07/05/2022
MAMBO 7 YANAYOUA MAISHA YAKO YA MAOMBI.
1. Kula kupita kiasi: Kula zaidi ya lazima usiku kutadhoofisha tu mwili wako.
2. Usingizi: Ni lazima uufundishe mwili kulala kidogo na kukesha. Usingizi unamaliza nguvu zako za kuomba. Ukweli ni kwamba, Usingizi mwingine ni mashambulizi kutoka kwa adui.
3. Uchafu wa roho na nafsi: Ponografia/picha chafu, mazungumzo/story za ngono na mawazo machafu ni wauaji wa stamina ya maombi. Mtu wako wa ndani atashindwa kila wakati k**a utamlisha mtu wako wa roho na vitu vichafu na vya kuchukiza.
4. Mazingira mabaya: Mazingira unayounda na kujikuta ni muhimu sana. Ikiwa wewe ni miongoni mwa wadhaifu wa maombi, masengenyo na waumini wa kimwili moto wako wa maombi utakufa. Kusengenya na kusengenyana kunaweza kukukatisha tamaa.
5. Kulisha vibaya mtu wako wa ndani. Ikiwa mtu wako wa roho hajashiba vizuri huwezi kuwa bingwa wa maombi. Husikilizi mahubiri, ni vigumu sana kusoma neno au makala za Kikristo basi maisha yako ya maombi yatakufa njaa.
6. Wasiwasi/Woga/Hofu: Hakuna mwenye masumbufu katika Moyo anakuwa shujaa wa maombi. Unapaswa kuua wasiwasi wako Ili uweze kupata stamina ya maombi.
7. Kukengeushwa kupitia kutazama TV, uraibu/addiction wa mitandao ya kijamii na Uraibu kwa mke au mume au rafiki . Fanyia kazi maisha yako ya maombi.-Dk. Myles Munroe