Goli bora la wiki limefungwa na Mzize dhidi ya TP Mazembe. Acha tusubiri mechi nyingine kama kuna lingine zuri zaidi ya hili.
Baleke naye yupo jukwaani kuwashuhudia Yanga.
Hawa TP Mazembe mbona lama wamejiamini sana, wanapiga na kitenesi swafi kabisa.
Denis Nkane huyu alikuwa Mbappe siyo Mbappe, Msuva siyo Msuva, Diaz siyo Diaz, Yamal siyo Yamal. Yaani alikuwa dogo anayeupiga mno.
Huyu hapa MOTM, inashangaza eeh? Siyo kawaida hata kidogo.
Prince Dube kumbe alikuwa na hat trick yake matatizoni. Amerudi na kasi ya ajabu sana.
Simba wanaongoza kundi kwa matokeo ya wenzie. Sema kundi gumu hili dah!
Takwimu: Simba 1-1 Sfaxien. Simba wamefanya kila kitu kwa bora kuwazidi Sfaxien, wameshdnwa kuongoza mechi.
Kikosi cha Yanga dhidi ya TP Mazembe. Huu ni utabiri wangu, Kibwana aanze badala ya Kibabage kwani siyo mechi ya kuwa wazi kila saa Job amepona? Aanze na Bacca leo.
Mzize amepona pia aanze mbele Mazembe hawatakiwa huru kuanzia nyuma kwani Mzize ni mzri kuanza pressing hadi kuzia, kama hayupo fit 100% basi aingie mapema kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Dube.
Chama aanze, hii mechi inahitaji akili kubwa ambazo siyo flop, Chama hajashuka kiwango akianza na mshambuliaji mbele na pembeni wat wanaokimbia ndo utaona ubora wake.
Pacome na Maxi wakimnie pembeni na kurudi, wakati mwingine waongeze idadi ya viungo katikati hasa wakati wa kuzia.
Aucho amepona, aanze leo na Mudathir Yahya, tmu itakuwa na pivot ya maana sana katikati na interval ya viungo itatoa mwanya kwa washambuliaji kukaa eneo husika wakati wa kushambulia.
Djigui Diarra, mara ya mwisho alionekana kama anamwa wengi hawakujua hata wapinzani MC Algiers hawakujua pengine. Hakucheza mchezo wake wa kisasa alikaa sana golini hakuchezesha timu. Leo anahitajika afanye tabia yake. Wasiwasi ni kama bado ana lile tatizo la sirisiri ndo Yanga inaweza haipo comfortable ikiwa na mpira nyuma.
Farid Musa, Aziz Ki, Boka Chadrack (kama amepona) na wengine muda wowote wanachukua nafasi kipindi cha pili
Kila la kheri Yanga 🇹🇿 .
Vipi aje kuchukua nafasi ya striker wenu?