Elisha Thompson

Elisha Thompson Elisha Thompson is a Tanzanian Filmmaker especially Documentary films and TV programs.

26/03/2023

UKOMBOZI KWA MATAPELI NA WEZI
MIKOSI inatokana na MAKOSA (Yaana MAKOSA ni mama wa MIKOSI).Kila unapotapeli au kuiba fuatilia huwa kuna mikosi/matatizo yanakutokea.Matatizo unayoyapata wakati mwingine huwa tofauti na kitu ulichoiba au tapeli.unaweza ukakuta umezaa mlemavu, kansa imeibuka katika mwili wako, umepoteza kiungo, kufa, nyumba imeungua, gari limeanguka,umenaswa na umeme, unatembea mti unakuangukia, unateleza bafuni na kupasuka kichwa, nk.Hiyo ni kanuni ya ulimwengu.Badilika usiridhike na kupiga hatua moja alafu unarudi nyuma hatua tano.Wagal 6:7b "kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna"
Rafiki hebu simamisha kupanda MIKOSI.
Hii inahusu hata wale wezi wa kutumia kalamu katika maofisi mbalimbali.
mtibora.blogspot.com

10/09/2022
9:MFUNDISHE MTOTO WAKO KUWAJIBIKAa-Utamfundishaje mtoto kuwajibika? Watoto hupenda kufanya kazi za nyumbani na wazazi, t...
10/08/2022

9:MFUNDISHE MTOTO WAKO KUWAJIBIKA
a-Utamfundishaje mtoto kuwajibika? Watoto hupenda kufanya kazi za nyumbani na wazazi, tumia fursa hiyo.K**a unafanya kazi fulani mpe kakazi kadogo kanako fanana na kazi unayofanya, mfano wakulima huwapa watoto wao kajembe kadogo nao wanakua wanalima pamoja na wazazi.Unapofanya hivyo unakua unachochea vichocheo vya mtoto vilivyoko ndani (plugins), mtoto unapomzuia kufanya kazi, kwamba hawezi au atajichafua unaua vichocheo vyake, atakapokua atachukia kabisa kupika, kufua, kuosha vyombo n.k.kwa hiyo usimzuie mtoto anapolilia kuosha vyombo, kufua n.k. bali mfundishe-dada anapoosha vyomba anamtengea pembene tuvyombo kidogo au nguo kwenye kibeseni kidogo.Hii itamfanya atakapokuwa mkubwa kufanya kazi za nyumbani na kazi za kuingiza kipato, hatakua mvivu(Methali 14:23a Katika kila kazi mna faida.)

b-Usiache mtoto kumpa kazi za nyumbani, kwa kuona kuwa ana kazi nyingi za shule.Inaonyesha watoto wanaopewa kazi za nyumbani, pia hufanya vizuri kazi za shuleni.Kazi za nyumbani zinamjenga mtoto kuwa MZALISHAJI na si MLAJI, zinamjenga mtoto kuwa MTOAJI na si MPOKEAJI. Mtoto aliyefundishwa kuwajibika ataweza kuyamudu maisha yake vizuri.Usimwache mtoto awe tegemezi alafu anapokua mtu mzima unamfungulia akaanze maisha-atashindwa na atarudi nyumbani.Pia mfundishe mtoto jinsi ya kutunza fedha, kutengeneza bajeti ya kwake binafsi hata bajeti ya siku ya nyumbani. Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee….Itaendelea….
mtibora.blogspot.com

8:MFUNDISHE MTOTO WAKO UNYENYEKEVUWagalatia 6:3 Maana Mtu akijiona kuwa ni kitu, na kumbe si kitu, huyo anajidanganya mw...
10/08/2022

8:MFUNDISHE MTOTO WAKO UNYENYEKEVU
Wagalatia 6:3 Maana Mtu akijiona kuwa ni kitu, na kumbe si kitu, huyo anajidanganya mwenyewe.
a-Usimwambie maneno yanayoweza kumfanya anie makuu zaidi ya upeo wake (Mfano all your dream can come true), yaani kila anachotaka katika maisha yake anaweza kukipata.Mtoto ataweza kufanikiwa pale atakapokuwa na malengo yaliyo kadri ya uwezo wake na atakapoyafanyia kazi kwa bidii.
Warumi 12:16b Msinie yaliyo makuu

b-Mfundishe mtoto wako kuomba msamaha.
Msaidie mtoto wako kutambua sehemu aliyokosea na kuomba msamaha.
Pia mfundishe mtoto wako kuwa na shukrani kwa MUNGU ya uumbaji, yeye kuwa hai na kupata mahitaji yote ya asili k**a hewa, maji n.k.Pia Mtoto aweze kushukuru kwa dhati pale anapotendewa mema na wenzake (Wakolosai 3:15c tena iweni watu wa shukrani)
Mtoto anapojifunza shukrani inampelekea kuwa mnyenyekevu.

c-Mfundishe mtoto kutambua na kukubali mwenzake anapomzidi, kwa maana hiyo asione wivu bali ajifunze kutoka kwa mwenzake.Haitakiwi kusema najitahidi ili ni mzidi fulani, bali najitahidi ili niwe katika nafasi nzuri. (Wafilipi 2:3 Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.)

d-Msisitize mtoto kuweka kipaumbele cha kuwasaidie wenzake.
Mshauri mtoto kuwatambua wenzake wenye shida na jadiliana nae atawasaidiaje, ikiwezekana hata wewe mzazi msaidie mtoto kutimiza utumishi huo anapowatambua wenzake wenye shida ambazo ziko juu ya uwezo wake.
Wafilipi 2:4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia nadni ya Kristo Yesu. …….Itaendelea…..
mtibora.blogspot.com

7:MFUNDISHE MTOTO WAKO KUTOKATA TAMAA-KUWA THABITIa-Kwa kumfundisha mtoto uvumilivu kutamfanya hata anapoanguka kusimama...
10/08/2022

7:MFUNDISHE MTOTO WAKO KUTOKATA TAMAA-KUWA THABITI
a-Kwa kumfundisha mtoto uvumilivu kutamfanya hata anapoanguka kusimama tena.Unaweza ukamuuliza mtoto, ukifeli mtihani utafanyaje, sikiliza jibu lake-k**a ni la kukataa tama, mpe mawazo yako ya kumjenga kuwa sio ndio mwisho kwamba anaweza fanya hivi na vile.Kwa hiyo k**a mzazi mtengenezee mtoto vimaswali vingi vya visa mkasa vinavyohusu kuanguka kwake na atafanyaje, au anayemtegemea akiondoka atafanyaje-msikilize majibu yake alafu jadili nae.
(Methali 24:16 maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; bali wasio haki hukwazwa na mabaya)

b-Mfundishe mtoto wako namna ya kujikwamua kwa mifano halisi. K**a mzazi mueleze mtoto historia yako ya ulipofanya makosa ukashindwa na baadae ukajifunza ukarekebisha makosa na kujikwamua katika kikwazo.Mtoto anapotumbukia katika changamoto usikimbilie haraka kumsaidia k**a hakuna madhara ya haraka-bali muulize ehe hapo unafanyeje kujikwamua, au utafanyaje siku nyingine k**a utatumbukia katika changamoto inayofanana na hii.
Methali 9:9 Mwelimishe mwenye hekima naye atazidi kuwa na hekima; mfundishe mwenye haki naye atazidi kuwa na elimu.

c-Mtoto hawezi kujifunza kutembea bila kuanguka.
Mtoto anapofundishwa uvumilivu, kutokataa tamaa, kujifunza kutokana na makosa n.k. mtoto huyu atakapokumbana na vikwazo ataweza kushinda, au atakapoanguka ataweza kusimama tena.Tukumbuke Mtoto hawezi kujifunza kutembea bila kuanguka, kwa hiyo anapoendelea kutengeneza maendeleo ya maisha yake lazima atakumbana na vikwanzo na sehemu nyingine kuanguka lakini atasimama. (Yakobo 3:2a Maana twajikwaa sisi sote katika mambo mengi.)
mtibora.blogspot.com

6:ADHABU KWA MTOTOMtoto anapokosa k**a mzazi unamuonya, akirudia kosa hilo hilo tena mzazi inatakiwa umtandike fimbo, il...
02/08/2022

6:ADHABU KWA MTOTO
Mtoto anapokosa k**a mzazi unamuonya, akirudia kosa hilo hilo tena mzazi inatakiwa umtandike fimbo, ila mzazi utaangalia na hali ilivyo, sehemu nyingine mtoto anaweza rudia kosa hilo hilo ila si kwa makusudi.Ila k**a mtoto anafanya makosa kwa makusudi na uzembe lazima afundishwe kwa viboko.Wakati wa kumchapa mtoto mzazi hakikisha una amani na mtoto ajue anachapwa kwa sababu gani, pia usimchape mtoto hovyo hovyo.Mchape mtoto matakoni, wala si mgongoni au kichwani.K**a utamchapa mtoto hovyo hovyo huku huna amani, hutamsaidia mtoto wako bali ndio utazidi kumpanda uharibifu.
(Mithali 23:13 Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa).Unaona Mtoto anatakiwa umpige au apewa adhabu ya viboko tu, usimpige mtoto kwa mikono unaweza kumuua ndio maana anasema UKIMPIGA KWA FIMBO HATAKUFA .Pia Usimpe mtoto adhabu ya kumchoma moto, kumshindisha njaa, kulima, kuchimba shimo n.k mtoto anatakiwa apewe adhabu ya kuchapwa fimbo tena kwa amani.
Mithali 23:14Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.
Unaona-Mzazi ambaye hutaki kabisa kumchapa mtoto wako kuna sehemu unakua unamsukumia mtoto wako kuzimu.
------Itaendelea-------
mtibora.blogspot.com

Tunaendelea na ujenzi wa watoto wetu-Kipengele cha Malezi.3-MUELEKEKEZE MTOTO AELEWA MATOKEO MABAYA NA MAZURIMtoto aelew...
30/07/2022

Tunaendelea na ujenzi wa watoto wetu-Kipengele cha Malezi.
3-MUELEKEKEZE MTOTO AELEWA MATOKEO MABAYA NA MAZURI
Mtoto aelewe matendo yoyote yana madhara mazuri au mabaya, kwa hiyo k**a atashindwa kujidhibiti/Self control atapata matokeo mabaya.Mueleze mtoto k**a ataweza kujidhibiti atapata matokeo mazuri.Kujidhibiti huleta matokeo mazuri.Hata sisi watu wazima tunajifunza tuwe wavumilivu, watu wengi wapepatwa na mabaya kwa kutojizuia/self control - mfano wengine wameua, ndoa zimesambaratika, mimba zisizo tarajiwa, kupoteza kazi, kufungwa, kufa n.k.
Wagalatia 6:7b kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

4-MUELEKEZE MTOTO WAKO KUWEKA VIPAUMBELE
Kujithibiti/Self control ni pamoja na kuweka vipaumbele.Mtoto wako aweze kuweka kipaumbele kufanya vitu vya msingi.Mfano-akitoka shule afanye mazoezi aliyopewa shuleni kabla ya kuendelea na michezo yake.Hali hiyo itamfanya hata akiwa mtu mzima ataweza kuweka vipaumbele, kufanya mambo ya msingi kwanza katika maisha yake.Wengi wanaopenda anasa, sio wazuri kuweka vipaumbele.Wafilipi 1:10a Mpate kuyakubali yaliyomema;
------Itaendelea-------
mtibora.blogspot.com

LET'S BUILD THE BODY PARTY 2-KIPENGELE CHA MALEZI-WATOTOMfundishe mtoto wako-Wengi hutumia kumfundisha mtoto wakati amek...
26/07/2022

LET'S BUILD THE BODY PARTY 2-KIPENGELE CHA MALEZI-WATOTO
Mfundishe mtoto wako-Wengi hutumia kumfundisha mtoto wakati amekosea, huku mzazi akiwa hana amani na mtoto hana amani.Katika hali hiyo mtoto hawezi kukuelewa wala neno lako litakua halina nguvu.Tenga muda rasmi wa kumfundisha mtoto/watoto wako.Andaa mada za kuwafundisha kutokana na umri wao.Wazazi wengi wamekwepa majukumu haya,wako bize sasa watoto wanaharibika wanageuka kua miiba ya kuwachoma wazazi.Baadhi ya wazazi wanapenda starehe, jioni ukipita nje sehemu za starehe utakuta magari mengi yamepaki-wakati muda huo ungetumika kufundisha watoto.
Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
1:MFUNDISHE MTOTO KWA MUONEKANO WAKO
K**a mzazi mtoto wako anajifunza kwa muonekano wako-namna unavyoishi na mwenzi wako, namna unavyovaa, unavyokula na kunywa-pia namna unavyokabiliana na mambo, jinsi unavyopokea mtoto anapokosea n.k Hakikisha unafanya vizuri. Mtoto anajifunza kwa jinsi ulivyo na kuyavaa maisha k**a yako-ndio maana watoto wa wavuvi wanakuwa wavuvi, wanasiasa wanakua wanasiasa.Kwa hiyo k**a utamfundisha mtoto vizuri wakati unafanya vibaya, kuna hatari akawa mbaya k**a wewe.Mtu alivyo mara nyingi ni kutokana na mazingira yake-labda awe na kiwango kikubwa cha kuyadhibiti mazingira.
2:MFUNDISHE MTOTO NAMNA YA KUJITHIBITI
Mzazi ukisema hapana kwa mtoto maanisha-sio unamkataza kitu fulani ambacho kinaweza kumuumiza alafu anapolilia unampa.Unaposema hapana itamsaidia kujiambia mwenyewe hapana kwa mambo mabaya, au hata kuwaambie wengine hapana kwa kumaanisha anaposhawishiwa kuingia katika madawa ya kulevya, umalaya na vitu vingine hatari.Pia kitendo cha mzazi kusema hapana kinaijenga nafsi ya mtoto kuvumilia, maana unachomkataza yeye alikuwa anakitamani sana, hali hiyo inamjengea kuvumilia vishawishi tangu mdogo.
Mathayo 5:37a Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo;Siyo siyo.

Yaani kujizuia katika vishawishi
Mtoto mwenye kiwango cha juu cha kujithibiti-anaweza kushinda vishawishi hata ambavyo vinaonyesha k**a vina faida, au vishawishi vyenye faida ya muda mfupi, kumbe ni hatari.
Mtoto ambaye hawezi kujidhibiti ni rahisi sana kutumbukia kwenye ukorofi,huzuni, matumizi ya madawa ya kulevya n.k
----Itaendelea-----
mtibora.blogspot.com

MTU AZINIYE NA MWANAMKE HANA AKILI KABISA.Baada ya kupost-maisha yako yalivyo ndio kiwango cha maarifa au elimu yako ili...
23/07/2022

MTU AZINIYE NA MWANAMKE HANA AKILI KABISA.
Baada ya kupost-maisha yako yalivyo ndio kiwango cha maarifa au elimu yako ilivyo-swali lilikuja hivi.
Mbona kuna watu wana Elimu lakini maisha yao mabaya?
Pia anasema wenye Elimu Wanamajivuno.
Jibu langu-Ki ukweli ukiona mtu anajivuna kwa Elimu dunia yake bado mtu huyo hajakamilika katika maarifa/Elimu.Maana Maarifa/Elimu ya Mungu inatuambia “Kila mtu amuone mwenzake bora kuliko yeye”.Kwa ujumla Post hii inazungumzia Elimu aina zote, yaani unatakiwa uwe na Elimu ya Mungu na Elimu ya Dunia.Na kuhusu Elimu Dunia hata k**a hujabahatika kusoma elimu rasmi na kupata vyeti bado unaweza kujifunza maeneo ambayo unashida/maaneo yanayoangamia Mfano unaweza kupata elimu ya ufugaji wa kuku, Elimu ya ndoa, Elimu ya malezi, Elimu ya ujasiliamali n.k.Wewe kijana uliyepata fursa ya kusoma Elimu rasmi soma kwa bidii, lakini pia jifunze na Elimu au maarifa ya Mungu. K**a utasoma vitabu vyooooote lakini hutasoma mambo ya Mungu, kusoma vitabu vya Mungu, kusoma Bibilia na kufuata bado Elimu yako haitakusaidia.Ndio maana unakuta kuna baadhi “sio wote, narudia tena kuna baadhi” hawa walimu wa Mavyuo wanawatishia kuwafelisha watoto wa k**e kwa sababu watoto wa watu wamekataa kuzini nao, na kuna watoto wengine wa k**e wanaogopa na wanakubali kuzini nao.Story hii nilikua nasikia lakini juzi alhamisi 21/07/2022 nimehakikishiwa na muhitimu wa chuo kimoja-jambo lililofanyika kwa muumini mwenzangu mimi ninaeandika-ansema mwalimu huyo wa chuo alimfelisha mtoto huyo wa k**e, aliporudi kufanya mtihani au sapu yake,mwalimua akumuambia bado “LAZIMA U CARRY-yaani arudie somo hilo mwaka mzima”. Basi kale kadada kakaogopa, imani yake ikafeli pale, ikabidi kakubali kuzini na huyo mwalimu.Unafikiri mwalimu k**a huyu jinsi alivyopanda uharibifu nae ategemee nini katika maisha yake-k**a sio kuharibiwa, maana kanuni ni kila mtu atavuna alichopanda. Unaona sasa, waalimu k**a hawa pamoja na Elimu ya kidunia, kwa kuwa wamekataa Elimu ya Mungu bado ni wajinga...

MAISHA YAKO YALIVYO NDIO KIWANGO CHAKO CHA MAARIFA AU ELIMU KILIVYOKiwango chako cha maisha katika eneo la ndoa, uchumi,...
20/07/2022

MAISHA YAKO YALIVYO NDIO KIWANGO CHAKO CHA MAARIFA AU ELIMU KILIVYO
Kiwango chako cha maisha katika eneo la ndoa, uchumi, watoto, afya ya kimwili, afya ya kiroho n.k kinategemeana na kiwango cha Elimu au maarifa uliyonayo au uliyoyapata.Maarifa yanapopungua katika eneo moja la maisha eneo hilo linaathirika.
Hosea 4:6a Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; (Kwa hiyo kazi yako iwe kujifunza mambo ya msingi Elimu Dunia na Elimu ya Mungu.Usipoteze muda kwenye mizaha, muda huo ungetumia kuongeza maarifa na kujenga maisha.)
Mithali 4:13 Mk**ate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.(Unaona Elimu au maarifa ni uzima wako k**a inapungua na uzima unapungua yaani uzima wa uchumi, ndoa n.k.Usifikiri Elimu linawahusu wanafunzi tu hapana, Elimu inahusu wote na ina vipengele mbalimbali, ukikosa elimu ya ndoa, au uchumi au malezi na uzima katika eneo hilo unaondoka ndio pale ndoa zinasambaratika au maadili ya watoto yanaharibika.Unaweza tumia mitandao vizuri kujifunza mambo mazuri na kujenga maisha yako.Kumbuka kiwango cha maarifa au Elimu kinapokua kidogo na afya ya maisha yako katika mzunguko wote unakua mdogo.Tutaendelea kujifunza Body parts nyingine-Kipengele cha Uchumi,Ndoa Malezi, Afya n.k ufanyaje ili visitawi.Nitakupa mtaji wa vipengele hivi kwa ufupi ufupi ila itakusaidia sana, lakini pia utakuwa umepata mwanga wa kuchimba zaidi katika maeneo hayo.
Ili kunifuatilia like page hii.Nimeamuamua kubadilisha account yangu binafsi kuwa page maana watu wamejaa.Account binafsi mwisho ni kuwa na marafiki 5000 ila page ni zaidi ya watu 5000. Asante na karibu.

28/06/2022

NAFASI ZA KAZI
Meira School inatafuta waalimu wanaoweza kufundisha
Masomo mbalimbali wakiwa nyumbani.

Sifa:
-Mwalimu awe na uwezo wa kurekodi masomo yeye mwenyewe kupitia screen recorder au Zoom.

-Aina ya masomo
• Ujasiliamali
• IT
• Afya na mazingira
• Video production
• Graphics designing
• Na masomo mengine

Mawasiliano tuma meseji kupitia facebook, whatsup 0717 163462 au email
[email protected]

Tembelea tovuti yetu:
https://www.meiraschool.com

08/06/2022

Introduction to SPSS SoftwareVisit our website below to watch more SPSS topics such as;-How to create a questionnaire. -Entering data in SPSS software.-Impor...

WEWE NI MWENYE HAKI.Warumi 10:10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, (Hapo ulipo unaamini kuwa una HAKI? Un...
19/03/2022

WEWE NI MWENYE HAKI.
Warumi 10:10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki,
(Hapo ulipo unaamini kuwa una HAKI? Unajua HAKI zako ni nini? Mfano HAKI za mtoto ni kucheza, ulinzi, kuishi, afya bora, lishe bora n.k.Sasa baadhi ya HAKI zako katika neno hili ni Uzima wa roho na mwili, Ulinzi, Baraka, Utajiri, Maisha marefu n.k.Sasa k**a hauamini kuwa una haki maana yake mambo hayo mazuri yanatoweka.Basi k**a umeamini malizia kukiri "mimi ni mwenye HAKI".

IMANI NDIO INAYOKUPA HAKI
(Haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani;-Wafilipi 3:9c)
Haki uliyopata si kwa matendo yako, japo unaendelea kujitahidi kufanya mema.Bali ni Haki uliyopata kwa IMANI kupitia YESU KRISTO.)
Wafilipi 3:9 tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani;
mtibora.blogspot.com

FEDHA RAFIKI MBAYA-UKIMPENDA SHUKRANI YAKE ANAKUUMIZA(1Tim 6:10 Maana shina moja la mabaya  ya kila namna ni kupenda fed...
20/01/2022

FEDHA RAFIKI MBAYA-UKIMPENDA SHUKRANI YAKE ANAKUUMIZA
(1Tim 6:10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi) Usiwe mtu wa kupenda pesa na usifikili watu wenye pesa nyingi woote ndio wanaopenda pesa hapana, hapa haijatajwa kiwango unaweza ukawa na roho ya kupenda pesa hata k**a wewe ni maskini, fukara au tajiri.Wengi wamepata matatizo kwa kutamani kupata fedha ndogo kwa njia isiyo halali.Kujivua/uproot na roho ya kupenda pesa ni kuwa mtoaji wa hicho ulichonacho-kwa kufanya hivyo unakuwa unajivua ktk roho/nguvu mbaya ya kupenda pesa.
mtibora.blogspot.com

UKITAKA WATOTO WAKO WABARIKIWE FANYA HII.Zaburi 37:26 Mchana kutwa hufadhili na kukopesha, Na mzao wake hubarikiwa.Zabur...
18/01/2022

UKITAKA WATOTO WAKO WABARIKIWE FANYA HII.
Zaburi 37:26 Mchana kutwa hufadhili na kukopesha, Na mzao wake hubarikiwa.

Zaburi 37:25 Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula.
(Kumbe matatizo ya watoto wengi chanzo ni wazazi.Wazazi walienda kinyume na mistari hii juu.Basi mzazi uwe mtu wa KUFADHILI na kutenda HAKI basi watoto wako wataishi vizuri,watabarikiwa,watakuwa watoto wazuri katika jamii.Mtoto aliyebarikiwa lazima na tabia yake itakua njema)
mtibora.blogspot.com

POKEA KIFAA CHA KUZIPIMA ROHO1 Yoh 4:1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mun...
30/12/2021

POKEA KIFAA CHA KUZIPIMA ROHO
1 Yoh 4:1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu. (Roho inayotokana na Mungu lazima iwe na UPENDO, ukimchukia mtu mmoja tu roho yako haitokani na Mungu kwani Mungu ni Upendo 1 Yoh 4:7..kila apendaye amezaliwa na Mungu..)Usihukumu watu kuwa freemason, jipime roho yako kwanza.Anasema mtawatambua kwa matunda, (Mathayo 7:16 Mtawatambua kwa matunda yao.) yaani k**a huna matunda ya roho; upendo,upole,fadhili,kiasi,uaminifu,furaha, amani n.k roho yako si ya Mungu.Basi unapojua tatizo ndio kwenye uponyo, fanya malekebisho au omba msaada maana giza haliwezi kujitoa lenyewe au mnyama hawezi kujitoa madoa yake mwenyewe.Roho ya Mungu inatoa matunda haya chini, hakikisha usiwe kinyume matunda haya;
Wagalatia 5:22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23 upole, kiasi; juu ya mambo k**a hayo hakuna sheria.
mtibora.blogspot.com

VITAMIN OF THE DAY PART 6- DONT WORRY GOD IS YOUR PROVIDER.Usiwe na wasiwasi Mungu anakutunza -wewe endelea kujituma kuf...
15/06/2021

VITAMIN OF THE DAY PART 6- DONT WORRY GOD IS YOUR PROVIDER.
Usiwe na wasiwasi Mungu anakutunza -wewe endelea kujituma kufanya kazi, ila wakati mwingine pamoja na kujituma huona k**a kuna mahitaji yanakuzidi na huwezi kuyatatua, sasa usiwe na wasiwasi amin Mungu atayatatua-usiwe na wasiwasi kuhusu ada za shule, kuhusu pango la biashara yako, kuhusu chakula kinaisha ndani, gari limeisha n.k.(Mathayo 6:31 & 32b Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32b kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
mtibora.blogspot.com

Jumamosi njemahttps://youtu.be/BBhzD_Rud4s
05/06/2021

Jumamosi njema
https://youtu.be/BBhzD_Rud4s

Ukitaka ukue katika viwango vikubwa katika kila maeneo yako basi sikiliza somo hili kwa utulivu mpaka mwisho.

VITAMIN OF THE DAY PART 4 - GOD WANTS YOU TO BE RICH(2Wakorinthi 8:9 Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi...
02/06/2021

VITAMIN OF THE DAY PART 4 - GOD WANTS YOU TO BE RICH
(2Wakorinthi 8:9 Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.) Maana yake Yesu alifanyika maskini ili sisi tuwe matajiri katika maeneo yote roho, mwili, ndoa, watoto, ndugu mpaka uchumi wetu.Ndio maana Yesu anamjibu Petro kila mtu aliyeacha ndugu watoto, mashamba atapokea mara mia hapa duniani na kuurithi uzima wa milele-Mat 19:29.Tafakari ili kumiliki.

ANGALIZO-UTAJIRI WA UCHUMI NI HALALI YETU KABISA ILA MBAYA NI KUPENDA FEDHA.
(1Tim 6:10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.) Usiwe mtu wa kupenda pesa na usifikili watu wenye pesa nyingi hao ndio wanaopenda pesa hapana, hapa haijatajwa kiwango unaweza ukawa na roho ya kupenda pesa hata k**a wewe ni fukara.wengi wamepata matatizo kwa kutamani kupata fedha ndogo kwa njia isiyo halali.Jitahidi kuwa mtoaji wa hicho ulichonacho-kwa kufanya hivyo unakuwa unajivua/uproot ktk roho/nguvu mbaya ya kupenda pesa.
mtibora.blogspot.com
https://www.instagram.com/elitson/

VITAMIN OF THE DAY PART 2- GOD PLANS TO PROSPER YOU. Tafakari kutwa nzima Mungu anakuwazia mema.K**a Mungu mwenye Nguvu ...
31/05/2021

VITAMIN OF THE DAY PART 2- GOD PLANS TO PROSPER YOU.
Tafakari kutwa nzima Mungu anakuwazia mema.K**a Mungu mwenye Nguvu anakuwazia mema mabaya hayatakupata. Mungu anakupenda sana sana . Yeremia 29:11 "Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho" (For I know what I have planned for you,' says the Lord . 'I have plans to prosper you, not to harm you. I have plans to give you a future filled with hope.)
mtibora.blogspot.com
https://www.instagram.com/elitson/

THE SECRET-SIRIUnapotafakari maneno ya MUNGU ndio unayaingiza ndani yako na kuyamiliki kufanya kile kilichoandikwa kiten...
29/05/2021

THE SECRET-SIRI
Unapotafakari maneno ya MUNGU ndio unayaingiza ndani yako na kuyamiliki kufanya kile kilichoandikwa kitendeke dhahiri kwako au wewe ubadilike uwe NENO.Ndio maana anasema NENO alifanyika MWILI-muujiza wa neno kufanyika mwili au kitu halisi unaendelea kufanyika hadi hivi leo kwako, SIRI ni kutafakari.Unapo tafakari una SOAK IN/Unaingiza ndani neno la Mungu, Roho ya Mungu/spirit of God, Faith/Imani and POWER of GOD/Nguvu ya Mungu.Angalizo ukiwa na maneno ya Mungu mengi kichwani k**a hutafakari huwezi kupata BIG IMPACT/Matokeo makubwa.Zab 1:2-3.
https://www.instagram.com/elitson/

VITAMIN OF THE DAY PART 1Leo siku nzima tafakari jambo hili huku ukiwa unaendelea na kazi zako, utaona siku yako itakavy...
26/05/2021

VITAMIN OF THE DAY PART 1
Leo siku nzima tafakari jambo hili huku ukiwa unaendelea na kazi zako, utaona siku yako itakavyokuwa nzuri.Neno: MUNGU ANAKUPENDA-unavyoona mama anavyompenda mtoto anambeba, anahangaika nae, sasa Mungu ni zaidi kwako anakupenda sana, k**a mzazi anavyompenda mtoto wake hata akiwa mwizi.Tafakari neno hili kutwa nzima, ukiona mawazo yanataka kuelekea kwingine ambako kunataka kukuumiza na kuondoa amani yarudishe kabla hayajachanganya.Tafakari kwa mapana-UPENDO unakuaje, Mtu akipenda kitu inakuaje, sasa Mungu ananipenda.Yoh 3:16-17
mtibora.blogspot.com

YOU ARE THE ONE WHO MAKE YOUR DAY GOOD OR BADWewe ndiye unayeifanya siku yako kuwa nzuri au mbaya.Kila sekunde inayopita...
23/05/2021

YOU ARE THE ONE WHO MAKE YOUR DAY GOOD OR BAD
Wewe ndiye unayeifanya siku yako kuwa nzuri au mbaya.Kila sekunde inayopita wewe ndio mchaguzi wa mema au mabaya.Kuwa makini kufanya maamuzi mazuri kila sekunde inayopita.Maamuzi hayo huanzia unakubaliana na mawazo gani yanayokujia kila sekunde ukiwa mwenyewe au mawazo unayoletewa au maneno unayonena.
"Kumb 30:15 Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya" Uchaguzi ni wako.
mtibora.blogspot.com

YOU ARE THE ONE WHO MAKE YOUR DAY GOOD OR BADWewe ndiye unayeifanya siku yako kuwa nzuri au mbaya.Kila sekunde inayopita...
23/05/2021

YOU ARE THE ONE WHO MAKE YOUR DAY GOOD OR BAD
Wewe ndiye unayeifanya siku yako kuwa nzuri au mbaya.Kila sekunde inayopita wewe ndio mchaguzi wa mema au mabaya.Kuwa makini kufanya maamuzi mazuri kila sekunde inayopita.Maamuzi hayo huanzia unakubaliana na mawazo gani yanayokujia kila sekunde ukiwa mwenyewe au mawazo unayoletewa au maneno unayonena.
"Kumb 30:15 Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya" Uchaguzi ni wako.
mtibora.blogspot.com

SHARTI LILILOJIFICHA KWA AJILI YA UPONYAJI WA MWILI WAKO. September 08, 2020   Mungu anataka kukuponya lakini ili akuponye shariti lake ni hili; (Warumi 8: 11…Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu katika wafu ataihuisha na miili ...

YOU BUILD YOUR LIFE FROM YOUR MOUTHYaani hivyo ulivyo; afya yako, ndoa, uchumi, maisha yako kwa ujumla ni matokeo ya uli...
22/05/2021

YOU BUILD YOUR LIFE FROM YOUR MOUTH
Yaani hivyo ulivyo; afya yako, ndoa, uchumi, maisha yako kwa ujumla ni matokeo ya ulivyojitamkia wewe mwenyewe.Usijitamkia maneno mabaya k**a; mimi msahaulifu, mimi kichaa, mimi hazinitoshi, mimi siwezi, mimi mgonjwa, mimi mjinga, mimi sina kitu n.k
Kuanzia sasa jitamkie mema tu."Mithali 18:21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake"
mtibora.blogspot.com
desertfilm.co.tz

"YOU ARE WHAT YOU EAT"Yaani ulivyo wewe ni matokeo ya ulichokula.Iwe maradhi,umaskini,utajiri,chuki,amani n.k. Yote ni m...
14/05/2021

"YOU ARE WHAT YOU EAT"
Yaani ulivyo wewe ni matokeo ya ulichokula.Iwe maradhi,umaskini,utajiri,chuki,amani n.k. Yote ni matokeo ya ulichokula, kula kwenyewe ni ulichosikia, ulichosoma, ulichoona, na ulichokula chakula halisi kupitia mdomoni kwako.
Kuanzia sasa kuwa makini na vitu unavyoangalia, unavyosoma,unavyosikia na vyakula halisi unavyokula kupitia mdomoni.Hakikisha unakula vitu vyenye afya ili uwe na afya maeneo yote.
www.mtibora.blogspot.com

Address

P. O BOX 208 DODOMA
Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Elisha Thompson posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category



You may also like