13/01/2023
FISI WALIOUWA WATOTO MWANZA WAULIWA:
Mwishoni wa Mwezi Desemba mwaka 2022, mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitatu alishambuliwa na kisha kuliwa na Fisi katika kijiji cha Mwangika wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza.
Mtoto huyo aliyekuwa ameenda kucheza na wenzake umbali kidogo na nyumbani kwako, alivamiwa na fisi huyo na kisha kuondoka nae hata baada ya watoto wenzake kupiga kelele wakihitaji msaada tayari Fisi huyo hakupatikana na badala yake wanakijiji na wazazi wa mtoto huyo baada ya kufanya msako waliambulia vipande vya mabaki mwili wa ya mtoto huyo.
Aidha kutokea kwa tukio la kuogofya kijijini hapo kuliibua hisia nzito kiasi cha kwamba, wananchi wa kijiji hicho kuanza kuogopa kwenda mashambani kutokana na kile kilichofanyika.
Kutokana na kutawala kwa hofu hiyo, ofisi ya mkuu wa wilaya ya kwimba aliaandaa kikosi cha askari wa wanyama pori ili kiweze kuja kuwasaka wanyama hao, hali iliyopelekea kutokuambulia Fisi hata mmoja kupatika.
Hata hivyo mara baada ya jitihada hizo kukwama uongozi wa serikali ya kijiji walijipinga kitafuta kikosi kingine cha watu wapatao 70 na mbwa 80 maalumu kinachotumia dawa za kienyezi kwa ajili ya kuja kuwaawa wanyama hao.
Kikosi hicho kilidumu kwa siku nne tu na kufanikiwa kuuwa fisi 9