
11/01/2025
Kuondoa wazo la uongo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa...🌱
💧
K**a vile mtumiaji huyu wa mtandao kwenye jukwaa la WhatsApp, watu wengi bado wanafikiri kwamba mabadiliko ya hali ya hewa ni ya asili ao kawaida ya dunia tu, na hayawezi ku kabiliwa na binaadamu, lakini ukweli wa kisayansi unasema vinginevyo. Ripoti ya GIEC (2021) inaonyesha wazi kwamba shughuli ao kazi za binaadamu (uchafuzi wa mazingira, ukataji miti, viwanda) ndio sababu kuu ya ongezeko la joto duniani, kuongezeka kwa ukame, mafuriko na majanga mengine.
Tuna jukumu la kutekeleza...imani na matendo vinaweza kukaa pamoja. Kulinda asili ao mazingira pia kuna maanisha kulinda viumbe vya Mungu.