28/10/2024
Dhana ya mzizi wa neno
mzizi wa neno ni sehemu ya neno ambayo haibadiliki hata neno lenyewe likinyambuliwa
Mzizi wa neno pia ni sehemu ya neno inayobeba maana kuu
aina za mzizi
✓Mzizi huru-mzizi ambayo inajitosheleza kimaana k**a neno kamili
maneno yenye asili ya kigeni ambayo kwa kawaida yana kiishio e,u,i katika kauli ya kutenda huwa na mzizi huru
mfano :Samehe Samehea Samehewa
mzizi hapa ni samehe ambayo pia ni neno lenye maana kamili
mzizi tegemezi: ni sehemu ya neno inayobeba maana kuu ila haijitoshelezi kimaana
maneno/vitenzi vinavyoishia kwa kiambishi a
huwa na mzizi tegemezi
taz :
cheza chezea chezewa chezesha
mzizi wa neno hapa ni chez:
Swali:
Taja mzizi wa neno katika maneno yafuatayo:
potea
Dhuru
haribu
samehea