09/11/2024
SANAMU YA BABA WA TAIFA YAZINDULIWA
Sanamu ya Baba wa Taita, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere imezunduliwa katika Bustani ya Mashujaa iliyopo jijini Havana, Cuba 🇨🇺 leo tarehe & Novemba, 2024.
Uzinduzi huo umefanywa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro pamoja na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nie wa Jamhuri ya Kuba, Mhe.
Anayansi Rodriguez Camejo na kushuhudiwa na Mawaziri kutoka Serikali ya Tanzania na Kuba, Makatibu Wakuu na Maafisa wengine Waandamizi kutoka pande zote mbili.
Kuzinduliwa kwa sanamu hiyo ni jitihada za Serikali ya Kuba na Tanzania katika kuenzi mchango wa Hayati Nyerere katika kuimarisha ushirikiano wa mataifa hayo mawili.