Queen aucer jab$

Queen aucer jab$ Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Queen aucer jab$, Record Label, Music, Nairobi.

26/11/2019

SIMULIZI: MY LIFE (maisha yangu)
MTUNZI: AISHA KHAN
SEHEMU YA 01

UTANGULIZI: kwa Jina naitwa Aisha Ibrahim mtoto wa Ibrahim Nina umri wa miaka 23 Naishi kwa mama mlezi Baada ya wazazi wangu wote kufariki kwasababu ya gari na kuniacha Mimi nimehitimu kidato cha Sita, kabla wazazi wangu hawajafariki tuliishi maisha ya furaha, yenye upendo ndani yake kiukweli baba yangu alikuwa anajituma Sana hivo maisha yetu yalikuwa mazuri maana tulikuwa na gari tatu baba yake, mama yake pia na Mimi yangu, nilipohitimu kidato cha Sita kwa kuwa nilikuwa nasomea udokta hivo nilipenda Baada ya kumaliza niende university Ila haikuchukuwa siku nyingi Baada ya kuhitimu wazazi wangu walipata ajali hapo hapo wakafariki, kwa kuwa nilikuwa sina ndugu wakaribu walijitokeza watu wengi wakidai walikuwa wanamdai baba, hivo kila kitu tulichokuwa nacho kilichukuliwa nikabaki hapo bila nyumba wala sehemu ya kujihifadhi, kwa bahati nzuri au mbaya nilipata msamalia mwema Aliekuwa Rafiki yake na marehemu mama yangu hivo alinichukuwa nikaenda kuishi kwake, mama huyo ana wavulana wakubwa wawili mmoja David mwingine Nicolas Pamoja na waschana wawili mmoja Nasra mwingine Sabrina, maisha yake ni mazuri mno maana alikuwa ni mfanyakazi wa selekalini, nilipofika kwa huyo mama maisha niliokuwa natarajia ntaishi sikuyapata maana nilitegemea ntapelekwa chuo k**a wengine ila Badala ya kupelekwa chuo niligeuzwa mfanyakazi wa ndani hata mfanyakazi aliekuwepo alifukuzwa nikabaki mimi, kiukweli Mimi sikuzowea maisha ya tabu au ya kufanya Fanya kazi ngumu ngumu.

SONGA NAYO!

Siku moja nilikuwa natoka Sokoni kuhemea nikakumbana na Rafiki yangu jina lake Nisha ndipo nikamsimamisha na kusema: Ndo unipite hivo!

Nisha alitabasamu kisha akasogea pale nilipo akasema: mwenzangu! Acha tu Enhe! Wapii!!

Nikamjibu: nyumbani, si unaona natoka market!

Nisha: tuachane na hayo embu nikuulize Unajuwa ni bahati kukuona maana Duh! Enhe unafikiriaje kuja chuo?

Nikamjibu: Mimi sio wakusoma tena maisha yangu ni mabaya sana.

Nisha: come on Aisha! Kumbuka una upeo mkubwa kuhusu uganga sasa Ukisema hutomalizia what about your life?

Nikamjibu: Hakuna usichokijuwa napitia wakati mgumu Sana kufikiria Unajuwa Nisha sasa hivi siwezi kuya control maisha yangu.

Nisha: I know but David Anasemaje?

Nikamjibu: Achana na David Yule sio mtu.

Nisha: by the way! Unajuwa Nampenda sana.

Nikamjibu: I know ila anatabia zakihuni.

Nisha: kwahio bado anakutaka?

Nikamjibu: of course haniheshimu k**a dada yake.

Nisha: mamy nenda home mi naenda kumuona daddy nikizani next week ntakuwa free.

Nikamjibu: nakuonea wivu.

Nisha: no! Ipo siku utapata uhuru ila shule letu linakuhitaji sana.

Nikamjibu: sawa Usikose kuja lakini.

Nisha: naku promise.

Tuliagana na Nisha akaondoka Nami nikaendelea na safari yangu, nilipofika nyumbani nilisimama nyuma ya mlango wa geti huku nikisita kugonga mlango maana nikiingia ndani matusi yanaanza, nikiwa nimesimama hapo alikuja David akiwa yupo ndani ya gari aliponifikia akisimamisha gari na kusema: wewe vipi?

Sikutaka marefu nilibisha hodi Mlinzi akafungua mlango nikaingia.

Baada ya siku moja nilikuwa Nipo jikoni David akaja huku akiimba mziki nilipoiskia sauti yake moyo ulihama ile nataka kutoka nje kwa bahati mbaya nikamgonga, David kwa uhuni wake alinishika mgongoni kisha akanivutia kwake huku akiendelea kuimba, kiukweli tabia ya David Ilikuwa hainifurahishi hata Kidogo ndipo nikaanza kujaribu kujitoa kwake, David kwa sauti ya Chini akaniuliza: come on Aisha! Mbona mgumu Sana wewe!

Machozi yalianza kunitiririka huku nikiwa najaribu kujitoa kwake, muda Huo alikuja Nicolas mdogo wake David alipofika hakupendezwa na kitendo kile ndipo akamuuliza: Ndo nini bro?

David aliniachia kwa zarau kisha akamuuliza: inakuhusu nini?

Nicolas: unachokifanya kwa Huyu binti this's violence.

David: kwahio!

David aliondoka na kutuacha hapo, kiukweli Sikuamini K**a Nicolas angenitetea mbele ya kaka yake namna hio maana sio Kawaida yake ndipo nikamwambia huku nikilia: Nashukuru.

Nicolas: kuwa makini na Huyu mtu.

Nilikubali kwa kutikisa kichwa kisha nikaendelea na kazi zangu, Nicolas hakuchukuwa Muda akaondoka, Nilipomaliza kuandaa nilianza kumfuata mmoja Baada ya mwingine kwenye chumba chake nilipofika kwenye chumba cha mama niliingia bila ya kubisha hodi maana mlango ulikuwa wazi, nilipoingia nilimkuta mama akiwa amekaa huku akisoma kitabu kiukweli jicho aliloniangalia nilijuta Kwanini niliingia bila kubisha hodi ndipo akaniuliza huku akiwa amenikunjia uso: hujui kubisha hodi?

Nilitetemeka mno ndipo nikamjibu: Nisamehe mawazo.

Mama: mawazo gani?

Nikamjibu: kuhusu shule.

Mama: utaenda mwezi kesho.

Alipoongea hivo aliangua kicheko kisha akasema: pole Sana my dear Kwanini unasahau mapema! Yatima hasomagi kwanza wewe sio Yatima si upo Juu ya miaka 18 eeeehh! Vumilia ndo hivo.

Nikamjibu: karibu mezani.

Mama mlezi: wewe ndo Umeandaa?

Nikamjibu: Ndio.

Mama: aisee uwe umepika vizuri si Unajuwa tena wewe mbovu wakupika.

Nikamjibu: mum Naomba niende chuo basi pesa utakayoitumia kwa kunilipia Ada ntairudisha Baada ya kumaliza chuo.

Mama: tatizo Watoto wangu wasome na wewe usome Unajuwa hii ni aibu kubwa upande wa familia yangu! Subiri wote wamaliza shule hata Sabrina msubiri amalize kidato cha tatu aingie cha sita akimaliza aingia chuo kikuu akimaliza wewe ndo Utaingia chuo unachokitaka ila yahitaji Subira.

Sikutaka marefu nilitoka nje huku nikiwa nimenywea nilipofika kwenye kordo machozi yalianza kunitiririka, muda Huo Sabrina alikuwa anatoka chumbani kwake huku akiwa ameshikilia glasi ya maji aliponiona Nipo kwenye mawazo mengi alisogea karibu yangu kisha akanimwagia maji akijifanya k**a kanimwagia kwa bahati mbaya, nilianza kuyakamua mavazi yangu huku maji mengine nikiyafuta usoni ndipo akasema: sorry sister Aisha.

Nikamjibu: usijali Kawaida Mdogo wangu.

Muda Huo alikuja Nasra na kusema: ooh my God! Sabrina umemfanyia nini mwenzio.

Sabrina: kwa bahati mbaya nimemumwagia maji.

Nasra alicheka na kusema: basi Umefanya vizuri maana ana siku nyingi haogi usimuone hivo.

Waliangua kicheko kisha wakaondoka huku wakijigamba, moyo uliniuma mno ila sikuwa na namna.

Majira ya usiku saa 3 nikiwa nipo chumbani huku nikijisomea vitabu mbali mbali kuhusu uganga alikuja mama mlezi na kusema: Muda huu wewe umelala si eti?

Nikamjibu: I'm sorry mum kazi zote nimemaliza.

Mama alinibania Pua na kusema: *I'm sorry mum kazi zote nimemaliza* Huna hata haya! Eti kazi zote Umemaliza embu Harakisha nikukute sebuleni.

Niliviacha vitabu kitandani nikaelekea sebuleni, nilipofika nilikaa kwenye kochi huku nikimsubiri aje, mama mlezi alipofika alisimama Juu yangu kisha akanirushia pesa na kusema: Harakisha muda huu na usichukuwe daladala maana pesa yangu haiwezi kuwa usafiri wako.

Nikammjibu: Hujanipa maelekezo.

Mama: nenda Sokoni.

Nikamuuliza: muda huu?

Mama: wewe sio wakunijibu hivo usione nimekunyamanzia Ndo ujione kwa kunijibu, narudia tena! Nyanyuka nenda Sokoni kaniletee tikitiki maji.

Nikamjibu: ila kuna genge Ipo hapo karibu.

Mama alinikata kibao na kusema: huoni aibu kunijibu hivo sasa Skia Ole wako usifike Sokoni utaniona na hakikisha umenunua kwa mama Ruqia na ntamuuliza k**a ulifika.

Nilijiinamia kwa uchungu ndipo nikanyanyuka na kutoka nje huku akinisindikizia matusi.

Nikiwa nipo njiani nilipiga hesabu kutoka tunakoishi kwenda Sokoni kwa mguu kuna mwendo mdogo Nikaona potelea Kote wacha nipande daladala.

Nilipofika Sokoni nilimtafuta Yule mama nikamkabidhi pesa kisha akanipa mzigo nikaanza safari yakurudi nyumbani, kwa kuwa pesa ilikuwa imeniishia Ilinibidi kutembea na mguu, nikiwa nipo njiani nilianza kuhisi nyuma nanyemelewa bila kupoteza muda nikaongeza mwendo kila nikiongeza mwendo na wao wanaongeza, Hofu ilinitawala huku nikijiuliza Kwanini waninyemelee, nilipofika sehemu flani kwenye uchocholo watu wale walijitokeza mbele yangu ndipo nikasimama huku macho yakiwa yamenitoka, walikuwa ni wavulana wa tatu ndipo mmoja akasema: hatuna muda wakupoteza we sister unatokea wapi?

Kwa sauti ya kigugumizi nikamjibu: ku ku kule.

Akanijibu: Aaaahhhh kule!!!

Walianza kunisogelea taratibu ishara wanataka kunibaka, ndipo nikaanza kurudi nyuma huku nikisema: mnisamehe jamani mwenzenu Nina Matatizo.

Mmoja Akanijibu: Matatizo yako hayatuhusu.

Nilipiga hesabu ya haraka haraka ukija kuangalia Hakuna watu waliokuwa wakipita maeneo hayo ndipo nikasema huku nikiwa nimejiamini: Ndio mnataka kunibaka ila sasa tatizo k**a Mpo tayari kufa na Mimi sawa maana Mimi ni mwasilika na sikutaka nimuambukize yeyote ila K**a Mpo tayari sawa Acha iwe hivo.

Mkaka mmoja alisita na kusema: jamani tuache.

Mwingine akamjibu: we vipi! Huu ni mkwala tu.

Akamjibu: sawa ila mtazame kwanza mtu mwenye haogopi inaonekana ameshaasilika.

Waliendelea kubisha mwishowe wakaniambia niache kila kitu Chini niondoke, aisee sikupoteza Muda niliyaacha Yale matikitiki maji kisha nikaondoka huku nikikimbia, nikiwa nipo njiani moyo ulisita kurudi nyumbani bila tikitiki maji ila sikuwa na namna Ilinibidi kusonga mbele kutokana pesa yote niliitumia kwa kununua tikitiki maji, nilifika nyumbani nimechelewa maana nilitembea kwa mguu yalikuwa ni majira ya saa Sita usiku, nilipofika getini niligonga mlango kwa muda mrefu Ila sikuweza kufunguliwa, ndipo nikaanza kumwita Mlinzi aje kunifungulia Ila sauti yangu haikusika, muda Huo Mlinzi alisogea getini akaniambia: Aisha! madame amekataa usiingie mpaka Yeye aje.

Nilishangaa kisha Nikamuuliza: unasemaje?

Kabla Mlinzi hajanijibu sauti ya mama mlezi iliskika akisema: wewe nimekwambia nini?

Mlinzi kwa heshima na kumuogopa boss wake aliondoka akiwa amejiinamia ndipo mama mlezi alisogea mpaka pale getini akafunguwa mlango Kidogo akasema: muda wote huu ulikuwa wapi?

Nikamjibu: Nilikuja na mguu ndo maana nimechelewa.

Mama:enhe! Mzigo Upo wapi?

Nikamjibu: nilikutana na.....

Kabla sijamalizia alibana mlango kisha akarudi ndani akisema: utajuwa wapi utalala!

sikutegemea K**a ingekuwa hivo ndipo nikaanza kuomba wanifungulie mlango Ila hawakuweza kuniskia, niliomba kwa muda mrefu mwishowe Mvua ilianza kunyesha, kiukweli Hofu ilinitawala mwilini nikaanza kulia huku nikiwa nimejikunja mbele ya mlango.

Upande wa Nicolas muda Huo alikuwa ametoka out na mpenzi wake, walikuwa sehemu nzuri huku wakipata kinywaji taratibu, wakiwa wanaendelea kuzungumza simu ya mpenzi wake ilianza kuita ila mdada Yule alionekana kupatwa na Hofu na akashindwa kupokea ndipo Nicolas akamuuliza: nini tatizo?

Akamjibu: Hamna shida ila nisubiri Kidogo nakuja.

Mdada Yule alinyanyuka na kuondoka, alichukuwa muda mrefu yupo huko Mpaka Nicolas akachoka ikambidi kumfuata huko huko, akiwa anazunguka zunguka alishangaa kumuona akiwa amekaa na mwanaume mwingine huku wakionekana k**a ni watu wenye mahusiano ndipo Nicolas alisogea pale taratibu, alipofika alisimama na kusema: Kwanini unidanganye eti nikusubiri Unakuja kumbe umekuja kukutana na mwanaume mwingine.

Mkaka Yule akasema: unaongea nini dogo! Huyu ni mpenzi Wangu kwani mlikuwa mmetoka nae!

Nicolas alimtazama kwa hasira mpenzi wake bila kujibu chochote akaondoka zake.

Upande wangu Mvua ilizidi kuwa nyingi nikaanza kutetemeka kutokana na baridi, nikiwa nimekaa hapo gari la Nicolas lilifika na kuniangazia taa usoni, niliziba macho yangu kutokana na mwanga mwingi, Nicolas aliponiona aliizima gari kisha akashusha kio akanitazama ninavohangaika na Mvua kwa sauti ya Chini Akaniambia: Njoo!!

Nikamuuliza huku nikiwa nalia: eti nini?

Nicolas: njoo!

Nilinyanyuka kwa shida nikamfuata huku nikitetemeka, nilipomfikia nilimtazama bila kuongea chochote ndipo Nicolas akafungua mlango na kusema: Ingia?

Nilijitazama nilivolowa ila Nikaona potelea Kote kwanza ni bahati nimepata ndipo nikaingia, Nicolas akasogea karibu yangu akaurudishia mlango ndipo akaniuliza kwa sauti ya Chini: mbona upo nje na hali ya kuwa ni usiku Sana tena Mvua Ipo inanyesha?

Nikamjibu kwa sauti ya majonzi: mama amekataa nisiingie.

Nicolas akiwa ananitazama machoni akaniuliza: Kwanini?

Nikamjibu: alinituma usiku Sana niende Sokoni na mguu nikamnunulie tikitiki maji nilivorudi sikuja nazo Ndo akasema nilale nje.

Nicolas: kwanini hujaja nazo?

Nikamjibu: kwasababu nilipokuwa narudi kuna kuna kuna.....

Nicolas: kuna nini?

Nikamjibu: kuna mateja walitaka....

Nicolas: walitaka kufanyaje?

Nikamjibu: kunibaka, Ndo nikaacha tikitiki maji Chini nikakimbia.

Nicolas: pole.

Nicolas alivua koti aliloluwa amelivaa akanipa nivae ili baridi isinipige, nilivaa huku nikitetemeka ndipo Nicolas Akaniambia: lala.

nilishangaa ila nikapotezea.

Majira ya saa tisa tulikuwa pale pale hatukuweza kuingia ndani Nicolas Usingizi ulimpitia tukiwa tupo hapo kwenye gari, nilimtazama Nicolas usoni ukweli alikuwa ni handsome kisura ndipo nikasema kwa sauti ya Chini: unaonekana hata wewe ni mpweke sana.

Nami nililala zangu, Majira ya asubuhi saa 12 Husna David Pamoja na Sabrina walitoka nje wakiwa wamevaa nguo za mazowezini wanaelekea kufanya mazowezi, walipotoka nje tu na kuliona gari la ndugu yao limepakiwa nje walishangaa mno ndipo Sabrina akasogea kuchungulia hakuamini kuniona Mimi ni melala zangu pia na kaka yake akiwa amelala ndipo wenzie wakamuuliza: nini kinaendelea?

Sabrina: mwite mama aje ajionee mwenyewe.

Unahisi nini kitatokea!
Usikose mkasa huu!

Jamani usiache ku like k**a umeipenda hii ni kihonjo k**a like zitakuwa nyingi tutaiendelea Mpaka mwisho.

22/11/2019

piansh

22/11/2019

bahar a gaya sab

22/11/2019

family ko.hlp kiya adi and pari ne

19/11/2019

Mormg guyz

Good nyte guyz
17/11/2019

Good nyte guyz

13/11/2019

Brothers for ever..WCB 4LIFE BIG UP BRO MODII

Penda nyie sana
12/11/2019

Penda nyie sana

11/11/2019

Hey

Unahisi k**a huyu ni nany??? If you know i will promote you with 500Tsh
04/11/2019

Unahisi k**a huyu ni nany??? If you know i will promote you with 500Tsh

K**a ww ni shabiki sugu wa WCB label hii dance inapatikana kwa wimbo upi?? Ukipata inbox me for 50shl credo for the firs...
30/10/2019

K**a ww ni shabiki sugu wa WCB label hii dance inapatikana kwa wimbo upi?? Ukipata inbox me for 50shl credo for the first 5 only

Hey guyz
28/10/2019

Hey guyz

Address

Music
Nairobi
012

Telephone

0725246714

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Queen aucer jab$ posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category



You may also like