Emmanuel Senzighe Project Manager wa Mradi wa Kilimo Tech Acceletor kutoka Sahara Ventures ni shirika linaloshiriki project mbalimbali za vijana katika Ubunifu na Ujasiriamali wa Teknolojia za kisasa.
@venturessahara @kilimotechaccelerator.
#teknoloji #ubunifu #maendeleo
#Usikivu Umetulia endelea kusikiliza 95.3 Smile Fm mkoa wa manyara.........
Mitaa yote #wameikubali
TUKIO KUBWA LA BURUDANI KWA MWAKA 2024 BABATI MANYARA.
Novemba 7.2024 ilikuwa ni Siku kubwa ya Ki historia kwa wapenda Burudani ya Muziki Babati mkoani manyara kwani ilikuwa ni nafasi ya ku enjoy burudani,live performance Pamoja na kupata picha na mastaa mbalimbali waliowahi kufanya vizuri miaka ya nyuma kuanzia miaka ya 2000.
Ugeni huo wa list ya zaidi ya wasanii 10 walifika kwenye studio za radio ya Smile Fm kwa ajili ya mahojiano mafupi na kuzungumza na mashabiki zao kupitia masafa ya 95.3.
ilikuwa ni Legends Tour ambayo imeacha kumbukumbu nzuri kutoka kwa mashabiki na wapenzi wa muziki wa zamani ilifanyika Babati katika uwanja wa Mpira wa Tanzanite Kwaraa huku steji ikishambuliwa na wakali kibao kama
@jaymoefamous
@sir_nature
@feroozgram
@soggydoggyanter
@afandesele1976
@inspectorharoun
@linahafrica
@matonyambili
@domokayatz
@officialdazbaba
@fidovato_official
@saa1nnt
@kingpusiofficial
@rich_onee
@dj_baby_flavour na wengine kibao
#LegendsTour 🔥 Novemba 7 pale Tanzanite Kwaraa ilitisha zaidi Kwa udhamini wa @matisuperbrandsltd kupitia kinywaji chake cha @strongdrygin
Tuambie Tukio gani la Burudani lilikukosha zaidi mwaka 2024
#HANANG MANYARA
waathirika wa maporomoko ya tope wilaya ya hanan'g mkoani Manyara Selina Omary nade kutoka Gendad na Timotheo Jeremia ngaida ambao kwa sasa ni wakazi wa kitongoji cha waret kwa niaba wa wananchi wengine waliokabidhiwa nyumba wamezungumza na Smile Tv na kutoa shukrani kwa Rais Dkt. Samia kwa kazi kubwa aliyoifanya tangu kutokea kwa janga hilo mpaka sasa wanapokabidhiwa nyumba hizo.
“Tunakumbuka upendo wa Rais Dkt. Samia; hakika alikuwa mfariji mkuu na tunaendelea kumuombea kwa Mungu. Kwako pia Mheshimiwa Waziri Mkuu tunakushukuru wewe kwa kuzielekeza Wizara na wadau mbalimbali kuja kutunusuru kutokana na janga lile Bila kuwasahau Red cross " walisema.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa Disemba 20 ,2024 amekabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope yaliyotokea Disemba,Mwaka jana wilaya ya Hanan'g mkoani manyara.
#smiledigital #smiletv #smilefmtz @ofisi_ya_mkuu_wa_wilaya_hanang @ofisi_ya_mbunge_hanang @manyara_rs
wakazi wa Kitongoji cha waret wilayani hanan'g mkoani manyara wakizungumza na smile fm wameonesha kufurahishwa na serikali ya Rais Dkt. Samia baada ya waathirika wa maporomoko ya tope hanan'g kukabidhiwa nyumba 109 jambo hilo limewapa imani zaidi.
mbali na hilo wamewakaribisha waathirika kwa ajili ya kuanza maisha mapya katika kitongoji cha waret.
mmoja wa wakazi kwenye eneo hilo amesema "ninafuraha kupata majirani wapya hivyo nawakaribisha tuishi pamoja"
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Ijumaa, Desemba 20, 2024) amekabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope yaliyotokea Desemba, mwaka jana wilayani Hanang, mkoani Manyara.
#BABATIMANYARA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mati Super Brands Ltd yenye makazi yake Babati Mkoani Manyara David Mulokozi hii leo Disemba 18,2024 ameingia kwenye kalenda ya mwaka huu kwa kufanya tukio litakalo weka kumbukumbu kwa wakazi wa manyara baada ya kutua na Helikota yake mpya katika uwanja wa Tanzanite kwaraa mkoani manyara akiwa na familia yake.
mmiiliki huyo wa Kampuni ya Vinywaji changamshi ya @matisuperbrandsltd amenunua ndege hiyo aina ya helikopta kwa lengo la kusaidia kupanua biashara zake kwa kuwafikia wateja maeneo mbalimbali kwa haraka.
#smiledigital #smiletv #smilefmtz
Ukinunua Dai Risiti na Ukiuza toa Risiti Kwani kwenda kinyume kuna adhabu kali "kwani kuna wajibu wa kudai na kutoa risiti na adhabu ya kushindwa kutoa ni faini ya adhabu ya vipande 200 na kipande kimoja sawa na Tsh 20.000/=ambapo ni sawa Kama na milioni mbili.
Hayo ameyazungumza meneja wa tra mkoani manyara alex katundu akiwa katika kipindi cha maskani smilefm 95.3
Kliniki ya Madaktari Bingwa Mkoa wa Manyara Kuanza rasmi Novemba 19 wilayani Simanjiro kambi hii ya Madaktari Bingwa na bobezi inaanza kuanzia leo Jumanne Hadi Tarehe 22 mwezi Novemba Mwaka huu
Kliniki maalumu ya Madaktari Bingwa wa ndani ya mkoa wa manyara yenye lengo la kutoa Huduma na matibabu kwa wananchi wa wilaya zote tano kwa kwa kutumia vifaa tuba vya ndani ya mkoa.
#nguvumoja #manyara
Mambo Ni fasta sana Fikia Mamilioni ya wanao kupigia wasikie Bishara yako 0684728971
#BURUDANI
Msanii wa hiphop kutoka arusha #fidovato amezungumza kuhusu inshu inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu msanii #puffydady
@juma_jux na mpenzi wake @its.priscy huko Nigeria kama mfalme! 🇹🇿🇳🇬
Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga Ametoa Pole kwa wahanga wote wa ajali ambapo Watu wanne wamepoteza maisha yao wakiwemo Wanafunzi watatu na Dereva mmoja katika ajali iliyohusisha Coaster na gari la mizigo aina ya Scania.
Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo August 31,2024 katika eneo la Gajal Babati Mkoani Manyara ambapo Coaster ilikuwa imebeba Wanafunzi kutoka Hanang kuelekea Mkoani Arusha na baada ya Kufika eneo hilo iligongana uso kwa uso na Scania.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Manyara Ahmed Makarani amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa lori kushindwa kuwa makini barabarani na kuigonga Coaster hiyo iliyokuwa imebeba Wanafunzi 33 wa Shule ya Sekondari Endasaki waliokuwa wakielekea Mkoani Arusha kwa ajili ya likizo baada ya kufunga Shule.