08/06/2021
HEKIMA 2 ZA SIAFU
Dini zimetufundisha twende kwa siafu tukajifunze njia zao ili tupate hekima
HEKIMA YA KWANZA
Siafu hawakati tamaa-kama wanaelekea mahali fulani na ukajaribu kuwazuia basi wanatafuta njia nyingine watapanda juu watashuka chini watazunguka eneo hilo wataendelea kutafuta njia nyingine mpaka waipate kamwe usikate tamaa ukaacha kutafuta njia ya kutimiza malengo.
HEKIMA YA PILI
Muda wote siafu wanafikiria kuweka akiba wanajua kuwa kunakipindi cha ukame kinakuja hivyo wanahakikisha wanajiandaa kukikabili kwa kuweka akiba ya kutosha ya chakula wanachovuna usimalize kile unachopata jiwekee akiba ikufae kwa matumizi ya siku zijazo na kwa ajili ya kuwekeza katika fursa ya kuongeza kipato mafanikio ni jumla ya jitihada ndogo za kurudia usiku na mchana.