Michuzi TV

Michuzi TV Karibu Michuzi Blog a.k.a Globu ya Jamii the most read Swahili blog on Earth

http://issamichuzi.blo

When I started this blog at Finlandia Hall in Helsinki, Finland, on Septermber 28, 2005, my aim was to bridge the news and information gap for the benefit of Tanzanians in the Diaspora. Since I was the first Tanzanian blogger operating from Tanzania ( http://issamichuzi.blogspot.com/2005_09_01_archive.html) about 4 years elapsed before others started blogging. Therefore I boast of millions of fait

hful old and new followers who have made Michuzi the most read Swahili blog on earth. Moreso its the top most blog with authoritative and authentic content.

  Wageni zaidi ya 800 kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) wamefanya ziara ya kihistoria katika eneo...
30/08/2024



Wageni zaidi ya 800 kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) wamefanya ziara ya kihistoria katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro jana tarehe 29 agosti, 2024.

Ziara hiyo ambayo imefanyika baada ya wajumbe wa TUGHE kumaliza semina iliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 26/08/2024 ina lengo la kuwaleta pamoja waajiri na wafanyakazi ili kupata uwelewa wa pamoja, kujadili na kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza mahala pa kazi.

Akiongoza ujumbe huo Mwenyekiti wa TUGHE Taifa Bw. Joel George Kaminyoge amesema lengo la ziara yao ni kutoa hamasa ya utalii wa ndani na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza utalii ambapo ziara hiyo imewapa fursa wanachama wao kujionea vivutio vya kipekee vinavyopatikana hifadhi ya Ngorongoro.

“Leo tumekuja na wanachama zaidi ya 800 kutembelea Kreta ya Ngorongoro kujionea moja kati ya vivutio bora vya dunia ambavyo ni sehemu ya urithi wa dunia, Tunaamini kwamba ziara yetu italeta tija na hamasa kwa wakuu wa taasisi kuwa na utaratibu wa kuwapeleka watumishi wao kufanya utalii wa ndani katika vivutio mbalimbali nchini” Alisema Bw. Kaminyoge

Akiwapokea wageni hao, Meneja wa huduma za Utalii na masoko wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Bi.Mariam Kobelo, alisema kwamba Mamlaka hiyo ipo tayari kuendelea kupokea makundi mbalimbali ya wageni na kuwahakikishia kuwa wanapata huduma bora ili kuendelea kutqngaza hifadhi hiyo na kuimarisha utalii ndani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanzanite Cooperates L.t.d aliyeratibu ziara hiyo Bi. Elina Mwangomo, ameleza kuwa kwa sasa kuna ongezeko kubwa la watalii wa ndani hali inayoongeza hamasa kwa wadau wa utalii kuendelea kuboresha huduma zao huku akieleza kuwa Ngorongoro imekuwa moja kati ya eneo ambalo linapendwa zaidi na wageni na watalii kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa watoa huduma za afya wa nchi wanachama wa kanda ya Afrika Mashariki kuon...
30/08/2024



WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa watoa huduma za afya wa nchi wanachama wa kanda ya Afrika Mashariki kuondoa vikwazo vinavyozuia wagonjwa wanaotafuta matibabu ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki.

"Hatua hii ni kwa manufaa ya wananchi wetu na kwa uchumi wa kikanda na ukuaji wa utalii tiba."

Ametoa wito huo leo (Ijumaa Agosti 30, 2024 ) alipokuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa 12 wa Shirikisho la Watoa Huduma za Afya Afrika Mashariki uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Njerere (JNICC). Dar es Salaam

Amesema nchi wanachama ikiwemo Tanzania zimejitahidi kuwekeza katika sekta ya afya na kupunguza gharama za kupeleka wagonjwa nje ya Kanda kwa matibabu.

"Kwa sasa ni wagonjwa wachache sana wanaosafiri nje ya nchi zetu kwa ajili ya matibabu, kwani karibu magonjwa yote makubwa sasa yanaweza kutibiwa ndani ya Afrika Mashariki.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa wawekezaji wa Sekta ya Afya kuwekeza nchini Tanzania kwa kuwa Serikali imetengeneza sera rafiki za uwekezaji hususan katika Sekta ya Afya kutokana na uhitaji wa huduma hizo nchini.

"Tunawakaribisha wawekezaji wote wenye nia ya kuwekeza kwenye sekta ya afya, Sera nzuri tunazo, Sheria na kanuni nzuri tunazo, mahitaji ya uwekezaji kwenye sekta ya afya ni makubwa na tunataka tupate teknolojia mpya na huduma za kibingwa."

Kadhalika amewataka wadau wa afya wa kanda kujadili mbinu mbalimbali za kuimarisha mifumo ya afya na kuwa na mikakati ya pamoja ya kukabiliana na magonjwa.

"Tumieni jukwaa hili kuweka mikakati ya pamoja ya kupambana na magonjwa ya mlipuko, magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ambukiza pamoja na magonjwa mapya yanayotokana na mabadiliko ya hali ya tabia nchi".

Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema uwekezaji uliofanywa na serikali kuanzia ngazi ya chini umewezesha ugunduaji wa magonjwa yakiwa katika hatua za awali.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe Dkt  Paul Lawala ,amesema waandishi wa habari, waju...
30/08/2024



Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe Dkt Paul Lawala ,amesema waandishi wa habari, wajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa inajenga jamii ambayo inatambua na kuthamini afya ya akili.

Dkt Lawala ameyasema hayo leo Agosti 30 ,2024 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu afya ya akili.

Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuboresha uelewa na ujuzi wa waandishi wa habari kuhusu masuala ya afya ya akili kupitia mawasilisho yatakayofuatiwa na mijadala , ili kuoanisha afya ya akili na utoaji taarifa sahihi kwa jamii kupitia vyombo vya Habari.

“Waandishi wa habari mna nafasi ya kipekee na ya muhimu katika jamii. Kupitia kazi zenu, mnatoa habari, elimu, na burudani, na kwa kufanya hivyo, mnaathiri kwa hasi au chanya jinsi watu wanavyofikiria, wanavyotenda, na wanavyojihusisha na masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na afya ya akili,”amesema Dkt Lawala

Ameongeza kuwa :”Kwa hivyo, tunapokutana hapa leo, ni muhimu kutambua kuwa vyombo vya habari vina nafasi muhimu sana katika kuelimisha umma kuhusu afya ya akili na kupunguza unyanyapaa unaohusishwa na afya ,changamoto na magonjwa ya akili,”

Akizungumzia kuhusu umuhimu wa mafunzo hayo alisema afya ya akili ni sehemu muhimu ya afya ya jumla ya mtu binafsi na jamii kwa kuwa Afya ya Akili ni Afya,Afya ya akili inamhusu kila mtu na hakuna afya bila afya ya akili.

Amefafanua kuwa hali hiyo imechangia kuwepo kwa unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya wale wanaopambana na changamaoto za Afya ya Akili na magonjwa ya akili.

Katika hatua nyingine amesema waandishi wa habari wanaweza kusaidia kubadilisha hali hii kwa kutoa taarifa sahihi, zinazoelimisha, na zenye uwiano uliotafitiwa kuhusu afya ya akili.

“Lengo la mafunzo haya ni kuwapa ninyi, waandishi wa habari, maarifa na ujuzi unaohitajika ili kuripoti kwa usahihi na kwa uwajibikaji kuhusu afya ya akili,”amesema

Ameongeza kuwa :”Tunataka kuhakikisha kwamba mnakuwa na uwezo wa kutambua habari sahihi, kuzuia kusambaza habari zilizopotoshwa, na zaidi ya yote, kuweza kutoa taarifa kwa njia ambayo inaondoa unyanyapaa na kuongeza uelewa katika jamii,

  Bunge la Tanzania limepitisha muswada wa marekebisho ya sheria zinazohusu ulinzi wa mtoto wa mwaka 2024 leo Agosti 30,...
30/08/2024



Bunge la Tanzania limepitisha muswada wa marekebisho ya sheria zinazohusu ulinzi wa mtoto wa mwaka 2024 leo Agosti 30, 2024 jijini Dodoma.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, akiwasilisha Muswada huo amesema madhumuni yake yanalenga kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa utekelezaji wa baadhi ya masharti ya sheria hizo ili kuimarisha ulinzi na maslahi bora ya mtoto.

Amebainisha kuwa, muswada huo umetoa mapendekezo katika sheria tatu ambazo ni Sheria ya Makosa ya Kimtandao Sura ya 443, Sheria ya Mtoto, Sura ya 13 na Sheria ya Msaada wa Kisheria, Sura ya 21.

Waziri Dkt. Gwajima amesema kazi ya kuboresha sheria na miongozo mbalimbali inayohusu ulinzi wa mtoto itaendelea kufanyika k**a kazi endelevu kwani, kwa sasa kasi ya mabadiliko kwenye jamii ni hasa katika mazingira ya maendeleo ya ulimwengu wa kidigitali.

"Kila mwaka hatutasita kuja na marekebisho ya Sheria kutokana na Kasi ya mabadiliko ya kijamii kwenye ulimwengu wa maendeleo ya kidigitali kwani, kasi hiyo pia inagusa maendeleo na ustawi wa maisha ya watoto wetu katika rika mbalimbali" amesema Waziri Dkt. Gwajima.

Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Michael Kembaki ameishauri Serikali kuhakikisha sheria zote zinazohusu ulinzi wa mtoto zipitiwe upya ili kuendana na mazingira ya sasa, kutenga bajeti ya kuendesha mabaraza ya watoto pamoja na kuongeza kasi ya kuajiri Maafisa Ustawi wa Jamii.

Nao baadhi ya wabunge wakichangia kuhusu Muswada huo wameipongeza Serikali kwa kuona umuhimu wa kufanya marekebisho ya Sheria zinazuhusu ulinzi wa mtoto ili kumlinda mtoto na mabadiliko ya sayansi na teknolojia na vitendo vya ukatili na udhalilishaji.

  Kampuni ya Barrick nchini kupitia Programu yake ya kuendeleza biashara za ndani ili ziweze kunufaika na sekta ya madin...
30/08/2024



Kampuni ya Barrick nchini kupitia Programu yake ya kuendeleza biashara za ndani ili ziweze kunufaika na sekta ya madini (Local Business Development Programme), Wajasiriamali wapatao 150 kutoka wilaya za Msalala, Kahama na Nyang’hwale, wanapatiwa mafunzo ya biashara ya wiki mbili ambayo yamefunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita.

Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha wajasiriamali waliopo katika maeneo yanayozunguka mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu kuweza kuchangamkia fursa za kibiashara, kunufaika na uwekezaji wa mgodi huo pamoja na kupata maarifa zaidi ya kuendesha biashara.

Mhita ameipongeza Barrick Bulyanhulu kwa kuendesha mafunzo hayo na kuwataka washiriki kutoka kata tatu zinazozunguka Mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu, kuchangamkia fursa za mikopo ya asilimia 10, inayotolewa na halmashauri zote ili kujikwamua kiuchumi.

Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Victor Lule, amesema Kampuni ya Barrick inaamini kwamba msingi wa maendeleo ndani ya jamii unatokana na watu na hatua sitahiki kwenye fursa zinazopatikana ndio sababu ya kuwekeza katika programu hii ili kuwahamasisha kuzitambua fursa hizo.
Kampuni ya Barrick inaendesha shughuli zake nchini kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.
Tangu Programu hii ianzishwe tayari imewafikia wafanyabiashara mbalimbali waliopo maeneo jirani na migodi ya Barrick North Mara na Bulyanhulu na yamewawezesha baadhi yao kuchangamkia fursa migodini na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Agosti 30, 2024 amesafiri kwa kutumia Usafiri wa treni ya Mwendo Kasi (SGR) kutokea Do...
30/08/2024



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Agosti 30, 2024 amesafiri kwa kutumia Usafiri wa treni ya Mwendo Kasi (SGR) kutokea Dodoma kwenda Dar es Salaam ambako atakuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa 12 wa Shirikisho la Watoa Huduma za Afya Afrika Mashariki utakao fanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).

  Watoa huduma ndogo za fedha  na vikundi vya kijamii nchini  vinavyojihusisha na huduma za mikopo vimetakiwa kuwapatia ...
30/08/2024



Watoa huduma ndogo za fedha na vikundi vya kijamii nchini vinavyojihusisha na huduma za mikopo vimetakiwa kuwapatia nakala ya mkataba wananchi wanaowakopesha mikopo.

Akizungumza katika program ya elimu ya fedha kwa wananchi wa Mji Mdogo wa Mikumi, Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Bi. Grace Muiyanza, alisema kuwa watoa huduma wanatakiwa kutoa mikataba kwa wanaowakopesha kwa mujibu wa sheria iliyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania.

Aidha Bi Muiyanza alisema mkataba ni mafungamano kati ya pande mbili ya mkopeshaji na mkopaji hivyo ni lazima kila upande uridhie makubaliano hayo kabla ya kuchukua mkopo na kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza changamoto zinazojitokeza wakati wa kurejesha mkopo na pia mkataba utakuwa ndio njia pekee ya kila mmoja kupata haki yake itakapotokea mgongano baina yao.

Pia, Bi. Muiyaza aliwasihi wananchi kabla ya kusaini mkataba wa mkopo ni vizuri kila mmoja akapata nafasi ya kuusoma na kuelewa masharti ya mkataba huo ili usije ukamfunga kwa vipengele ambavyo vitasababisha ugumu wa kurejesha mkopo wake.

‘’Mkataba ni masharti ya pande mbili, hakikisha umeusoma na kuuelewa mkataba, na hata k**a ujui kusoma nenda kwa maafisa wa maendeleo ya jamii wakueleweshe masharti yaliyomo kwenye mkataba huo maana ukiamua kusaini bila ya kuuelewa utakuwa umeshakubaliana na masharti na utakuwa umesaini masharti yatakayokuja kukufunga baadae’’. Alisema Bi Muiyaza

Awali akifungua mafunzo hayo Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Mji Mdogo Mikumi Bi. Edith Mlay, aliwataka wananchi wa Mikumi kuitumia fursa hiyo ya kujifunza masuala ya fedha ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali wanazokutana nazo kutoka kwa baadhi ya watoa huduma za fedha.

Bi. Mlay aliongeza kuwa elimu ya fedha ni muhimu sana kwa wananchi wa Mikumi kwa sababu mji huo umekusanya makundi muhimu ya kijamii yakiwemo ya wakulima na wafugaji, hivyo elimu hiyo itawasaidia wananchi hao kutumia fursa ya uwekezaji zilizopo katika sekta ya fedha baada ya kuuza mazao yao.

  WATU 6,597 miongoni mwao wakiwemo wajasiriamali 97 katika wilaya  tano za Karatu, Ngorongoro- Loliondo, Monduli, Longi...
29/08/2024



WATU 6,597 miongoni mwao wakiwemo wajasiriamali 97 katika wilaya tano za Karatu, Ngorongoro- Loliondo, Monduli, Longido na Arusha DC wamepatiwa elimu na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusiana na viwango.

Elimu hiyo ilianza kutolewa na maofisa wa TBS katika wilaya hizo za Mikoa ya Arusha na Manyara kuanzia Agosti 16 na itahitimishwa Agosti 29, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na kampeni hiyo, Meneja Uhusiano na Masoko wa TBS, Gladness Kaseka, alisema elimu hiyo inatolewa kwa wananchi kupitia maeneo ya wazi, ikiwemo minadani , stendi, sokoni na maeneo mengine yenye mikusanyiko ambapo watu wengi wamejitokeza kwa wingi kupata elimu hiyo.

Kwa mujibu wa Kaseka kampeni hiyo ina lengo la kuelimisha wananchi kuhusiana na umuhimu wa kutumia bidhaa zilizothibitishwa ubora, jinsi ya kutoa taarifa za bidhaa hafifu pamoja na zile ambazo hazijaisha muda wake wa matumizi.

Alihimiza wananchi kabla ya kununua bidhaa wahakikishe wanasoma kwa umakini taarifa zilizopo kwenye vifungashio ili kujiridhisha k**a bidhaa hizo zimethibitishwa ubora na k**a hazijaisha muda wake wa matumizi pamoja na taarifa zingine za msingi.

Kwa mujibu wa Kaseka TBS imeamua kufikisha elimu hiyo kwa wananchi kwa kutambua kuwa vita ya bidhaa hafifu sio ya Shirika hilo peke yake, bali ni ya Watanzania wote.

Aidha, alitaka wananchi waache kununua bidhaa kwa mazoea na badala yake waangalie muda wake wa mwisho wa matumizi na pindi wakikutana na bidhaa ambazo hazina ubora, au zimeisha muda wake wa matumizi au kutilia mashaka bidhaa yoyote wasisite kuwasiliana na TBS kupitia namba ya bure ya kituo cha huduma kwa wateja.

  Serikali inaendelea na majadiliano na Kampuni za Nishati za Kimataifa kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa kuchakata na ku...
29/08/2024



Serikali inaendelea na majadiliano na Kampuni za Nishati za Kimataifa kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa kuchakata na kusindika Gesi Asilia ili kuwa kimiminika-LNG.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga alipokuwa akijibu swali bungeni kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Alhamisi, Agosti 29, 2024.

Swali hilo la msingi limeulizwa na Mhe. Aida Joseph Khenani (Mbunge wa Nkasi Kaskazini) ambaye alitaka kujua ni lini Mkataba kati ya Tanzania na Wawekezaji wa Gesi Asilia wenye thamani zaidi ya sh. 70 Trilioni utaletwa Bungeni kuridhiwa.

"Mradi wa LNG ni mradi wenye manufaa makubwa kwa Taifa na majadiliano haya ni muhimu, ndio yatakayoweka msingi wa kodi, mirabaha pamoja na ulinzi wa Tanzania kunufaika kiuchumi. Hivyo suala la mradi wa LNG ni kipaumbele kwa Serikali," amesema Mhe. Kapinga.

Kuhusu suala la kuagiza gesi ya LPG kwa mfumo wa uagizaji kwa pamoja, jambo hili linaendelea kuchakatwa, pia Serikali inaendelea na hatua za ujenzi wa gati katika Bandari ya Dar es Salaam ili kuwezesha Meli kubwa kushusha gesi ya LPG.

  Tanzania imeeleza mpango na utayari wake katika uendelezaji wa nishati ya nyuklia ikiwa ni moja ya vyanzo mbadala vya ...
29/08/2024



Tanzania imeeleza mpango na utayari wake katika uendelezaji wa nishati ya nyuklia ikiwa ni moja ya vyanzo mbadala vya nishati safi ya umeme kwa maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa jamii.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko wakati akiwasilisha Mpango wa Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Masuala ya Nishati ya Nyuklia kati ya Marekani na nchi za Afrika (US-Africa Nuclear Energy Summit) unaoendelea Jijini Nairobi, Nchini Kenya.

Katika mkutano huo unaojumuisha viongozi katika Sekta ya Nishati, Watunga Sera na Wataalam kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, Dkt. Biteko amesema Tanzania iko tayari kuendeleza nishati ya nyuklia ikiwa ni moja ya vyanzo vitakavyoiwezesha nchi kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika na ambayo inakidhi viwango vya kimataifa katika uhifadhi wa mazingira.

“Utayari wa Tanzania katika kuendeleza na kutumia nishati ya nyuklia unatiliwa mkazo katika Sera ya Nishati ya mwaka 2015, Sera ya Madini ya mwaka 2009, Mpango Kabambe wa Kuendeleza Sekta ya Umeme na Mkakati wa Nishati Jadidifu ambapo nyaraka zote hizi zinatambua umuhimu wa nyuklia kukidhi mahitaji ya nishati nchini.” Ameeleza Dkt. Biteko

Amesema chini ya uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali inaendelea kuchukua hatua muhimu zitakazowezesha matumizi ya nishati nyuklia k**a moja ya vyanzo vya nishati safi ambapo hadi sasa Tanzania ina mashapo ya madini ya urani takriban tani 58,500 ambayo yanaweza kutumika k**a chanzo cha uzalishaji wa nishati ya nyuklia.

Amefafanua kuwa, uwepo wa vyanzo mbadala wa vya umeme utawezesha nchi kuboresha mashirikiano yake ya kibiashara na nchi nyingine ndani na nje ya bara la Afrika na hivyo kuboresha uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

“Mpango huu wa kuwa na umeme wa kutosha utawezesha hatua ya kuunganisha gridi za umeme miongoni mwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika na baadaye katika maeneo mengine ya Bara hili.” Amesema Dkt.Biteko

  Wadau wa sekta ya afya mkoa wa Manyara wametakiwa kuhakikisha wanafanya miradi inayoendana na maadili ya Mtanzania.Hay...
29/08/2024



Wadau wa sekta ya afya mkoa wa Manyara wametakiwa kuhakikisha wanafanya miradi inayoendana na maadili ya Mtanzania.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga wakati akifungua mkutano wa wadau wa afya mkoa wa Manyara wenye lengo la kujadili mwenendo wa afya katika mkoa.

Mhe. Sendiga amesema kuwa ni vyema wadau wakatilia mkazo suala la Lishe na Utapiamlo, usafi wa mazingira na Tiba Mbadala.

Amewaomba wadau kushirikiana katika vipaumbele vya mkoa ili sekta ya afya iweze kushamili ikiwemo Bidhaa za afya ikiwemo madawa, vifaa tiba na vitendeakazi, huduma za uzazi na mtoto, magonjwa ya kuambukiza na yale yasiyopewa kipaumbele.

Mwisho amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuendelea kuimarisha afya mkoa wa Manyara ambapo mpaka sasa unajumla ya hospitali 12, vituo vya afya 37 na Zahanati 219. Ujenzi wa hospitali za wilaya mpya mbili Mbulu, na halmshauri ya Babati, ukarabati wa hospitali Kongwe - Kiteto, Mbulu Mji, Babati Mji, ujenzi wa vituo vya afya na Zahanati kila Halmashauri, ujenzi wa majengo ya dharura kule Mbulu mji, Hanang' na Babati mji.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wakuu wa wilaya, wakurugenzi, watendaji wa serikali na wadau wa maendeleeo wa mkoa.

  Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Menejimenti, Rasilimali Watu na Utawala Bw. Peter Mwakiluma amehitimisha mafunzo ya kuwajen...
29/08/2024



Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Menejimenti, Rasilimali Watu na Utawala Bw. Peter Mwakiluma amehitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko kwa kuwataka kuwa na misingi ya utumishi bora kwa kuvaa mavazi nadhifu sambamba na kufika kazini kwa muda unaotakiwa.

Bw. Mwakiluma amesema mtumishi wa umma hupimwa kwa nidhamu yake katika kuwahi kufika ofisini, mavazi anayo yavaa pamoja na kutekeleza majukumu husika.

"Inashangaza kuona mtumishi anachelewa kufika kazini lakini huyo huyo anataka muda wa kutoka atoke muda ule ule sasa jamani tutakuwa hatuwatendei haki wananchi", alisema Bw. Mwakiluma.

Katika mavazi amesisitiza kuwa mtumishi wa umma hutambulika kwa mavazi yake ambayo yapo kwenye msingi wake, akisema mavazi yenye maandishi hayatakiwi sambamba na kuvaa nguo zenye kuonesha sehemu kubwa ya mwili hayatakiwi.

Pamoja na kuhimiza hayo, Bw. Mwakiluma amempongeza Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Bi. Suzana Magobeko kwa kuandaa mafunzo hayo kwani yatakuwa na mchango chanya katika utekelezaji wa majukumu kwa watumishi wa kitengo hicho.

Amesema mafunzo k**a hayo ni muhimu hata kwa vitengo vingine kwani yanaongeza ari mpya kwenye ufanyaji kazi.

  Wakala wa Vipimo  Tanzania (WMA), imewahamasisha watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Ilala, kujenga...
28/08/2024



Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA), imewahamasisha watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Ilala, kujenga tabia ya kuwa makini na namna vipimo vinavyotumika kila wanapopata huduma na mahitaji mbalimbali.

Afisa Vipimo kutoka WMA Ilala, Yahaya Tunda, amesisitiza hayo leo, Agosti 28, 2024 wakati akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya WMA kwa watumishi hao wa NSSF, ambapo amebainisha kuwa jukumu kubwa la Wakala ni kumlinda mwananchi dhidi ya matumizi batili ya vipimo katika maeneo ya biashara, afya, usalama na mazingira.

Aidha, ameongeza kuwa majukumu mengine ya WMA ni kuiwakilisha nchi katika masuala ya Kivipimo ya kikanda na dunia, kufanya ukaguzi katika maeneo ya uzalishaji, njia za usafiri na maeneo ya biashara, na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa taasisi na wadau wa vipimo.

Tunda amefafanua kuwa, pamoja na kwamba WMA inawajibika kumlinda mwananchi dhidi ya matumizi batili ya vipimo, lakini wananchi pia wanapaswa kujilinda na kuchukua tahadhari hususani wanapopata huduma au mahitaji.

“Ni vyema kuwa makini na kujiridhisha kwamba vipimo vinavyotumiwa na mfanyabiashara ni sahihi na vimehakikiwa na WMA. Mathalani, ukienda kununua mbao, nenda na futi yako iliyohakikiwa, halikadhalika ukienda kununua saruji hakikisha inapimwa kwa usahihi kwenye mizani iliyohakikiwa. Vivyo hivyo kwa nyama, mboga mboga na bidhaa nyingine zote.”

Akifafanua zaidi, amesema kwa wenye magari, wanapokuwa katika vituo vya kujazia mafuta, wahakikishe wanakuwa makini pindi wanapohudumiwa, na ikitokea kutoridhishwa na upimaji husika, wawasilishe shauri hilo katika Ofisi za WMA zilizoko mikoa yote Tanzania Bara pamoja na mipaka yote ya nchi ili kusaidia kupunguza athari za udanganyifu katika vipimo na hivyo kuchagiza maendeleo.

Vilevile, ameongeza kuwa WMA inaendelea kupanua wigo wa huduma zake kwa kujikita katika maeneo mapya ya uhakiki wa Dira za Maji na Mita za Umeme ili kuhakikisha kuwa kunakuwepo na usawa katika utoaji wa huduma na malipo sahihi ya huduma hizo.

  Walimu zaidi ya 40 kutoka katika shule 20 Wilayani Ludewa Mkoani Njombe, wameanza mafunzo ya mbinu za stadi za kufundi...
28/08/2024



Walimu zaidi ya 40 kutoka katika shule 20 Wilayani Ludewa Mkoani Njombe, wameanza mafunzo ya mbinu za stadi za kufundisha Ili kukuza kiwango Cha ukuaji wa kusoma, kuandika na kuhesabu (K*K).

Mafunzo hayo ambayo hutolewa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Uwezo yamezinduliwa rasmi na Afisa Elimu msingi Mkoa wa Njombe Nelasi Mulungu kwa niaba ya Katibu Tawala mkoa Bi. Judica Omary.

Bi. Malungu amesema kuwa tatizo la K*K kwa mkoa wa Njombe lipo hasa kwa wanafunzi wa darasa la kwanza, lapili na darasa la tatu hivyo mafunzo hayo yatakuwa chachu ya ukuaji wa elimu kwa wanafunzi hao.

Grayson Mgoyi ni Mkuu wa Idara ya mawasiliano na uchechemuzi kutoka shirika la Uwezo Tanzania amesema mafunzo haya kwa Wilaya hiyo ya Ludewa yanafanyika kwa mara ya pili ambapo mwaka uliopita walimu 80 kutoka katika shule 40 walipatiwa mafunzo hivyo na sasa insfikisha jumla ya walimu 120 waliopata mafunzo Wilayani humo.

  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,  Dkt. Doto Biteko leo amewasili jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya kushi...
28/08/2024



Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko leo amewasili jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Pili wa Masuala ya Nishati ya Nyuklia kati ya Marekani na nchi za Afrika ( US-Africa Nuclear Energy  Summit).

Mkutano huo wa masuala ya Nyuklia  utahusisha mijadala kuhusu utayari wa Sekta ya Nishati katika kusimamia mnyororo wa thamani kwa ajili ya uendelezaji wa nyuklia pamoja na umuhimu wa kuwashirikisha wanawake na vijana katika Sekta.

Katika ziara hiyo, Dkt. Biteko ameambatana na Watendaji kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini.

  Mbunge wa Jimbo la Mlimba mkoani Morogoro, Godwin Kunambi amelalamikia vitendo vya matumizi mabaya ya madaraka kwa baa...
28/08/2024



Mbunge wa Jimbo la Mlimba mkoani Morogoro, Godwin Kunambi amelalamikia vitendo vya matumizi mabaya ya madaraka kwa baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa kwa kuk**ata watuhumiwa kisha kuwaweka ndani pasipo kuzingatia sheria inayowapa mamlaka hayo.
 
Kunambi ametoa malalamiko hayo bungeni Jijini Dodoma akihusisha tukio la kuk**atwa kwa wananchi 11 wa jimbo lake hivi karibuni huku akimtuhumu Mkuu wa Wilaya ya Kilombero akishirikiana na Mkuu wa Mkoa kutekeleza jambo hilo wakati wa mkutano wake wa hadhara wa utatuzi wa mgororo wa ardhi  baina ya wananchi wa kijiji cha Chiwachiwa na msitu wa hifadhi wa TFS, huku akiliomba bunge liunge mkono hoja yake.
 
Hata hivyo Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson wakati akitolea ufafanuzi hoja hiyo amesema kuwa sheria imewapa mamlaka Wakuu wa Wilaya na Mikoa kuagiza kuk**atwa kwa watu au mtu endapo watahisi wanahatarisha usalama wa watu wengine au wanahatarisha usalama wao binafsi, licha ya kuwepo kwa changamoto ya utekelezaji wa sheria hiyo.

Hata hivyo Spika amemueleza Mbunge huyo kuwa hoja yake haijakidhi masharti ya kujadiliwa k**a hoja ya dharura bungeni.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan afungua  Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wa...
28/08/2024



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan afungua Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 28 Agosti, 2024.

  Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa misitu imezindua kampeni ya kupanda miti zaidi ya Bilioni moja katika...
28/08/2024



Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa misitu imezindua kampeni ya kupanda miti zaidi ya Bilioni moja katika mikoa ya kaskazini ili kunusuru barafu ya mlima Kilimanjaro. Kampeni hii ya upandaji miti inakwenda sambamba na utekelezaji wa mikakati ya kupanda zaidi ya miti milioni 8 kwa mwaka katika Mkoa wa Kilimanjaro, utoaji elimu kwa umma kuhusu upandaji miti, na uhifadhi wa mazingira kupitia vipindi vya redio, televisheni, matamasha na maadhimisho mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. 

Naibu Waziri wa maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mhe. Prof. Patrick Alois Ndakidemi Bungeni Mjini Dodoma aliyetaka kujua Serikali imechukua hatua gani za muda mfupi, wakati na muda mrefu kunusuru theluji inayotoweka katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Aidha, Mhe. Kitandula alisema kuwa sababu kubwa ya kupungua kwa theluji katika Mlima Kilimanjaro ni ongezeko la joto duniani kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi yanayochangiwa na ongezeko la shughuli za kibinadamu hususan ukataji wa miti, kilimo, uchomaji moto katika maeneo yanayozunguka mlima, uwepo wa mvua chache na vipindi virefu vya ukame, na upepo mkavu kutoka bahari ya Hindi.

Mhe. Kitandula aliongeza kuwa kwa mikakati ya muda wa kati  Serikali inajielekeza katika kuhimiza matumizi bora ya ardhi na kuimarisha ulinzi katika maeneo yanayozunguka Mlima Kilimanjaro na kutekeleza mipango ya kudhibiti na kupambana na uchomaji moto mlimani.

Aidha, kwa upande wa mikakati ya muda mrefu, Mhe. Kitandula alilieleza bunge kuwa Serikali inaendelea kushirikiana na mashirika ya kikanda na kimataifa kutekeleza mikakati ya pamoja ya kuhimili na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni pamoja na kuboresha teknolojia za kilimo, kuongeza ufanisi wa matumizi ya maji, kupunguza uzalishaji wa gesi chafu na kurejesha mifumo ikolojia kwenye mlima na maeneo yanayozunguka.

   ——Uongozi, Menejimenti na Watumishi wote wa Wizara ya Afya tunakupongeza Dkt.  kwa ushindi wako wa kishindo kwenye Uc...
27/08/2024


——
Uongozi, Menejimenti na Watumishi wote wa Wizara ya Afya tunakupongeza Dkt. kwa ushindi wako wa kishindo kwenye Uchaguzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika.

  Na Mwandishi Wetu, Arusha.Tanzania inajivunia hatua ilizochukua za kuziba pengo la kidijitali nchini kwa kuongeza upat...
27/08/2024



Na Mwandishi Wetu, Arusha.

Tanzania inajivunia hatua ilizochukua za kuziba pengo la kidijitali nchini kwa kuongeza upatikanaji wa huduma bora za mtandao wa kasi kwa taasisi za Serikali na umma kwa ujumla kupitia utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed Khamis Abdulla ameyasema hayo leo Agosti 27, 2024 akifungua kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mradi huo kinachofanyika jijini Arusha.

Amesema kuwa anatambua mchango mkubwa wa Benki ya Dunia wa kuwezesha mapinduzi ya uchumi wa kidijitali nchini kupitia ufadhili wa mradi wa Tanzania ya kidijitali ambao pamoja na mambo mengine unahakikisha jamii zote za watanzania haziachwi nyuma katika zama hizi.

“Kupitia mradi huu hatujengi miundombinu bali tunatengeneza fursa za kidijitali kwa Watanzania kwa kuwaunganisha na huduma za kidijitali na kuweka msingi imara wa bunifu za TEHAMA zitakazolipeleka taifa letu mbele.”, amesema Katibu Mkuu Abdulla.

Bwana Abdulla amesema lengo la Serikali kupitia Wizara ni kukuza uchumi wa kidijitali kwa kuhakikisha miradi inayotekelezwa chini ya mradi wa Tanzania ya kidijitali inafanyika kwa ubora na kasi inayotakiwa ili kuijenga Tanzania yenye uwezo mkubwa wa matumizi ya teknolojia ya kidijitali.

Ameizungumzia miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa minara 758 Tanzania Bara na Zanzibar, itakayowezesha mawasiliano vijijini na upatikanaji wa huduma ya mtandao wa kasi kwa ofisi 968 za umma ili kuongeza uwajibikaji na ufanisi.

Ameongeza kuwa wamejianga kuwajengea uwezo wataalamu wa TEHAMA 500 kwa kufadhili mafunzo ya muda mrefu na mfupi ndani na nje ya nchi ambapo mpaka sasa watumishi wa umma 50 tayari wanaendelea na mafunzo ya muda mrefu nje ya nchi maeneo ya teknolojia zinazoibukia.

Kwa upande wake Bw. Paul Seaden, Kiongozi wa Kikosi kazi wa Benki ya Dunia amesema kikao hicho cha tathmini ya mradi ni muhimu ili kufanya mapitio na kuhakikisha mradi unaendelea kutekelezwa kwa ufanisi na matokeo chanya.

Mwisho ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano inayoutoa na wapo tayari kumalizia miaka miwili iliyobakia ya utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa Tanzani

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa...
27/08/2024



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mkoani Kilimanjaro tayari kwa kuelekea mkoani Arusha ambapo ni Mgeni Rasmi kwenye Ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kitakachofanyika kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) tarehe 28 Agosti, 2024.
Mhe. Dkt. Samia amewasili uwanjani hapo akitokea nchini Kenya ambapo alihudhuria hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mhe. Raila Amolo Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), tarehe 27 Agosti, 2024

27/08/2024

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo...
27/08/2024



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi tayari kwa kuhudhuria hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mhe. Raila Amolo Odinga, Waziri mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya anayewania nafasi ya Mwenyekiti Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) ikiwa ni mualiko kutoka kwa Rais wa nchi hiyo Dkt. William Samoei Ruto. Hafla hiyo itafanyika katika Ikulu ya Nairobi na kuhudhuriwa na Wakuu wa nchi mbalimbali, tarehe 27 Agosti, 2024.

  Kufuatia mwaliko wa Rais William Ruto wa Kenya, Rais Samia Suluhu Hassan leo Agosti 27, 2024 anatarajiwa kufanya ziara...
27/08/2024



Kufuatia mwaliko wa Rais William Ruto wa Kenya, Rais Samia Suluhu Hassan leo Agosti 27, 2024 anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi nchini humo.

Akiwa nchini Kenya pamoja na mambo mengine Rais Samia atashiriki hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Waziri Mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika.

Hafla hiyo itafanyika Ikulu Jijini Nairobi na kuhudhuriwa na Wakuu wa Nchi mbalimbali.

Address

Kumbukumbu

255

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Telephone

+255713422313

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Michuzi TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Michuzi TV:

Videos

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Opening Hours
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Videos
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share