23/05/2024
📶 TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO ALHAMISI MAY 22, 2024
⛳ Ipswich imempa Meneja Kieran McKenna mkataba mpya ulioboreshwa kwa matumaini ya kusalia naye huku kukiwa na nia ya Manchester United , Chelsea na Brighton kumchukua.
SOURCE : The Sun Football
⛳ Chelsea Football Club wako kwenye mazungumzo na wawakilishi wa McKenna kuhusu kocha huyo mwenye umri wa miaka 38 kuwa Meneja wao mpya kwa ajili ya msimu ujao.
SOURCE : Football Insider
⛳ Kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva, 29, anaweza kuondoka msimu huu ikiwa Manchester City itapokea ofa ya takriban £50m.
SOURCE : Football Insider
⛳ Timu ya taifa ya England football team inaweza kumteua Meneja wa zamani wa Chelsea Mauricio Pochettino ikiwa Gareth Southgate ataondoka wadhifa wake baada ya Euro 2024.
SOURCE : Telegraph
⛳Kocha anayeondoka Chelsea Muargentina Mauricio Pochettino, 52, angependa kuzungumza na Manchester United iwapo watamfuta kazi Meneja wao Erik ten Hag.
SOURCE : Times
⛳ Chelsea Football Club imeunda orodha fupi ya wagombea wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi ya Pochettino na wanatarajia kufanya uteuzi baada ya siku chache zijazo.
SOURCE : The Athletic FC
⛳ Mshambulizi wa SSC Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 25, anatazamiwa kukataa ofa kutoka kwa klabu za PSG Paris St-Germain na Saudi Arabia huku akitarajia kuhamia katika Ligi ya Premier huku Chelsea ikimhitaji zaidi.
SOURCE : Teamtalk
⛳ Arsenal wako tayari kumnunua kipa wa Feyenoord na Uholanzi Justin Bijlow, 26, huku wakitarajia mlinda lango wao wa England Aaron Ramsdale, 26, kuondoka msimu huu.
SOURCE : The Mirror Sports
⛳ Tottenham Hotspur wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Brazil Richarlison, 27, ili kutoa nafasi kwa mshambuliaji wa Uingereza na Bournemouth Dominic Solanke, 26.
SOURCE : talkSPORT
⛳ Wawakilishi wa mchezaji wa ManchesterCity Kevin De Bruyne walifanya mazungumzo na klabu mpya ya MLS San Diego FC , lakini hakuna daalili kwamba kiungo huyo wa kati wa Ubelgiji, 32, yuko tayari kuhamia Marekani.
SOURCE : The Athletic FC
⛳Crystal Palace wameafikiana na beki wa kati wa Morocco na Real Betis Chadi Riad, 20, katika mkataba wa thamani ya hadi £14m.
SOURCE : Standard
⛳ Golikipa wa England Jordan Pickford, 30, ametoa dalili ya wazi kwamba atasalia na Everton Football Club licha ya kuivutia Chelsea.
SOURCE : The Mirror Sports
⛳Mkurugenzi wa michezo wa Crystal Palace Dougie Freedman, 49, amekataa ofa kutoka kwa Newcastle United kuchukua nafasi ya Dan Ashworth katika nafasi k**a hiyo na atasalia na The Eagles.
SOURCE : Football Insider
⛳Mshambulizi wa Slovenia Benjamin Sesko, 20, ambaye yuko kwenye rada ya Chelsea FC na Arsenal, ataamua hatimana yake kabla ya michuano ya Euro ikiwa anataka kusalia RB Leipzig au kuondoka.
SOURCE : Fabrizio Romano
⛳ Newcastle wanakaribia kuwasajili wachezaji wawili wa safu ya ulinzi ya Uingereza Tosin Adarabioyo, 26, na Lloyd Kelly, 25, ambao watakuwa wachezaji huru mikataba yao katika klabu ya Fulham na Bournemouth itakapokamilika msimu huu, huku Eddie Howe pia akimtaka fowadi wa Crystal Palace Michael Olise, 22, ingawa Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa wa kikosi cha wachezaji chini ya miaka 21 ambaye anamezewa mate na vilabu vingi lakini yupo tayari kufanya kazi na Eddie Howe.
SOURCE : Teamtalk