Brian ngugi

Brian ngugi The home of laughter

03/01/2024

Hi guys

12/01/2023

𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄𝐒: 𝐒𝐔𝐋𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐂𝐒𝐓𝐯 πŸπŸ‘π“π‡ 𝐉𝐀𝐍
𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟏

Wakuu k**a kawaida weka LIKE πŸ™ŒπŸ™πŸ™
Major amekesha akikunywa tu. Amekunywa hadi wine imeisha na bado hajatosheka. Hizi ni stress tu zinammaliza. Ameishi kulala na mkewe leo hii anangalia bed ni kubwa tu,mkewe yuko nje kwa baridi na Fatima yko chumbani mwake hana wasiwasi.

Kumbe Kaka na Sultana,manze waliona hii siri lazima ibakie kuwa siri. Wakamchukua Kokan,Kaka akambeba hadi wapi,huku kichakani. Waliambatana na Sultana hadi pahali Kaka akachoka. Kubeba mfu si mchezo. Kaka aliambia Sultana haezi pita hapa wanaeza onekana. Sultana anashindwa sasa atafanya nini na hizi nuksi. Kaka aliambia Sultana wamuache Kokan hapa k**a wamemficha kisha kesho alfajiri wakuje kumbeba waende kumtupa kulee. Kaka alitafuta tumiti miti akaufunika mwili wa Kokan hadi siku itakayofuata.

Mida bado ni usiku. Major alitoka kiasi akaenda msalani kisha kurudi,mbele yake,aliona mtu ako kwa bed,nani huyo? Fatima. Wueh! Major na venye amelewa kuona ule urembo Fatima amevalia akiwa kitandani aliona hii mali hata k**a nimelewa siezi acha bna. Nakuambia ile kitu Major alifanyia Fatima usiku,eeh! Acha tu!

Walilala ikafika asubuhi. Bi Asiya ameamka kutengeneza breakfast. Anakatakata nyanya,kitunguu na steelwhool🀣🀣Hapo kando anakaanga smokie tano,mbili za Major,mbili za fatima alafu kale kamoja ni kake. Kwa blender ni juice anatengeneza. Yaani breakfast ya wadosi ina maajabu,unaeza dhani ni siku ya sherehe. Sisi akina yakhe breko tumezoea tu suturungi na kitunguu saumu,huku ni mapochopocho.

Kwa Salama ndio pia anaamka. Alikuja kuona k**a Sultana alirudi akampata k**a amelala,akaanza kumuamsha kumbe karembo kalikua kanaota,kalishtuka mbaya mbovu hadi kakamshtua Salama karibu atoke kijiko🀣 🀣

Asiya ashamaliza round one ya upishi,amekuja kutafuta nguo za kufua huku kiasi. Ni harakati ya kazi za kila siku lakini leo anashangaa nguo za Fatima zinafanya nini huku. Hadi hapo kando akaona koloni ya Fatima akashindwa,hivi personal things za Fatima zinafanya nini huku,akajua lazima hawa walifanya kitu. Asiya alijisemea ili kulinda ndoa ya Ua lazima afanye kitu.

JJ na yeye,kumbe pia walilala chumba kimoja na Dida. Ndo hawa ndio wanaamka,kwanza Dida ndio anaanza kuamka amka. Wacha aangalie aone alilala na JJ,alishtuka hadi akaamka mbio. JJ aliamka akamuuliza ni nini? Dida akamuuliza nilifikaja hapa nikalala na wewe? JJ akamuuliza kwani are we not together? Dida akamwambia of course,we ain't together anymore.

Kumbe Asiya na yeye,ebu sasa angalia maajabu,alienda akavalia nguo ya Bi Ua na akavaa wig ya Bi Ua kisha akatuambia nini,Fatima k**a unajifanya unaona mbele,basi hapa umeingia cha k**e. Mimi naitwa Asiya kuja ukabiliane na mimi,alafu Asiya anasongeza kawig venye Ua huwa anafanya na kulamba mdomo k**a Bi Ua. Fatima,utajua hujui,baaasi. Kimeumana na Asiya hataki mchezo.

Bi Salama na yeye akiwa kwake akipika uji wa majani chai,aliitwa na Maria mbio mbio akaambiwa madhe,hebu kuja mbio huku ndani,mambo si mazuri...

𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟐
JJ alimwambia Dida k**a hunitaki basi useme tu na k**a unanipenda njoo ulale. Dida alimwambia msee,I have a boyfriend na mimi kubaki huku was because of mum si ati nakupenda. JJ alicheka tu "ati uko na boyfriend" boyfriend mgani sasa🀣🀣

Tufike huku sebuleni,Asiya akiwa kwenye mavazi ya Bi Ua ameletea Major breakfast chumbani mwake na usisahau huku ndani Fatima yuko. Asiya hata hakubisha alisukuma tu akaingia. Kufika ndani,Fatima amelala hapo na Major hayuko kitandani. Fatima kufungua macho,akaona haya,huyu ni Asiya ama Ua ama ni AsiUa🀣🀣Asiya aliondoka na chai akarudi nayo jikoni.

Salama alikuja kuangalia Sultana akapata akilia tu akidhani huenda Sultana anaumwa. Sultana alimwambia yeye haumwi ni ndoto alikua nayo,alikua akiota na mazimwi za kutisha. Salama alimuuliza na jana ulienda wapi na Kaka kwa sababu ulirudi usiku sana,mlikua mumeenda wapi? Sultana ni kulia tu hataki kuongea.

JJ pia ameamkia jikoni kutafuta kabreakfast.Akiwa tu hapo,Dida alikuja akamwambia JJ I am sorry kukuambia I have a boyfriend,I didn't mean to hurt your feelings.

Kwa Salama waliona Sultana anasweat sana na kutapika hadi Maria akasema itabidi wamuite daktari. Salama alisema ni kweli itabidi wamuite daktari na daktari wa karibu ni Kokan tu. Sultana kusikia ni Kokan,alikataa akasema yeye hataki Kokan kabisa. Hawana habari Kokan mwenywe hayuko🀣🀣

Huku kwa Kaka,Buya alimuuliza jana ukiingia ulikua na wasiwasi sana,kuna nini? Kaka alimwambia mzee usijali,kwa sasa tushughulikie hali yako kwanza. Kaka alitaka kuondoka lakini Buya akamwambia akae kwanza kuna jambo anataka wazungumzie. Acha tuwape nafasi wazungumze,sisi twende kwa JJ na Dida tuone k**a kuna lipya.

JJ alikuja kukaa hapa nje na akafuatwa na Dida huku Dida ni msamaha tu anaomba. JJ alimwambia actually achana tu na hii story. Dida aliona vyema kisha akamuuliza sasa plan yake ni ipi? JJ alimwambia plan yangu sasa hivi ni kuhakikisha kupata ukweli wa kumleta mamangu kwa hali yake ya kawaida.

Asiya na yeye alifuatwa na Fatima. Fatima akamuuliza mbona unarudi na chai? Asiya akamuuliza unajisikiza kweli,mimi nakaa kukuletea breakfast wewe? Fatima akamuuliza na kwani haya mapochopocho ulikua unaletea nani? Asiya akashika wig na kuangalia Fatima venye Ua huwa anaangalia. Fatima akacheka tu akamuuliza so unamaanisha ulikua unaletea Major. Fatima alicheka sana hadi akauliza Asiya kwani pia huwa unamezea Major mate sio🀣🀣Fatima ndio anashangaa sana na Asiya hadi anamwambia wewe mwenyewe na cheap make up unadhani unaeza mvutia Major? Kwa taarifa yako,Major ni wangu mimi Fatima na ukome sana na hii upuzi wako. Wueh! Asiya ashaanza kumpea Fatima compe🀣🀣🀣Nairobiii, huyu anakupea yule....

Follow Brian ngugi

10/01/2023

𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄𝐒: 𝐒𝐔𝐋𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐂𝐒𝐓𝐯
𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟏
Please,niwekee LIKE ndio uendele kusoma aki,ama nikukujie kwako sai nikule mboga zoooote

"Nipige", Major alimwambia JJ. Ikabidi Asiya na Dida wakuje mbio kuwatoanisha lakini wapi, JJ anataka mamake. Major aliambia JJ utaumia. ama uondoke kwangu, lakini JJ akaona dawa ya moto si supu moto akaenda shoka, makosa. Major pia kuona hivyo, aliendea nini? Bunduki kwa nyumba.

Huku kwa Kokan nakwo, Kokan hataki kuachika, alimshika Sultana akamwambia unajua hili kovu ni juu yako, kukuacha sikuachi.

JJ wakati anajaribu kuvunja mlango amtoe mamake, Major ashakuja na bunduki, akafyatua risasi juu akaambia JJ, one more step nakusukumia risasi ya kichwa tunakuzika kesho. Asiya aliambia tu JJ please don't move or do anything.

Hebu tufike kwa Salama. Sada ashaambia Salama kila kitu venye Major anasema ati alimuua babake. Salama alimwambia iweje wakati sisi sote tunajua babako alikufa kwa ugonjwa wa moyo. Salama wanajua ukweli hadi aliambia Sada sikiza, wakati ulikuja si ulipata tayari Major ashafika nyumbani, huenda hata ni yeye alimuua babako akakusingizia wewe. Sada akakumbuka akajua bydha way, Major alikua nyumbani na alikua anaishi kambini, alikua anafanya nini nyumbani? 1+1=2,baaaasi. Thanks Salama kwa kutukumbusha.

JJ na yeye ameona huku hakai. Alikuja chumbani kuchukua bag atoke lakini Dida alimwambia please, don't go. JJ alimwambia kulingana na hasira niko nazo nikibaki hapa mmoja wetu kati yangu na baba ataenda kwenye chumba cha serikali either jela ama mortuary, heri tu niende.

Turudi kwa Salama. Sada alianza kujilaumu akamwabia Salama angejua hata hangetoa mimba, aghalau. mtoto wake angekua mkubwa hata kuliko Sultana. Salama akamwambia for now tuyaache hayo tujue huyu Major tutamfanya aje.

Kwa Major akiwa chumbani, Fatima alifika akampata akivaa akamuuliza. Major kwani waenda wapi? Major alimwambia nataka kuenda pahali kutuliza akili zangu. Fatima akamwambia wee na wee usijali kwa sasa kujutia kumbuka mimi niko hapa kwa ajili yako na nasimama na wewe wakati wowote. Ona venye Fatima anamshika shika Major ndevu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚wueh, fear women.

All in all huku kwa Salama, washaelewana na Sada cha kufanya na wacha hivyo, hata wakati Sada anajiblame kwa kutoa ujauzito Salama anajilaumu kwa Major kumharibia usichana wake.

Kokan na yeye alimfungia Sultana akamwambia k**a ni hivyo sasa, huku kwangu hutoki, akaweka kafuli. Sultana anamwambia mimi nataka kuenda kwetu lakini wapi, Kokan alimshika wakaanza kumenyana. Kumbe kwa ile haraka, Sultana in the name of self defense alimsukuma Kokan, mwanaume akagonga kichwa akapasuka mbaya mbovu, makosa. Kokan, ni Mungu tu k**a angali uhai.

𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟐
Sultana yeye haoni lakini kulingana na ukimya anahisi kuna tatizo hapa. Alianza kumuita lakini wapi "Ko.. kok...Kokan" Kimya. Sultana alimguza akaona huyu si wa dawa wala maji alianza tu kulia akimwambia tafadhali Kokan amka, nilikua natania tu. Lakini wapi. Shida tena Kokan alifunga mlango na ako ufunguo na Sultana hajui uko wapi soo kutoka tena ni balaa, maskini wa Mungu Sultana.

Tufike kwao nyumbani, Salama amekaa anajiuliza Sultana mbona harudi na alisema tu anaenda hapa mbele anarudi ona sasa. Salama hana habari Sultana wake ako kwenye masaibu. Salama alianza tu kuhisi mambo si mazuri kwanza akagonga maharagwe yakamwagika, hiyo ni kisirani.

Salama akiwa amekaa hapo, mlangoni kulibishwa akadhani ni Sultana lakini ni Kaka na Maria. Maria amekuja kuishi huku. Kaka alimuuliza Salama Sultana yuko wapi, akaambiwa hata yeye anamngoja alitoka na hajarudi.

Nyumbani kwa Babu, anapata nafuu kila uchao. Sada amekuja kumjulia hali ajue mambo ni vipi.

Kumbe Major na yeye, alikuja kwa bar kulewaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ndio huyu amekunywa mbaya mbovu. Ilifika wakati wa kulipa, badala ya kupeana 100,akapeana 1000 na imagine Cynthia hakaezi rudisha change πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚mnaona uzuri wa kuwa Waitress πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.

Kaka aliambia Salama aende kumuangalia Sultana lakini Salama akamwambia usiwe na wasiwasi tuliahidiana na Sultana sitakua namchunga so achana na yeye. Kaka. akamwambia apana Sultana kukaa peke yake hatari sana na ndio maana nimeleta Maria akuje akae na yeye. Maria akaambia Kaka wewe kijana, mimi si mfanyakazi na k**a hiyo ndio imenileta huku tafuteni mwingine πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Salama akamwambia Maria msichana wangu, Sultana anakuhitaji sana.

Kiasi tufike kwa Babu, alimuuliza Sada k**a aliambia kakake? Sada akamwambia sikumwambia na k**a yeye ndio alitaka kukuua Iam sure ashajua uko uhai. Babu alimwambia simuogopi kamwe, k**a yeye israel basi na aje kuniua. Lakini kumbuka kuna picha zenye Sada alitoa kwa Major na sasa hii ndio sababu yake.

Sada wakati alitoa zile picha, Babu kuziona akajua si huyu ni babako marehemu alafu huyu mwingine alikua wakili wake, msiri sana. Yani Sada amepata majibu bila hata kuuliza swali moja ju yeye alikua anataka kujua, huyu mzee mwingine ni nani na Babu kwa kuangalia tu hivi ashamjua na ashaambia Sada. Baaaasi. let the game begi...beningingiπŸ˜‚πŸ˜‚Kesho majaliwa sehemu ni ya kumi na tano kumi na sita ya Sultana.

Follow me Brian ngugi

07/01/2023

Growth will also feel like loss. It will make it impossible for you to fit in places you used to be comfortable in. It will cause you to question narratives you had stayed with for years. You will try going back to the same lifestyle and friends you had settled in but you won't fit anymore.

Growth will cause you to feel lost in place, the same way you would feel when you're in the steps between two floors. You've left one floor after deciding you've had enough of it, but you're not on the next one yet. It will feel frightening but you will also feel alive and vibrant. This is because your psychology was designed for increase and growth, and every time you move forward your whole being comes alive.

But because of fear of change and laziness about working on ourselves, we often gravitate towards settling and maintaining status quo. Yet after a while we begin to lose taste and fervour for life. So we shake ourselves up and learn something new, we work on our habits, we let go of harmful company, we stretch ourselves at work and set higher financial goals. Then we begin to feel alive again.

Solution? Stop wrestling with what you were created to be. You're designed for growth such that the moment you stop growing you start dying.

You cannot spend your life being a stay-at-home anything. Something in you will die and vices will sprout in you like gossiping and sociopathy, in an attempt to channel your energy to something.

Neither can you stay at one job or position for life, however well it pays. You will find yourself in alcoholism and depression because of the lack of motion in your life.

Your happiness will never come from procrastination and avoidance of taking the next step, but in courageously moving forward. Even if you fail at it, the attempt itself already counts like a lesson and growth, and you can attempt again more intelligently.

Growth is the oxygen for your soul. Step out and breathe.

Brian ngugi

06/01/2023

𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄𝐒: 𝐒𝐔𝐋𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐂𝐒𝐓𝐯 πŸ—π“π‡ 𝐉𝐀𝐍
𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟏
Its late guys but si mnaelewa masaibu! Cha muhimu,nishawasababishia,si pia msababishe na LIKE k**a zoooote. Lets goooo...

Leo tunaanza tofauti kiasi,tunarudi nyuma 38yrs ago. Acha sasa niwaonyeshe nini kilifanyika 38yrs ago huku nyumbani kwa Major Jabali. Kabla ya Major Jabali,kulia na Seniour Jabali,babake Major sasa. Siku moja Sada akitoka matembezi zake,alipata babake amelala hapo chini kwa floor. Alianza kumuita, "baba,babaaa,babaaaa" lakini akabu ikawa,babake Sada kwisha maneno. Sada alilia sana,kisha punde si punde,Major akafika,kwanza alikua amevalia nguo za GSU,akapata Sada akimshika babake hapo chini. Major na yeye akaanza kuuliza Sada mbona umeua mzee,lakini Sada yeye anajuua hajafanya kitu but Major hakumpa nafasi ya kujieleza,akachukua rungu akanza kumtandika Sada ikabidi Sada atoroke aende mbio kabisa. Thats what happened,ndio Sada akatoroka,na sasa ndio amerudi maajuzi.

Fatima na yeye alionyesha Dida ile picha ya Maria. Dida akaangalia Maria kwa picha akakumbuka alikutana na yeye kwa barabara tukatusiana,lakini akaambia mamake,mwenye nilimuona si huyu. But Doda amekumbuka vizuri sana akajua ni yule msichana.

Tufike kwa Salama,anamwambia Zuu arudi kwa mume wake. Zuu alimuuliza na Sultana je,hutahitaji usaidizi? Salama alimwambia I will manage but for now please nenda kwa mume wako.

Ebu turudi kwa Sada,aliambia Major sikiza,sikuondoka wakati baba alikufa kwa ubaya,lakini wewe mwenywe unajua chenye kilifanyika kwa baba. Ilikuaje? Fatima akafia hapo,anajua ukweli wa mambo na sasa mimi tena huyoo,ju nyinyi hamjui ukweli wa mambo,acha niwarudishe kulee nyuma tena. Hii ni kitendawaili cha venye babake Major alikufa. Wakati mmoja,Sada akiwa na Salama walikua wanaishi chumba kimoja na wakati moja,babake Sada akapiga simu kutaka kuongea na Sada lakini Sada akaambia Salama ashike amwambia hayuko. Babake Sada aliacha ujumbe akamwambia akija mwambie namhitaji nyumbani kuna dharura lakini wakati kuridi nyumbani,alipata babake ashakufapale sakafuni lakini swali ni Sada alikua ametoroka nyumbani kwa nini? Alikua na ujauzito na akaavya,makosa. Thats why alihepa.

Hii yote,Sada anakumbuka akiwa na Major,Asiya na Fatima hapa, Hata Major mwenywe hana habari kuna wakati Sada aliavya mimba na akatoroka.

Hatimaye kwa Salama,Sultana na mamake walirudi. Mamake alimsihi sana akamwambia tafadhali mwanangu,usiwai jaribu kufanya hatua mbaya k**a hiyo. Sasa ungekufa mimi k**a mamako ningefanya nini? Na k**a unaona nakukazia sana,leo nakupa uhuru wa wewe kufanya chenye unafanya. Ukitaka kuoleka na Kokan,nenda mama,ukisema unataka kuoleka na JJ,mama nenda,nitakua sawa. Hata ukisema utataka kuzalia mtoto wako hapa,chochote utasema nitasikiza mwanangu ilimradi usifanye uamuzi tena k**a wenye ulikua umefanya.

Kokan akiwa kwake,mwanaume hatulii.lakini punde si punde,mlangoni akasikia kunabisha. Akauliza ni nani? JJ akamwambia ni mimi fungua mlango ama nipite nao sasa hivi. Kimeumana🀣🀣🀣. Kumeb wakatio huo,Dida amekuja mlangoni kwa JJ kumtafuta pia,hajui JJ ako kwa Kokan na hajakuja kwa uzuri.

Dida alishuka chini akakuja akamuona Sada,akamuuliza k**a amemuona JJ? Sada akamwambia JJ hajapatikana lakini shida ni simu ya JJ aliacha nyumbani,so hata kumpigia simu ni uselesss. Sada alimsishi sana Dida asimame na JJ kwa sababu yenye yanafanyika huku anahitaji sana usaidizi.

Sultana na yeye pia alitoka,akaambia maake anafika pembeni kiasi atarudi. Mamake alimwambia nisawa lakini uhakikishe unawahi kurudi mapema,kuna wageni wanakuja.

𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟐
Sada alingoja Major akiwa nje akakuja akanza kupekua pekua kuna kitu anatafuta na alikipata. Ni picha haswa za babake. Kuna picha mbili alizipata akaanza kuzilinganisha.

Huku kwa Kokan,alifungua mlango,JJ kuingia,Kokan akaanza kuuliza JJ anataka nini? JJ alimwambia niko na hasira sana na please,niko hapa kuuliza maswali si wewe kuniuliza. Swai la kwanza,babangu alikupea pesa za kufanya harusi ya Sultana sio? Kokan akamwambia ndio,alah,shida? JJ akamuuliza swali la pili,uliambia Sultana anipe talaka,mzee alihusika? Kokan alimwambia bro,usiniuliza maswali mingi hivyo na k**a unataka kujua,kaa ukijua mimi ndio first born wa babako na chochote unafanyiwa wewe,mimi nilifanyiwa kitambo sana hata k**a mimi si damu yake. JJ alijam,akamsukuma Kokan akagonga kichwa kwa meza. JJ ana hasira sana.

Sada na yeye alipatikana na Major,akamwambia chukua vitu zako uondoke huku. Sada alicheka tu akamwambia huku siondoki mimi,naondoka tu kwa masaa na nitarudi. Fatima pia alikua hapo,akaambia Major basi napenda unavyokua na hasira hivi.

Huku kwa Kokan nakwo,kumbe kugonga kichwa kwa meza,aliamka akiwa amechemka,makosa. JJ alitandikwa mangumi za tumbo kwa uzo,mbaya mbovu,hadi akanguka chini. Kisha akaambia JJ sikiza,mtoto wa Sultana akizaliwa,I will name him after your father,Jabali. JJ,kusikia hivyo,nguvu zikarudi tena,akashtua Kokan akasonga nyuma,na akaamka akamwekelea ngumi ya kichwa kwa kifua,Kokan akaanguka kwa kitu kisha JJ akaamua kumuua sasa. wah,makosa. Kaa si wanakijiju kufika na kuwatoanisha,Kokan sai angekua kaburi.

Zuu na yeye kurudi nyumbani,alipata wenye deni ya babake wamefika. Akaanza kujitetea akiwaambia atawalipa lakini wakamwambia anyamaze,kwa sababu deni la babake lishalipwa lote na bwanake. Kumbe Mwanzele kaliamua kulipa deni kila kitu. Zuu hakua na otherwise,aliweka sahihi kuonyesha deni lishalipwa jambo shingo upande. Wazee wa deni washapata pesa zao na haoo wakaenda. Zuu akadhindwa alie ama afurahie.

Huku kwa Kokan,JJ alimpa onyo Kokan,akamwambia chunga sana kujihuzisha na babangu,hananga msamaha. Kokan alimwambia najua lakini hela singekataa bwana. JJ akamwambia ole wako ajue ulihusika kuchafua boma yake,utajua hujui.

Sultana na yeye,sasa kamekuja wapi huku. Kuna pahali Sultana alikuja na kufika akafurahi,kwani ni wapi? Siku ya Jumatatu tukutane papa hapa. SULTANA EXTRAS zinakuja kesho saa mbili
Follow Brian ngugi

04/01/2023

𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄𝐒: 𝐒𝐔𝐋𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐂𝐒𝐓𝐯 πŸ“π“π‡ 𝐉𝐀𝐍
𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟏
Wakuu! Like muhimu sana,niwekee tukiendelea kusoma. Mlidhani sitaeka ju kwa tv hakuna now that nimeeka usininyime LIKE ✌️.

Tuliachia kwa Babu,Kokan ashaendea dawa lakini anachelewa sana hadi Salama anashangaa huyu amegwama wapi tena. Sada aliambia Salama bydha way,sisi tunajua Kokan hana kazi,hana watu hizi pesa anakimbilia posa amezitoa wapi? Mwanzele akamtetea akasema huyo ni daktari huenda anahustle. Zuu akaambia Mwanzee nyamazisha hiyo shimo ya uso..nkt! Kisha Zuu akauliza Babu k**a anaeza sema chenye kilifanyika,ama k**a ni Mwanzele alihusika aseme ndio maana hataki msaada wake. Babu anajua ni kweli chenye Zuu anasema lakini hataki kusema.

Zuu na Mwanzele walitolewa nje na Mwanzele kakaanza kuomba msamaha,kanaambia Zuu arudi nyumbani na hatamkosea tena. Zuu alimwambia huko kwako mimi sirudi. Mwanzele alimwambia mbona unapea Salama mizigo wakati zake zimemshinda? Zuu akamwambia mimi sitakaa kwa Salama,kwanza naenda kwa Salama nichukue vitu zangu naenda kukaa kwa babangu,makosa. Kwa nini? Kwa sababu,huko kwa babake Zuu ndio Kaka anakaa na ndio Buya na Maria wamejificha. Balaa!

Tufike ufuoni,Sultana alitembeza miguu hadi huku,kazi imekua ni kulia nakuwaza JJ,akiangalia kando,analia akiwaza JJ,akiangalia juu machozi na JJ tu. Maskini wa Mungu katoto ka wenyewe katafanya nini,,Kokan huyu anataka posa,JJ pale alimkataa akidhani mtoto si wake. Katafanya nini haka kapii🀣🀣

Zuu na Mwanzele,walikuja hadi kwa barabara wakifwatana,lakini Mwanzele aliamua kuwa mwanaume,alimpigia kelele,akamwambia skiza mwanamke wewe,mimi ni mume wako na utazidi kuwa wangu na k**a ni pesa za babako za kulipa deni ndio hizi hapa,chukua elfu kumi. Zuu akachukua lakini akauliza Mwanzele,hizi pesa umetoa wapi? Ametoa kwa Major. Zuu alimwambia Mwanzele,heri nikunywe suturungi na steelwhool k**a es**rt lakini pesa za kutoka kwa Major,sitaki. Zuu alimrudishia.

Kumbe Fatima na yeye,alipigiwa simu na yule jamaa gaidi wake mwenye alipewa kazi ya kutafuta Buya. Fatima alimwambia nilikuambia k**a ni simu unapiga hakikisha ni mwili wa Buya ama pesa zangu unanipa,k**a huna lolote,usinipigie.

Kaka,huku kwa Babu,alimuita Salama,akamwambia shangazi,Zuu anasema anataka kuja kuishi kwa babake wakati unajua wageni wako,wako huko,tutashikwa? Salama alimwambia sikiza Kaka,k**a ni Zuu niachie mimi,nitamueka sawa. Kaka akamwambia ni hatari,yafaa ufanye jambo ama Maria uende ukae na yeye alafu Buya ajue kwenye ataenda. Kumbe wakiongea hivyo,Zuu ashafika kwa Salama kuja kuchukua vitu zake lakini kufika hapo nje,akapata mazawadi za Kokan zimetandikwa mateke na Sultana mwenywe hayuko. Yuko ufuoni lakini Zuu hajui aliko. Alianza kumuita.

Dr. James,Nandwa Kokan,ndio huyu ashakuja na dawa kumtibu Babu. Kwanza alivaa miwani,ju sisi watu huwa tunavaa miwani we only see naked things🀣🀣🀣Alianza kumtibu na kumdunga Babu mawaya kwa mwili. Sada yuko pale anaangalia tu kila hatua. Babu,dawa zinaingia tu pole pole bila tatizo. Shukrani kwa Kokan. Sada aliuliza Kokan hiyo sindani umemdunga ni ya nini? Kokan akamwambia huyu mzee hakua anakufa maji,inaonekana aligongwa na kitu na kwa miguu lakini atapata nafuu aende kupewa huduma za kwanza. Sada akamuuliza huduma ipi wakati wewe ndio daktari hapa? Kokan akamwambia mimi nataka mtu aamke anipe ruhusa ya kumuoa Sultana mengina ataenda hosi. Sada alimwambia na kweli wee ni wazimu🀣🀣

𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟐
Kokan alimaliza kazi na akaenda.

Mwanzele na yeye,alimpigia Major simu,akamwambia boss wangu nisikize,Babu ashaokolewa na atapona. Major akamwambia mimi sitaki kujua,nishakupa pesa fanya kazi yenye yafaa ufanye ole wako ukose kukamilisha kazi. Kumbe Major,alijua Babu yuko salama,akamlipa Mwanzele akuje amalizie Babu😒😒.

Kokan akitoka,alikuja kwa Salama penye alikua na Kaka,akawaambia kazi yangu nishamaliza sasa nataka Sultana wangu. Salama alimwambia sikiza,hakuna mazungumzo tunafanya k**a Babu hajapata nafuu na si nafuu apone kabisa. Kokan akawaambia hivi ndio iko sindio? Hamjui Kokan ni kusema nini.

Sultana na yeye,alikuja hadi ufuoni na hakaoni kanasikia tu sauti ya maji. Kachunge sana,maji yana kina kirefu I say!

Mwanzele baada ya kuongea an Major alikuja chumbani akachukua pesa zi ngine zenye alikua ameficha huku na ana mingi sana na usisahau ni Major alimpea amuue Babu na bado hajakamilisha. Kalianza kuzihesabu kumbe hata hakajui hesabu,kanafika elfu nane,kanasahu kanasema mia tisa🀣🀣

Wacha sasa Kokan,afike kwa Salama apate tuzawadi twake tumetandika tandikwa,alianza kulaumu akina Salama. Kaka akamwabia saa ngapi wakati tumetoka kwa Babu wote. Zuu alikuja akasema lazima ni Sultana kwa sababu nimepata iko hivi na Sultana hayuko nasikia ameshika njia ya kuenda baharini. Kaka,Salama na Zuu wakatoka mbio kuelekea baharini wakaacha Kokan akilia tu hapo🀣🀣

JJ na Dida wakiwa kwa barabara,walimuona Fatima amesimama na jamaa wa boda hapo. JJ akamwambia Dida unaona,huyo ni mamako na unaona chenye anafanya na ukimuuliza atapingana so huyu mamako si wa kuaminika hata kidogo. Fatima leo kapatikana red handed.

Sultana na yeye ameamua kujitosa majini. Lakini sasa ebu angalia hapa,Sultana ameingia majini kujimaliza,lakini wakati huo huo,Bi Ua na yeye anasumbuliwa na kitu,anataka kutoka lakini amefungiwa. Wakati anang'ang'ana kufungua mlango,Sultana anaendelea kusonga majini. Wakati tu Sultana anafika ndani kabisa ya maji,Bi Ua hatulii kabisa anataka kutoka hata yeye mwenywe hajui ni nini kinamsumbua lakini dhamira zake zinamwambia mambo si mazuri hata kidogo,kwa nini? Kwa sababu mtoto wake wa kipee,Sultana,akajizamisha majini,
Follow me Brian ngugi

03/01/2023

𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄𝐒: 𝐒𝐔𝐋𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐂𝐒𝐓𝐯 πŸ’π“π‡ 𝐉𝐀𝐍
𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟏
Hope sijachelewa saaaaaana wakuu but all in all tunaanzia kwa Salama. weka like.

Sada anaambia Salama,nik**a nalazimisha uhusiano wetu sana na nimeishi kukuuliza kuhusu Sultana na hutaki kuniambia mbona? Salama akamuuliza umekuja kuniuliza ama kuniona? Sada akamwambia,unajua ukweli,unataka kumuoza mtoto na huna idhini,k**a uko serious sasa,nenda uite shangazi wa Sultana wakuje basi. Lakini punde si punde,Zuu alifika,ashapigiwa simu na Kaka,akaambia Salama,Kaka amesema twende kwa Babu tumuage. Salama akashindwa tangu lini Babu anaenda safari? Zuu akamwambia si kuaga ya safari,I think Babu ni kuenda anaenda.

Dida na yeye akiwa kwa barabara na JJ ndio Kaka anafungua akapata try to call me ya Kaka. Akaambia JJ stop the car. JJ akasimamisha gari na Dida akatoka nje akasimama hapo kando. JJ akamuuliza kuna nini tena?

Kokan na yeye,kwa Salama aliitwa akaambiwa wee endelea kuimba wakati tunaambiwa Babu ako hali mahututi. Kokan akawaambia hakuna,nawajua sana,tangu lini Babu akawa hali mbaya wakati juzi tu tumekua na yeye,najua mnataka nitoke lakini hapa sitoki. Sada akaambia Kokan,naona chenye kilikuchoma masikio kilichoma hadi ubongo. Husikii tunaambiwa Babu yuko hali mbaya kijana. Kokan akamwabia wee pia utaacha kuingilia vita hazikuhusu alah🀣🀣Kokan anadhani story ya Babu is made up hana habari,Babu ni kuenda anaenda.

Buya na yeye akiwa na Maria chumbani,walisikia sauti za wamama wa Kokan. Maria akatoka kiasi kuchungulia ni akina nani. Buya alikua na wasiwasi lakini ni wapita njia tu wanaenda kwa Babu. Yaani Kokan anatembea na wamama k**a wazimu tu. Kufika kwa Babu,alianza kupiga kelele akiuliza huyu Babu yuko wapi? Kaka alimwambia sikiza Kokan,wewe ni daktari lakini ni k**a hunanga akili,huwezi sikia mzee yuko mahututi huku ndani na uko tu hapa story ni posa tu. Wakaingia wote chumbani.

Kufika chumbani,Babu,yuko hali mbaya. Salama alimguza akashtuka tu akajua huyu si wa dawa wala maji. Akatoka nje na akamuita Kaka akamuuliza ilikuaje? Kaka akawaambia nikifika baharini,niliona Babu amefungwa fungwa na manyavu na boti lake liko upside down. Like Kaka aliwaelezea kila kitu chenye aliona na akasema Babu alisema asiambie mtu. Kokan anawaambia waharakishe amalizana aendelee na shughuli zake za posa🀣🀣

Kokan walirudi chumbani wakaona Babu anaweza zungumza,lakini sasa,Kokan badala ya kushughulikia Kokan,alianza kuambia Babu venye anataka kumuoa Sultana na anataka baraka zake. Sada aliambia Kokan na kweli huna kichwa mzuri,unasema posa wakati Babu yuko hali mbaya,si at least umuhudumie kwanza asii. Mwanzele pia ndio anafika,its now 4 days since kaondoke,sijui kametokea wapi.

Nyumbani kwa kina Sultana,ndio anatoka chumbani,kufika hapo nje akabishana na vile vizawadi vyenye Kokan alikua ameleta. Sultana alishika akaanza kuvitandika kwa hasira na kuharibu haribu,kumbe hata ni mkarango tu Kokan alikua amekuja nayo🀣🀣

𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟐
Kokan alijitetea akasema hata k**a yeye daktari hana vivaa vyake kwa sababu alikua amekuja kwa poza wala si magonjwa. Mwanzele aliwauliza k**a anaeza saidia? Zuu akamuuliza sasa wewe unaeza saidia nini mwanaume fidhuli wewe. Sada ilibidi aingilie kati akamwambia aache Mwanzele aongee,lakini Babu alianza kuongea,akawaambia k**a ni Mwanzele,manze mimi siendi. K**a ni Mwanzele anapeana msaada afadhali nife mimi. Kumbuka,Babu yuko hivi kwa sababu ya Mwanzele na hata Sada mwenyewe anajua Babu akisema hivi lazima hii hali ya Babu,Major anahusima.

Akina mama huku nje nao,walianza kuimba zile nyimbo za kumsifu Kokan,lakini Kaka na Sada walitoka nje wakawaambia watoke waende huku kuna mgonjwa. Lakini akina mama wakaambia Sada,sisi tuko hapa hadi Kokan atupe pesa zetu tumeimba sana. Sada alicheka tu akawaambia huku Kokan hamna,nyi nendeni. Lakini Sada alishindwa,Kokan ametoa wapi pesa? Akaanza kuconnect dots.

Sultana na yeye alitoka kwao akaja barabarani kutembea,kwanza akianza kusikiza zile kelele za wamama wakiimbia Kokan,anaumwa sana.

Dida na JJ washafika restaurant wakule na kunywa kiasi. Wameitisha kaugali na tunyama. Aaah na Dida anakula ugali kubwa aje? Kwani ako njaa ama🀣🀣JJ na Dida walikuka wakienjoy sana kisha Dida akauliza JJ,hii ball ya Sultana what do you think about it. JJ akamwambia mimi sina maoni. Dida akamwambia unajua kila mtu anadhani ball ni yako? JJ akamwambia please achana na hiyo story for now tukule.

Turudi kwa Babu,Kaka alichukua simu kutaka kumpigia Dida simu,kumbe wakati huo,Maria alikua anachungulia,Kaka akamuona. Alikuja mbio akauliza Maria shida yako nini,unataka kuonekana? Lakini Buya alimisunderstand Kaka,akadhani huenda hizo sherehe za harusi ni za Kaka. Sasa Kaka anajaribu kueleza lakini Buya amekasirika sana anamwambia mpuzi unaoanga harusi na hujaambia binti yangu. Kaka alimwambia sina wakati wa kuwaeleza na naona mnaingilia maisha yangu sana. Kaka hakuwaambia Babu mgonjwa na harusi ilikua ya Kokan alienda tu.

Enyewe Maria pia aliona wameingilia maisha ya Kaka sana akaambia Buya manze,heri nirudi tu streets. Kisha Maria akaanza kukumbuka ile siku ya harusi yake na Luwi. Kulitokea noma na kikaumana,kisha yeye akafaulu kuhepa,akakutana na gari usiku hapo Mombasa road akawasimamisha akaomba usaidizi na hivyo ndio alijpata Mombasa...mambo bado.
Follow Brian ngugi

03/01/2023

𝐔𝐏𝐃𝐀𝐓𝐄𝐒:𝐒𝐔𝐋𝐓𝐀𝐍𝐀 πŸ‘π‘πƒ 𝐉𝐀𝐍
𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟏
Happy New Year Team Sultana! kumbuka kuweka like ukiendelea kusoma.

Tunaanzia kwa Major,JJ anamtafuta Sada hamuoni. Alikuja kuuliza Asiya lakini Asiya pia hajamuona. Kumbe JJ alitaka kumuona Sultana lakini alitaka atumie Sada. Asiya alimwambia pengine utamngoja tu yeye akirudi basi utamtuma.

Maria na yeye amekuja kuogelea na kumba akiwa majini,Kaka amesimama anamuangalia hadi Maria akauliza Kaka,msee rada? Kaka akamwambia ni venye nataka twende nyumbani. Maria alimwambia wee buda ishia nitakuja mwenyewe nyumbani. Maria anayafurahia sana maji.

Kwa Buya akiwa na Salama,Buya aliona kuna kitu kinasumbua Salama sana,hadi akauliza Salama kuna nini?Salama alimwambia manze nimeulizia kuhusu uti wa mgongo wako kupata tiba si rahisi na sasa usipoamka twende tutafute matibabu huenda ukaishi kulala tu. Buya akisikia hivyo,alianza tu kulia😒😒na ndio maisha hayo,leo u mzima kesho kilema!

Salama alirudi kwake,akapata Zuu akiwa na furaha,akamuuiza sasa wewe unasmile smile nini? Zuu akamwambia shangazi,yaani ukatoka asubuhi unarudi sasa hivi? Hadi ukalala nje? Salama akamwambia sikiza,Zuu,wewe si mume wangu,usinitibue wewe kunifuatilia fuatilia. Salama hataki Zuu ajue ametoka kumuona Buya,ju Zuu hajui Buya ako kwa Kaka. Kaka pia alifika akaona mamake yuko pale,akamuuliza kwani ulilala huku? Salama akamuita Kaka pembeni akamwambia huyu mamako asijue unakaa na Maria na Buya italeta shida sana. Kisha Kaka akatoa wazo,akaambia Salama waambie Dida kuhusu Buya huenda akamsaidia,lakini Salama alikataa,akamwambia hilo jukumu tuachie Buya mwenyewe wala sio sisi,lakini kiidogo hivi,wakiwa tu wamesimama hapo,Kokan na wageni wakafika🀣🀣🀣

Salama walishangaa sana kuona Kokan na akina mama wanakuja wakiimba. Kokan na yeye,anaitwa Mimi Sijali,hana wasiwasi hata kidogo. Sultana akiwa chumbani alisikia makelele nje akashindwa kuna nini tena,lakini hana habari,Kokan amekuja na beshte yake anaitwa Mbuzi. Salama alimshika Kokan mkono,akamuuliza huu upuzi gani unaleta hapa? Kokan akamwambia sikiza Salama,ningetaka sana kutuma jamii yangu ikuje kuniombea posa kwa niaba yangu lakini nimeona nikuje mwenyewe. Salama alimwambia naona wewe una kichwa mbaya Kokan,lakini Kokan alimwambia wee bweka lakini hapa sitoki k**a sijajua tarehe ya harusi🀣🀣Salama alimtuma Kaka aende kumuita Babu. Follow Nandwa Isaac for more updates.

Kwa Major,Fatima alikuja kumkuta Asiya akaanza kumpa msomo lakini Asiya alimwambia mimi hayo yenu sijui,tangu haya yatokee nimejifunza kunyamaza nashughulika na yangu tu. Fatima alimshika akamwambia sikiza,hayo maongezi yangu na Major nikiyasikia pahali,utajuta kuzaliwa. kumbuka,siku ya Ijumaa,Major akiongea na Fatima kuhusu kifo cha babake Major,Asiya alisikia na ndio maana anampea msomo anamwambia ole wake aseme ama asemezee mtu atajua hajui.

Sultana na yeye alitaka kutoka lakini Zuu akamzuia,akamwambia huko nje mwenye ako ni Kokan an amesema anataka kukuoa rasmi. Sultana hakufurahia ju sasa Kokan amefanya wanakijiji wote wajue ana ujauzito. Hakufurahia kabisa lakini atadu?

𝐏𝐀𝐑𝐓 𝟐
Dida na yeye anampigia Kaka simu,lakini inaenda unanswered. 'Anasinyika' sana,(nimeanza kuweka kiluhya hapo)🀣🀣

Upande wa Buya,Maria ndio anafika. Alikuja akapata Buya akilia,akamuuliza mzae,rada,nini inaendelea? Buya akamwambia hakuna shida lakini chakula chako kiko hapo. Maria akamwambia achana na story za food kwanza,ni nini kinaendelea? Nilidhani nikikuleta huku utapona lakini sioni dalili. Buya akamwambia ndio changamoto za maisha na kumbe venye nilimkataza binti yangu Dida kuto kuja huku nikitumia Kaka. Maria alimwambia manze itabidi uwe na courage niling'ang'ana sana kukuleta huku na siezi taka kuona ukiteseka,itabidi ubelieve tu sasa.

Kaka na yeye kufika kwa Babu,alipata mwanakijiji,akaulizwa yani Babu alinusurika kifo na nyinyi kazi ni mbwembwe tu karibu afe maji? Kaka akamwambia lakini ni mimi nilimnusuru kutoka majini na akasema yuko sawa. Mwanakijiji alimwambia Babu hayuko sawa kabisa,enda huko ndani umuone.

Kaka kuingia chumbani mwa Babu,mzee ako hali mbaya,anatetemeka,k**a generator. Kaka akamuuliza Babu,si ulisema uko sawa mbona tena? Lakini hata Babu kuongea tu haezi ongea. Kamzee kalizamishwa majini kakakunywa maji kisamaki kibahari😒😒

Dida na yeye kuona Kaka hashiki simu zake,akasema nini? "Kaka anadhani ni mjanja,let me go show him,what I am made of" hii ina maana,Dida anatoka kwa Major,moja kwa moja hadi kwa Kaka,and that is one,very big mistake. Dida akitoka,alikutana na JJ hapo nje. JJ akamuuliza waenda wapi Dida? Dida akamwambia kwenye naenda is non of your business,nipishe nitoke. JJ alimwambia come on,tumepitia mambo mob but please,don't go. JJ alikataa akamshika Dida akamzuia asiende.

Ona sasa mwanaume mwingine huku🀣🀣Kokan amekataa haezi toka kwa Salama,wamecheza hadi wamechoka tu na ameamua huku hatoki k**a hajaonana na Sultana. Kumbe wakati huo huo,Sada akafika,akauliza Kokan kelele za nini huku? Kokan akamwambia wewe mwanamke,usiingilie haya huoni Salama mwenyewe amekaa huko ametulia. Sada akaambia Kokan,mimi siongeleshwangi hivyo,chunga sana masikio yako isiende tena.

Sultana akiwa na Zuu,walisikia sauti ya Sada na Sultana akajua basi,k**a Sada amefika hapa,sasa JJ ashajua pia. Zuu akamwambia wasiwasi wako ni JJ ama Kokan,si wewe mwenywe ulishika ujauzito wa Kokan,ulikua unafikiria nini.

Sada alikuja kuongea na Salama,akamwambia siamini unataka kumuoza binti yako kwa hili zimwi linaitwa Kokan. Salama pia alimwambia hata hajui chenye kinaendelea,pia amepatikana tu off guard.

Upande wa Fatima,alikuja kuongea na Major. Major akamwambia,kwa sasa Fatima tufikiria kumpata Buya mume wako na baada ya hapo,mimi k**a Major sitakuacha hivyo tu. Fatima akamuuliza so unamaanisha nini? Major alimwambia hili swala la Dida na JJ,sidhani k**a hawa watoto wanapendana so tukubali tu. Fatima akamuuliza so unataka tutupilie mbali mambo ya ndoa ama? Major akamwambia kitu k**a hiyo,lakini wakiwa tu hapo,wakasikia JJ na Dida wakicheka kwa furaha na hili likamshangaza sana Major,lakini Major akibaki akiwa na mshangao,huku Fatima anabaki akiwa na tabasamu,sina budi pia kubaki nikiwaambia,kipindi cha hapo kesho kinaishia hapa. Hadi kesho majaliwa.

Follow Brian ngugi

Address

Maua

Telephone

+254798752411

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Brian ngugi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share