20/10/2020
🌱
_____________________
Kuna majira katika maisha huwezi kuyakwepa. Ni majira ya MAUMIVU na UGUMU wa hali ya juu.
Ni yale majira ukiwa kitandani kwako unakosa usingizi na unasema:
“Nadhani sasa ndio basi tena, nimefika mwisho, Niangalie kitu kingine hapa ndio basi tena”.
Huu ni wakati wa kawaida kwa kila mwenye ndoto kubwa.
Ni maumivu ya kawaida kwa mtu mwenye malengo makubwa.
Kuna maumivu mengine yatatokana na Makosa ambayo utakuwa umefanya mwenyewe.
Usiendelee kujihukumu, jisamehe, jifunze na fungua ukurasa mpya usonge mbele.
Huwezi kuinuka kwa kuendelea kulia na kusikitika.
Katika kipindi hiki unaweza kupata presha kubwa sana ya kulaumiwa kwa ulichofanya, kuchekwa kwa aibu iliyokukuta ama watu kukutolea mifano ya watu waliofeli katika jambo fulani.
Take heart and make one more step (Jitie moyo na chukua hatua nyingine moja leo).
Una kitu kikubwa ndani yako na HATIMA yako ni kubwa sana.
Watu wenye hatima ndogo hawakutani na hizi changamoto kwa sbabau ni k**a wanapanda mlima mdogo, USIJILINGANISHE nao.
Wewe hatima yako ni k**a MLIMA MREFU sana unahitaji pumzi na njiani kuna kuchoka na kuhisi kuishiwa nguvu.
Don’t Quit!
Haya unayopitia leo yanakutengenezea USHUHUDA, yanakuimarisha na yanakujengea TABIA zinazohitajika kwa ajili ya mafanikio yako.
Be Strong!
Kesho yako Inang’ara kuliko jana na leo yako.
Be confident!
Chochote unachopitia leo,jiambie “Ingawa napitia magumu haya, SITAKATA TAMAA”- Go through it but never Quit!
Tufanye ushuhuda pale Youtube @ ama bonyeza 👇👇 https://youtu.be/t9j6MLw1n1o
RAY MUSIC
🌱