo yanayotolewa na JKT yawasaidie vijana kuwa wazalendo wa kweli wanaothamini utaifa, umoja na mshik**ano wa Watanzania na wanaopenda kufanya kazi kwa moyo wa kujituma na kujitolea", amesema Rais SAMIA