03/02/2019
NEVER DOUBT JESUS/KAMWE USIMTILIE SHAKA YESU.
Mwezi November na December 2018 ni miezi ambayo sitaisahau haraka kwenye maisha yangu kwa sababu mbali mbali. Sababu ya kwanza ni Changamoto au mashindano ya nafsini ambayo nilipitia, hii ilikuwa ni changamoto kubwa. Ya pili ni changamoto mbali mbali za maisha ya kawaida nilizopitia katika maisha yangu ya kila siku zikawa kubwa na zenye kunisababishia msongo wa mawazo.
Katika kipindi hicho, mashindano yaliibuka ndani yangu, sauti ikisema nami wazi kabisa kwamba sitamaliza mwaka 2018. Kwamba sitavuka tarehe 27/12/2018 (Ndugu zangu wanaelewa umuhimu wa tarehe hii kwangu na familia kwa ujumla). Katika kipindi hicho nikaanza kupata maumivu ya kichwa k**a vile msumari ukichoma ndani ya kichwa upande wa kulia. Hali hii ikawa ikijirudia rudia na Ile sauti ikiendelea kuongea ndani yangu kwamba sitamaliza mwaka, kwamba nitakufa kabla ya tar 27/12.. hali hii ikazidi hata ikaanza kuumba hofu ndani yangu. Nikawa naanza kutafakari maisha yangu na wanangu na jinsi watakavyoishi bila mimi.. Jinsi Mke wangu atakavyopata shida, jinsi huduma itakavyoendelea bila mimi... je nitakumbukwa kwa jambo gani, na mambo mengine mengi sana. Hali ile ya kuumwa kichwa iliendelea kunisumbua kwa zaidi ya wiki 3 katika mwezi Disemba
Nikiwa katika hali hiyo, ndani yangu sauti ya upole ikainuka na kuanza kunikumbusha mambo ambayo Mungu amenishindia nyakati mbali mbali katika maisha yangu, jinsi ambavyo Mungu ameniponya Magonjwa zaidi ya mara 3 kwa Kuomba katika roho.. kwa kupambana na hiyo Roho ya ugonjwa kwa maombi.. Mwaka 2013, 2017 hata 2018. Hiyo sauti ikanihamasisha kwa upole, . Taratibu nikaanza kuzitafakari shuhuda za uponyaji niliopata kwa Bwana.. Imani ikaumbika ndani yangu. Nikasema k**a Mungu aliniponya mara zote tatu, hawezi niacha leo. Siku ya tar 27/12/18, kweli yale maumivu yaliendelea kichwani Mwangu, yakanisumbua, nakasikia msumari unachoma upande wa kulia ndani kichwani.
Siku hiyo Ilikuwa ni siku ya ibada na tulikuwa na ratiba ya Maombi ya kufunga mwaka kanisani. Nikiwa kanisani roho ikaamka kupambana ndani yangu... nikaweka worship music kwenye simu yangu, earphones masikioni, nikiwa kanisani. Nikaanza kuomba katika Roho, kunena kwa Lugha na kuomba Zaburi 103. After 40 Minutes of intense Prayer, Msumali ukachomoka, maumivu ya kichwa yakaondoka, nikapata uponyaji. Mumivu hayo hayakurudi tena toka saa hiyo. Nimevuka mwaka salama, niko hai, namtukuza Yesu Kristo.
Mathayo 11:1-6, Luka 7:18-23 Yesu Vs Yohana Mbatizaji
Habari hii ni kuhusu Yohana Mbatizaji ambaye alituma wanafunzi wake kuuliza habari za Yesu kwamba Yeye ndiye Masihi au tusubiri Mwingine? Nimejifunza mambo kadhaa kwenye habari hii ambayo yanahusiana na kichwa cha ushuhuda huu.
👉 Yohana hakuwa Mgeni na Yesu, alimfahamu vema kibinadamu (Note Mariamu mama wa Yesu na Elizabeth Mama wa Yohana walijuana vema k**a ndugu)
👉Yohana alikuwa nabii mkubwa sana, wa kiwango cha juu kuliko manabii wote kwa kuwa alikuwa na wito wa kumwandalia njia Kristo na alipewa kumtambua Kristo Kiroho na kumtambulisha kwa ulimwengu.
👉 Yohana ndiye alimtambulisha rasmi Kristo k**a mwanakondoo wa Mungu.. akatambua kwamba yeye anapaswa kupungua/Kunyenyekea ili Yesu Kristo azidi/huduma yake ichukue nafasi
It bothered me so much kuona Nabii huyu Mkubwa akiingiwa na hofu na kutuma watu kuuliza k**a Yesu ndiye Masihi au tumtazamie Mwingine. Nikagundua kwamba Matarajio ya Yohana juu ya Mwenendo wa Kristo, taabu aliyokuwa akipitia, vyanzo vya habari alizopewa na wanafunzi wake akiwa gerezani vyote vilichangia kumbadili kabisa fikra yake, kumtia mashaka kiasi hata kumwondolea imani na kumkatia tamaa Yesu Kristo.
Na ndivyo ilivyo mpaka sasa, matarajio uliyonayo toka kwa Kristo au juu ya Kristo, Mazingira na Changamoto unazopitia, Aina ya watu/Sauti unazosikiliza, vyote vinaweza kukuondolea au kukujengea imani kuhusu Kristo.
Majibu ya Yesu pia yalinifundisha jambo
👉 Yesu hakujibu swali aliloulizwa na Yohana. Alifanya matendo, mambo makubwa na kuwaagiza waliotumwa kwenda kumweleza Yohana kile walichoona na kusikia.
👉 Uamuzi wa kuamini au kutokuamini ulikuwa juu ya Yohana, kutokuamini kwake kusingebadili chochote.. wala kuathiri chochote.
👉 Alichosema Yesu Mstari wa 6 (Matt 11:6) na Luka 7:23 kimenipa kutafakari na kujenga hiki ninachokushuhudia. Yesu anasema "Heri Mtu Yule asiyechukizwa nami." Lugha inayotumika kwenye kiingereza tafsiri yake ni
LESSONS
👉 Yesu unayemtilia shaka ataendelea kuwa Yesu Kristo, habadilishwi wala kupungua chochote kwa kuto kuamini kwako. Usipomwamini ni kwa hukumu yako na uharibifu wako wewe mwenyewe.
👉 Yesu unayemkatia tamaa ataendelea kuponya, kufungua, kuokoa, kuweka huru, kuabudiwa na kutukuzwa siku zote. Hapati hasara.
👉 Yesu unayemkatia tamaa ataendelea kuaminiwa, ukikata tamaa na kurudi nyuma ni kwa hasara yako binafsi.
👉 Yesu unayemkatia tamaa hatashughulika kujibu maswali yako ya mashaka, ni juu yako kuamini katika ukuu wake na uweza wake. Hata Usipomwamini ataendelea kuaminiwa..
👉 Yesu halazimiki kutenda k**a unavyotaka ili kukufurahisha, atafanya vile apendavyo siku zote, ni juu yako kukubaliana naye au kumwacha.
Chagua kuamini leo, Chagua kupambana na kila sauti inayokusudia kujenga mashaka ndani yako juu ya uaminifu wa Yesu Kristo, Upendo wake, na nguvu zake. Timiza wokovu wako leo kwa kuogopa na kutetemeka.
Mwamini Yesu Kristo na hata siku moja usiruhusu shetani aumbe mashaka ndani yako hata ukamkatia tamaa Mwana wa Mungu. Fight a good fight of faith. Mshike Yesu usimwache.
Ndani yake tunaishi, tunakwenda na kuwa na uhai wetu (Acts 17:28)
JESUS CHRIST IS LORD/YESU KRISTO NI BWANA.
Shalom
Pst. Nathan K. Daimon
The Greater Light of Glory
Dar es salaam, Tanzania