11/02/2023
Aina 10 ya nyoka wakupendeza duniani
• Hoja muhimu ni kwamba nyoka,anaweza kuwa kiumbe wa kipendeza lakini kwa mara nyingi lakini bado hawaeleweki.
• Nusu ya hawa nyoka ambao tunawapenda kwa ajili ya umbo lao huwa ni wenye sumu kali kwa hivyo ni bora kuwaangalia tu tukiwa mbali kwa ajili ya usalama wetu.Kwa sasa hakuna dawa ya kudhibiti makali ya sumu kutoka kwa nyoka wa samawati ambaye anafahamika k**a Blue Malayan coral .
• Nyoka wa kupaa wa paradice (Paradice flying snake) huwa hapai angani bali yeye hutambaa na kuruka kwenye miti .
Kunazo zaida aina 4,000 za nyoka duniani katika sayari yetu ya ulimwengu huu wa kupendeza. Na kwa hivyo zimechangia nafasin kubwa kwa wanayama wakupendeza katika sayari hii. Hivyo basi kutengeneza orodha ya nyoka wa kuvutia sana ulimwenguni si jambo rahisi, lakini aina ya nyoka ambao nimewaorodhesha hapa ni wale amabao wanavutia sana.
Hawa nyoka wanaishi katika sehemu tofauti ulimwenguni. Wengine wakiwa wanaishi chini ya ikweta, hivyo basi namaanisha sehemu k**a vile ,Afrika ya Magharibi, Afrika ya Kati ama Amerika ya Kusini. Na wengine wanaweza kupatikana katika Kusini Mashariki mwa Asia. Marekani na India. Baadhi ya hawa nyoka hupenda kufanya makaazi katika maeneneo yenye maji, wengine huishi kwenye misitu , kwa hivyo vigumu kuwagunduwa nyoka hawa.
Baadi ya hawa nyoka amabao nimewaorodhesha hapa , hupenyeza katika maakazi yetu na kusababisha maafa ya watu, licha ya hayo hatufaai kupuuza uzuri wa hawa nyoka.
Bila kupoteza muda basi tuanze kuwaorodhesha hawa nyoka ambao urembo wake hauwezi kusahaulika machoni pa watu.
1.Nyoka wa kumetameta(xenopeltis unicolor)
Kwanza tunamwangazia nyoka aina ya kumetameta, kuna ina mbili za hawa nyoka wa kumetameta yani familia ya xenopeltis ambao wanajulikana k**a nyoka wa jua au wa kumetameta . Hawa wanapatikana katika kusini mwa Mashariki mwa Asia, na katika visiwa vilivyoko karibu. Hi familia ya Xenopelitis unicolor iliwekwa katika kundi la Taksonomia na Bw Casper George Carl Reign Wardt mwana sayansi wa wanyama wa Uholanzi mnamo mwaka wa 1827. Hawa nyoka wanapatika katika nchi k**a vile, Mynamar,Uchina ya Kusini, Laos, Vietnam, Malaysia na Thailand.
Hawa nyoka wa kumetameta wanapata urembo wao wa kuvutia kutakana na magamaba yaliyoko kwenye mwili yao ,wao pia mwili huu una rangii kadhaa ambazo ni kijivu,nyeusi ama kahawia zinazo ongeza mvuto.
Nyoka wa kumetameta ni vigumu sana kukumbana nao kwani wao hupenda sana kukaa katika maeneo fiche k**a vile chini ya ardhi. Wakati wa mwingine wao huja juu ya ardhi katika shughuli ya mawindo wakati wa asubuhi na jioni. Ukiwaona kweli picha yao kamwe haifutiki katika machoni pa watu, kwani hawa nyoka magamba yao huagizi mwanga wa jua na kufanana k**a Upinde wa mvua.
2.Nyoka wa upinde/ili Mokasine (Farancia erytrogramma).
Nyoka wa upinde au Ilimokasine ni aina nyingine spesheli ambayo jina lake kweli linaendana sambamba na maumbile yake. Baadhi ya hawa nyoka huwa kwenye maji pia urembo huu wao huonekana sana kwenye tumbo zao, maridadi ya rangi tofauti k**a vile rangi nyekundu,manjano , rangi nyeusi kahawia na rangi ya chungwa huchangia sana katikamvuto wa hawa nyoka. Kunazo aina mbili ya jamii ndogo ya hawa nyoka lakini kwa bahati mbaya . ilifipo fika mwaka wa 2011 aina moja ya hawa nyoka ilikuwa imetokomea.
K**a vile wanayama wengine wa kuvutia, nyoka hawa wa ili mokasine hukaa katika maeneo fiche ,kwenye vimbwi vya maji ambavyo vimejaa mimea kule Amerika ya Kusini mwa Mashariki. Cha kushangaza hawa nyoka huwa wapole kwa wanadamu , hawawezi kumdhuru mtu. Bila shaka hawa nyoka huifadhi nguvu zao kwa ajili ya kuwinda vyura na mijusi. Hawa nyoka wana majina mengi tu yakiwemo; nyoka mwenye laini nyekundu(red-lined snake),nyoka mwenye michirizi(striped wampum)Japo hawa nyoka ni wakubwa . hawana sumu yakuwadhuru watu pamoja na wanyama wengine .nyoka huyu ana uwezo wa kuwa dhuru wanyama wadogo ambao anawala k**a chakula chake.
3.Nyoka mwenye kope za macho. (bothriechis schegelii)
Hawa nyoka ni wa kupendeza Zaidi katika hii orodha , katika familia ya viperdae ambayo ni aina ya nyoka wa rangi tofauti na za kipekee, kwa hivyo hawa nyoka wana kope za macho ambazo zime simama twisti , rangi ya nyoka hawa ni manjano, hawa kwa kweli wanaogopesha na wana macho makubwaa.
Hawa nyoka wenye mvuto wa kipekee hupatikana katika aneo la Amerika ya Kusini na Amerika ya Kati. wanapendelelea kufanya makao katika maeneo tulivu k**a vile misitu yenye matawi mengi na yenye giza. Watafiti wamebaini kwamba hizo kope zinawasaidia hawa nyoka kujificha dhidi ya adui. Kimaumbile, hawa huwa ni wadogo ikilinganishwa na nyoka wengine. Licha ya hawa nyoka kuwa na sumu kali huwa hawapendelei kuwa shambulia wanadamu. Huwashambulia tu wanyama wadogo k**a chura na mjusi na ndege kwa ajili ya lishe yao.
4.Nyoka wa kupaa wa paradice. (chrysopelea paradisi)
Huyu nyoka wa kupaa ni hatari sana katika jamii ya ofidiobofia(ophidiophobe’). Licha ya kupewa jina nyoka wa kupaa , hawa wanauwezo wa kuruka na kutambaa katika mti mmoja hadi mwengine katika miti iliyoko karibu. Ukimwangalia nyoka huyu akiruka kweli inapendeza , yeye hufanya mwili wake kukuwa na uweza wa kuruka kwa urahisi na kuvutia. Kuna aina tofauti ya nyoka katika jamii ya chrysopelea. Na kila nyoka husimama katika nafasi yake kulingana na mvuto na urembo wake. Huyu nyoka huwa na madoa doa katika mwili wake wenye rangi tofauti k**a vile kijani, manjano,nyekundu na rangi ya chungwa. Huyu nyoka huishi katika misitu yenye unyevunyevu kule Asia ya kusini ya Mashariki.
5.Nyoka wa samawati wa Malayan coral(calliophis bivirgatus)
Huyu nyoka anavutia lakini ni hatari sana , sumu yake huweza kuangamiza adui kwa haraka sana. K**a vile nyoka katika orodha hii . huyo nyoka hupatikana kule Asia ya Kusini Mashariki. Kichwa chake huwa nyekundu k**a damu na mkia wake huwa ni wa rangi ya samawati.mwili wake huwa na michirizi . kwa hivyo ni nadra sana kuwapata hawa nyoka na kuwafanyia utafiti ikizingitiwa kwamba wanafanya makao yao katika sehemu fiche k**a chini ya ardhi, kwenye mashimo ndani ya misituna na milima mikubwa.Japo huyu nyoka hana matata , ni rahisi Sanaa kumuua mtu .K**a umemwona huyu nyoka basi wewe ni miongoni mwa watu wachache duniani ambao wamemwona nyoka huyu.
6.Nyoka mwenye magamba ya unywele (Atheris hispida)
huyu nyoka ambaye ana umbo la kipekee , magamba yaliyoko kwenye mwili wake yanamfanya kuvutia Zaidi na kufana mnyama anaye fahamika k**a dragon. Huyu nyoka huwa rangi yake hung’aa, kichwa chake huwa kipana na macho makubwa k**a yale ya kinyonga. Hawa nyoka wa sampuli hii hupatakana katika rangi tofauti, mfano kuna wale nyoka wa kijani, manjano,rangi ya chungwa , kahawia na kijivu.Hupenda kufanya makao katika eneo la joto na kwenye misitu ya yenye mvua . hawa hupatikana katika Afrika ya Kati na Afrika ya Magharibi, katika nchi za;Cameroon,Nigeria,Uganda,Kenya na Ghana.
Japo hawa nyoka hawapendi uzushi, wanauwezo wa kudhuru mwanadamu na hata kusababisha kifo.
7.Cobra wa India.(Naja naja)
Huyu nyoka , Cobra wa India ndiye anaye fahamika sana ulimwenguni kwa nyoka za sampuli hii. Vilevile kuna king cobra nyoka ambaye sio nyoka wa familia hii.kunayo majina mengi ambayo ni maarufu miongoni mwa nyoka hawa k**a vile cobra wa Asia . nyoka huyu maumbile yake humfanya kufanana k**a amevalia kofia na miwani meusi . Huyu huwa ni mkubwa na ana urefu wa futi 5 na ni mnono.Huwa na rangi tofauti na ana uwezo wa kufanya makazi katika maeneo yote ulimwenguni. Huyu nyoka anapatikana haswa kule India, Pakistan,Nepal,na Srilanka. Pia hufanya makao yake mahali ambako kuna maji, viugulima,na pahali ambapo kuna mawe na miti. Sumu yake huwa ni hatari sana, imesababisha maafa ya watu wengi kule India .
8.Nyoka mwekundu wa kalifoinia.(Thamnophis sirtalis infernalis)
Je ungependa kumwona nyoka mpole?, nyoka huyu wa califonia ni mpole na anarangi za kupendeza mno. Nyoka huyu vile jina lake , inapatikana katika vidimbwi na kando ya ufuo wa bahari kule kalifonia. Ni nyoka ane ngaa sana na kumfanya kuvutia kwa rangi zake , haswa rangi yake nyekundu.. huyu nyoka anauweza wa kuogelea na pia anambinu tofauti za kuwinda chakula chake. Yeye hula samaki,panya na ndege. Huyu nyoka sumu yake haiwezi kimdhuru mtu na pia huwa hapendi fujo kwa wanadamu. ni mwenye umbo mdogo.
9.Nyoka Kipepeo. (Bitis nasicornis)
Huyu ni nyoka wa kuvutia lakini ni hatari sana . yeye humfanana kifaru, nyoka wa sampuli hupatika katika maumbile na viwango tofauti. Pia yeye hukaa katika maeneo tafauti ambako panaweza kumsitiri. Huyu nyoka . pembe zake ni nzito na zimemfanya kuwa maarufu sana katika ulimwengu huu kwani ameonekana kuwa wa kipekee .hizi pembe ni fupi na nzito,zina rangi rangi . huyu nyoka huishi katika Afrika ya Kati na Afrika ya Magharibi katika nch za ; Ghana,Sudan,Cameroon na Uganda. Yani kiufupi huyu hukaa sana maeneo yenye misitu na maji. Ambako yeye hujificha mchana na usiku hufanya mawindo . sumu yake huwa ni kali sana hufanya maangamizi kwa muda mfupi. Kwa bahati nzuri watafiti wamepata dawa ya kutuliza na kuuwa makali ya sumu ya nyoka huyu. Lakini kwa kawaida utajiepusha sana kukutana na nyoka huyu.
10.Nyoka wa mti wa zumaridi (corallus caninus).
Huyu nyoka ndiye anaetufungia orodha ya kumi bora. Nyoka wa mti wa zumaridi hujiviringa kwenye mti, huwa mdogo akijiviringa namna hii. Rangi yake huwa ni ya kijani na laini zilizo jiviringa na kuchaora umbo la zigizagi lenye rangi tofauti. Cha kushangaza ni kwamba nyoka wa sampuli hii huwa na rangi tofauti wakati wanapo kuwa wadogo, hubadilika na kuwa rangi ya mti wa zumaridi wakati wanapokuwa wakubwa, wakiwa wachanga huwa na rangi ya chingwa na nyekundu, macho yake huwa ya kijani na kinjano. Huyu ni nyoka mwenye uwezo wa kupanda miti kwa ustadi sana. Anapatikana katika maeneo ya Amerika ya Kusini, Brazil, Venzuela ,Guianas na Colombia , hizi nchi ambazo zinauzunguka msitu wa Amazon. Nyoka wa sampuli hii hufanya mawindo yake usiku na huwinda panya,ndege na mijusi na vyura.
Hapa ni mkusanyiko wa maelezo kuhusu hawa nyoka 10 kiufupi.
Nafasi Jina la nyoka Mahali inakopatikana
1 Nyoka wa kumetameta(xenopeltis unicolor) kusini mwa Mashariki mwa Asia
2 .Nyoka wa upinde/ili Mokasine (Farancia erytrogramma). Amerika ya Kusini mwa Mashariki
3 Nyoka mwenye kope za macho. (bothriechis schegelii) Amerika ya Kusini na Amerika ya Kati.
4 Nyoka wa kupaa wa paradice. (chrysopelea paradisi) Asia ya kusinimashariki
5 Nyoka wa samawati wa Malayan coral(calliophis bivirgatus) Asia ya Kusini Mashariki
6 Nyoka mwenye magamba ya unywele (Atheris hispida) katika Afrika ya Kati na Afrika ya Magharibi,
7 Cobra wa India.(Naja naja) India, Pakistan,Nepal,na Srilanka
8 .Nyoka mwekundu wa Kalifoinia.(Thamnophis sirtalis infernalis) kalifonia
9 .Nyoka Kipepeo. (Bitis nasicornis) Afrika ya Kati na Afrika ya Magharibi
10 Nyoka wa mti wa zumaridi (corallus caninus). Amerika ya Kusini