13/12/2024
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambaye pia ni Mshauri wa Rais katika masuala ya Afya na Tiba, Prof. Mohamed Janabi, ametoa wito kwa jamii kuzingatia njia za kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza, akisisitiza kwamba magonjwa hayo ni changamoto kubwa kutokana na gharama na usumbufu wa kuyatibu.
Prof. Janabi amesisitiza kuwa ratiba ya kula inapaswa kuzingatia mahitaji ya mwili, badala ya kufuata mazoea yasiyo ya lazima huku akihimiza jamii kufikiria afya zao kwa kuzingatia lishe bora, mazoezi, na mbinu za kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza.
"Kunywa chai asubuhi sio lazima. Najua mtasema Profesa Janabi amekataza watu kunywa chai, lakini naomba niweke wazi: neno breakfast maana yake ni kuvunja funga. Mimi binafsi huanza kula saa sita mchana na kisha nakula tena saa mbili usiku."
Ameendelea kufafanua kuwa hospitalini hawajawahi kukutana na mgonjwa aliyelazwa kwa sababu ya kutokunywa chai:
"Hatujawahi kumlaza mtu hapa Muhimbili kwa sababu tu hajanywa chai, wala mtu hajawahi kufariki kwa sababu hiyo."
Prof. Janabi ameeleza pia jinsi anavyopanga ratiba yake ya chakula akisema:
"Kuna siku nakula matunda saa sita mchana kisha nakuja kula tena saa kumi na mbili jioni. Siku nyingine, chakula cha kwanza ninaingiza mdomoni saa nane mchana na baadaye kula tena saa kumi na mbili jioni. " Amesema prof janabi
Una maoni gani 😀✍️
Follow Ukurasa Wetu wa Instagram 👇
https://www.instagram.com/mudumohtz