NABII MWAMPOSA AVUTIWA NA MAOMBI YA DEC.9, AALIKA WANANCHI KUSHIRIKI KIKAMILIFU.
Mchungaji na Nabii wa kanisa la Arise and Shine nchini Tanzania Apostle Boniface Mwamposa ametoa rai kwa wananchi wote wa Arusha kujitokeza kwa wingi leo Jumatatu Disemba 09, 2024 kwenye maombi maalum ya kuuombea Mkoa wa Arusha ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Christian Makonda.
Kwenye sehemu ya mahubiri yake jana Jumapili Disemba 08, 2024, Nabii Mwamposa ameitaja siku ya leo kama siku ya kukombolewa kiroho, akimpongeza Mhe. Makonda kwa maono yake hayo ya kuikomboa ardhi ya Arusha, akitamani pia kushiriki na wakazi wa Arusha katika maombezi hayo.
Leo Jumatatu wakati wa kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanzania bara, Mkoani Arusha kunafanyika matembezi na maombi maalum ya kuombea Mkoa wa Arusha kuanzia saa mbili kamili asubuhi, matembezi yakianzia kwenye mzunguko wa barabara ya Impala na kumalizikia kwenye mzunguko wa mnara wa Mwenge Jijini Arusha.
NABII MKUU MHE. DK. GeorDavie Royal Mkuu AMTABIRIA Mkuu wa Mkoa wa Arusha #Paul_Makonda KUENDELEA KULA MEMA YA NCHI NA "SIKU MOJA UTANIKUMBUKA"
DAYOSISI YA KASKAZINI KATI KUHUDHURIA MAOMBI KUIOMBEA ARUSHA DISEMBA 09, 2024.
Naibu Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Kati Jijini Arusha, Mchungaji Julius Tarakwa Laizer ametumia sehemu ya mahubiri yake hii leo Jumapili Disemba 08, 2024 kwenye usharika wa Elerai, kuwasihi waumini wa kanisa hilo na wananchi wa Arusha kujitokeza kwa wingi Jumatatu ya Disemba 09, 2024, kwenye Maombi maalum ya kuombea Mkoa wa Arusha yaliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Christian Makonda.
Maombi hayo maalum yataanza majira ya saa mbili asubuhi kwa matembezi yatakayoanzia kwenye Mzunguko wa barabara wa Impala (Impala Round About) na kisha kumalizikia kwenye barabara ya mzunguko wa mnara wa Mwenge ambapo mbali ya Maombi kutoka kwa Viongozi mbalimbali wa dini, kutakuwepo na mafundisho na kumtukuza Mungu kwa njia ya Uimbaji kupitia Vikundi, kwaya na waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili.
Mchungaji Laizer akisisitiza kuhusu maandiko matakatifu ya Biblia kwenye Kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati 7:14, amesema ni muhimu mwananchi kuombea ardhi anayoikanyaga kila siku, sehemu inapoishi familia pamoja na maeneo ya kazi na hivyo kusema ni muhimu kila mmoja kushiriki kwenye maombezi hayo ya kuombea Arusha.
Maombi hayo yanakwenda sambamba na maadhimisho ya Miaka 63 ya uhuru wa Tanzania bara, yakiwa na kaulimbiu isemayo "Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara; Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji Wananchi ni Msingi wa Maendeleo yetu"
"Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda anafanya kazi ya Mungu" Askofu Maasa
Samia Suluhu Kwanza Makonda Rc Paul Elinipa Lupembe