Darubini Tv

Darubini Tv The best online television Kwa matangazo ya biashara wasiliana nasi kwa simu namba
0764 308558

11/04/2023
15/06/2022

MWANDISHI WA HABARI ARUSHA KUSHIKILIWA NA WATU WALIO JITAMBULISHA POLISI

Mwandishi wa HABARI wa Wasafi Media Protte Mmanga amek**atwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi maeneo ya Chuo Cha Technical College Arusha wakisema kuwa wanampeleka kwa RCO ajili ya kumhoji na Polisi hao walikuwa na Gari namba za usajili T576 DTJ

Hata hivyo ofisi ya mpelelezi wa Mkoa Rco imesema kuwa Haina Taarifa hizo za kuk**atwa kwake.
na hii si mara ya kwanza kutokea manyanyaso na ukatili kwa waandishi wa habari kutekwa na kufanyiwa vitendo viovu katika mikoa mbali mbali

10/06/2022

Mahak**a ya Hakimu Mkazi Arusha imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake sita katika kesi ya uhujumu uchumi namba ishirini na saba ya mwaka 2021 kutokana na hati ya mashtaka kuwa na mapungufu pamoja na ushahidi kugubikwa na maswali mengi.

18/03/2022
10/03/2022
02/12/2021

Mfalme alipata hamu ya kula samaki akaamua kutembelea ufukweni siku hiyo ikawa samaki hakuna wavuvi wote wamekosa samaki
Wakati anarudi na wafuasi wake ndipo akakutana na Mvuvi mmoja tu alie bahatika kupata samaki watatu 3 Mfalme akataka kuwanunua Mvuvi akakataa kuwauza samaki wake.

Mfalme akaomba auziwe japo mmoja Mvuvi akamwambia Mfalme huyu samaki mmoja naenda kumkopesha sijui k**a nitalipwa,
Na huyu mwengine naenda kulipa deni sijui k**a nitalimaliza na huyu wa tatu naenda kumtupa.

Mfalme akachukizwa kwa majibu yale akaamuru anyang'anywe wale samaki nae atupwe gerezani,Akiwa kwenye Kasri Mfalme akaamuru yule mvuvi aletwe mbele yake ili amuhoji.Kwanini umekataa kuniuzia mimi samaki wakati unaenda kumkopesha tena hujui k**a utalipwa,,? Wapili unaenda kulipa deni na hujui k**a utalimaliza,,? Kisha mwengine unaenda kumtupa wakati mimi nina shida na samaki,,?

Mvuvi akamjibu Mfalme
Huyu ninae kwenda kukopesha sijui k**a nitalipwa naenda kuwapa wanangu
Kwani kuwaudumia watoto hujui k**a na wao watakuhudumia.

Na huyu ni nae kwenda kulipa deni sijui k**a nitalimaliza nawapelekea wazazi wangu,
Kwa waliyo nitendea siwezi kuwalipa hata niwape nini.

Na huyu ninae kwenda kumtupa naenda kumpa Mkewangu,Kwani hao hawajui kushukuru wala kutosheka, hata uwape nini siku akicharuka tu atasema hujamfanyia chochote tokea umuoe.

09/10/2021

MAPENZ NIACHE MAANA UMENITESA SANA
Ni real story ya mwana dada farida baada ya kuwa katika hali ya kulizwa kuumizwa kila mara na swala zima la mapenz
Ni baada ya kuwa na mpenz wake praygod na kutambulishana mpaka nyumbani na baada ya siku walifikia muhafaka wa kufunga ndoa kabla ya ndoa ilikuwa ni send off ila praygod hakuweza fika kwenye send off na kuzua utata mkubwa
Dar? Kumbe praygod ana mke na watoto wa3 na wale wazazi waliokuja nae mwanzo si wazazi wake bali aliwakodisha kwa pesa ili wazazi wa farida watambue yakwamba hawa ni wazazi wenzake na si mara ya kwanza kwa praygod kufanya hivo
Hata utajiri wake wengi hawajui kazi yake ndipo mwanamke mrembo sana katokea akamfata farida uku analia na kumnongoneza masikioni ndipo farida alipaza sauti na kusema noooooooooo!!!!!??
K**a wataka niendelee na hii story comment neno nimependa nami nitaendeleza hii story

04/10/2021

MKASA WA KUSISIMUA: MAFANIKIO YASIKUFANYE UKADHARAU ULIPOTOKA, KUMBUKA WALIOKUSAIDIAGA
# Inasikitisha sana
Maureen alizaliwa na kulelewa na Mama ambaye ni kichaa wale wakuzunguka na kuokota vitu barabarani, pamoja na ukichaa wake lakini yule mama alimlea vizuri binti yake akimpa chakula mpaka alipofikia umri wa kwenda shule. Kwa bahati nzuri Maureen alipata msamaria mwema ambaye alimsomesha, ingawa yule msamaria mwema alijaribu kumchukua yule Mama na kukaa naye lakini haikusaidia. Mama yule alionekana kuchoka na kuzeeka mno kutokana na ugumu wa maisha anayopitia na hali yake ya ukichaa, alionekana k**a bibi wa miaka 90, ngozi yake ilionekana kusinyaa na macho kufifia, hii yote ni kutokana na kushinda kutwa nzima akizunguka juani majalalani, masokoni na barabarani kuomba mwanae Maureen apate kitu cha kula.
Kila aliporudishwa nyumbani siku mbili alirudi mtaani kuokota makopo na kula matakataka. Pamoja na ukichaa wake lakini kila siku ilikuwa ni lazima kwenda kwenye ile nyumba alikokuwa akilelewa binti yake Maureen kumsalimia na kila siku alikuwa akibeba chakula kwaajili ya binti yake.
Ili Maureen ale kile chakula illibidi kila siku kumuwekea chakula kizuri kwenye mfuko na pale alipokuwa akiomba basi walimpa kile chakula na yeye kabla ya kula alimletea binti yake. Maisha yaliendelea hivyo mpaka Maureen alipoenda chuo ndipo Mama alibaki mpweke akizunguka zunguka tu mtaani. Kule chuoni Maureen alifanya vizuri na alipomaliza chuo alifanikiwa kupata mchumba.
Alirudi kumtambulisha kwa wale wazazi waliomlea, lakini chakushangaza tusiku aliyorudi kumtambulisha mchumba wake na Mama yake alikuepo. kwa uoga na aibu aligoma kabisa kumtambulisha, ingawa yule mama alimng'ang'ania lakini alidanganya kuwa ni kichaa tu ambaye alizoea kumpa zawadi. Siku iliisha na mipango ya harusi ikafanyika, baada ya miezi mitatu ikafanyika harudi kubwa na ya kifahari.
Wakiwa katikati ya sherehe Maureen alishangaa kumuona Mama yake anaingia akiwa maevaa nguo zake chafu vilevile, Mama alisogea mpaka mbele watu wakimshangaa akatoa mfuko wake wa chakula na kumkabidhi binti yake ili ale. Maureen aliukataa na kuanza kupiga kelele lakini kabla hajafanya chochote Mume wake aliuchukua ule mfuko na kuufungua kisha kuanza kukila kile chakula.
Watu wote walishtuka na kuanza kushangaa, lakini yule bwana harusi alichukua Mic na kusema. Huyu ndiye Mama mkwe wangu, Mama mzaa chema. Najua mnamshangaa na hali yake lakini kwa hali hii hii ndiyo alimza na kumlea mke wangu na ndiye atakuwa Bibi wa watoto wangu" Kila mtu alibaki kushangaa hata yule binti alishangaa huku machozi ya kimtoka, yule kijana alimgeukia mkewe.
"Najua sababau za wewe kuficha lakini unapaswa kutambua kuwa nakupenda na nampenda Mama yako k**a vile ninavyompenda Mama yangu. Ulimwengu mzima utamuona kichaa lakini yeye ndiye aliyekuzaa na kukufanya uwe hivi leo. Unavyoniona hivi Baba yangu alinizaa na kunitelekeza, pamoja na pesa zake akili zake lakini alinitelekeza, sasa hembu jiulize kichaa ni nani kati ya mwanaume aliyetelekeza mwanae au Mama k**a huyu ambaye mpaka leo anajua bado ni mtoto na anakujali kwa chakula?"
Ukumbi mzima uliibuka kwa vifijo, watu wakishangilia Maureen akiwa anatokwa na machozi alimkumbatia Mama yake, alichukua kile chakula na wote wakaanza kukila. Yule kijana ndiyo alimualika kwani siku aliyoenda kutambulishwa na kumuona alihisi kitu hivyo akaamua kufuatilia mpaka alipoujua ukweli. Alijua sababu ya mchumba wake kuficha lakini alitaka ulimwengu mzima kujua kuwa hajali na anampenda bila kujali historia yake.
HAKUNA K**A MAMA, UPENDO WAKE HAUNUNULIWI WALA HAUPUNGUI USICHOKE KUMUAMBIA NAMNA UNAVYOMPENDA.
K**a unampenda mama yako kwa namna yeyote alivyo hebu kwa ujasiri TYPE AMEN kisha SHARE post hii kila atakaeiona baraka za mama yako zitawale maisha yako.

11/09/2021

:Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Naibu katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi. Amina Mohammed, Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

09/07/2021
01/07/2021

Address

ARUSHA
Arusha

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Darubini Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share


Other News & Media Websites in Arusha

Show All