17/05/2022
Hizi ni baadhi ya taarifa utakazozisikia katika Matangazo yetu ya leo jioni.
-Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo inaadhimisha hii leo kile inachokiita miaka 25 ya ukombozi wake tangu pale Hayati rais Laurent Dรฉsirรฉ Kabila alimpomfurusha madarakani Hayati rais Mobutu Seseseko. Ila, miaka 25 baadaye, raia wa Congo wanajiuliza maana ya "ukombozi" huo.
-Mataifa ya Bara Afrika yamehimizwa kuanzisha hazina ya pamoja itakayosaidia katika kuendesha miradi ya kibinafsi na baadae kusaidia bara hilo kujiepusha na utegemezi wa misaada ya ughaibuni kuendeleza miradi yao. Hii miongoni mwa kauli zingine ndizo zimetawala kongamano la 9 la miji ya Bara Afrika linalondelea nchini Kenya.
-Rais Joe Biden wa Marekani amebadilisha uamuzi wa mwaka 2020 wa mtangulizi wake, Donald Trump, wa kuwaondoa wanajeshi wa Marekani kutoka Somalia. Msemaji wa idara ya Usalama ya Marekani Adrienne Watson amesema mara hii nchi hiyo itapeleka wanajeshi takribani 500, wakiwa pungufu ikilinganishwa na 700 waliondolewa na Trump.
-Urusi imesema wapiganaji wa Ukraine 265 waliokuwa wamejificha kwenye kiwanda cha chuma cha Azovstal kwenye mji wa Mariupol kwa wiki kadhaa sasa, wamejisalimisha chini ya makubaliano yaliofikiwa na Kyiv.
-Na vuguvugu la Hezbollah la Lebanon na washirika wake wanaounga mkono harakati za kundi hilo wamepata pigo baada kupoteza wingi wa viti bungeni katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumapili nchini humo.