30/06/2024
Riwaya hii imeandikwa na:-
Azizi Mang’ulo
S.L.P
Turiani_Morogoro_Tanzania.
Simu na; 0743 653 145
0654 272 553
Baruapepe; [email protected]
[email protected]
NANI NIMPE KESI YA MAUAJI?___01
‘’Utafuatisha maneno nitakayo kwambia!’’
‘’Sawa mchungaji!’. Wakati viapo vya ndoa vikiendelea, kwenye moja ya Kanisa liitwa NURU YA MUNGU. Bibi harusi ambae alikuwa anaitwa Betha, akasema kumwambia mchungaji.
‘’Samahani mchungaji, naomba niingie chumbani mara moja!’’
‘’Kuna nini tena?’’ Mume mtarajiwa akamuuliza Betha, baada ya Betha kusikika anaomba ruhusa ya kutoka kidogo.
‘’Usijari mume wangu, nataka kujiweka sawa dakika moja tu, nakuja’’
‘’Sawa!’’. Basi baada ya ruhusa hiyo, Betha alitoka juu pale ya jukwaa la Madhabahu. Na moja kwa moja akaelekea kwenye chumba kidogo, ambacho kipo ndani ya kanisa lile la Nuru ya Mungu. Tukio lililofanya baadhi ya watu kanisani pale, waanze kuulizana kuna nini tena?. Mbona bibi harusi, katoka jukwaani wakati wa kutamka viapo vya kuishi milele vikiendelea?.
Ila Mchungaji Paschal Barnabas, aliwatoa hofu waumini kwa kuwaambia.
‘’Msiwe na hofu jamani, bibi harusi yupo sawa kabisa. Ameenda kurekebisha kitu, kwenye nguo yake. Maana hakipo sawa, ila anarudi sasa hivi’’. Jibu hilo lilifanya kundi la watu, waliopo kanisani pale. Kwaajili ya ndoa ile takatifu. Washangilie na kupiga vigere gere vya furaha kweli kweli. Ila dakika tano zikapita, bila bibi harusi kutoka ndani pale.
‘’Mbona hatoki huyu?’’. Baliki alimuuliza Sauda, ambao wawili hao. Ndio walikuwa wasimamizi/wasaidizi wa maharusi wale. Yaani Baliki alikuwa msaidizi wa Bwana harusi, na Sauda alikuwa msaidizi wa Bibi harusi. Na hii ni baada ya kuona muda, unazidi kukimbia Bibi harusi hatoki ndani.
‘’Hata sijui kwakweli’’ Sauda alijibu, ndipo Baliki akasema.
‘’Basi nenda kamwangalie, ili zoezi tulikamirishe haraka’’
‘’Sawa’’.
Baada ya maagizo hayo, Sauda akaanza kupiga hatua. Kwaajili ya kwenda kumtizama Bibi harusi. Ila kabla ya kufika popote, Sauda akaulizwa swali na Mchungaji Paschal.
‘’Wapi na wewe unaenda?’’
‘’Nataka nimtizame Betha, huenda kuna changamoto amekutana nayo’’
‘’Sawa, ila sio busara kwenda huko bila mimi kutoa ruhusa’’. Kauli hii ya Mchungaji, ilifanya Sauda alirudi kinyuma nyuma. Na kwenda kusimama pale pale, ambapo alisimama mwanzo. Baada ya kuhisi Mchungaji Paschal, hakupenda yeye aingie ndani pale bila ruhusa yake.
‘’Hebu ngojeni nikamtizame huyu binti, kujua amepatwa na khadhia gani!’’ Mchungaji Paschal, aliwaambia watu ambao walikuwa mbele pale. Kisha akaelekea kwenye kile chumba, ambacho Betha aliingia.
Hatimae Mchungaji Paschal, akaingia ndani pale. Na kumkuta Betha, amekaa kwenye kiti kajiinamia. Paschal kwa hasira akamuuliza Betha.
‘’Ujinga gani unafanya Betha eeh?’’. Betha aliinua macho yake ambayo yalikuwa yanatoka machozi, na kumtizama Mchungaji Paschal. Na Mchungaji nae, akarudia tena swali lile lile.
‘’Nakuuliza ujinga gani huu, unafanya eeh!’’
‘’Huu unaona ni ujinga sio?’’. Betha alimjibu Paschal, kwa kumuuliza swali. Kisha akaendelea kwa kusema, huku machozi yakimtoka.
‘’Ni nani anaeweza kuvumilia, kuachana na mtu anae mpenda. Hali ya kuwa ana uwezo wa kusitisha hilo? Na huu sio ujinga, wewe ndio sababu ya haya yoye. Kwanini lakini unanifanyia hivi Paschal?’’.
Betha aliongea kwa hasira kweli kweli, maneno yaliyo fanya Paschal. Awe kimya muda wote, asijue aseme nini kwa Betha juu ya hayo malalamiko. Na ndipo Betha, akasimama kisha akaja mpaka alipo Paschal na kumwamia.
‘’Paschal siwezi kuolewa na Simon!’’ Mchungaji Paschal, aliinua macho yake. Kumtizama Betha kwa mshangao, juu ya kauli ile aliyo iongea. Halafu sasa Paschal, akaanza kwa kusema.
‘’Nini unasema Betha! Hivi nani atakuelewa juu ya huu upuuzi unaotaka kuufanya? Kanisa limejaa ndugu zako, ndugu wa Simon. Unaanzaje kusema huwezi kuolewa nae, hali ya kuwa kila kitu kilishaa kamilika?’’
‘’Najua ila sipo tayari, nahitaji kuolewa na wewe!’’.
Paschal aliinamisha kichwa chini kwa sekunde kadhaa, ndipo Betha akamuuliza Paschal.
‘’Vipi mbona husemi chochote?’’
‘’Najiribu kufikiria’’
‘’Unafikiria kitu gani Paschal, wakati tulishaa kubaliana kuwa utamuuwa mkeo kwaajili yangu!’’
‘’Najua Betha ila…!’’
‘’Ila kitu gani? Unataka kuniambia nini? Wewe ndio Mchungaji wa hili kanisa. Utakacho kisema chochote lazima kifuatwe, nenda mbele za watu. Waambie Betha amegoma kufunga ndoa na Simon, shughuli inakuwa imeishia hapo’’.
Upande wa Bwana harusi na wapambe wake, na wana ndugu wote Kanisani pale. Wakaanza kuingiwa wasi wasi, baada ya muda kuzidi kwenda bila Bibi harusi, kutoka kwenye chumba ambacho aliingia.
‘’Atakuwa kapatwa na nini huko?’’ Watu wakaanza kuulizana kanisani pale.
‘’Sauda hebu nenda kamwagalie!’’ Simon ambae ndio Bwana harusi, akamwambia Sauda kwa sauti ya chini kabisa. Kweli Sauda akapiga hatua kadhaa, akafika kwenye mlango wa chumba kile. Kisha akaita kwa sauti ya chini huku akigonga mlango.
‘’Betha! Bethaaa!’’. Upande wa ndani Betha na Paschal, maongezi yao yakasimama kidogo. Kwaajili ya ule mlango ambao ulikuwa unagongwa na Sauda.
Na ndipo Paschal akaamua, kuvunja ukimya kumwambia Betha kwa sauti ya chini sana.
‘’Kuwaambia watu, kuwa hutaki kuolewa na Simon. Ina wezekana, ila sasa ni vipi watu watanichukulie, ikitokea mke wangu kafa na mimi nikakuoa wewe?’’. Maneno haya ya Paschal, yalifanya Betha ashushe pumzi kidogo, na muda huo huo Betha akatoa sauti kubwa. Kumjibu Sauda, ambae alikuwa akiita.
‘’Sauda nakuja sasa hivi hapo sawa shoga!’’
‘’Sawa ila muwahi kidogo jamani’’ Sauda alijibu, kisha akanyamaza kimya akiwa pale pale mlango. Na sikio lake akiwa kalitega, upande wa ndani kusikia ni kitu gani, kinacho endelea ndani pale. Ambapo Betha aliomba kuingia kwaajili ya kujiweka sawa.
‘’Enhee! Kwahiyo ulicho amua ni nini sasa? Maana mimi uliniambia nifanye nikafanya, kwako wewe kwanini inakuwa ngumu kufanya?’’ Betha alimuuliza Paschal, swali ambalo lilifanya Paschal. Aendelee kunyamaza vile vile, kwa tafakari za viwango vya juu.
Na baada ya ukimya wa nusu dakika, Paschal alimshika Betha mabegani. Kisha akamwambia.
‘’Nipo chini ya miguu yako Betha, naomba twende, tukaendelee na ndoa. Halafu tutajua nini cha kufanya baada ya hili kupita!’’
‘’Nipo chini ya miguu yako, eti naomba ukaendelee na ndoa! Mshenzi mkubwa wewe! Sasa ngoja nitoke huko nje, nikawaambie waumini kila kitu. Wewe si umeshindwa ngoja uone!’’. Betha aliongea maneno hayo, huku akiwa kaanza kuchana chana gauni lake la Harusi. Ambalo alikuwa amelivalia, jambo lililofanya Paschal aanze kumzua kufanya vile.
‘’Betha una nini lakini, hebu acha haya mambo!’’ Paschal alimwambia Betha na kumzuaia pia. Huku upande wa mlangoni Sauda alisikia zile kurupushani, haraka akaondoka. Kwaajili ya kwenda kutoa taarifa, ya mambo yanayo endelea ndani pale.
Wakati Paschal akipambana na Betha, kumzua asifanye alichokuwa akikifanya. Kwa bahati mbaya, Betha alianguka kinyume nyume. Na kichwa chake, kipigiza kwenye moja ya sanduku la mbao ambalo lilikuwa ndani pale. Na kumfanya Betha aanze kutapa tapa chini pale alipo anguka, na hapo hapo Betha akaanza kutokwa na damu puani, pamoja na mdomoni. Tukio lililofanya Mchungaji Paschal, achanganyikiwe kweli kweli.
‘’Betha! Betha! We Betha! Amka nitaenda kuwambiwa watu, kuwa hutaki kuolewa Betha amka!’’. Paschal alimwita Betha, bila mafaniko yoyote yale. Na muda mchache wa kutapatapa kwa Betha umauti ukamkuta pale pale msichana yule, akiwa mikononi mwa Mchungaji Paschal. Tukio lililoleta hofu kuu kwa Mchungaji Paschal Barnabas.
‘’Kule ndani nahisi kuna kitu, hakipo sawa kwakweli!’’ Sauda alimwambia Baliki, ambae ndio alikuwa msimamizi mwenza kwenye ndoa ile ya Betha na Simon.
‘’Kuna nini’’ Baliki alimuuliza Sauda.
‘’K**a kuna marumbano hivi’’
‘’Marumbano ya nani na nani?’’
‘’Mchungaji na Betha!’’
‘’Mh! Mchungaji na Betha. Inawezekana vipi?’’
‘’Hata sielewi kwakweli, yapaswa tumwambie Simon. Ili aende kuuliza kuna tatizo gani’’
‘’Sawa ngoja nimwambie basi’’
‘’Sawa!’’.
Baada ya kupewa taarifa ile Baliki, taratibu alimsogelea Simon. Kisha Baliki akamwambia Simon.
‘’Oya Mzee hebu fanya wende kwenye kile chumba, maana Sauda anasema kuna mzozo kausikia ndani pale’’
‘’Mzozo wa nani tena?’’ Simon aliuliza kwa mshangao kiasi.
‘’Ni kati ya Mchungaji na mkeo!’’
‘’Mchungaji na mke wangu. Wana mzozo gani tena?’’
‘’Sijui Kaka, labda ungeenda. Ili ujue shida ni nini’’
‘’Poa’’. Baada ya taarifa ile. Simon akaanza kupiga hatua moja moja, kuelekea ulipo mlango wa chumba kile kidogo kilichopo kanisani pale.
Hatimae Simon, akafika mpaka kwenye mlango wa chumba kile.
‘’Ngo ngo ngo ngo! Mchungaji!’’ Simon aliita, huku akigonga mlango ule. Zaidi ya mara tatu, ila hakujibiwa na yeyote. Ndipo Simon akaamua kuufungua mlango, kisha akaingia mpaka ndani ya chumba kile cha kanisa. Nani ataisoma hii Riwaya…? Ni kisa kizuri sana cha kusisimua. K**a kimekuvutia basi weka kura yako hapo kazi hii iendelee. Inaitwa NANI NIMPE KESI YA MAUAJI.