Darubini Ya Lugha

Darubini Ya Lugha Am a teacher of Swahili, a father and a Chelsea fun.

Tuzidi kuelimishana.👇👇
20/03/2025

Tuzidi kuelimishana.👇👇

Kauli ya siku 👇👇
27/11/2024

Kauli ya siku 👇👇

Tuzidi kujielimisha tukikuzana.
09/11/2024

Tuzidi kujielimisha tukikuzana.

25/04/2024

Bainisha virai kwenye sentensi hii:

Musa angelima mapema angevuna vizuri.

11/04/2024

tiktok.com/

Follow my TikTok page. Let's grow together

10/04/2024

Je,unafahamu ni makosa kusema.
Lisaa
Masaa

Mfano: Safari yetu ilichukua masaa matatu.

Kiswahili sanifu ni saa!!
Safari yetu ilichukua saa tatu.

https://www.youtube.com/Kwa wapenzi wa lugha ya Kiswahili si tusaidiane kukua jamani. Mnifikishe subscribers angalau 50 ...
06/04/2024

https://www.youtube.com/

Kwa wapenzi wa lugha ya Kiswahili si tusaidiane kukua jamani. Mnifikishe subscribers angalau 50 ili niweze kupatiwa nafasi ya kuenda LIVE.🙏

Kwa wapenzi wa lugha hii yetu ashirafu ya Kiswahili 🇰🇪

06/04/2024

Kanusha.

Mama yu mgonjwa.

25/03/2024

Hasidi mpe kiti akae/Hasidi mpishe njia apite.

Tunahimizwa kuwalipa wabaya wetu kwa mema.

03/01/2024

Maskini hana makuu, haja yake ni nafuu aidha Maskini hachagui,apewacho hupokea.

Miaka 9 mtawalia nikifunza somo la Kiswahili darasa la 8,nachukua fursa hii kujishukuru kwa matokeo mazuri niliyokuwa ni...
25/11/2023

Miaka 9 mtawalia nikifunza somo la Kiswahili darasa la 8,nachukua fursa hii kujishukuru kwa matokeo mazuri niliyokuwa nikiandikisha licha ya changamoto nyingi. Naamini niligusa wengi na kuwafanya wakipende Kiswahili. Mtaala wa 8:4:4 kwangu ulikuwa shwari. Nikiamini katika maisha huwa mashindano. Kuna mshindi na mshinde. Daima niliibuka mshindi japo haikuwa rahisi. Kuingia 6:30am na kutoka 6:30pm huku wengi wakidhani sikuwa na la kufanya. Kejeli na masimango nilivumilia ili tu niridhishe nafsi yangu. Wengi hawakuelewa.

Asante sana Nakuru,Kiambu, Kajiado na tena Kiambu.

Asante kwa maelfu ya wanafunzi niliowahi tagusana nao. Najivunia jinsi mlivyofurahia lugha ya Kiswahili. Daima nyinyi ni mabalozi wangu.

Ufanisi huu nauelekeza kwa mama yangu mzazi. Wewe ndiwe umeishi kuwa wa kwanza kupata habari za ushindi matokeo yatolewapo.

Mungu zidi kunipa bidii,maarifa na ubunifu tunapoingia kwenye daraja jingine la umilisi wa C.B.C
Historia yangu itaandikwa mahali.🙏

KCPE RANGE 0-99 marks 2060 pupils100-199 marks 383025 pupils200-299 marks 650278 pupils300-399 marks 352782 pupils400-50...
23/11/2023

KCPE RANGE
0-99 marks 2060 pupils
100-199 marks 383025 pupils
200-299 marks 650278 pupils
300-399 marks 352782 pupils
400-500 marks 8525 pupils

29/10/2023

"Hakuna majuto katika maisha. Ni funzo huwa tunajifunza."

24/10/2023

Mradi unapumua, mengine yote yanawezekana.Usiende nguu kamwe!

19/10/2023

"Iwapo hutafuata unachotaka,hutawahi pata. Iwapo hutauliza,daima jibu litasalia kuwa La! Iwapo hutajaribu kupiga hatua,daima utasalia papo hapo. Jibidiishe mwanangu. Ipo siku."

18/10/2023

Makovu kwenye mwili wangu huelezea kisa changu. Hunikumbusha jinsi ambavyo maisha yalijaribu kuniangusha japo yalishindwa. Mungu ni mkuu.

12/10/2023

"Kuna jambo moja gumu ambalo sote tunafaa kujifunza. Katika maisha yetu yote lazima tuishi kung'ang'ana iwapo tunahitaji kuishi vyema. Haijalishi wewe ni nani,hadhi au cheo chako, lazima uendelee kung'ang'ana kwa chochote utakacho. Ufanisi haujileti tu,hutafutwa."

12/10/2023

"Daima usiwahi kumsahau aliyekusaidia wakati wengine wote walipotoa vijisababu."

Address

Elburgon
Rift Valley

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Darubini Ya Lugha posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Darubini Ya Lugha:

Share