![Kibu Denis Prosper ( ) mshambuliaji wa Simba Sc, amekuwa moto wakuotea mbali kwenye kampeni hizi za kimataifa kwenye Kom...](https://img5.medioq.com/766/896/1564333347668962.jpg)
16/01/2025
Kibu Denis Prosper ( ) mshambuliaji wa Simba Sc, amekuwa moto wakuotea mbali kwenye kampeni hizi za kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu wa mwaka 2024/25.
Licha ya wadau mbali mbali kuandika maneno ya kumnyooshea vidole kutokana na kiwango cha msimu uliopita, yeye ameamua kusimama katika ukweli na kuamini kile ambacho anakifanya, tena kwa ustadi wa juu.
Kibu msimu huu kwenye Kombe la Shirikisho amehusika pakubwa katika matokeo chanya ya Club hiyo kwani tangu kuanza kwa kampeni hizi tayari amesha cheka na Nyavu mara tatu. Akifunga goli moja kwenye hatua ya mtoano dhidi ya Al Ahli Tripol baadaye katika hatua ya makundi akifunga magoli mawili muhimu dhidi ya Cs Sfaxien Fc katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Yeye ndiye mchezaji wa Simba anayeonga kwa kupiga mashuti kuelekea Langoni, lakini pia ndiye mchezaji wa Simba anayeongoza kufanya mikimbio (dribbles).
ni Baller.