FGA Tv

FGA Tv Official Facebook account for Fountain Gate Academy Online Tv. Get in touch via our social media pl

Rais wa Fountain Gate Academy Ndg Japhet Makau (Wa kwanza Kushoto) akiambatana na Msimamizi Mkuu wa Shule za Fountain Ga...
04/01/2025

Rais wa Fountain Gate Academy Ndg Japhet Makau (Wa kwanza Kushoto) akiambatana na Msimamizi Mkuu wa Shule za Fountain Gate Ndg Joseph Mjingo (Wa Pili kushoto) pamoja na Viongozi wengine yupo hapa kwenye Bonanza la wafanyakazi wake katika Uwanja wa Shule ya Msingi Maisaka Babati mkoani Manyara.

Bosi amesema ni siku maalumu Kwa wafanyakazi kufurahi, kucheza, kunywa na kufurahi Kwa pamoja.





Mchezo wa kwanza wa Mpira wa miguu ulikuwa kati ya FGA Staffs dhidi ya Timu ya H/Mji ya Babati.Mchezo huo umetamatika Kw...
04/01/2025

Mchezo wa kwanza wa Mpira wa miguu ulikuwa kati ya FGA Staffs dhidi ya Timu ya H/Mji ya Babati.

Mchezo huo umetamatika Kwa FGA Staffs kuibuka na ushindi wa 1-0.

Tuko mbashara kabisa kwenye YouTube channel yetu ya FGA TV.



Unajua kuvuta kamba wewe? Hivi ndivyo ushindani ilivyokuwa kwenye mchezo wa kuvuta kamba ndani ya Bonanza la wafanyakazi...
04/01/2025

Unajua kuvuta kamba wewe? Hivi ndivyo ushindani ilivyokuwa kwenye mchezo wa kuvuta kamba ndani ya Bonanza la wafanyakazi wa Fountain Gate Academy.

Tuko mbashara kabisa kutoka hapa Fountain Gate Manyara ndani ya Chaneli yetu ya FGA TV pale YouTube.

Wafanyakazi wanaendelea na ushiriki wao kwenye michezo mbalimbali.Mpaka Sasa Michezo iliyochezwa ni Kukimbiza kuku,  Kuk...
04/01/2025

Wafanyakazi wanaendelea na ushiriki wao kwenye michezo mbalimbali.

Mpaka Sasa Michezo iliyochezwa ni Kukimbiza kuku, Kukimbia na Gunia, pamoja na riadha.

Michezo mingine inaendelea.

Tuko pia mbashara katika YouTube channel yetu ya FGA TV.

Bonanza la FGA GET TOGETHER linafanyika hapa Babati mkoani Manyara huku wafanyakazi wa Fountain Gate Academy wakiwa wame...
04/01/2025

Bonanza la FGA GET TOGETHER linafanyika hapa Babati mkoani Manyara huku wafanyakazi wa Fountain Gate Academy wakiwa wamechangamka mapema tu.

Bonanza linafanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Maisaka Babati mjini.



Imekuwa siku njema kwa wakazi wa Babati mkoani Manyara kwani wafanyakazi wa Fountain Gate Academy wamepita katika maeneo...
03/01/2025

Imekuwa siku njema kwa wakazi wa Babati mkoani Manyara kwani wafanyakazi wa Fountain Gate Academy wamepita katika maeneo mbalimbali kuzungumza na wakazi hao juu ya uwepo wa Shule ya Awali na Msingi Fountain Gate Manyara iliyopo maeneo ya Mruki.

Wafanyakazi kazi hao wamepita Maeneo ya Bonga, Singe, Mruki, Mrara, Majengo ya zamani, Majengo mapya, Sinai, Sawe, Mkoani, Block X, Hangoni na Kwere kueneza habari za Shule hiyo ambayo zamani ikifahamika k**a Shule ya Awali na Msingi Rift Valley.

2025 HILI NI CHIMBO JIPYA 🔥🔥.



Baada ya wafanyakazi wa Fountain Gate Academy kuwasili Babati mkoani Manyara katika Shule ya Awali na Msingi Fountain Ga...
03/01/2025

Baada ya wafanyakazi wa Fountain Gate Academy kuwasili Babati mkoani Manyara katika Shule ya Awali na Msingi Fountain Gate Manyara, Kimefanyika kiako kiufupi baada ya kupata challah.

Kikao hiko kilichoongozwa na Msimamizi wa Shule za Fountain Gate Ndg Joseph Mjingo kilikuwa maalumu kuwakaribisha wafanyakazi wa Fountain Gate Academy kutoka Ihumwa Dodoma na Mlimwa C Dodoma ambapo wakiambatana na wafanyakazi wa Fountain Gate Malawi.

Kumbuka Babati itasimama Kwa muda Kwa ajili ya FGA GET TOGETHER.

2025 HILI NI CHIMBO JIPYA 🔥.



Disemba 30, 2024 kulilipotiwa tukio la Bondia Hassan Mgaya kufariki dunia baada ya kupigwa TKO katika pambano la raundi ...
03/01/2025

Disemba 30, 2024 kulilipotiwa tukio la Bondia Hassan Mgaya kufariki dunia baada ya kupigwa TKO katika pambano la raundi sita lililofanyika Tandale kwa mtogole, ambalo halikua la ubingwa dhidi ya aliyekuwa mpinzani wake Paulo Elias.

Katika hali ya kusikitisha ripoti zinaeleza kwamba Hassan alikubaliana na Promota wa pambano hilo malipo yangelikuwa ni Shilingi za kitanzania 60,000.

Je ni malipo halali Kwa mchezo wenye hatari k**a huu?

2025 HILI NI CHIMBO JIPYA 🔥🔥.

Real Madrid wanajua kuwa Kila mchezaji Duniani ni ndoto yake kucheza kwao, yaani hilo halipingiki wao ndio watawala wa S...
03/01/2025

Real Madrid wanajua kuwa Kila mchezaji Duniani ni ndoto yake kucheza kwao, yaani hilo halipingiki wao ndio watawala wa Soka la Dunia kwenye ngazi ya Klabu.

Linapokuja suala la wao kuhitaji huduma ya Mchezaji huwa wameweka Misingi yao ambayo huwatamanisha wachezaji hao kuona ni Timu ya ndoto zao. Nyuma ya haya Yuko mwamba mmoja hivi Juni Calafat ambaye ni skauti Mkuu wa Klabu.

Sasa wamehamia Kwa mlinzi wa Pembeni wa Liverpool Trent-Alexander Anord. Anord tayari ameonyesha nia ya kujiunga na Real Madrid tayari na ukizingatia mkataba wake unaenda ukingoni msimu huu, basi hata hawazi kabisa huku wakiwa wanapambana kumpa mkataba mpya.

Madrid wamepeleka ofa ya Euro 25M. Liverpool wanaonekana kuwa wagumu kukubali ofa hiyo LAKINI hapa wanaweza kujikuta hawaambulii kitu chochote.

Msimu ukiisha Anord anakuwa huru, nini maana yake? Real Madrid watampata Trent Kwa pesa sifuri kabisa, yaani wachague wao.

2025 HILI NI CHIMBO JIPYA.

✍️



Msafara wa Fountain Gate Academy tawi la Dodoma umefika Kondoa na kupumzika Kwa Dakika kadhaa kabla ya kuendelea na safa...
03/01/2025

Msafara wa Fountain Gate Academy tawi la Dodoma umefika Kondoa na kupumzika Kwa Dakika kadhaa kabla ya kuendelea na safari kuelekea Babati mkoani Manyara Kwa ajili ya GET TOGETHER.

Manyara TUNAKUJA🔥🔥🔥

Leo wafanyakazi wa Idara zote za Taasisi ya Fountain Gate Academy tawi la Dodoma wanasafiri kuelekea Babati mkoani Manya...
03/01/2025

Leo wafanyakazi wa Idara zote za Taasisi ya Fountain Gate Academy tawi la Dodoma wanasafiri kuelekea Babati mkoani Manyara Kwa ajili ya tukio kubwa la GET TOGETHER.

Hii ni maalumu Kwa ajili ya kuwakutanisha wafanyakazi wa Idara zote pamoja na kuweza kufurahi baada ya kazi kubwa ya Mwaka 2024 na kuianza vyema safari Mwaka 2025.

Safari hii imedhaminiwa na Rais wa Fountain Gate Academy Ndg Japhet Makau Kwa kushirikiana vyema na uongozi mzima wa Fountain Gate Academy.

BABATI TUNAKUJA 🔥🔥🔥

2025 HILI NI CHIMBO JIPYA




"Kabla ya kufanya kazi na Arne Slot sikudhani k**a yuko vizuri hivi. Lakini baada ya kuanza kufanya nae kazi Wala sikush...
03/01/2025

"Kabla ya kufanya kazi na Arne Slot sikudhani k**a yuko vizuri hivi. Lakini baada ya kuanza kufanya nae kazi Wala sikushangazwa nilitegemea hili hapo sikumfikiria Kwa ukubwa"

"Ni mzuri kwenye kuchambua mambo hasa madogo, na Wala sio mbinafsi pale anapokosea yuko Bora sana kwenye mbinu".

Mohammed Salah mshambuliaji wa Liverpool juu ya ubora wa Kocha wao Arne Slot.

2025 HILI NI CHIMBO JIPYA.



Nyota wa Tanzania Clara Luvanga na timu yake ya Al Nassr FC mpaka sasa wamekusanya alama 27 baada ya kushinda mechi zote...
02/01/2025

Nyota wa Tanzania Clara Luvanga na timu yake ya Al Nassr FC mpaka sasa wamekusanya alama 27 baada ya kushinda mechi zote 9 za mzunguko wa kwanza Ligi Kuu ya Wanawake Saudi Arabia, wakik**ata nafasi ya 1 kwenye msimamo.

Clara na wenzake wameonyesha nia ya kuutetea ubingwa wa Ligi Kuu nchini humo ambao pia waliitwaa msimu uliopita.

2025 HILI NI CHIMBO JIPYA

“Quality ya wachezaji wa Yanga na Tabora inafanana sisi Yanga tunatofautiana Rangi tu wao wana kijani na Njano sisi tuna...
02/01/2025

“Quality ya wachezaji wa Yanga na Tabora inafanana sisi Yanga tunatofautiana Rangi tu wao wana kijani na Njano sisi tuna Nyeupe ila wachezaji wetu na wao ni Sawa ndio Maana tumewafunga 3 hakuna timu imewafunga Yanga 3 Azam Fc wao wamewafunga lakini ni 1 na sisi tumewafunga Azam Fc 2-1.

Nikizungumza quality yetu na wao ni moja tunakubaliana hata Benchi la ufundi la Yanga linalingana tena unaweza kuta tumewazidi”

Afisa Habari wa Tabora United Christina Mwagala akizungumza na Mwandishi wa Habari wa Wasafi.

2025 HILI NI CHIMBO JIPYA 🔥🔥

.fc

Mshambuliaji wa Klabu ya Fountain Gate Seleman Mwalimu yupo katika wakati mgumu Kwa Sasa kufuatia hali ya majeruhi anayo...
02/01/2025

Mshambuliaji wa Klabu ya Fountain Gate Seleman Mwalimu yupo katika wakati mgumu Kwa Sasa kufuatia hali ya majeruhi anayoipitia kwa Sasa.

Hiyo imefanya apitwe kwenye orodha ya ufungaji na mshambuliaji wa Singida Black Stars Elvis Rupia mwenye magoli Nane huku hapo Awali k**a hajaumia alikuwa ndiye kinara akiwa na Magoli Sita.

Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara imekwenda mapumziko mpaka Mwezi Machi Mwaka huu huku inaweza kutoa faida Kwa Selemani Mwalimu kurejea katika hali nzuri na kuongeza upinzani kwenye kufumania nyavu.



Rais wa Fountain Gate FC na Mkurugenzi wa Fountain Gate Academy Ndg Japhet Makau akitoa salamu zake ya Mwaka Mpya. 2025 ...
02/01/2025

Rais wa Fountain Gate FC na Mkurugenzi wa Fountain Gate Academy Ndg Japhet Makau akitoa salamu zake ya Mwaka Mpya.

2025 HILI NI CHIMBO JIPYA.



Nimeona wadau na Mashabiki wa Simba wamezielekeza hasira zao Kwa bwana mdogo Ladack Chasambi hasa mara baada ya kusema h...
01/01/2025

Nimeona wadau na Mashabiki wa Simba wamezielekeza hasira zao Kwa bwana mdogo Ladack Chasambi hasa mara baada ya kusema hakuna mchezaji ndani ya Simba anayemuona k**a Role model wake.

Alienda Kwa Majira zao na kumchagua Max Mpia Nzengeli 'Mbappe wa Kindu'. Hilo lImewanyima raha Mashabiki wa Simba huku maswali yakiwa kwanini achague mchezaji kutoka kwa mahasimu wao, Ni mawazo yake asilaumiwe.

Shida Iko hapa, Chasambi hakufahamu k**a kuwahusisha mahasimu wao kwenye mazungumzo yake k**a kuna athari yoyote. Bila shaka kwake alijua yuko huru kuzungumza lolote lile.

Simba ina Idara ya Habari na mawasiliano inayoongozwa na Ahmed Ally. Ahmed Ally na wenzake ni Gatekeepers wa Klabu ya Simba (Gatekeeping theory) yaani hawatakiwi kuruhusu hali yoyote ya sintofahamu inayosababishwa na mawasiliano itokee.

Je, wanawafundisha Hawa wachezaji Kujua Kipi cha kuzungumza na kipi hakifai kuzungumzwa mbele ya vyombo vya habari? Je, Kuna Misingi gani wameiweka kuzuia taharuki k**a hii iliyotokea?

Kumbe basi k**a hayo yangefanyika kusingekuwa na mambo k**a haya.

Kabla ya kumlaumu Chasambi anzeni na Ahmed Ally na jopo lake.

Heri ya Mwaka Mpya.

✍️

2025 HILI NI CHIMBO JIPYA.



Ripoti kutoka ndani ya Manchester United zinaeleza Kiungo wa Timu ya Taifa ya Brazil Casemiro hayuko kwenye Mipango ya K...
01/01/2025

Ripoti kutoka ndani ya Manchester United zinaeleza Kiungo wa Timu ya Taifa ya Brazil Casemiro hayuko kwenye Mipango ya Kocha Ruben Amorim.

Casemiro rasmi anaingia kwenye orodha ya wachezaji watakaoachwa wakati wa dirisha kubwa la usajili.

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when FGA Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to FGA Tv:

Videos

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Videos
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share