25/08/2024
π·βοΈ Uchambuzi
βπ»Mechi kuanzia dakika ya kwanza mpaka ya 98 ni k**a vile ya mpira wa kikapu , hakuna aliye park Bus , hakuna aliyetaka ku control mchezo ni kupishana tu na mechi ikiwa hivi huwa inaamuliwa na nini ? Ni nani atakuwa mfanisi mbele ya goli ( hasa ukizingatia timu zote kwenye kuzuia walionekana wana shida bado )
βπ»Kitu unawapa credit kubwa Chelsea ni kutoa adhabu katika kila kosa na pengine hata ingekuwa mbaya zaidi ya 6 kwa Wolves
1: Kwasababu ya Wolves ya kutokuwa compact katika muundo wao wa uzuiaji , Chelsea walitumia wachezaji wengi ndani ya uwanja ...kwanini ?
2: Ili wafike mbele haraka na kwa idadi kubwa ya wachezaji wakiwa na 3-2-2-3 ( Gusto anaingia ndani kuwa na Caicedo wakiwa mbele ya Fofana Colwill na Cucurella ) huku Enzo na Palmer juu zaidi nyuma ya washambuliaji
3: Hii iliwapa Chelsea : idadi kubwa ya wachezaji mbele na walifika haraka , hasa kwa pasi za chini zaidi " ground passes " zenye kasi .
4: Hapo ndio nampa credit yake Jackson , akicheza goli la Wolves kalipa mgongo alikuwa k**a daraja kwa wenzake : mipira kutoka kwa walinzi na viungo wa chini Jackson anashuka nyuma ya viungo wa Wolves na ku connect na : Palmer + Enzo
βπ»Wolves walicheza vizuri kipindi cha kwanza , runs za kutosha , quick passing kwenda mbele , kushinda second balls na nafasi nzuri za kufunga , kipindi cha pili ndio ilikuwa kinyume chake . Hapo Chelsea walikuwa wanafanya " Pass forward, run forward " halafu malizia nafasi
NOTE
1: Najua Maresca atawaambia vijana wake mshindi mzuri sana lakini kwenye uzuiaji kuna kazi ya kufanyika
2: Matheus Cunha, Larsen na Lemina hao ndio wameitendea haki jezi ya Wolves leo
3: Caicedo apunguze idadi ya touches mguuni kabla ya pasi
4: COLD PALMER ... hata hatumii nguvu , akili nyingi , ufundi wa kutosha , jicho la pasi , anajua spaces zipo wapi ( Hat trick ya assists )
5: MADUEKE .. ni k**a amemwambia kocha hii namba yangu . Tangu dakika ya kwanza alikuwa hatari . Ait Nouri akameze Panadol .