16/10/2024
Mwanzoni kabisa, Sylivester Stallone alikuwa mwigizaji aliyefulia kabisa katika vigezo vyote vya kuchalala. Kuna wakati alifulia hadi akaiba mkufu wa mkewe na kuuza. Mambo yalimuwia magumu hadi ikafika mahali hana mahala pa kuishi. Ndio, kwa siku 3 alilala kwenye kituo kikubwa cha mabasi cha New York. Kutokana na kushindwa kulipa kodi na kushindwa kujinunulia chakula. Hali yake ilifikia mahali pagumu kabisa hadi akalazimika kumuuza mbwa wake kwa dola $25 pekee. Anasema siku hiyo aliondoka akilia machozi.
Wiki mbili baadae, alitazama pambano kali la ngumi kati ya Mohammed Ali na Chux Wepner na lile pambano lilimpa hamasa ya kuandika skripti ya filamu maarufu, ROCKY. Aliandika hii skripti kwa saa 20! Akajaribu kuiuza na akapata ofa ya dola $125,000 kwaajili ya skripti pekee. Lakini Stallone alikuwa na OMBI MOJA TU. Alitaka kuigiza nafasi ya STAR kwenye ile movie. Alitaka kuwa MUIGIZAJI MKUU, Rocky mwenyewe. Lakini studio wakamwambia HAPANA. Walitaka kutumia MUIGIZAJI MAARUFU.
Walisema, "alionekana k**a kichekesho na aliongea k**a masihara." Akaondoka na skript yake. Wiki kadhaa baadae, ile studio ikampatia ofa ya dola $250,000 kwaajili ya ile skripti pekee. Akaikataa. Wakaongeza tena ofa ikawa dola $350,000. Bado akaikataa tena. Walitaka filamu yake, lakini hawakumtaka yeye. Akasema, HAPANA. NI LAZIMA AICHEZE HIYO FILAMU.
Baada ya kitambo kidogo, ile studio ikakubali, wakampa dola $35,000 kwaajili ya skripti na wakakubali awe nyota wa ile filamu! Baada ya hapo kilichotokea ni historia! Filamu ikashinda kipengele cha filamu bora, kipengele cha filamu iliyoongozwa vizuri, kipengele cha filamu bora iliyo editiwa vizuri kutoka kwa taasisi kubwa maarufu ya kutuza kazi za sanaa na wasanii ya Oscar Awards. Pia Stallone alitajwa kuwania tuzo ya MUIGIZAJI BORA! Na filamu ya ROCKY ikaingizwa katika kumbukumbu ya filamu bora nchini Marekani k**a moja ya filamu bora kabisa kuwahi kutengenezwa!
HAKUNA ANAYEJUA UNACHOWEZA KUFANYA ZAIDI YAKO WEWE MWENYEWE! Watu watakupima kutokana na MUONEKANO wako. Na kupitia VITU ulivyonavyo. Lakini Wewe Endelea Kupambana! Pambania nafasi yako kwenye historia. Pambania utukufu wako. USIWAHI ASILANI KUKATA TAMAA!
Hata k**a itamaanisha kuuza vitu vyako na kuishi katika mazingira magumu, NI SAWA! Lakini UNGALIPO HAI, STORI YAKO BADO HAIJAISHA.
Endelea kupambana! Endelea kuamini katika ndoto zako na kujipa tumaini. Pambana Utafanikiwa!!!
Asante kwa kusoma na kushea ππΏππΏππΏ