Muyombo TV

Muyombo TV The Oasis of News Africa

  Shirikisho la Soka la Senegal limetoa taarifa rasmi ya kuachana na kocha wao Mkuu wa timu ya Taifa hilo Aliou Cisse.Ba...
02/10/2024

Shirikisho la Soka la Senegal limetoa taarifa rasmi ya kuachana na kocha wao Mkuu wa timu ya Taifa hilo Aliou Cisse.

Baada ya kuwa na matokeo yasiyoridhisha ndiyo imepelekea Taarifa ya uamuzi huu kutolewa na Shirikisho la Soka la Senegal.

Shirikisho la Soka la Senegal kwa sasa linawapa kipaumbele makocha wa ndani kuliko makocha wa kigeni katika kutafuta kocha mkuu mpya.

Aliou Cissé alikuwa kocha mkuu wa Senegal tangu 2015. Aliiongoza SENEGAL kucheza mechi mbili mfululizo za Kombe la Dunia na kuwaongoza hadi kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza mwaka wa 2021.

Katika AFCON 2023, Senegal ilitolewa katika hatua ya 16 bora.



🇰🇪🇺🇬🇹🇿
🇰🇪🇺🇬🇹🇿

  Zaidi ya watu 100 wanatarajiwa kumshtaki mwanamuziki wa rap Sean 'Diddy' Combs kwa unyanyasaji wa kingono, ubakaji na ...
02/10/2024

Zaidi ya watu 100 wanatarajiwa kumshtaki mwanamuziki wa rap Sean 'Diddy' Combs kwa unyanyasaji wa kingono, ubakaji na kutumiwa vibaya kingono .

Wakili Texas,Tony Buzbee aliwaambia waandishi wa habari kuwa baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa waathirika ni pamoja na watoto wadogo ambao walinyanyaswa walipokuwa na umri wa miaka tisa.

Wakili anayemwakilisha Combs, Erica Wolff alisema rapa huyo amekanusha madai hayo na kusema madai ni ya uongo na yenye lengo la kumuharibia sifa.



🇰🇪🇺🇬🇹🇿
🇰🇪🇺🇬🇹🇿

  Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameahidi kuwa Iran italipa gharama kubwa kwa kufanya shambulio la makombora...
02/10/2024

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameahidi kuwa Iran italipa gharama kubwa kwa kufanya shambulio la makombora dhidi ya Israel Jumanne hii. Akizungumza kutoka kwenye mkutano na baraza lake la usalama la kisiasa, Netanyahu alisisitiza kuwa Iran imefanya "kosa kubwa" na kuahidi kuwa litalipwa.



🇰🇪🇺🇬🇹🇿
🇰🇪🇺🇬🇹🇿

  Msanii nyota kutoka Nchi ya Marekani    anatarajiwa kutua Nchini Afrika Kusini kwa mara nyingine baada ya miaka 10, am...
02/10/2024

Msanii nyota kutoka Nchi ya Marekani anatarajiwa kutua Nchini Afrika Kusini kwa mara nyingine baada ya miaka 10, ametangaza kuwa atatumbuiza katika uwanja wa FNB Jijini Johannesburg, Disemba 14 mwaka huu.

Tiketi za show hiyo ya Breezy zimeanza kuuzwa na bei ya chini ni (R 600) TSh. 94,170/= na tiketi ya juu zaidi ambapo utakaa kwenye Lounge ya Hall Of Fame ni (R 5.744.25) sawa na TSh. 901, 789/=



🇰🇪🇺🇬🇹🇿
🇰🇪🇺🇬🇹🇿

  Rapa Sean 'Diddy' Combs ameripotiwa kuwa anataka kukata rufaa kwa mara ya tatu ili kupata dhamana kutoka gerezani ikiw...
02/10/2024

Rapa Sean 'Diddy' Combs ameripotiwa kuwa anataka kukata rufaa kwa mara ya tatu ili kupata dhamana kutoka gerezani ikiwa ni wiki mbili zimepita tangu kukamatwa kwake.

Mwanamuziki huyo anayekabiliwa na Mashtaka mbalimbali ikiwemo ulaghai na usafirishaji wa binadamu imeelezwa kuwa tayari ameongeza nguvu ya Wanasheria wawili akiwemo Anthony Ricco na Alexandra Shapiro ili kuongeza nguvu kwenye kesi yake.



🇰🇪🇺🇬🇹🇿
🇰🇪🇺🇬🇹🇿

   Mwanamuziki wa Marekani anayetamba kwa miondoko ya R&B Chris Brown huenda akakumbana na Mashtaka ya unyanyasaji wa ki...
02/10/2024

Mwanamuziki wa Marekani anayetamba kwa miondoko ya R&B Chris Brown huenda akakumbana na Mashtaka ya unyanyasaji wa kingono kwa wanawake.

Chris Brown sasa anakabiliwa na mashtaka ya unyanyasaji wa kingono hii ni baada ya mwanamke mmoja kuibuka na kudai kuwahi kufanyiwa unyanyasaji na msanii huyo maarufu Duniani.

Kupitia Documentary mpya (Chris Brown A History of Violence) ambayo inatarajiwa kutoka Oktoba 27 mwaka huu, kuna ushahidi wa matukio ya kinyanyasaji yaliyowahi kufanywa na msanii huyo tangu tukio la kumpiga aliyewahi kuwa mpenzi wake mwanadada Rihanna mwaka 2009.

Katika trela ya Documentary hiyo mshtaki mpya ambaye utambulisho wake umefichwa anasikika akisema “Sikuwahi kuzungumza jambo hili hadharani lakini nadhani sasa ni wakati sahihi na hii ndiyo namna pekee anaweza kusimamishwa”



🇰🇪🇺🇬🇹🇿
🇰🇪🇺🇬🇹🇿

  Aston Villa na West Ham zinajiandaa kuwasilisha ofa ya Pauni 25 milioni kwenda Valencia kwa ajili ya kumsajili mshambu...
02/10/2024

Aston Villa na West Ham zinajiandaa kuwasilisha ofa ya Pauni 25 milioni kwenda Valencia kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo, Mhispania Hugo Duro, 24, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Duro ameonyesha kiwango bora tangu msimu uliopita hali iliyozivutia timu nyingi kutaka kumsajili. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028 na kuna uwezekano akahamia Ligi Kuu England msimu ujao.



🇰🇪🇺🇬🇹🇿
🇰🇪🇺🇬🇹🇿

  Klabu ya Manchester United imeshinda rufaa yao ya kadi nyekundu ya Bruno Fernandes dhidi ya Tottenham.Hii inampa ruhus...
02/10/2024

Klabu ya Manchester United imeshinda rufaa yao ya kadi nyekundu ya Bruno Fernandes dhidi ya Tottenham.

Hii inampa ruhusa Bruno kucheza mechi zijazo.



🇰🇪🇺🇬🇹🇿
🇰🇪🇺🇬🇹🇿

  Erling Haaland mchezaji wa Manchester City ameweka rekodi ya kibabe kwenye Uefa Champions League,▫️ michezo 41 ▫️ maba...
02/10/2024

Erling Haaland mchezaji wa Manchester City ameweka rekodi ya kibabe kwenye Uefa Champions League,

▫️ michezo 41
▫️ mabao 42

Huyu jamaa ni goli mashine 🙌



🇰🇪🇺🇬🇹🇿
🇰🇪🇺🇬🇹🇿

  Usiku wa leo Arsenal watacheza mchezo wao wa kwanza wa nyumbani wa kampeni ya Ligi ya Mabingwa Jumanne hii ya October ...
01/10/2024

Usiku wa leo Arsenal watacheza mchezo wao wa kwanza wa nyumbani wa kampeni ya Ligi ya Mabingwa Jumanne hii ya October 1 dhidi ya mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint-Germain (PSG).

Mchezo huu utapigwa kuanzia majira ya saa 4 usiku. Nani kuibuka na ushindi usiku wa leo?



🇰🇪🇺🇬🇹🇿
🇰🇪🇺🇬🇹🇿

  Mara baada ya kuibuka na ushindi timu ya Al Nassr, inayoshiriki Ligi kuu Saudia Ronaldo akaendeleza rekodi yake ya kut...
01/10/2024

Mara baada ya kuibuka na ushindi timu ya Al Nassr, inayoshiriki Ligi kuu Saudia Ronaldo akaendeleza rekodi yake ya kutupia kamba nyavuni.

Al Nassr 2️⃣ ➖ 1️⃣ Al Rayyan

⚽ 45' Sadio Mane (🎯 Al Ghannam)
⚽️ 76' Ronaldo (🎯 Ghareeb)
⚽️ 87' Roger Guedes (🎯 Bencharki)

Cristiano Ronaldo amefikisha mabao 9️⃣0️⃣4️⃣ katika Maisha yake ya soka.

Takwimu zake msimu huu:

🏟️ Mechi: 10
⚽ Mabao: 9
🅰️ Assists:2

Umri wake ni miaka 39



🇰🇪🇺🇬🇹🇿
🇰🇪🇺🇬🇹🇿

  Klabu ya Wekundu wa Msimbazi  imemtambulisha rasmi nyota wake mpya Kiungo Mshambuliaji Matata, Mpanzu Elie Nkibisawala...
01/10/2024

Klabu ya Wekundu wa Msimbazi imemtambulisha rasmi nyota wake mpya Kiungo Mshambuliaji Matata, Mpanzu Elie Nkibisawala.

Naskia huu ndio Ubaya Ubwela Wenyewe sasa 🙌



🇰🇪🇺🇬🇹🇿
🇰🇪🇺🇬🇹🇿

   Gwiji wa soka wa Cameroon  ’o amepigwa marufuku na Shirikisho la Mpira Duniani (FIFA) siku ya leo Jumatatu kutohudhur...
01/10/2024

Gwiji wa soka wa Cameroon ’o amepigwa marufuku na Shirikisho la Mpira Duniani (FIFA) siku ya leo Jumatatu kutohudhuria michezo yoyote ya timu ya taifa kwa miezi sita.

Eto’o, ambaye amekuwa rais wa shirikisho la soka la Cameroon tangu 2021, alikabiliwa na mashtaka mawili kutokana na tukio la Kombe la Dunia la Wanawake wa U-20 nchini Colombia mnamo Septemba 11.

FIFA haikueleza undani wa kilichotokea katika mchezo wa hatua ya 16 bora ambao Brazil walishinda dhidi ya Cameroon 3-1 baada ya muda wa ziada.

Eto’o alivunja sheria za kinidhamu zinazohusiana na “tabia ya kukera na ukiukaji wa kanuni za mchezo wa haki” na utovu wa nidhamu wa maafisa.

“Marufuku aliyowekewa Bw. Eto’o inamzuia kuhudhuria mechi za wanaume na wanawake zinazohusisha (Cameroon) timu za makundi na umri,” FIFA ilisema katika taarifa.



🇰🇪🇺🇬🇹🇿
🇰🇪🇺🇬🇹🇿

  Timu ya PSG imemuondoa winga wake  Ousmane Dembélé kwenye kikosi chao cha UEFA Champions League kwaajili ya mechi yao ...
30/09/2024

Timu ya PSG imemuondoa winga wake Ousmane Dembélé kwenye kikosi chao cha UEFA Champions League kwaajili ya mechi yao dhidi ya Arsenal kutokana na masuala ya kinidhamu

Uamuzi huo umekuja baada ya Dembele kuzozana na meneja Luis Enrique baada ya mechi yao dhidi ya Rennes.



🇰🇪🇺🇬🇹🇿
🇰🇪🇺🇬🇹🇿

  Kwa mujibu wa Hyper Man wa Staa wa Muziki kutoka Nchini Nigeria   amedokeza kuwa Staa huyo na Mke wake   wanatarajia k...
30/09/2024

Kwa mujibu wa Hyper Man wa Staa wa Muziki kutoka Nchini Nigeria amedokeza kuwa Staa huyo na Mke wake wanatarajia kufanya sherehe ya Harusi ya Tatu na itakuwa bora na yenye kuvutia kushinda iliyopita ambayo ilipewa jina na na ya sasa itaitwa .



🇰🇪🇺🇬🇹🇿
🇰🇪🇺🇬🇹🇿

  Mchezaji nyota    ametangaza rasmi kustaafu soka la Kimataifa. Griezmann hatoichezea tena timu ya taifa ya Ufaransa. “...
30/09/2024

Mchezaji nyota ametangaza rasmi kustaafu soka la Kimataifa.

Griezmann hatoichezea tena timu ya taifa ya Ufaransa.

“Nimeufunga huu ukurasa mzuri wa maisha yangu, asanteni kwa kumbukumbu zote.” amesema nyota huyo mwenye umri wa miaka 33.

Griezmann alianza kuitumikia Les Bleus mwaka 2014, akicheza jumla ya michezo 137 na kufunga mabao 44. Mwaka 2018 aliiwezesha Ufaransa kutwaa Kombe la Dunia na mwaka 2022 kukamata nafasi ya pili.



🇰🇪🇺🇬🇹🇿
🇰🇪🇺🇬🇹🇿

  Kocha Mkuu wa timu ya Manchester United, Eric Ten Hag amesema; “Sifikirii kuhusu kufutwa kazi hata kidogo. Sote tulifa...
30/09/2024

Kocha Mkuu wa timu ya Manchester United, Eric Ten Hag amesema;

“Sifikirii kuhusu kufutwa kazi hata kidogo. Sote tulifanya uamuzi wa kuwa kitu kimoja”.

"Wamiliki, wafanyakazi, wachezaji, mimi mwenyewe. Tulifanya uamuzi kutokana na mapitio ya wazi ya kile tunachopaswa kufanya”.

“Tulijua kuwa itachukua muda. Tuko kwenye ukurasa mmoja pamoja”.

FT: Man Utd 0-3 Spurs



🇰🇪🇺🇬🇹🇿
🇰🇪🇺🇬🇹🇿

  Jean Charles Ahoua amehusika kwenye magoli 5 kati ya 9 ambayo Simba imefunga katika mechi 3 za ligi kuu ya NBC . Amefu...
27/09/2024

Jean Charles Ahoua amehusika kwenye magoli 5 kati ya 9 ambayo Simba imefunga katika mechi 3 za ligi kuu ya NBC . Amefunga goli 1 na kutoa pasi za usaidizi (Assist) 4. Na hapo bado anaizoea ligi 🙌

Huyu ndio MVP wa Simba msimu huu 🦁



🇰🇪🇺🇬🇹🇿
🇰🇪🇺🇬🇹🇿

Address

Boko
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Muyombo TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Muyombo TV:

Videos

Share

Category