"Sasa Niwaulize Nairobi, Si mtaniua na Majina, Mlianza na Hustler, mkakuja Survivor, Zakayo sasa ni Kasongo. Sasa hii majina mtaongeza ifike ngapi jameni?" Rais William Ruto
BIKETI ANA MLINZI MKALI!
Bi Mary Biketi aliyewahi kuibua hisia mitandaoni Kwa kuweka picha akiwa na aliyekuwa gavana wa kakamega Wickliffe Oparanya ambaye hivi sasa ni waziri wa vyama vya ushirika na biashara ndogondogo.
Kanda ya video akiwa na mlinzi wake
#Habari
Hii Leo gavana wa Trans Nzoia George Natembeya Ilikabidhi pikipiki 25 kwa maafisa wa nyanjani wa kilimo katika wadi zote 25 ili kuboresha usafiri na ufanisi wao.
Bosi huyo wa Kaunti amesema kuwa hilo litawawezesha kuwafikia wakulima wengi zaidi na kutoa misaada na huduma muhimu za kilimo.
SALASYA NA ECHESA WAGOMBANA MBELE YA UMMA
"Wewe kijana wewe wacha kihehere, wacha bangi wewe... wewe umejengewa nyumba wewe..."
Sarakasi za Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Kalerwa Salasya na Rashid Echesa zachukua mkondo mpya, Watupiana maneno ..
#Habari
Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Maghulamu ya Kolanya kwenye kaunti ya Busia waliopata ajali wiki jana na kukimbizwa kwa matibabu ya Dharura wa kwenye hospitali ya Kocholya.
Wanagenzi hao waliojeruhiwa wanaonekana wakirundikwa sakafuni kama magunia ya mahindi, wengi wao wakiwa wamepoteza fahamu.
Ripoti zinaonyesha kuwa hakukuwa na dawa hospitalini, walimu na wazazi wakilazimika kwenda kununua dawa nje ya hospitali kabla ya watoto kuhudumiwa, ingawa hakuna aliyepoteza maisha, wanafunzi hao walitibiwa majeraha ya tishu laini na kuachiliwa.
Hii ni changamoto kubwa kwenye Kaunti hiyo ya Busia kupitia kwa Gavana Paul Otuoma.
#Habari
Rais William Ruto ameanza misururu ya mikutano katika eneo la Kamukunji Jumatatu huku akikagua miradi ya maendeleo katika eneo hilo.
Rais amehutubia mkutano wake wa kwanza katika eneo la Eastleigh, ambapo alielezea mipango yake ya maendeleo.
Anatazamiwa kufanya mkutano mdogo katika uwanja wa Kamkunji jijini Nairobi baadaye siku leo na kuhitimisha siku yake ya kwanza ya ziara katika Jiji la Nairobi.
SALASYA NA ECHESA WAGOMBANA MBELE YA UMMA
"Wewe kijana wewe wacha kihehere, wacha bangi wewe... wewe umejengewa nyumba wewe..."
Sarakasi za Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Kalerwa Salasya na Rashid Echesa zachukua mkondo mpya, Watupiana maneno ..
Gavana Natembeya anawachanua kidogo
#Habari
MAOVU YA POLISI NCHINI UGANDA
Kiongozi wa upinzani Katika Taifa jirani la Uganda Robert Kyagulanyi Ssentumu almaarufu Bobi Wine ameweka kanda ya video kwenye ukurasa wake wa Facebook inayoonyesha maovu ya vitengo vya usalama Katika Taifa Hilo.
Video hiyo inaonyesha jinsi maafisa wa Polisi wanavyo wakabili wafuasi wa upinzani Kwa kutumia nguvu kupita kiasi.
Je huu ni ungwana??
#Habari
Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya alishangiliwa na waombolezaji kwenye hafla ya mazishi ya marehemu mbunge wa Malava Moses Malulu Injendi alipotambulishwa.
Anasema angepewa nafasi ya kuwahutubia waombolezaji dunia ingepasuka.
"It's true ningepata hiyo microphone hapo dunia ingepasuka ,the good thing Shinali the mp of ikolomani did was to make sure I don't step forward as one of kakamega county mps the crowd could have demanded I deconstruct them in a manner that they deserve .The future of western kenya is in the safe hands and we are coming out so strongly." Salasya
#Habari
Baada ya Mbunge wa Malava Moses Malulu Injendi kuzikwa hapo Jana ambapo mazishi yake yalihudhuriwa na viongozi wakuu serikalini wakiongozwa na rais William Ruto, Mbunge wa Kimilili Didmus Wekesa Barasa ambaye hakuungana na na wenzake hiyo Jana, Mapema hii leo imekuwa zamu yake.
Mjumbe huyo wa Kimilili alitua Kwa kishindo Katika Boma la marehemu mbunge Injendi Kwa kutumia Helkopta na kutoa heshima na rambirambi zake za mwisho Kwa mwenzake kabla ya kufañya mazungumzo na familia pamoja na wakaazi.
Lakini Swali ambalo linasalia miongoni mwa vinywa vya wakaazi ni je, mbona hakuungana na viongozi wenzake hiyo Jana kwenye hafla rasmi??
Video Kwa Hisani
#HiviSasa
Hotuba ya Cleophus Malalah yawasisimua waombolezaji Kule Malava Kaunti ya Kakamega.
"Huyu Wetangula ako hapa lakini hayuko sure kama yeye ni Speaker, hata next week Raila anakujia kiti cha Prime Minister ambayo ni ya Mudavadi''
Aliyekuwa kuwa seneta vilevile katibu mkuu wa chama cha UDA Cleophus Malalah.