Simulizi Za Tyson Juba 254

Simulizi Za Tyson Juba 254 Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Simulizi Za Tyson Juba 254, Digital creator, jubatyson70@Gmail. com, Mombassa.

SIKU YA KWANZA KWENYE PENZIBaada ya kumaliza mtihani wa darasa la nane mwaka Jana nlirudi nyumbani kwetu kutoka shule kw...
14/07/2023

SIKU YA KWANZA KWENYE PENZI

Baada ya kumaliza mtihani wa darasa la nane mwaka Jana nlirudi nyumbani kwetu kutoka shule kwani nlikua nkisoma katika shule ya bweni. Katika tembeatembea zangu za hapa na pale hapo ndipo nlikutana na rafiki yangu kipenzi wazamani kwani ata yeye pia alikua amemaliza darasa la nane. Alinirukia kwa bashasha na kunikumbatia .Vipi kaka habari za masiku ni nzuri sana nlimjibu vipi mama na dugu huko ? Wapo salama sana hio nivizuri hata kwetu tupo salama.
Hapo ndipo tukaa kando ya barabara natukaanza kupiga gumzo. Tulkumbushana mambo mengi sana ya zamani. Juma aliniuliza nakumbuka ilesiku ya kuiba maembe kukashikwa na yule babu kule ....hahaha aki wewe ata husahau maana ile siku kijasho chembamba ilitoka nkikutazama mwenzangu machoz alikua yakikulenga lenga. Alipasua mbarika. Kisha akamiambia unamkumbuka Yule demu mwenye alikua ana kupenda sana pale shule kabla undoke kwenda shule ingine? Mmmmmmm! Halima? Enheee basi nlikutana nae juzi amekua mzuri sana na isitoshe alikuulizia sana hadi aliniambia nkikuona unipe namba ya rununu ilimuweze kuwasiliana kwani ana kumiss sana.mmm wacha wewe......kweli kaka . Apo ndipo akili yangu ilianza kuduwaa kimawazo hadi Juma alikua akiongea smuskizi tena. Beka Bekaa nlishutuka na kisha nkatabasamu kwni ata mm nlikua natamani sana kukutana na yeye Halima ata asingeniambia bado ningemuulizakwani walikua wanakaa mtaa mmoja. Bila kusita nlipea haraka haraka namaba zangu.kisha tukaagana na kisha kila mtu akashika njia yake . Usisahau kumpa hizo namba ( please )

Nlielekea nyumbani huku mawazo akinisonga juu ya rafiki yangu kipenzi Halima. Nlipofika nlijiwekeza kwa kitanda nikipanga msitari ntakayo mwambia Halima kwani nlikua najiona nimekua barobaro. Nlitamani ata Juma akutane nae siku hiyo ili ampe zile namba . Mara tu Baada ya masaa machache nliskia kabambe yangu ikiita moyo ulinidunda kwani nlikua nafikiri tayari Halima ujumbe umemfikia. Nliondika kwa kishindo kuangalia ivi ata alikua ni mama yangu.

06/07/2023

Kwanza ningependa kuwashukuru wote wenye watajumuika pamoja na Mimi kwenye fan page hii .
Hii page ni ya hadhithi za asili ,mapenzi na maisha Kwa ujumla Ivo basi nawakaribisha nyote.

Leo ntaachia hadith yangu ya Kwanza hapa uskae mbali

Address

Jubatyson70@Gmail. Com
Mombassa

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Simulizi Za Tyson Juba 254 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share



You may also like