11/01/2026
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng.Godfrey Kasekenya amezungumzia umuhimu wa viongozi mkoani Arusha kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna bora ya kutunza na kulinda miundombinu inayojengwa ili idumu kwa muda mrefu, kupendezesha na kuchochea ukuaji wa mji huo wa utalii nchini.