Kisi Digital

Kisi Digital NYUMBANI KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI .... MARKETING NA MAUJANJA YA MTANDAONI NA KUTOBOA MAISHA
Click πŸ‘‡Chat with me
https://wa.link/7dy0k7

Baada ya ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo uliopita dhidi ya Tabora United leo tena wamemshushia kipigo kizito Fountain...
25/08/2024

Baada ya ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo uliopita dhidi ya Tabora United leo tena wamemshushia kipigo kizito Fountain Gate Fc cha bao 4-0.

Stori kubwa ni Mukwara Kuingia kambani ,Huku Ahoua akiendelea qlipo ishia , Jezi namba 10 mgongoni what a Performance...! Hapa Simba wamepata mtu kweli kweli .

Ana uwezo wa kusogea na ball ,anaenda kushoto kulia anapunguza ,anaassist anafunga ni kiungo mshambuliaji haswa .

Tukiachana na ubora wa wachezaji wengine ila huyu Mavambo ni level Nyingine ...najaribu kuwaza wangekuwa wote wapo timu moja na Aucho sijui nani angekuwa anakaa benchi mwingine anacheza.

Mwqmba fundi kweli kweli , anatuliza ball ,Anascan ,anapass Aqurate pass ...hapotezi mpira Hovyo aliye mleta huyu jamaa , wanasimba inabidi mkeshe mkimuombea alete wachezaji wengine .

Fountain Gate Good game ...! Wanawachezaji Wazuri βœ… wanapush ,wanasogea , lakini kwenda kushindana kwa battle na Simba ndipo mahali walipo kosea .

Kivipi ...?

Quality ya Fountain ni ndogo ukilinganisha na Simba ...Option pekee kwanza ilitakiwa kuamua kukaa nyuma then kumtumia Kihimbwa na Ambundo kukimbia na mpira pembeni mwa uwanja na kwenda kuidhuru Simba kwa sababu mara kadhaa Zimbwe na Kapombe walikuwa juu .

Kuamua kwenda kupishana ni k**a mmejiandalia kifo wenyewe ilibaki tu kuamua mkazikiwe wapi ...ukicheza hivi na timu yenye Quality kubwa utahisi k**a unaweza kufunga lakini muda wowote mtaitwa kati tuπŸ˜†πŸ˜….

Heshima ,Heshima ,Heshima Fountain walikosa ....4-0 ni matokeo ambayo wamestahili tena na zaidi .

Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ 0628210865 .

# πŸ”₯

Kocha mkuu wa Azam Fc Yousuf Dabo jana wakati wa mchezo dhidi ya APR Kule Kigali Rwanda aliondolewa kwenye benchi la ufu...
25/08/2024

Kocha mkuu wa Azam Fc Yousuf Dabo jana wakati wa mchezo dhidi ya APR Kule Kigali Rwanda aliondolewa kwenye benchi la ufundi la Azam Fc na timu hiyo kuongozww na kocha msaidizi Bruno Ferry .

Bado haijajulikana sababu hasa zilizo mfanya Dabo kuwa sio sehemu ya Bechi la Ufundi jana la Azam Fc je,Utovu wa nidhamu au laah !

Ferry alivalia Microphone huku mara kadhaa kionekana akizungumza inawezekana alikuwa anaongea na kocha mkuu wap Dabo ...

Je hili lilisababishwa kufungwa kwa Azam Fc??

Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ 0628210865 .

# πŸ”₯

Dabo ni kocha mzuri sana ...Ndani ya uwanja timu inacheza vizuri , intensity kubwa ,kasi Nk. Uwepo wa wachezaji k**a Sil...
25/08/2024

Dabo ni kocha mzuri sana ...Ndani ya uwanja timu inacheza vizuri , intensity kubwa ,kasi Nk. Uwepo wa wachezaji k**a Silla Djbrill ,Feisal ndani ya Azam Fc inarahisisha kazi yake sana.

Kabla ya mchezo Dabo anakuwa makini sana kumsoma mpinzani na kujua aingiaje ili kumkabili kwenye mechi husika na mara kadhaa anafanikiwa.

Shida yake nini !?

Tatizo la Dabo linaanzia pale tu anapojibiwa mbinu zake ndani ya kiwanja , yaani mbinu zake zinapofeli ndani ya kiwanja ,amekuwa mtu ambaye hana mbinu mbadala na mgumu kubadilika haraka ...yaani kung'amua tatizo na kutafuta Suluhisho .

Aliingia na mbinu za mabeki 3 mbele Ya Yanga akaja kubadilika mwishoni mwa kipindi cha kwanza ambapo tayari alishapigww bao 3 na mwisho zikafika 4 akawa tayari ameshachelewa.

Dhidi ya APR mchezo wa Dar ,

TATIZO....Vital O alikuwa anacheza nyuma sana ya mpira na kusogea kwa kushtukiza ..

SULUHISHO....Alikuwa hana haja ya kucheza na viungo wengi katikati toa viungo wa kati weka winga zinazo kimbia sana pembeni na zinazo weza kudribble k**a Nado , amekuja kufanya hivyo mwishoni kabisa kipindi cha pili hii ingerahisisha kuivuruga safu ya ulinzi na kulazimisha nafasi za kufunga makosa k**a foul, kona ,Penalty zingeweza kuwasaidia sana.

Mchezo wa Jana dhidi ya APR.

TATIZO...Mechi ilikuwa na intensity kubwa , refaree alikuwa mtu wa kuuma kipyenga (kupotezea foul ndogo ndogo), uwanja hauruhusu kupiga sana Pasi , Mpinzani (APR) anafanya Pressing kutoka juu Mnapo anzisha mpira.

Azam ilifungwa pin kutoka nyuma , walikuwa hawana nafasi ya kuanziasha na kutengeneza shambulizi kutoka nyuma ,hivyo timu ilikuwa haitembei, ukikaa na mpira sekunde 4 wanakuja kucheza rafu APR ,Mchezaji akipata mpira haoni mtu wa kumpa akitoa pasi uwanja hauruhusu inapotea .

SULUHISHO.

Dabo alihitaji kubadili mpango mapema sana , badala ya kufanya build up kutoka chini alihitaji long balls kuvusha mpira kutoka kwenye mstari wa kwanza wa Pressing Ya APR Na kwa kuwa nafasi zinakuwa zinaachwa nyuma inakuwa rahisi wao kuscore (unahitaji uharaka mkubwa.)

Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ 0628210865 .

Klabu ya Yanga imevuna jumla ya Millioni 50 ikiwa ni pesa kutoka kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambapo anatoa Tsh. M...
24/08/2024

Klabu ya Yanga imevuna jumla ya Millioni 50 ikiwa ni pesa kutoka kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambapo anatoa Tsh. Million 5 kwa kila bao ambalo linafungwa kwenye mechi ya ushindi kimataifa .

Kwenye mchezo wa kwanza Yanga ilishinda 4-0 na leo 6-0 na kufanya Aggregate 10-0 na kuitupa Vital O ya Burundi nje ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Sasa Yanga itakutana na klabu ya kutoka Ethiopia Nigd Bank ambayo imesonga mbele kwa kumtandika SC Club Villa ya Uganda kwa jumla ya mabao 2-1.

Nani kusonga mbele zaidi ?

Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ 0628210865 .

# πŸ”₯

Chama Mwamba wa Lusaka leo amekichafua sana dhidi ya Vital O ikiwa Yanga imepata ushindi wa Bao 6-0 ikisonga mbele .Kwa ...
24/08/2024

Chama Mwamba wa Lusaka leo amekichafua sana dhidi ya Vital O ikiwa Yanga imepata ushindi wa Bao 6-0 ikisonga mbele .

Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ 0628210865 .

# πŸ”₯

Azam Fc imepokea kichapo cha bao 2-0 mbele ya APR ya Rwanda na kutupwa nie ya michuano ya kombe la ligi ya Mabingwa bara...
24/08/2024

Azam Fc imepokea kichapo cha bao 2-0 mbele ya APR ya Rwanda na kutupwa nie ya michuano ya kombe la ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Azam alishinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Dar es salaam baada ya kichapo leo Aggregate ni 2-1.

Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ 0628210865 .

# πŸ”₯

Timu ipi? Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow  wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ ...
24/08/2024

Timu ipi?
Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ 0628210865 .

# πŸ”₯

Klabu ya Manchester United imepoteza mchezo wa ligikuu ya England kwa bao 2-1 mbele ya Brighton.Ikiwa ni mechi ya pili m...
24/08/2024

Klabu ya Manchester United imepoteza mchezo wa ligikuu ya England kwa bao 2-1 mbele ya Brighton.

Ikiwa ni mechi ya pili msimu huu ambapo mwanzo walishinda bao 1-0 mbele ya Fullham.

Je , kwa mwenendo huu Unaiona wapi United Msimu huu ??

Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ 0628210865 .

Β 

# πŸ”₯

Kiungo mshambuliaji mpya wa kikosi cha  atakuwa nje ya kikosi kwa wiki 2 kufuatiwa na majeraha aliyo yapata kwa maumivu ...
24/08/2024

Kiungo mshambuliaji mpya wa kikosi cha atakuwa nje ya kikosi kwa wiki 2 kufuatiwa na majeraha aliyo yapata kwa maumivu ya miguu.

Mutale aliumia kwenye mechi dhidi ya Tabora United na kushindwa kumaliza mchezo baada ya kuchezewa rafu ,mechi iliyopigwa weekend iliyopita na simba kushinda bao 3-0 kwenye dimba la KMC Complex Mwenge.

Pancha mapema tu Kuna kutoboa hapa?

Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ 0628210865 .

# πŸ”₯

24/08/2024

Huyu πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ

Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ 0628210865 .

# πŸ”₯

HUYU BABA HARIDHIKI πŸ˜…πŸ˜†?β€œKwenye mpira hakuna kinachoisha Kwenye mchezo wa kwanza lakini angalau tuko sawa kwa ushindi wa ...
23/08/2024

HUYU BABA HARIDHIKI πŸ˜…πŸ˜†?

β€œKwenye mpira hakuna kinachoisha Kwenye mchezo wa kwanza lakini angalau tuko sawa kwa ushindi wa magoli manne lakini akili zetu hatuwezi kuwa sawa kwasababu tulishinda magoli manne tunatakiwa kucheza kila mchezo kwa 100% na kujaribu kufanya vizuri mbele ya mashabiki zetu,”.

Kocha wa Yanga Sc, Miguel Gamondi akiongea na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa marudiano wa ligi ya Mabingwa dhidi ya Vital’O ya Burundi.

Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ 0628210865 .

# πŸ”₯

" Yanga hakuna bosi wa kitengo cha habari ,mimi ndie bosi wa habari ila tuna Afisa habari wa klabu ambaye ni Ally Kamwe....
21/08/2024

" Yanga hakuna bosi wa kitengo cha habari ,mimi ndie bosi wa habari ila tuna Afisa habari wa klabu ambaye ni Ally Kamwe....

Kuhusu Haji Manara ni Mwanachama hai wa klabu ya Yanga ila kwa sasa tunaangalia majukumu mapya ndani ya klabu tumkabidhi.

Mkataba wa wachezaji wetu ni Siri ila hadi sasa Stephane Aziz Ki ndie Mchezaji Ghali zaidi kwenye kikosi chetu cha Young Africans.

Mimi ni Raisi na sio mfanyakazi wa Yanga ,Rank za wafanyakazi wa Yanga zinaanzia kwa C.E.O hivyo sipo kwenye mahesabu ya wanao pokea mshahara kwenye klabu , mimi ninabiashara zangu ambazo zinaniingizia kipato hivyo sipokei hata 100 kqma mshahara kutoka Yanga Sc."

Ni baadhi ya majibu ya Raisi wa Yanga , Engeneer Hersi Said alipokuwa anafanya mahojiano na Wasafi Fm kupitia kipindi cha Jana na Leo.

Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ 0628210865 .

Β 

# πŸ”₯

Amendika Manara katika Ukurasa wake wa Instagram kuwa Doto Magari amewahi kumshikia Panga akiwa na Rafiki Yake ila kwa s...
21/08/2024

Amendika Manara katika Ukurasa wake wa Instagram kuwa Doto Magari amewahi kumshikia Panga akiwa na Rafiki Yake ila kwa sasa amekuwa mtu wa Tofauti sana katika maisha.

"Nikikumbuka miaka michache tu nyuma mlipotaka kunidhuru pale Kinondoni Studio wewe na mwenzio kwa kunitolea Panga, Wallah Mganga ni Mungu tu.

Wewe ni mfano halisi wa Binadamu aliyepewa ufunuo mpya wa maisha, Wewe unatakiwa utumike k**a Insparation kwa Maelfu ya Vijana wanaoendelea kuishi na Uovu mwingi mitaani.

Kinachonivutia zaidi kwako huigizi na hutumiii nguvu kubwa bali unaishi vile vile katika uhalisia wako,

Hakika hii Picha ni Super sana kwetu Watu wa Mjini, imetuheshimisha mno na tutaiwekea Fremu ili siku moja tutambe nayo"

Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ 0628210865 .

# πŸ”₯

20/08/2024

ILA HAWA JAMAA JAU SANA πŸ˜‚πŸ˜…πŸ€£
Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ 0628210865 .

# πŸ”₯

THANK YOU FRED MICHAEL KOUBLAN....Meneja wa habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmedi Ali amethibitisha  kuwa klabu hiyo...
20/08/2024

THANK YOU FRED MICHAEL KOUBLAN....

Meneja wa habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmedi Ali amethibitisha kuwa klabu hiyo imeachana na mshambuliaji Fred Michael ambapo amesema Kocha wa Simba hajaridhishwa na kiwango chake hivyo mshambuliaji mpya Christian Ateba amechukua nafasi yake.

Hapo vipi wana Simba ?

Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ 0628210865 .

# πŸ”₯

Msanii wa K**e anaye fanya vizuri katika game ya bongo fleva  ameingilia kati na kupaza sauti juu ya haki za binti aliye...
20/08/2024

Msanii wa K**e anaye fanya vizuri katika game ya bongo fleva ameingilia kati na kupaza sauti juu ya haki za binti aliye bakwa kwa zamu na wanaume 5 huko Dodoma na kujinasibu kuwa wametumwa na afande ili kumfanyia ukatili huo binti kutoka Yombo Dovya jijini Dar es salaam k**a alivyo jitambulisha katika video ambayo ilikuwa ikirekodiwa na wabakaji hao wakati wa tukio.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zuchu amesema licha ya watu hao 4 kati ya watano walio fanya tukio hilo kuk**atwa na kufikishwa mahak**ani lakini Afande ambaye aliyekuwa anatajwa katika video ile k**a ndio alio watuma ni lazima na yeye afikishwe katika vyombo vya sheria .

Zuchu anaungana na mastaa wengine mbalimbali ambao nao wamepaza sauti juu ya jambo hilo na kutaka kuona haki ikitendeka kwa vitendo hivyo viovu.

Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ 0628210865 .

# πŸ”₯

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeitaka klabu ya Yanga kulipa kiasi cha dola 80,000 (sawa na Sh 217 miliono) baada y...
20/08/2024

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeitaka klabu ya Yanga kulipa kiasi cha dola 80,000 (sawa na Sh 217 miliono) baada ya kushindwa kesi iliyokuwepo baina yake na klabu ya Benchem United juu ya usajili wa winga Augustine Okrah πŸ‡¬πŸ‡­.
Hukumu hiyo imetolewa jana August 19, 2024 na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), ambayo pia iliambatana na Yanga kulipa kiasi hico ndani ya siku 45.
Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ 0628210865 .

# πŸ”₯

Staa wa muziki wa Bongo Fleva  amethibitisha kutumiwa barua kutoka Baraza la Sanaa la Taifa   akiambiwa kuwa Wimbo wake ...
20/08/2024

Staa wa muziki wa Bongo Fleva amethibitisha kutumiwa barua kutoka Baraza la Sanaa la Taifa akiambiwa kuwa Wimbo wake wa haujazingatia maadili.
Kwa mahitaji ya simu kali na kijanja watafute & follow wapo Kariakoo Agrey jengo la Dubai plaza /piga sasa πŸ‘‰ 0628210865 .

#

Address

Ubungo
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kisi Digital posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Kisi Digital:

Videos

Share