Nkubason News

Nkubason News Follow my page to get all current news

DERBY.Hapo ni Benjameni Mkapa Studium, nini maoni yako kuelekea mechi hii ya kukata shoka. 🔨
05/11/2023

DERBY.

Hapo ni Benjameni Mkapa Studium, nini maoni yako kuelekea mechi hii ya kukata shoka. 🔨

Jeshi la polisi mkoa wa Mtwara linamtafuta Hadija Msamati anayeshukiwa kuhusika kwa vifo vya wanaume wawili.Kaimu k**and...
01/10/2022

Jeshi la polisi mkoa wa Mtwara linamtafuta Hadija Msamati anayeshukiwa kuhusika kwa vifo vya wanaume wawili.

Kaimu k**anda wa Polisi Wilayani Masasi, Nicodemus Katembo amezungumza na wandishi wa habari hapo jana September 30, amesema; Hadija Msamati amehusika kwa mauaji ya wanaume wawili waliomgombania mpaka umauti wao.

Ameongeza kusema watu hao walijulikana kwa majina ya Ibrahim Shabani na M***a Bakari, wamepigana kwa kutumia magogo ya miti na hivyo kufikia umauti.

"Hili tukio limesababishwa na wivu wa mapenzi ambapo imebainika kuwa baada ya tukio hilo mwanamke Hadija Msamati amekimbilia kusiko julikana ambapo kwa taarifa ya Daktari baada ya uchunguzi walibaini chanzo ni kuvuja damu kwa wingi mwilini"

Amesema Kamanda Katembo.
Daaah😭 mapenzi shikamo!!


Duuuh!! Ndo wasanii wetu hawa sasa 😂😂
29/09/2022

Duuuh!! Ndo wasanii wetu hawa sasa 😂😂

Mkoa wa Mtwara umekuwa na Idadi kubwa ya Wazazi ambao hawawapeleki Watoto kupata Dawa za kufubaza makali ya VVUWatoto we...
14/09/2022

Mkoa wa Mtwara umekuwa na Idadi kubwa ya Wazazi ambao hawawapeleki Watoto kupata Dawa za kufubaza makali ya VVU

Watoto wengi wanaokosa huduma hiyo ni wenye umri chini ya Miaka mitano ambapo Wazazi hawataki Watoto wajue hali zao Kiafya.



Soma- https://jamii.app/MtwaraVVU

Taarifa kuhusu mwanamuziki wa Tanzania Raymond Shaban Mwakyusa maarufu k**a Rayvanny kugura Lebo ya muziki ya WCB Wasafi...
14/07/2022

Taarifa kuhusu mwanamuziki wa Tanzania Raymond Shaban Mwakyusa maarufu k**a Rayvanny kugura Lebo ya muziki ya WCB Wasafi imekuwepo hasa baada yake kufungua Lebo yake kwa jina Next Level Music – NLM. Kampuni hiyo ya NLM ilizinduliwa rasmi tarehe 9 mwezi Machi mwaka 2020 hafla ambayo ilihudhuriwa na Diamond Platnumz mmiliki wa WCB. Lakini katika hafla hiyo, Rayvanny alifafanua kwamba yeye atasalia kuwa chini ya WCB.

Hivi maajuzi, mwanamuziki huyo alitoa jina la kampuni ya WCB kwenye wasifu wake wa mtandao wa Instagram jambo ambalo lilisababisha wengi wadhanie kwamba hatimaye amegura. Lakini mtangazaji wa kituo cha redio cha Clouds Fm nchini Tanzania Burton Mwemba maarufu k**a Mwijaku alifafanua kwamba Rayvanny bado hajaondoka WCB lakini anaendelea kufanya taratibu za kuondoka.

Kulingana na Mwijaku, Rayvanny anastahili kulipa milioni 800 za Tanzania kwa WCB ili aondoke k**a ilivyoainishwa kwenye mkataba wake ila hajaweza kufanya hivyo. Pesa hizo zilipunguzwa akatoa kidogo ila usimamizi wa WCB ukadai alipe pesa zote kwa pamoja ndipo wamwachilie. Pesa hizo inasemekana zinatolewa na mwekezaji ambaye alimpa Rayvanny hela za kufungua Next Level Music ambaye ni raia wa Zimbabwe.

Sasa taarifa rasimi ni kwamba msanii huyo amejitoa katika Lebo ya WCB na kuamua kujisimamia mwenyewe na Lebo yake mpya Next Level Music, hii ni baada ya click fupi aliyojirecord akimshukuru Msanii Mlezi wake Diamond Platnums pamoja na uongozi mzima wa Lebo hiyo.

Endelea kuwa karibu na NEWS kupata taarifa mbalimbali.

"NATUMIA BANDO LA MILIONI 3 KWA SIKU" AGGY BABYMuigizaji wa Bongo Movie Aggy ameshangaza umma baada ya kusema kwamba ana...
10/07/2022

"NATUMIA BANDO LA MILIONI 3 KWA SIKU" AGGY BABY

Muigizaji wa Bongo Movie Aggy ameshangaza umma baada ya kusema kwamba anatumia bando la milioni tatu kwa siku hivyo linamlia sana pesa zake.

Hivi unadhani mtandao gani utakuwa na bando la kiasi hicho cha pesa?

Kwa mastory yote ya town like page yetu Facebook na kutufollow Instagram Nkubason news hakika hutopitwa na chochote saa 24.
News.

Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Singida, Thomas Ngiracha amesimamishwa kazi kwa tuhuma za kujihusisha kimapenzi na Mwa...
09/07/2022

Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Singida, Thomas Ngiracha amesimamishwa kazi kwa tuhuma za kujihusisha kimapenzi na Mwanafunzi wa Kidato cha Nne wa Shule hiyo

Mwanafunzi aliwasilisha barua ya malalamiko akielezea usumbufu anaoupata kutoka kwa mwalimu huyo na ndipo malalamiko yake kufika hadi kwenye k**ati ya nidhamu. UPDATES

Soma - https://jamii.app/TuhumaKwaMwalimu

POLISI mkoani Mwanza inamshikilia mwanafunzi wa kidato cha pili anayesoma Shule ya Sekondari St Apostos, Yela Sylvester ...
09/07/2022

POLISI mkoani Mwanza inamshikilia mwanafunzi wa kidato cha pili anayesoma Shule ya Sekondari St Apostos, Yela Sylvester maarufu Cosmas (17), kwa kosa la kudanganya wazazi wake kuwa ametekwa ili ajipatie fedha.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Jumanne Muliro amewaeleza waandishi wa habari kuwa tukio hilo ni la Aprili 27, mwaka huu saa nne usiku katika Mtaa wa Mahaha wilayani Magu.

Amesema hiyo ni baada ya kijana huyo kusindikizwa kwenda shule na mzazi hadi kwenye Kituo cha Mabasi cha Buzuruga jijini Mwanza na kupakizwa kwenye basi la Sheratoni, linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Geita.

Lakini, hakwenda shule na badala yake aliitumia simu namba 0689447247 na kutuma ujumbe mfupi kwa baba yake, huku akiificha laini yake ya zamani ya simu, kwa madai kuwa alikuwa ametekwa kwa lengo la kujipatia fedha.

“Kwenye ujumbe aliomtumia baba yake, alidai kuwa endapo wasipomtumia fedha hizo atapelekwa na watekaji nchini Zambia kufanya kazi, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria,” amesema Kamanda Muliro.

Amesema polisi walifanya ufuatiliaji wa taarifa hizo za kutekwa kwa mwanafunzi huyo na kumtia nguvuni kijana huyo akiwa salama Lamadi wilayani Magu, akiwa na laini ya simu aliyoitumia kumdanganya baba yake kuwa alikuwa ametekwa.
“Tunaendelea kumhoji na uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahak**ani ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake,” alisema Kamanda Muliro.

Katika tukio jingine, Polisi imewak**ata watu watatu kwa kosa la kupatikana na kilogramu 15 za bangi na watuhumiwa wengine wawili kwa kosa la kupatikana na pombe ya moshi lita 33.

Kamanda Muliro alisema tukio hilo ni la kati ya Machi na Aprili katika operesheni kabambe inayoendelea.

Aliwataja watu waliok**atwa na bangi kuwa ni John Marwa (26), Bhoke John (30) na Maria Stephano (25) wote wakiwa ni wakazi wa Kishiri Wilaya ya Nyamagana.

Aliwataja watuhumiwa waliok**atwa na lita 33 za pombe ya moshi kuwa ni Mkemwa Matono (45), mkazi wa Fumagila na Vedastina Tibikunda (30) ambaye ni mkazi wa Bugarika jijini Mwanza.

“Tunaendelea kuwahoji watuhumiwa, na siku hizi mtaona waliok**atwa ni wanawake, siku hizi unakuta mwanamke anasafirisha bangi k**a furushi,” alifafanua. Aliongeza kuwa polisi inaendelea na mahojiano na watuhumiwa watafikishwa mahak**ani pindi uchunguzi utakapokamilika.
News

New world
09/07/2022

New world

17/03/2022

Address

Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Nkubason News posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Nkubason News:

Videos

Share


Other News & Media Websites in Dodoma

Show All

You may also like