Jeshi la Israel laua watu zaidi ya 29 baada ya kuishambulia hospitali Gaza
Powered By: @maembe_motors & @e360mart_
Mo Music ameachia wimbo mpya, 'Mimi Na Wewe', akishirikiana na @VanillahMusic kutoka @KingsMusicRecords, baada ya ukimya wa muda mrefu. Wimbo huu unaleta matumaini kwa mashabiki wa @mo_musictz, ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu. Tayari wimbo huu unapatikana kwenye majukwaa ya kidigitali.
Urusi imeipatia Belarus makombora ya "Oreshnik" kama sehemu ya ushirikiano wao wa kijeshi unaoendelea. Hatua hii inalenga kuimarisha uwezo wa ulinzi wa Belarus huku ikiashiria mshikamano wa karibu kati ya mataifa haya, hasa katika muktadha wa mvutano na nchi za Magharibi.
Powered By: @e360mart_
Baba Levo amempongeza msanii wa @KondeGang, Ibraah, kwa kuachia EP yake mpya 'Air Piano', yenye nyimbo saba, ikiwemo 'Leo' aliyoimba na @Harmonize_tz,. EP hiyo, iliyotolewa Disemba 6, 2024, imeonyesha juhudi za Ibraah, huku Baba Levo akisisitiza kuwa inathibitisha kuwa Ibraah ana uwezo wa kubishana muziki wake unopokosolewa.
Baba Levo ameonyesha furaha yake kwa mchango wa Harmonize kwenye ulingo wa bururdani na muziki nchini Tanzania. @officialBabaLevo amefichua kuwa @Harmonize_tz na yeye wanapendana, pia amekuwa akimpa pesa kila mwezi kwa ajili ya michezo yao maalum.
Baba Levo amemsisitiza Harmonize kumsaidia msanii @Ibraah_tz, ambaye yupo chini ya lebo ya Harmonize, @KondeGang ili kufikia viwango vya kimataifa.
Baba Levo, ametangaza rasmi tamasha kubwa la vichekesho lijulikanalo kama 'Wana Stand Up', linalotarajiwa kuwashirikisha wachekeshaji wengi maarufu kutoka Tanzania.
Tamasha hili litafanyika Disemba 20, 2024, katika ukumbi wa Mlimani City, kuanzia saa 11 jioni hadi saa sita usiku. Tukio hili limekusudiwa kutoa burudani kwa mashabiki wa vichekesho, huku likiwa ni jukwaa la kuonyesha vipaji vya wachekeshaji wa Tanzania.
Mashabiki wanatarajiwa kushuhudia shoo iliyotawaliwa na wachekeshaji wenye vipaji adimu. Baba Levo amesisitiza kuwa tamasha hili litakuwa ni tukio la kihistoria Tanzania.
Ni zaidi ya ubunifu tangazo la Serengeti Lite na Diamond Platnumz
Umelichungulia tangazo jipya la @DiamondPlatnumz na @serengetibeer? Kampeni ya Lite Your Imagination inalenga kuleta mapinduzi ya kifikra kwenye ubunifu hasa kwa vijana wenye ndoto za kufanya makubwa kwenye career walizochagua. Kutazama zaidi tangazo hilo tembelea page ya @serengetibeer. #LiteYourImagination
Msanii wa Afropop kutoka Rwanda, @BruceMelodie, ameachia wimbo “Niki Minaji” akishirikiana na kundi maarufu la Afrika Kusini, @BlaqDiamond. Wimbo huu, uliorekodiwa Kigali, ni mchanganyiko wa Amapiano na Afropop, ukionyesha ujumbe wa upendo wa kipekee.
Bruce pia ametangaza albamu yake ya kwanza, 'Colorful Generation', itakayotoka mapema 2025, ikiwa na kolabo na wasanii wakubwa kama Joeboy, Bien, na Shaggy. Albamu hii itaadhimisha utofauti wa muziki wa Kiafrika huku ikiimarisha nafasi ya Bruce kama msanii wa kimataifa.
Mwaka huu, Bruce amefikisha streams milioni 150 na kushinda tuzo ya Msanii Bora wa Rwanda kwenye Trace Awards. Ana mpango wa ziara Afrika kutangaza albamu yake mpya na kusambaza muziki wa Rwanda ulimwenguni.
Usijisumbue na wasiwasi wa ubora na usalama wa gari unalonunua. Maembe Motors wanakuhakikishia usalama wa pesa zako. Tembelea ukurasa wao wa Instagram @maembe_motors na chagua gari lako leo.
Infinix wamekuja na ofa kabambe! Unaponunua Infinix HOT 50 Pro+, simu nyembamba zaidi katika daraja la kati, utapata Infinix XE 28 Earbuds kwa kuongeza TZS 10,000 tu, na kufanya bei kamili kuwa TZS 510,000 badala ya TZS 547,000.
Pia, utapata ofa ya GB 96 za intaneti kutoka Tigo pamoja na warranty ya mwaka mzima.
Promotion hii inafanyika nchi nzima.
Ratiba ya week hii:
••Tarehe 2 watakuwa Mkoa wa Mwanza kituo Dampo center.
••Tarehe 3 Kahama soko la Mkulima.
••Tarehe 5 na 6 Arusha Bus terminal.
••Trh 6 Moshi stendi.
Kwa taarifa zaidi tembelea @infinixmobiletz
John Waryuba, Mkurugenzi Mtendaji wa @Tushiya.Foundation, amezindua rasmi taasisi hiyo Jana, Alhamisi, Desemba 5. Lengo kuu la Tushiya Foundation ni kuwapa vijana mafunzo maalum yanayolenga kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kujipatia ajira kwa ujumla.
Muasisi na Mwenyekiti Mtendaji wa @ccawardsafrica, Dkt. Diana Simon Laizer, @dr_dianalaizer ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima katika Biashara na Ujasiriamali (Honorary Doctorate in Business and Entrepreneurship) na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Oxford, nchini Uingereza.
Sherehe ya kutunukiwa ilifanyika Jumatatu, jijini London, ambapo Dkt. Diana alitambuliwa kwa mchango wake mkubwa kupitia Consumer Choice Awards Africa (CCAA) chini ya uongozi wake mahiri.
Akielezea kupewa heshima hiyo, Dkt. Diana alisema:
"Namshukuru Mungu Mwenyezi kwa kuniongoza kila hatua katika safari hii. Mafanikio haya ni kwa ajili ya vijana wote duniani wanaotamani kufikia viwango vya juu katika taaluma na maisha kwa ujumla. Haijalishi umetoka katika mazingira yenye bahati au ya kawaida, unaweza kuwa chochote unachotamani maishani mradi tu uwe na malengo thabiti."
Consumer Choice Awards Africa, iliyoanzishwa mwaka 2019 nchini Tanzania, imeendelea kupanua wigo wake. Mwaka huu, tuzo hizo zimetolewa nchini Kenya, Malawi, na Afrika Kusini, huku mipango ikiendelea kuzipeleka katika nchi nyingine za Afrika.
Tuzo hizi zimekuwa jukwaa muhimu la kutambua ubora wa bidhaa na huduma barani Afrika, zikiongozwa na maono thabiti ya Dkt. Diana Simon Laizer, ambaye sasa anatambuliwa kama mmoja wa viongozi wa kipekee katika sekta ya biashara na ujasiriamali.