CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimepasuka rasmi baada ya Makamu Mwenyekiti wake Tundu Lissu, kutangaza nia ya kugombea uenyekiti unaoshikiliwa na Freeman Mbowe, aliyedumu kwenye kiti hicho kwa miaka 20.
Awali Lissu alitangaza kutetea nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti, lakini amebadilisha mtazamo wake, badala yake akamuandikia barua Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, akimuarifu uamuzi wake wa kuitaka nafasi ya juu kabisa katika chama hiki cha upinzani.
Uamuzi wa Lissu kuitaka nafasi hiyo imetajwa kama sehemu ya kuendeleza joto na mpasuko kutokana na baadhi ya wadau wa chama hicho kuamini ni Mbowe tu anayeweza kushikilia kiti cha Mwenyekiti wa Chadema.
“Mzee Edwin Mtei na Mzee Bob Makani hawakutaka kukaa madarakani mpaka watakapolazimishwa kuondoka kwa aibu. Waliandaa utaratibu wa kuondoka madarakani kwa hiari yao,” Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema.
Maneno ya Lissu kuhusu viongozi kungángánia madaraka ni kama kejeli kwa Mwenyekiti wake Mbowe, aliyeshikilia nafasi hiyo kwa miaka 20 huku kila anayetangaza nia ya kuitaka nafasi hiyo kutimuliwa kwenye chama hicho.
VIDEO:
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imefanya mageuzi makubwa kwenye Katiba ili kuendelea kuimarisha ushiriki na kuongeza ufanisi wa sekta binafsi nchini.
Akizungumza leo Desemba 12, 2024 jijini Dar es Salaam kwenye kikao na wahariri na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Raphael Maganga amesema maboresho hayo yalipitishwa na mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika tarehe 20 Novemba, 2024.
Maganga amesema maboresho hayo yamefanywa kwa kuzingatia maazimio ya kikao cha 13 na 14 cha Baraza la Taifa la Biashara cha tarehe 7 Juni, 2022 na 9 Juni, 2023, ambayo pamoja na mambo mengine Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliagiza kufanyika kwa maboresho hayo kama anavyomnukuu, "Taasisi za Sekta Binafsi nchini ziimarishe uhusiano miongoni mwa wadau wa sekta binafsi na taasisi zao zisomane/zishirikiane, waimarishe miiko na maadili ya sekta binafsi (Private Sector code of Conduct."
"Hivyo kama TPSF tuliona agizo la Mh. Rais ni muhimu sana katika kuhakikisha sekta binafsi nchini ina uratibu madhubuti wa vyama vya biashara, inakuwa sekta inayotii sheria, na yenye nidhamu (Coordinate, disciplined and Compliant Private Sector)." ameongeza Maganga.
Aidha amesema katika maboresho hayo, jina la taasisi hiyo limebadilishwa kuwa Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector Federation - TPSF) badala ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector Foundation - TPSF) ili kuondoa mkanganyiko uliokuwepo juu ya taasisi hiyo kuonekana kama shirika la kutoa misaada (charity).
Vilevile Shirikisho hilo, litaongozwa na Baraza la Uongozi (Governing Council) ambalo litashughulika na wanachama na changamoto zao, na chini yake kutakuwa na Kamati Tendaji (Executive Committee).
Pia, kutakuwa na wawakilishi wa kongani 25 sawa na wale wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) badala ya konga 10 za awali, ambapo sasa katika kila kila konga kutakuwa na makundi mengine madogo (sub clusters) zenye wanachama walio kwenye kundi moja kuweza kuku
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, amenyimwa Ukumbi wa kufanyia mkutano wake Makao Makuu ya Chadema kutokana na mgogoro wa kuwania uenyekiti ndani ya chama hicho na kulazimika kutangaza nia yake ya kuwania nafasi ya Uenyekiti katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Uamuzi wa Lissu wa kufanyia mkutano wake Mlimani City ulikuja saa chache baada ya kunyimwa ukumbi ndani ya Makao Makuu ya chama chao, hali inayoendeleza joto la mgogoro Chadema.
“Kwa jinsi tu minyukano jinsi ilivyo katika mitandao huko, tungefanyia Makao Makuu ingeweza kuleta sintofahamu. Tumekuja huku ili niwe na uwezo na uhuru wa kuzungumza na nyie wote bila hofu.
“Miezi michache iliyopita kuna bwana mmoja alitangaza nia ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa chama chetu na kama sikosei alitangazia nia hotelini pamoja na kwamba yeye ni Mwenyekiti wa Kanda ya Victoria,”Tundu Lissu Mgombea Uenyekiti Chadema.
Mgogoro wa Chadema unatokana na uwepo wa kambi mbili zinazomuhusisha Mwenyekiti wake Freeman Mbowe na Lissu wakichuana kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema.
Hapo zamanı Morogoro ulikuwa ni moja ya mikoa yenye Viwanda vingi Tanzania kabla ya kushuka kwa hadhi yake.
Maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Morogoro inarudisha hadhi yake ya Viwanda na kushindana na mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
#MaonoYaSamia
#Morogoro
Tanzania imeibuka na Tuzo 14 kwenye tuzo kubwa za utalii Duniani za World Travel Awards kipengele cha Afrika
Kwenye Tuzo hizi Tanzania ilichukua tuzo ya African Leading Destination (Sehemu Inayoongoza kwa utalii mwaka 2024), Africa's Leading Festival & Event Destination 2024 (Eneo bora la kufanya matamasha na matukio ya utalii Afrrika) ikipewa Zanzibar, Tanzania, Africa's Leading Tourist Board 2024 (Bodi Bora ya Utalii Afrika) ikipewa Bodi ya Utalii Tanzania TTB. Kivutio bora cha utalii ikapewa mlima Kilimanjaro na Mbuga Bora ya utalii ikapewa Serengeti National Park.
Gosheni Safari’s, wamepata tuzo ya Kampuni bora ya uendeshaji utalii barani Afrika (Africa's Leading Tour Operator 2024), Kampuni ya utalii inayowajibika Afrika 2024 (Africa's Responsible Tourism Award 2024) amepata Twiga Tours, Wakala bora wa utalii Afrika 2024 (Africa's Leading Travel Agency 2024) amepata Blueberry Travel.
Tuzo ya Africa's Leading Luxury Tented Safari Camp 2024 amechukua Siringit Serengeti camp huku Africa's Leading Luxury Safari Lodge 2024 akipewa &Beyond Grumeti Serengeti River Lodge, Tanzania, Africa's Leading Luxury Safari Company 2024 ikapewa kampuni ya &Beyond kutoka Tanzania.
Tuzo ya Kisiwa bora cha utalii imepewa kisiwa cha Thanda cha mafia, Tanzania, tuzo ya wakala bora wa usafiri wa burudani Afrika (Africa's Leading Leisure Travel Agency 2024) imeenda kwa Satguru Travel huku kampuni bora ya kukodisha magari ya biashara kwa Afrika mwaka 2024 (Africa's Leading Business Car Rental Company 2024) tuzo yake imeenda kwa kampuni ya Budget.
Haya ni matokeo ya uwekezaji mkubwa uliofanywa kwenye sekta ya utalii Pamoja na kuitangaza Tanzania nje ya nchi tangu kufanyika filamu ya Tanzania The Royal Tour iliyofanywa na rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan mwaka 2022.
#SamiaApp
#Utalii
Huduma ya Msaada wa kisheria bure "Mama Samia Legal Aid Campaign" inayoendelea kutolewa na Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imeshafikia jumla ya wananchi 409,638 kote nchini, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha upatikanaji wa msaada wa kisheria kwa umma.
Kampeni hiyo imezinduliwa rasmi Mkoani Iringa na itatekelezwa kwa siku 10 mfululizo, kuanzia leo hadi tarehe 19 Disemba 2024.
Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Peter Serukamba, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Mhe. Ibrahim Ngwada, ameeleza kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuimarisha upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria na kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu sheria na haki za binadamu, hasa haki za wanawake na watoto.
Amesisitiza kuwa kampeni hiyo inahusisha ushirikiano mkubwa kati ya Serikali na wadau mbalimbali wa kisheria, ili kuhakikisha huduma za msaada wa kisheria zinawafikia wananchi popote walipo.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Franklin Jasson Rwezimula, amesema kuwa kampeni hiyo ni ya kitaifa na inaendelea kutekelezwa kwa ushirikiano wa ngazi za kitaifa, kimkoa, na Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
Dkt. Rwezimula amesema kuwa huduma hiyo inalenga kuwafikia wananchi wa mikoa yote 26 ya Tanzania, ambapo tayari mikoa 7 imeshapata huduma hiyo.
Kesho, tarehe 11 Desemba 2024, kampeni hiyo itazinduliwa rasmi mkoani Mara, baada ya hapo, itazinduliwa mkoani Songwe tarehe 12 Desemba 2024, kisha mkoani Morogoro, Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa wananchi wa mikoa yote ya Tanzania wanapata huduma za msaada wa kisheria kabla ya kumalizika kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Kampeni hiyo ni hatua muhimu katika kuboresha upatikanaji wa haki za kisheria na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu haki zao, kutatua migogoro ya aina mbalimbali ili kuwezesha jamii kuwa na ufanisi zaidi katika utawala wa sheria
Rais wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan alishiriki kwenye filamu ya Tanzania The Royal Tour iliyozinduliwa Aprili 19, 2022 na kutangaza fursa za utalii na uwekezaji zilizopo Tanzania. Rais Samia aliamini Filamu hiyo ingechangia kukua kwa sekta ya utalii na kuongeza idadi ya watalii kutoka nje na ndani ya nchi.
Watalii wameongezeka kutoka Watalii 1,409,800 mwaka 2020/21 hadi kufikia 3,784,214 mwaka 2023/24 lengo ni kufikia Watalii 5,000,000 mwaka 2025/2026. Pia imechangia Pato la Taifa kutoka asilimia 14.9 mwaka 2020/21 hadi kufikia asilimia 17.2 lengo ni kufikia asilimia 18.9. Royal tour imeongeza fedha za kigeni kutoka asilimia 5.3 mwaka 2020/21 hadi kufikia asilimia 25 mwaka 2023/24 lengo ni kufikia asilimia 27
#MaonoYaSamia
#SamiaApp
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA - Bara, Tundu Lissu, amesema maneno ya baadhi ya watu wanaomshambulia mitandaoni hayamuogopeshi wala kumfanya asiendele na majukumu yake ya kisiasa, huku akisema kuwa anatembea na risasi mgongoni, hivyo hawezi kutishwa na maneno ya aliowaita Mashujaa wa mitandaoni.
Akijibu swali la Mwandishi wa Habari leo, Desemba 10, 2024, jijini Dar es Salaam, aliyehoji msimamo na kauli ya Lissu kuhusu wanaompiga mawe mitandaoni,
“Watakaoniambia Mbowe ondoka ni wanachadema hawa, watakaoniambia Mbowe gombea ni wanachadema hawa na viongozi wangu. Tutaelewana mambo yetu ya ndani yanawahusu nini? mie nashangaa tu mitandaoni yaani pilipili usizokula za kuwashia nini” Feeman Mbowe-Mwenyekiti wa Chadema Taifa.
“Kila siku mnazungumza mnadanganywa, ni hivi mazungumzo katika mambo ya Kijamii upende usipende ni fiche ya lazima. Niwape mfano kule mashariki ya kati Israel wanapigana na Palestina na kwingineko na mamia ya watu wanauwawa lakini ni wangapi mnajua vita inapoendelea kule nchini QATAR-DOHA kuna mazungumzo ya kutafuta amani yanaendelea?” Feeman Mbowe-Mwenyekiti wa Chadema Taifa.
“Kauli za ndani kwamba hakuna maandalizi, sikilizeni Jamani acheni kudakia vitu vidogo vidogo yaani vile vya uchimvi uchimvi. Inawezekana kila mmoja ana mtazamo tofauti, hiki ni Chama cha Siasa kuna watu wenye mitazamo tofauti lakini kuna maeneo tunakubaliana na kuna maeneo tunaweza tukabishana, na huo ndiyo ubinadamu wenyewe” Feeman Mbowe-Mwenyekiti wa Chadema Taifa.
“Manaibu Makatibu Wakuu na nyinyi kwa sababu tunakwenda kuimarisha hasa upande wa mabalozi wa kisiasa. Na mabalozi wengi wa upande wa kisiasa, kwenye ubalozi kuna aina mbili professional na wa kwangu wanaoniwakilisha huko. Tunawarudisha ili ili waje watuunge mkono kwenye kampeni za Uchaguzi huku,”Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan